Kaka habari za kasi na kazii teh teh heheh

Pole na Shuhuli,

Mimi leo Mdau kwa mara pili natinga tena Hebu soma hiyo ticket ya daladala hasa mistari miwili ya chini.

Wadau nawakilisha!!!!

Regards

David Ekonjo

ICT Engineer Executive

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Safi sana kwa ubunifu huu wakutuma ujumbe.ningewashauli wadau wengine wanaosoma blog hii kama mnamiliki au wazazi wenu wana miliki daladala au chombo chochote cha usafiri watumie ubunifu huu kuweka ujumbe ambao utaelimisha jamii sana sana tulenge ukimwi.najua ujumbe utawafikia na tutaweza kuokoa maisha ya watu.

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha....lol jamani mbavu na meno yangu.


    Bablii

    ReplyDelete
  3. hii ni tamu kuliko zote...bora kula mia tatu kwa halali kuliko millioni kibao kwa widhi. meseji imefika baba

    ReplyDelete
  4. yaonekana siku hizi kila mtu executive

    ReplyDelete
  5. Hahahaha! Tanzanians knows how to have fun, hata katika mambo ya kusikitisha lazima furaha iwepo.
    I love my country, Tanzania

    ReplyDelete
  6. Duh, daladala washachoka na maisha usawa huu!

    ReplyDelete
  7. Mdau huo mstari wa mwanzo hauna shida tunaelewa ni dhumuni la kazi yake, ila mstari wa mwisho nahisi muandaaji wa hii sentensi kuna vitu vinamsumbua kichwani na moyoni mwake akatamani kutusikizisha nasi,simshangai sana kwani kuna usemi unasema limjazalo mtu ndilo limtokalo.

    Hii sentensi inanikumbusha ule wimbo wa mchiriku uliopigwa marufuku unaosema "NIBEBESHE NIBEBESHE NIBEBESHE UKIMWI NIHANGAIKE NAO". kabla ya kupigwa marufuku sikuupenda yale maneno yake nikawaza huyu anaeimba wimbo huu analalamika au anashangilia?.

    Ah! kuna neno linasema uhuru wa mtu uheshimiwe ila hapa mimi hapana, kama walipiga marufuku ule wimbo ulikua unawasha masikio kwa kuhamasisha ukimwi, na hii sentensi inawasha machoni kwa kila anaeitazama, ningependa kama nazo zikatazwe naziharibiwe zote. zilizotengenezwa. Nakemea.

    ReplyDelete
  8. Ni upumbavu mtupu sasa bora HIV maana yake nini

    ReplyDelete
  9. that is fun but kuhusu hiv sio kitu cha kuwa fun of si unajua bidii tunazozifanya kuumaliza sio za kupuuza

    ReplyDelete
  10. ekonjo je ni wewe tulisoma wote pale mbeya day?

    ReplyDelete
  11. Kuna watu hapo juu hawana hata sense of humour. Eti wanakomaa kuwa kauli ya "Bora HIV kuliko Richmond" ipigwe vita.

    Guys hiyo ni kauli ya kisanii ambayo lengo lake ni kufurahisha watu na wakati huo huo kuelezea ubaya wa ufisadi kama wa Richmond.

    Haimanishi kuwa kweli aliyeandika anafagilia HIV.

    ReplyDelete
  12. Hey hiyo ni usanii mzuri sana...ujumbe umefika na wataelimishwa wengi ...kwa vile kama HIV imeua watu wengi na nitishio kwa jamii basi wasiojua richmond waelewe kuwa Richmond uizi wake ni sawa na mauti pia. Richmond inaua uchumi wa nchi...yote ni mauti..

    Mafisadi wanakula hela zinazotengwa kwa ajili ya magonjwa au maendeleo ya watu. Maji vijijini hayafiki kisa hela zimeliwa na mafisadi je watu wanaokufa na magonjwa yakutokana na maji yasio masafi si sawa na ukimwi tu...

    Ukikosa lishe bora utakufa, majimasafi utakufa, malaria utakufa, ukimwi unaua...sasa stay or find a way to eliminate both...

    mwee mimi naona wanaelimisha watu ....

    ReplyDelete
  13. Ujumbe umefika ila swali langu ni kwa ICT Engineer Executive wewe sio fisani...???? Kulikoni kwenye madaladala na title yote hiyo? Au ulikua unafanya research?

    Yaani ungekua huku mamtoni na title yako hiyo bwana wangu tungekusikia tu kama moshi kwenye chimney...

    ReplyDelete
  14. huyu anaelezea machungu yake kwa ufisadi unaoendelea hivyo kwake ni bora afe kuliko kuteseka na maisha ya kunyoywa ni kama kifo kile

    ReplyDelete
  15. ni vizuri tuwe na utaratibu wa kusoma risiti zetu tunazopewa kwenye daladala zingine zina mafundisho kwa jamii,bbc walishauliza wateja fulani wa tabata juu ya maandishi yalio kwenye risiti zetu

    ReplyDelete
  16. ANON WA 8:57AM UMENIFURAHISHA KWELI NA NYIMBO YAKO YA NIBEBESHE. HAO WENYE SENSE OF HUMOUR ACHANA NAO,I UNDERSTAND WHAT YOU ARE SAYING.

    ReplyDelete
  17. Wewe Anon wa 11.13 unamuuliza kama mlisoma wote Mbeya,wakati haujajitambulisha. Je ina maana hilo darasa zima mlikuwa mnasoma wanafunzi wawwili tu?. Be seious ndugu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...