Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kutangaza Baraza la Mawaziri kesho - Jumanne (12/02/2008) saa 4.00 asubuhi katika Ikulu Ndogo ya Chamwino, Dodoma.

Wahariri/Waandishi/Wapiga picha wawe wamewasili ifikapo saa 3.00 asubuhi, na wale wenye waandishi wao Dodoma wawaelekeze vyema ili wazingatie muda.

Vyombo vya Televisheni vinavyohitaji kutafuta signals na kuweka vyombo vyao sawa wanaweza kuja kuviweka leo jioni au kesho mapema asubuhi pale Chamwino. Tafadhali TVs ziweke scrolling message ili wananchi waelewe pia.

Wale wote watakaochelewa kufika hawataruhusiwa kuingia pindi Rais akishaingia.

Tunaomba tushirikiane kufanikisha kazi.

Ahsante na karibuni.


P. Kibanga
MHRM
Ikulu, Chamwino
DODOMA.
11/02/2008

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Michu mwambie da Premi siku nyingine afikirie muda angalau na sisi wa ughaibuni tupate nyuzi on taimu.
    Kwa mtaji huu kesho ntaamka habari zishadoda sisi wa ughaibuni ndi wahitaji habari zaidi!

    ReplyDelete
  2. Bw.Michu je Unahabari kuwa Mzee wetu wa Itikadi(Kingunge) naye kaamua Kustaafu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...