HABARI ZA LEO BWANA MICHUZI,
SISI WAFANYAKAZI WA UWANJA WA NDEGE WA NYERERE TB II TUNA MALAMIKO AMA MA DUKU DUKU YALIYOJAA NA TUMEONA LEO TUWEKE WAZI ILI ANGALAU IJULIKANE NINI KINACHOENDELEA.
MICHUZI WEWE NI FREQUENTLY FLYER UNATUMIA SANA UWANJA HUU. NADHANI UNAKUMBUKA KUWA MWANZONI OFISI ZOTE ZA TICKETING, BUREAU DE CHANGE ZOTE ZILIKUWA NDANI, THEN MWAKA JANA MWISHONI TULIFUKUZWA KAMA MBWA TUKATOLEWA NJE ETI KWA AJILI YA KIUSALAMA NA KULIKUWA NA UJIO WA NAIBU WAZIRI MAMA MAUA DAFTARI. WATU HATUKULALA,MAFUNDI WALIKESHA KUTWA KWA UJENZI NA KUPAKA RANGI KUTA,HII INAONYESHA NI JINSI GANI HAWANA MPANGILIO NA MAMBO YAO.
TULIKUBALI NA TUKAVUMILIA.SASA IKAJA SEHEMU YA KUPEWA VITAMBULISHO VYA AIRPORT,WAFANYAKAZI WOTE WA NJE TUMEPEWA VITAMBULISHO VYA KUISHIA UTAWALA NA SI KWINGINEKO,NA BEI WALIYO CHARGE TZS 20,000/= NI SAWA NA VYA WAFANYAKAZI WENGINE. HII HAIJATULIA KWA KWELI.
SASA MALALAMIKO YETU NI KUWA KUNA BUREAU INAITWA GALAXY INAMILIKIWA NA DADA RAIA WA ASIA, RESHMA DOSSA, IKO NJE. LAKINI GHAFLA JUZI WAMEMPATIA TENA NAFASI NYINGINE NDANI KWA AJILI YA KUFUNGUA BUREUA NA HILI LIKO WAZI KIBANDA KIPO NA KIMEANZA KU OPERATE JANA. SASA MWENZETU ANA MILIKI OFISI MBILI NJE NA NDANI NA ANA KITAMBULISHO CHA KUMRUHUSU KUINIGA NDANI.NA KULIKUWA NA MKUTANO SUALA HILI HALIKUWEPO; SASA KULIKONI??? NDIO HAYA MAMBO AMBAYO RAIS HATAKI KUYAFUMBIA MACHO.
NANUKUUU WARAKA ULIOTUMWA KWETU WOTE WAFANYAKAZI BAADA YA KULIONA HILI.
KULIKONI????
10FEB 2008.
MKURUGENZI WA UWANJA UNALITAMBUA HILI??RAIS NJOO USAFISHE NA AIRPORT.HAKI SAWA KWA WOTE.
KWA NINI GALAXY BUREAU (RESHMA) IWE TENA NDANI?? BASI NA VIBANDA VYOTE VYA NJE VIRUDISHWA NDANI AMA TUPEWE VITAMBULISHO VYA KUINGIA NDANI. HII SIO HAKI NA SI HALALI.( NDIO UFISADI HUU) NINI KINACHOENDELEA HAPO?? BASI HATA IMALASEKO BUREAU WANA HAKI YA KUPEWA.
KULIKONI???????TUNAHITAJI MKUTANO NA VIONGOZI WA UWANJA TENA KWANI HILI SUALA HALIKUWEPO MWANZO.
BY WAFANYAKAZI WA OFISI ZA NJE.
UKIMWI UTUUE NA MAFISADI PIA!!!!!!
