
hizo ni juhudu za katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa koffi annan akisaidiwa na rais wetu mstaafu benjamin william mkapa na jk ambaye alienda kupiga nyundo ya mwisho kabla viongozi hao hawajakubali hata kukaa meza moja, acha kukubaliana na hata kupiga picha pamoja namna hiyo
mojawapo ya masharti ya muafaka huo ni kwamba nafasi ya waziri mkuu itaundwa na kushikwa na mdau wa chama kilicho na wabunge wengi bungeni na ndiye atakayekuwa mkuu wa shughuli za serikali kama bongo. hapo piga, ua ama garagaza huyo pinda wao atatoka odm na si ajabu akawa yeye raila odinga
Hao wamepigwa mkwara na Wamerekani...jana Cony kasema wasipofikia muafaka watachua hatua za kinidhamu juu yao, Jk kaenda kuongezea chachu wamefyata mkia, kudadadek Kinya......Kumbukeni wanasiasa wa Afrika ni wabinafsi hawaangalia watu wanavyotaabika, wanaangalia matumbo yao.
ReplyDeleteSasa Big Ben itakuwaje? maana hakutaka mambo haya yaende fasta maana huku home kimeo, si unajua isue ya mafisadi, wadau wanasema afikishe kwenye mkondo wa sheria au afirisiwe....mmenisoma?? basi naomba kuwakilisha
Condolese alisema ameshindwa na wanagombana vitu visivyo na maana...Alisema alikwenda sijui lin kuona nini ni suluhisho akaona wanachotaka ni kama watoto wadogo...I wan this I want that..
ReplyDeleteGood news kwakweli,lakini wale 1000 waliofariki kutokana na upuuzi wa hawa wapumbavu wawili??Mungu awalaze mahala pema peponi.Angurumapo simba(A.S.U, geuka nyuma usome kwenye kioo!) mcheza nani?
ReplyDeleteDuu afadhali mmemaliza na kufikia muafaka,afadhali mkapa arudi kwao lindi msimu wa kupanda mihogo umefikia,JAMANI LAKINI MKAPA MFUPII!! DUU
ReplyDeletewakubwa safi sana,manake ilikuwa big issue na wakati ilikuwa ndogo uroho tuu,kweli JK UNATISHA UMEENDA UKO WAMEFYA,sasa mkapa karibu nyumbani tujibu tuuma zetu au vipi,waelezee wadanganyika ili wakuelewe kuhusu kiwila au cyo,
ReplyDeleteTanzania siyo mchezo, si unaona hawapatani mpaka watanzania wawili na mghana mmoja walipotimia. Nchi langu zuri kudadek
ReplyDeleteJamani wadanganyika sasa Mzee mzima amemaliza Mapatanisho Kwa watani wetu wa jadi ana anarejea vyema kabisaaaaaaaaa lakini mnatakiwa kujua kwamba kipindi akiwa madarakani hatakama alituibia lakini asilimia kubwa walikuwa hawakosi riski kwani Ukiangalia Machingazzzzzzzz walikuwa wanajipatia rizki zao barabarani bila woga wowote. je leo hii Machingazzzzzzzzzzzzzz wako wapi?
ReplyDeleteWalala hoi pia tusioweza kwenda Woolweth na kwa akina Mariedo tulikuwa tunaponea pale posta kwenye Mitumbazzzzzzzzzzzz jioni kwa bei nafuu kabisaaaaaaaaa je sasa inawezekana tena????
Hata mimi nikiambiwa leo Jamaa arudi madarakani tukirudi Bongo tuweze kuendelea kujipatia matunda na mitumba kwenye matoroli bila kuyafwata Tandale na Tandika nampatia namba moja yangu.
Mdau kutoka BondeeeeeeeeeeM
MSEVENI ALIKIMBILIA KUUTAMBUA USHINDI WA KIBAKI, SASA YUKO WAPI?
