Twanga pepeta bendi yenye wapenzi wengi mjini Muscat kuliko bendi nyingine yeyote kutoka bara la Africa, inaendelea kutingisha jiji la Muscat kwa style ya pekee katika sherehe za kila mwaka zinazofanyika mjini Muscat ambazo hujulikana kwa jina la “MUSCAT FESTIVAL”

Bendi hiyo ambayo hufanya maonyesho yake kila siku katika “Muscat Festival” imekuwa kivutio kikubwa, watu hujaa mpaka wengine kukosa pa kukaa.

Mpiga gita la bezi Jojo Jumanne nae amejipatia umaarufu mkubwa, kwa kutaniwa kila siku kuwa ni Mrufiji wa kwanza kuja Muscat.

Twanga wanategemewa kumaliza shoo ya mwisho siku ya Jumamosi na Jumapili wanarudi Tanzania

Mdau Fadhili na Muscat.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nisikia LOWASSA kafariki hivi ni kweli?

    ReplyDelete
  2. Sasa wewe Anony,pamoja na kumuombea mabaya huyo Lowasa, hapa penye habari ya Twanga Pepeta wakiwa Muscat hiyo habari ya kifo inaingilia wapi sasa?. Watu wengine Bwana.

    Poa twanga tunawafagilia na hiyo ziara yenu ya kwenye MUSCAT FESTIVAL. Bongo wana wa miss

    ReplyDelete
  3. wawa twanga mnakandamiza kibara twende kazi

    ReplyDelete
  4. Embu huyo mdau anaejiita Fadhili atuletee picha za hao mashabiki tuwaone. Asitufunge kamba hapa, pengine wanatumbuiza viti huko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...