KWA KWELI INABIDI RAIS AKIMALIZA YA HUKO ATUME WATU WAKE WAJE WACHUNGUZE NA HUKU ,KUNA BAADHI YA VIONGOZI WAKO MUDA MREFU ILA HAWATAMBUI WAJIBU WAO,NA TUMEWACHOKA .TAA INAHITAJI MABADILIKO SANA,RE SHUFFLE ....TUMECHOKA KUONA SURA HIZO HIZO AMBAZO HAZINA UFANISI WA KAZI,WANAPANDA NA KUSHUKA NGAZI ZA UTAWALA TU,CHAI ZA FLAMINGO CAFETERIA NA SOGA MA OFISINI LAKINI HAKUNA KINACHOFANYIKA.UWANJA UNAVUJA MAJI OVYO,MVUA IKINYESHA UPANDE WA ARRIVAL WATU HAWAWEZI KUPOKEA NDUGU/JAMAA ZAO.,SASA WANAACHA KUSHUGHULIKIA VITU KAMA HIVI WANAHANGAIKA NA MAMBO MENGINE..-TUNA MENGI YA KUONGEA,TUNAOMBA SUALA HILI ULIFIKISHE MAHALI PAKE.ASANTE SANA LIFANYIE KAZI,UFISADI UKO KILA KONA ILA SI HUUU WA MACHO MACHO NAMNA HII....TUMECHOKA.


Kwa kweli aliyotoa maelezo hayo ni msema kweli kabisa yaani uongozi wa airport umekuwa ukiwakumbatia hawa ndugu zetu wenye asili ya kiasia!
ReplyDeletebig up uliyetuma hii post!!!!!!!!!
Bwana Michuzi, nafarajika sana ninapo ona watanzania wengi ndani na nje ya nchi wanafaidika kupitia blog hii.
ReplyDeleteMimi binafsi kabla sijaanza kazi lazima nichungulie kuonana nini kinaendelea huko nyumbani. Kusema kweli swala hili la unjustince nchini Tanzania limeshaota mizizi.
Watanzania wenye asili ya Asia wanachangia kwa kiasi kikubwa kukandamiza haki ya sheria, vile vile kuongezeka kwa rushwa ndani ya nchi.
Kama airport wameamua kufanya maamuzi ya kuwatoa wafanyabiashara wadogo wadogo ndani ya uwanja, basi ni haki kwa kila mfanya biashara kuwa na office nje ya uwanja, na si vinginevyo.
Ni ufahamu wangu kwamba insider wengi kutoka serikali wanapitia blog mara kwa mara, basi ningepeta kuwauliza wapi haki sawa kwa kila mtanzania? Jee swala kama hili sio chanza cha double standard? Jee tutashinda mafisadi kwa njia hii, ikiwa the whole system is corrupted?
Tanzania ni nchi changa sana, nchi ambayo inasafari ndefu sana, lakini safari yetu inaweza kupata dosari kama tutafungia macho mambo ya unyanyasaji, ubaguzi na rushwa. Ni imani yangu kwamba swahala hili litawafikia walengwa na waliousika watahadhibiwa mara moja. Rushwa ni rushwa, hata iwe sawa na kibaba cha unga bado ni rushwa. Mimi binafsi naomba TAKUKURU wavalie hili swala njuga, na kama kuna aliyehusika kupindisha haki kwa raia hawa wema wenye kutafuta ridhiki yao, basi afikishwe mbele ya sheria ili haki ichukue mkondo wake.
Mdau wa US
Doh! hiyo niaibu kubwa,uwanja wa ndege wa kimataifa unavuja wakati wa mvua kiasi watu wanashindwa kupokea wageni wao kwa raha!!,kweli hapo kunamafisadi,inabidi iundwe tume ya kuwachunguza watu wanalipia huo uwanja wanaposafiri,sasa inakuaje uvuje?
ReplyDeleteLa haula kwa kweli yaliyosemwa hapo ni ukweli ,tena hayajamalizwa yote....inatia sana uchungu na hasira. Uwanja unaoza kwa ajili ya watu wachache.
ReplyDeleteNa katika suala hili la kumpatia mdosi ofisi ndani nasikia kuna wakuu wawili wanahusika vilivyo..wanafahamika sasa sijui inakuwaje hapa wana taka kuleta mambo ya BOT NA RICHMOND ...hatutokaaa kimya sasa tutasema ukweli.AIRPORT INAVUJA MAJI WANAKAA KUWASUMBUA VIJANA WA MASU KUTWA,VYOOO VICHAFU NA VIBOVU KUTWA VINAJI LOCK,HAWAJAMALIZA MAREKEBISHO KWENYE BAADHI YA MAOFISI NJE,HAWAONI HAYO WANAONA YA MHINDI.