ReplyDeletehaya kazi kwenu big ben, tunakusubiri tanzania, na sisi tueleze ukweli watanzania wako, wana tanzania.
ReplyDeleteMaraisi wawili, Mgombea urais wa zamani mmoja, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa mstaafu mmoja na Dr. LOVE PIMBI.
ReplyDeleteKama kweli wamepatana mbona wamemweka JK katikati yao? Au ndiyo hivyo tena ili picha iweze kupigwa? Manake hawakawii wakisimama jirani kupeana kichapo..
ReplyDeleteSafi sana, ila CCM wananishangaza (hapa nina maana JK na Ben), kwetu Moshi unafuka, Zanzibar. Mazungumzo hayaishi, kwa wenzetu mbio kuokoa, huo ni UJUHA, kwanini na kwetu wasiweke mambo sawa "Charity begins at home", kweli mpaka uchaguzi mpya 2010 ndio waunde kamati nyingine ya mazungumzo. Hawako serious!.
ReplyDeleteKILA MTU ANAMUA KUISHI AU KUFANYA JAMBO FULANI KWA MANUAA YAKE AU JAMII INAYO MZUNGUKA.UKIMSIKILIZA RAILA KATIKA HOTUBA YAKE AMESEMA KWAMBA SIO VIZURI WAKENYA WAUMIE KWA AJILI YA MASLAI YAKE BINAFSI , KWA KUJIWAKILISHA MWENYEWE ANAJUTA KWA MAAFA YALIYOTOKEA KWA SABABU YA WAFUASI WAKE KUMPENDA SANA PIA ANATOA NASAA KWA VIONGOZI WA VIZAZI VIJAVYO KUWA WAVUMILIVU WASIJIVUNIE UMAARUFU WAO KWA UMWAGAJIDAMU. KWA KWELI SIO JAMBO RAHISI KWA MTU MWENYE USHAHIDI WA KUDHULUMIWA NA SAUTI NA NGUVU YA KUJITETEA KUBWAGA MANYANGA. ANASTAILI PONGEZI. INAWEZEKANA KATIKA HISTORA YA DUNIA WAKO WATU WALIOTOA MATAMSHI KAMA HAYA LAKINI HUWA NI WAKATI WAMESHAKUWA WAZEE SANA. ILA KIUBINADAMU NI VIGUMU SANA HATA PINOCHET ALISHINDWA. INABIDI UTAFITI WA KINA UFANYIKE ILI NJIA MBADALA ZA KUTULIZA GHASIA ZIGUNDULIKE KWASABAU INAELEKEA MAKADIRIO YA MAAFA YANAYOTOKANA NA MAANDAMANO HASA KATIKA NCHI MASIKINI YANAAMBATANA UPORAJI MALI HAPA NDIPO KUNAKUWA NA AGENDA MBADALA. WANAPOINGIA WANA USALAMA NDIO TUNAPATA MAAFA. SASA INABIDI FORMULA ZA KUTULIZA GHASIA ZIFANYIWE UTAFITI
ReplyDeletePole wananchi wa Kenya sababu hakutakuwa na chama cha upizani cha kuikemea serikali iwe Bungeni au nje ya Bunge maana wote wanaunda serikali Kibaki na Odinga
ReplyDeleteRaisi Kibaki anachagua mawaziri na viongozi Raila Odinga anasimamia utendaji kama waziri mkuu!.Hivyo wakiingia bungeni lao moja!Ukitukana kibaki unatukana Odinga na ukimgusa Odinga unamgusa Kibaki! Na wao ni serikali moja isiyogawanyika wanapomkabili raia.
Wakiamua kuwa mafisadi wote hakuna wa kuwapigia kelele ndani ya bunge na serikali sababu kwenye serikali ni wao na kwenye bunge ni wao.
Kwa ufupi upinzani Kenya umekufa kifo cha mende! Na siasa moto za kenya zimewekwa maji baridi ya barafu.
