wadau, hadi sasa nadhani kuna baadhi yetu hasa tulio hapa nyumbani bado kumaizi kwamba kwa wenzetu huko ughaibuni njia hii ya kupashana habari kwa njia ya blog ina thamani karibu sawa na vyombo vingine vya habari kiasi kwamba wana-blog hupata nafasi sawa na wanahabari wengine katika kila kitu.

hivi ninavyoongea kuna huyu mdau david lane weighs (pichani), mwanaharakati mashuhuri wa kimarekani, ambapo mwakilishi wake yumo kwenye msafara wa rais bush katika safari yake ya kuja afrika ambapo blog yao inaripoti kupitia:http://www.one.org/blog/category/bush-africa-trip/?id=238-626880-x5jTv2&t=4
mdau david anatumia blog ya taasisi yake kufanya kampeni ya kuhakikisha kwamba rais yeyote ajaye wa marekani aje afrika katika kipindi cha kwanza cha utawala wake na sio mwishoni. katika kampeni hiyo anahamasiha wadau wake waweke majina yao kwenye orodha maalumu ambayo baadaye itatumika kama kielelezo cha 'sauti ya watu' juu ya jambo hilo la rais wa marekani kutakiwa kuzuru bara hili mwanzoni na sio nchani mwa utawala wake.

aidha, mie mwenyewe sikuwa naelewa umuhimu wa blog hadi nilipokuwa helsinki mwaka 2005 na kukutana na mdau mkuu ndesanjo macha jijini helsinki ambapo yeye alikuwa amealikwa kuhudhuria kikao kilichokuwepo akiwa kama mwana blog, na sio mwandishi wa kawaida wa vyombo tulivyozoea kama nilivyokuwa mimi. hapo ndipo nami nikaanza ku-blog baada ya kuuona umuhimu wa teknolojia hii. (ndesanjo macha utampata pia kwa kubofya hapa)
natoa changamoto na ushauri kwa wadau wengi wengine na tujiunge tuikuze fani hii ya blog hapa kwetu bongo. kwa ambao wamekwishaanza nawapa hongera na kuwataka waendeleze libeneke bila kuchoka. pia tusiwe wachoyo kusaidia wale wanaotaka kuanza na hata kuwaunga mkono ambao ndio kwanza wameanza.

sina uhakika itachukua muda gani kwa wakulu wetu hapa bongo kumaizi umuhimu wa njia hii ya kisasa na ya haraka na rahisi kupashana habari kuwa ina umuhimu kama vyombo vingine vya habari na kuitambua rasmi. lakini inshallah iko siku tutafikia huko. lakini taratibu ndio mwendo na safari ndefu huanza kwa hatua moja...


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. BBC wanasema yao CNN wanasema yao sisi hatujui mambo ya militari base tunajua jamaa ni mtalii na msamaria mwema mwenye upendo wake. Wengine inawauma kwa yeye kuja kutembea huku. Tunaomba msije kujenga vituo vya silaha za kikemia. Maisha yetu yana thamani japo tunaishi kwa dala 1 kwa mwezi vyovyote vile nyie semeni tu Afrika tupo kivyetuvyetu mje msije poa tu. Ziara ya huyu jamaa itasaidia kuongeza pato la fedha za kigeni kwa njia ya utalii. Ahsante mzee. tuatkua zawadi ya simba ukamuweke kwenye zoo lako.

    ReplyDelete
  2. Uncle Michuzi naona kiswahili kidogo kimekupiga chenga leo, kwenye hii habari hapo mwanzoni kuna neno umekosea,(kama sio mimi ambaye nimeelewa vibaya) hima kaka, kama umekosea , rekebisha haraka kabla waoshavinywa hawajaliona.....
    wadau kuna baadhi yetu hasa tulio hapa nyumbani bado KUMAIZI....???!!!!

    ReplyDelete
  3. Na mimi hili neno pamoja na kua ni mswahili hii ni mara ya pili kulisikia, mara ya kwenza nililisikia kwenye cd moja ya taarabu ya wimbo wa mke mwenza unatumia neno hilo kama sikukosea kusikia sasa nikawa nasema hili neno lina maana gani? sentensi ilisema nanukuu" nimeshamaizi ndani wataka nitoa, nikikukufungia kazi nyumba hii hutakaa"na leo tena nakutana nalo humu hivyo ninahamu kubwa kujua tafsiri yake ili niongeze kamusi yangu kichwani.

    ReplyDelete
  4. OK Michu nami nimesaini hiyo pertition kwa kumwandikia moja kwa moja Obama maana ndiye atakuwa rais ajaye wa US.

    ReplyDelete
  5. Maana ya neno 'kumaizi' ni kugundua/fahamu/tambua au msisitizo ku realize. Mbona ni neno la kishwahili la kawaida tu? yaani nyie wadau ndio mnalisikia leo?

    ReplyDelete
  6. Anon 11:03 AM EAT. We utakuwa na ugonjwa, tena huwo wako ni ugonjwa m'baya sana, ugonjwa wakujiona unajuwa kila kitu, na usichojuwa wewe basi sicho. Hauna haja ya kuanza kumshambulia michuzi eti ooh "naona leo kiswahili kimekupiga chenga.." Kumbe wewe ndo hujui kiswahili, kwa taarifa yako Michuzi haja kosea, tena katumia neno mujarab katika sentesi yake, kama hujui neno "MAIZ" lina beba maana pana zaidi ya neno tambua, kutokana na sentesi yake michuzi. Kwa hiyo michuzi aliposema...baadhi yetu hasa tulio hapa nyumbani bado kumaiz.." amekwenda na lugha haswaa.Tafuta kamusi ya kiswahili ujifunze lugha yako. Itakuwa aibu kiswahili hujui na ke english cha watu pia hujui. we wajuwa kulugha cha kwenu tu (check out ulimwengu wa utandawazi huu).
    Usijione unajuwa kila kitu, usilolijuwa omba kuelimishwa.

    ReplyDelete
  7. Anon wa 11:03am ulie mwambia michuzi kapigwa chenga na kiswahili ,wewe ndio umepigwa chenga bora ungesema hufahamu kama anon wa 12:10pm,neno maizi lina maana nyingi kufahamu,kugundua,kujua,kung'amua,kutambua na mengine mengi nafikiri wadau wengine watachangia kuwafahamisha msio jua maana.

    ReplyDelete
  8. "KUMAIZI" sijawahi sikia hii...WAKULU ndo nini?

    ReplyDelete
  9. Anon wa 4:50:00 nawewe umechapia neno mujarab hapo si mahala pake, hilo hutumika kwenye fani ya tiba, mfano dawa inayofaa kutibu na kuponya ugonjwa fulani huitwa `dawa mujarab.' Si haba tuendelee kuelimishana na kukienzi kiswahili chetu.

    ReplyDelete
  10. NA NYIE MLIOKWISHAANZISHA BLOGU MSHIRIKIANE BASI BADALA YA KILA MMOJA WENU KU-PRIORITIZE ZAIDI UMAARUFU WA BLOGU YAKE/IDADI YA VISITORS BADALA YA KUHAKIKISHA MNAUTUMIKIA UMMA KWA BLOGGING.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...