Mdosi mwenyewe ni jeuri ,anatukana wafanyakazi,wateja ovyo,ana kesi kibao sub-police station ndani,nani ambaye hajagombana naye??leo hii wanamthamini sana kuliko hata ngozi iliyofanana na wao.
TUNASEMA SHERIA IFUATE MKONDO WAKE.....ATOKE NJE AWE SAWA NA WENGINE ,KAMA KUNA KITU CHA ZAIDI BASI WASSEME NA SISI TUFANYE HIVYO.
TUMECHOKA TUMECHOKA TUMECHOKA.
MAANA JENGO ZIMA WAMILIKI WATAKUWA WAHINDI YAANI MR. SADRUDIN NA BI .RESHMA DOSSA/
duh kaka michu hiyo issue ni kweli uongozi wa T.A.A umeoza kwa rushwa za wazi
ReplyDeletebadala ya kushuhulika na kuziba uwanja usivuje maji wanashuhulika na hawa makabacholi
kama jana ungekuja airport ni aibu kwa jinsi palivyojaa maji ya mvua sehemu ya kupokelea watu (arrival)
Nimesoma malalamiko ya hawa jamaa wa uwanja wa ndege (ofisi za nje) kwa masikitiko sana. Nafikiri katika sekta ambayo waziri wa mawasiliano Dk. Kawambwa aanze nayo ni Uwanja wa ndege. Kwanza tatizo la management si uozo huo tu ulioonyeshwa na hawa waganga njaa wenzetu wa ofisi za nje. Kwa ujumla utendaji wa shirika unaendelea kuoza kila kukicha. Kwanza kiwanja kinazidi kufa, utalitambua hili mara ukiingia kwaajili ya check in. Kwa kiwanja cha Dar hasa ikiwa kipindi cha joto utaona aibu, utapigwa joto mpaka unaingia ndani ya ndege. Air conditions zote zimekufa na hakuna jitihada zozote zinazofanyika. Belt ya kupandia ngazi imekufa na pameachwa ovyo. Halafu hata MH. Raisi alishaona uozo na kusema hawezi kununua ndege za shirika (Yaani ndege zetu wenyewe), sababu ndio haohao waliouwa za mwanzo bila kununua hata moja mpya, aibu sana. Nafikiri management yote inabidi isafishwe, yaani wale wote wasiowajibika kwa maslahi ya Taifa aka MAFISADI waondolewe maramoja. Naamini wapo watendaji wazuri wenye mikakati endelevu, hivyo wakati wa kusafisha uozo ni sasa, raisi Kikwete shuka chini kidogo uendelee na kusafisha UFISADI huu uliokithiri. Wako MKWELI.
ReplyDeleteMleta hoja asante sana maana uko wazi na maelezo yako yanaleta uchungu wa kupambana zaidi na mafisadi pamoja na wazembe.
ReplyDeleteKama yalivyosimuliwa ni kweli, basi pamoja na kupambana vikali dhidi ya huo uongozi mbovu, mimi bado pia NAULIZA KWA SAUTI KUBWA KUWA HATA YEYE MWENYEWE GALAXY BUREAU (RESHMA),JE KATIKA DHAMIRA, NA ROHO NA AKILI ZAKE NA MAADILI YAKE YA KIBIASHARA NA DINI YAKE (HATA KAMA NI YA KUTOMWAMINI MUNGU) HAISI KUWA NA KATAZO LA KIJAMII (SOCIAL INHIBITION) KATIKA HILO ALILOLIKUBALI?
MAMBO YA NAMNA HII NDIYO YANALETELEZA JAMII FULANI KUANZA KUTUKANWA MATUSI YA UJUMLA KITU AMBACHO KWA KWELI SI HAKI!