Wewe mdau wa friday 29, 1:28 hujui nini unaandika alafu umeandika kiushabiki lazima uwe wa kule kule unajijua nimemaanisha nini wa kule kule.
ReplyDeleteMimi ndio maana hata kupiga kura sikwenda nilijua wote wajanja tu hao.Masingasinga hujuana kwa vilemba.
ReplyDeleteSasa hao wanagawana vyeo mlalahoi yuko hoi kambi za wakimbizi!
Natoa pongezi za dhati kwa MwanaDiplomasia Namba Moja wa Bara La Afrika Mheshimiwa Koffi Annan kwa kazi kubwa alioifanya kuwapatanisha Raila na Kibaki hadi suluhu ikapatikana akisaidiwa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Mama Graca Machel Mandela.Ilikuwa kazi ngumu iliyo hitaji uvumilivu na ustadi mkubwa.Lakini hatimaye muafaka umepatikana na Wenzetu wa Kenya watarejea katika amani na maisha yao ya kila siku.Kinacho endelea Kenya ni kwamba Raila atakuwa Mkuu wa Serikali na Kibaki akiwa Rais wa Nchi.Mabadiliko ya haraka katika Katiba yatafanyika Alhamisi ijayo ili makubaliano hayo yaweze kuwa na kinga ya kisheria.Lakini cha muhimu zaidi ni kwamba katika kipindi cha miezi kumi na mbili ijayo,Katiba itarekebishwa kabisa ili ipatikane mpya itakayo weka misingi mipya ya mfumo wa utawala ambapo vyeo vya Rais wa Nchi(Head of State) na Mkuu wa Serikali(Head of Government)vitabainishwa zaidi na madaraka ya kila kiongozi yatatenganishwa ili kupunguza madaraka makubwa kupita kiasi yaliyo kuwa yakimfanya Rais wa Nchi kuwa NUSU MUNGU.Lazima tuwapongeze wenzetu WaKenya kwa hilo.Hapa kwetu nimeona baadhi ya watu wakifananisha Uwaziri Mkuu wa Kenya/Raila na kusema ni sawa na ulivyo Uwaziri Mkuu wa Tanzania/Pinda.Hiyo siyo sahihi.Kuna jitihada za makusudi za kutaka kuwaziba macho Watanzania wasitambue ukweli wa mabadiliko ya kisiasa yanayo endelea nchini Kenya.Hata sisi Tanzania tutalazimika kushinikiza mabadiliko hayo katika Katiba yafanyike ili kutenganisha vyeo hivyo viwili vya Waziri Mkuu kama Kiongozi wa Serikali atakaye toka katika Chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi bungeni,na Rais wa Nchi ambaye hatahusika na uteuzi wa Baraza la Mawaziri wala katika shughuli za kila siku za serikali.Mabadiliko hayo Tanzania yanakuja penda usipende wapo wanao jaribu kupindisha pindisha mambo ili wasibanwe katika uwajibikaji.Rais Kikwete alikwenda kushuhudia makubaliano ya hatua za mwisho za viongozi wawili Raila na Kibaki.Lakini kazi yote ilikuwa imesha malizwa na Koffi Annan akisaidiwa na Mkapa na Mama Graca Machel Mandela.Watu wengine wasipende kujizolea sifa za bure kwa kazi iliyo hitimishwa na wengine.Hilo ni katika kuliweka sawa tu Watanzania wasije wakapotoshwa na watu wenye tabia ya kujikomba komba.Tumewastukia.Sisi sote tuungane na wenzetu wakenya katika kuwasaidia ili wafanikishe jitihada zao za mageuzi ya kisiasa katika hali ya amani,upendo na mshikamano wa kitaifa.Kufanikiwa kwao ndiyo kufanikiwa kwetu.Mungu Ibariki Afrika!
ReplyDeletelakini wakenya wanaonekana kuwa na matatizo, hata uchaguzi wameshindwa kufanya kwa amani, sasa watu kama hao, uongoziw ao utakuaje, walau tanzania.
ReplyDelete