M/s GALAXY, USIPOTOKA NJE AU KULAZIMISHA NA WENGINE KUPEWA NAFASI KAMA YAKO NDANI, BASI MIMI BINAFSI,FAMILIA YANGU NA RAFIKI ZANGU NA WAGENI WENGINE WANAKAOSHAWISHIKA NA USHAWISHI WANGU NITAKAOUWASILISHA KOKOTE HATA KATIKA VITABU MF. LONELY PLANET N.K, MAGAZETI, MITANDAO NA VIJARIDA VYA WASAFIRI WAENDAO NJE, TUNAKUWEKEA VIKWAZO VYA KIUCHUMI KWA KUKUSUSA HATA KAMA UTASEMA LEO KIWANGO CHAKO CHA KUBADILISHA FEDHA NI EURO 1 = TSHS. 1 KWA WANUNUAJI WA EURO AU EURO 1 = TSHS. 1,000,000 KWA WANUNUAJI WA TSHS!
KIAPO CHANGU NYAKATAKULE:
Sitasubiri uundwaji wa tume maana pia zitaongeza gharama za maisha yetu bila kuwafanya wanaochunguzwa kulipia gharama hizo. Palipo na ukweli wa ukiukwaji nitakukarabati sawia kwa kadiri ya uwezo wangu Mungu nisaidie!
mmh balaaa tena tunasikia M/s Reshma analeta kashfa na kusema kuwa MWENYE WIVU AJINYONGE, na hiii yote jeuri kwa sababu anajuaa ana watu wanaomsaidia na aliowaweka mikonnoni mwake ,ila hiyo haisaidiii kitu.
ReplyDeleteTena anajigamba huku na huko akiongea kwa sauti,ila akae ajue kwamba anazidi kuwachomea moto hao waliomsaidia...VIMEO ndio anawakandamiza kwenye BOT NA RICHMOND sasa,ngoja waone kazi watu hawanyamazi na hawatoishia hapo..tumechoka na upendeleo.
asante.kwani yeye amweza ana nini hata sisi tushindwe tuna nini???????
Kwanza huyo mr virji hapo flamingo kajaza wahindi kibao na hawalipiwi hata work parmit!je wenzetu mlio ukerewe mnapata uhaueni huo?
ReplyDeleteanawatumia watu wa immigration kwa njia anazojua yeye ili asiwalipie hizo gharama za WORK PARMMIT!
in short airport ni uhozo mtupuu,ufisadi wa hali ya juuuu!
Rushwa hadi toroli la kubebea mzigo utakuta majamaa wameyakumbatia na kujifanya anataka akusaidie kusukuma huku anakuangalia mijicho ya fisi kutegemea mfupa wa mkono utamdondokea wakati ukiupunga pale unapotembea kusogelea toroli lile,
ReplyDeletemijamaa ya usafi ishamaliza shift inahang around haiondoki, inaniudhi na yanatia aibu. kero hiyo pia ishughulikiwe.
Ni kweli Mr Michuzi Airport yetu haina mpangiliao na ni chafu sana ukilinganisha na hata Aiport ya watani wetu wa jadi (KENYA)bado hatuwafikii hata chembe.Tupo nyuma sana na inalete picha mbaya hasa wageni wanapowasili toka nje.
ReplyDeleteKwani kuna kipindi nilikuwa natoka Zurich na watasha tulipofika Airport wote wakaanza kucheka wakasema what the hell is this country Airport!!
Walishangaa sana japo walisifu sana jiji la DAR lakini Airport yetu is Rubbish tangu miaka 10 iliyopita hakuna matengenezo yoyote.
Ndugu yangu lazima ujue kuwa tunaishi kwenye system ya ki capitalist. Kama yeye anacho na wewe huna hamuwezi kuwa sawa.
ReplyDeleteWahenga walisema mwenye nacho anaongezewa. Kubali yaishe kama una bureau de change punguza rate maana huyo reshma gharama anazoingia kujiweka hapo kwa mwaka nadhani hatodumu.
Aliye juu mngoje chini. Wivu utakuumiza roho hadi lini. Nenda kahonge hela nyingi kama alivyohonga yeye basi na wewe naimani watakupa hiyo nafasi. Kama huwezi acha kulalamika.
Ni sawa na mimi nilalamike kuwa rafiki yangu ninaemjua analala hotel ya movenpick wakati mimi niko kwenye guest house. Aliye nacho si sawa na maskini.
Wahenga walisema MWENYE NACHO ANAONGEZEWA. Mimi kwangu naona huna kesi. Alafu watalii wengi huwa hawabadilishi hela nyingi wakifika tu. Sana sana watakuwa wanachange hela ndogondogo tu na hizo haziwezi kumfikisha kokote huyo dada.
Basi msikonde Wanawaneee!! nawahakikishieni kati ya Tar.16 hadi 19feb.mambo ulimswanoo hapo JK Airport... alafu mnene akishaondoka basi turejee kwenye yale Mambo yetu yale...
ReplyDeleteBongo jamani! si-mchezo.
we anon feb13 3.14
ReplyDeleteHawo watasha uliotoka nao Zurich walisema "“What the hell is country Airport?”" walijuwa na maana gani?
ha ha jamani kwa mlio nje ni kwamba sasa ivi uwanja ule wa ndege unatisha nilifika pale juzi kwanza vyoo vya upande wa depurture vimefungwa nikajaribu kuuliza nikaambiwa vina mwezi sasa eti wanatengeneza sasa nikaenda upande wa arrival kule nako vyoo vinafanya kazi tundu moja tu kwanza ni vichafu hakuna mfano hata ubungo ni pasafi nako nikauliza madereva tax wakasema kuwa ni wiki sasa sasa nauliza kama mlijuwa mnauhaba wa vyoo kwa nini msiweke tangazo kubwa watu wakajuwa kuwa vyoo havifanyi kazi? kweli hii ni aibu uwanja wa ndege unakua na tundu moja la kujisaidia, sasa ilo moja kwenye parking za magari vile vya kufunga na kufungua kuruhusu magari havifanyi kazi sasa ni zaidi ya miezi mitatu wanakupa ile kadi manual hakuna maelekezo yoyote jinsi ya kugesha gari badala yake ukipaki sehemu sio husika unatozwa faini ya sh 20,000 sasa kwa nini wasiboreshe huduma kama mwekezaji kashindwa kazi si watafute mwengine wa mpatie iyo tenda? au ndio mnapeana kazi kwa kujuaana maana ile parking tunasikia ni mradi wa mkubwa fulani akishirikiaana na UONGOZI WA TAA. sasa ukija kwenye uongozi kuna PONJORO anaitwa SADRU huyu mhindi amechukua sehemu kubwa sana ya biashara ya pale uwanja wa ndege ndani na nje huyu jamaa kuna taarifa kuwa anahonga ama kushirikiana na viongozi wa TAA anawapa rushwa na kuwanunulia magari na hivi karibuni amehamisha ofisi za polisi na kupewa yeye afanye biashara eti kawajengea ofisi kule terminal one hivi kweli inakuingia akilini jeshi la police unalihamisha sehemu kama uwanja wa ndege na kumpa SADRU afanye biashara sasa izo kodi kwa nini msizibe paa linalovuja waliweka SCREEN hapa tangu zimewekwa hata kazi hazifanyi ukifanikiwa kuona ule mradi wa kuweka screen utashangaa ni mamilioni sasa hata kazi hazifanyi kwa nini msisitoe kama hazifanyi kazi kitu kingine uwanja wa ndege wa hauna hata maabenchi ya kukaaa mabenchi yapo sema ya mbao kwanza hayana hadhi ya INTERNATIONAL AIRPORT hata tazara wanawashinda wameweka masofa hela zinakwenda wapi?? kazi kukumbatia wahindi na kuwapa BIASHARA kweli uwanja wa ndge unazorota kwa wakubwa kufanya mambo kama hawajaenda shule kuna vijana wamezagaa pale wa kihuni wao kazi yao kudaka na kuwarubuni abiria na kuwadanganya kuwa wao ni maaagent wa TOURS SAFARI wanajulikana na wana muda mrefu sana pale huoni wakichukuliwa hatua wapo na wanendelea na kazi ilihali kuna maofisi makubwa ya tOURS pale kweli hii tutafika tunaomba uongozi wa TAA uangalie haya habari za kukumbatia WAKINA SADRU tutawatuma kina MWAKYEMBE waje pale sasa ivi hatutaki UTANI ofc za polisi mzirudishe kwa uongozi wa TAA na SADRU mumpeleke kule TERMINAL I na sio mnatuletea blaa blaa hapa miundombinu mrekebishe taa na vyooo na mambo yanayohusu sio kupokea hela za matangazo na hali ya uwanja hamrekebishi kweli inaboa
ReplyDeleteJamani eeeh!! Hiyo hali ya hapo airport inashtua kidogo. Lakini mimi nadhani tunaelekeza hasira zetu in the wrong direction. Tusimkasirie jamaa aliyepewa nafasi, tuwakasirie waliompa nafasi baasi ya kufukuza wengine. Wewe ungepewa opportunity ya kufanya biashara yako iwe poa ungekataa? kwahiyo dosari iko kwenye uongozi, as far as I am concerned. Haya majengo yanahitaji maintenance jamani na kama mnasema kuna ubovu kibao including vyoo na kuvuja, hiyo inaniambia kuna uzembe au incompetence mahali fulani.. Ndugu zangu nakuombeni tuache hii tabia ya kuwaita ndug zetu wenye asili ya kiasia "MAGABACHOLI" haaimsaidii mtu na namlaani yule taahira aliyeanzisha msemo huo, tunatakiwa kuukomesha mara moja. Tusipofanya hivyo basi tusishangae kama hawatuamini, hawatuthamini wala hawatupendi.
ReplyDeleteTusimtake Rais kushughulikia dari la airport kuvuja, hilo ni suala la kushughulikiwa na mtu wa chini na si Rais.
Mdau - Boston, US
Mhindi kamwaga dola/euro. Nyie mnataka kumwaga shilingi mnategemea nini? Corruption bureau wanasemaje hapo?
ReplyDeleteHizi ndio sababu zilimfanya Idi Amin afukuze wahindi Uganda na Mugabe anyang'anye wazungu mashamba,why do they get special treatment?
ReplyDeleteNdugu michuzi ni mimi Mbegy tena Nataka nami nitoe nasaha au muongo mkono kwa bwana aliyetoa malalamiko yake kuhusiana na mipango ya hapo Airport, Sheria isiangalie utaifa iwe ina apply kwa usawa sasa basi kama hayo asemayo mlalamikaji ni kweli basi Serikali yetu haina msimamo kama alivyosema KULIKONI????? Ukimwi Utuuwe Na Watoa Rushwa!
ReplyDeleteMambo ya Airport ni uozo mtupu kuanzia majengo mpaka wahudumu wao sitaki kukumbuka yaani ukifika tu sijui wanajua wewe umebeba gunia la hela wanaomba wananiuzi kitu kidogo tuu wanaanza dili jamani kubadilika ni issue sijui ila Mungu atusaidie na kutuondolea wala rushwa sehemu zote za huduma muhimu.
ReplyDeleteNataka tu kuwajulisha kuwa hili swala tumeli-file tayari na si muda mrefu tutatuma wasaidizi wetu watatuletea ripoti na ikiwezekana tutakwenda wenyewe kumaliza duku duku la wanaohisi wameonewa na itabainika kuwa kuna kasoro basi tutapeleka taarifa kamili kwa wahusika na sheria itafata mkondo wake. Tutaendelea kutimiza Ahadi ya Rais yakuwa serikali yake ya awamu ya nne si ya kuchezewa hata kidogo na ndiyo maana tunawahahakishieni malalamiko yenu yemetufikia na kwa moja au nyingine tutayaangalia wapi kuna tatizo. Ahsante
ReplyDeletesallams ,
ReplyDeletesasa nasikia kuna issue ya kulipia vyoo ,kila ofisi inatakiwa kulipia Tzs 10000/= .sasa swali ni kwamba je,ofisi zilipe! na hao wanaokuja kusindikiza na kupokea ndugu zao je watalipia???na mateksi drivers nao watalipia???
Ila inabidi kwa kweli waweke ustaarabu wa kutenga vyooo kwa ajili ya STAFF na WASIO STAFF ,yaani ikibidi wakabidhi funguo kwa kila ofisi ambazo zitalipia bill ya choo,isiwe unalipa kwa ajili yaa wengi hapana hiyo itakuwa ngumu,
VYOO NI VICHACHE AIRPORT KWA UPANDE WA WANAWAKE NI VIWILI NA GENTS NI VIWILI,SASA HAPA WACHUKUE USTAARABU WA KUFUNGA KIMOJA NA KUANDIKWE STAFF ONLY NA KIMOJA KIWE CHA PUBLIC,HATA HIVYO SEHEMU KAMA AIRPORT KWENYE WINGI WA WATU ,HAPAKUSTAILI KUWEKWA VYOO VYA KUKAAAA KWA KUEPUKA MLIPUKO WA MAGONJWA MBALI MBALI,HASWA UPANDE WA KINA MAMA MAANA BIN ADAMU TUMETOFAUTIANA .
KWA KWELI AIRPORT MPAKA IJE ISIMAME IWE NZURI NI BAADA YA KUFANYA MABADILIKO,VIONGOZII WAMEJISAHAU SANA WANAKAA WANASUBIRI POSHO OFF THEY GO,HAWAJALI MAENDELEO KATIKA UWANJA..NI AIBU KWA WAGENI KWA KWELI KUANZIA KWENYE MA BENCHI,NDANI HAKUNA SEHEMU ZA KUKAA ,WAMEWEKA VITI 3 KWA AJILI YA WATU WENYE MATATIZO,SASA NDEGE NI NGAPI KWA SIKU NA ZINAKUWA NA WAGONJWA WANGAPI,JE WAKAE KWENYE STYLE YA KUPAKATANA AMA??? ZINGATIENI HILI,UPANDE WA ARRIVAL KWENYE VISA VITI NI VICHACHE NA VIMECHOKA TAYARI NA WATU WANAKAAA SANA KUSUBIRI VIZA PALE NA AIR CONDITIONS HAZIFANYI KAZI,DEPARTURE VILE VILE,KILA KONA NI TATIZO,NJE NDIO MVUA IKINYESHA NDIO BALAAA KUNAVUJA HATA NYUMBA ZA MANZESE ZINA AFADHALI,UONGOZI,UONGOZI,UONGOZI JAMANI BADILIKENI ANGALAU.
WANASAHAMU KUWA WANA WAJIBU WA KUTEMBELEA WATEJA WAO NA KUWAULIZA NINI TATIZO AMA HATA RAHA WAPATAZO,HAWANA DAILY ROUTINE KATIKA HILI WAMEJISAHAU KABISAAAA.
KAZI NI KUANGALIA HAO WENYE HELA NA KUWAFANYIA MIPANGO AMBAYO SI SAHIHI,HATA NGOZI NYEUSI PIA INA HELA KWANI WAKISEMA KUWA KUNA NAFASI YA KUWEKEA VIBANDA NDANI TENA KUNA MTU ATAKATAAA,KWANI RESHMA AMEWEZA ANA NINI NA SISI TUSHINDWE TUNA NINI???TENA ALIFANYA SIRI SANA AKIDAI KUWA SIATAKI WAMBEA NYOKO ZAO WASIJUE,SASA TUNAMWAMBIA NYOKO NI YEYE MWENYEWE NA MBEA NI YEYE ASIYEKAA NA KUTULIZA MATAKO OFISINI KWAKE KUTWA KUPEPEA.
Asidharau watu na kutukana watu kabisa ,asitegemeee wamemsaidia kumpa kibanda na watamsaidia kwenye mingine pia ,NO WAY JEURI YAKE AACHE NA ANYAMAZE TU APITE WATU KAMA KISHADA NA KUCHAPULISHA MIGUU YAKE.
HATUTOCHOKA KUSEMA TUTASEMA NA TUNASHUKURU MUNGU SUALA HILI TUMELIPELEKA MBELE ZAIDI NA LIMEPOKELEWA SASA WASUBIRI MOTO KUWAKA TU. NA KAMA SI KESHO BASI IPO,KILA KITU KINA MWANZO NA MWISHO.
BYE.