KAKA MICHUZI,

HII NI BARABARA YA KUTOKA TARAKEA KWENDA MARANGUNA HAPA NI ENEO LA TARAKEA KIBAONI , AHADI ZA KUJENGWA KWA BARABARA HII NILIZISIKIA TOKA NIKO MDOGO MPAKA NIMEZEEKA.
KWASASA NI JAMBO LA KUFURAHISHA SANA KUONA BARABARA YA KWENDA ROMBO IKIFANYIWA KAZI KWA BIDII ZOTE NA UTAALAMU WA UHAKIKA KAKA MICHUZI HII BARABARA NAFIKIRI WAROMBO WOTE WANAIFURAHIA.
MDAU
CHARLES SALAKANA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ebana eeh Moshi kuna kibaoni kibao,hivi ina maana gani?Wenyeji wa MOshi naomba mnieleze.

    ReplyDelete
  2. duh ebwana nimefurahi san akusikia iyo road inajengwa aisee mimi natokea pale pale rombo yaani wala huulizi ila kwa sasa nipo mbali nimefarijika sana kusikia kama inajengwa kwa kweli ilikuwa imechoka mbaya yaani balaa mara ya mwisho nilipitia njia ya himo nikatoboza mwika njia ilikuwa inautelezi na haijatulia maana ile ya marangu ndio kiama

    BIG UP WAROMBO!! BIG UP WACHAGA!! BIG UP MBUNGE PESAMBILI MRAMBA chukua hela huko uje uimarishe kwako bwana achana na hao wanachukua wanapeleka kwa wenzao wewe leta ROMBO

    ReplyDelete
  3. Na barabara hii itamalizika kabla ya siku ya kiama!!!

    ReplyDelete
  4. asante sana salaka kwani dada yako nilo huku mbali na nyumbani ,kuona hapo nimefurahi sana,nisalimie dada angela

    ReplyDelete
  5. Huku tukilazimishwa kutaja majina yetu ya kweli itakuwa tunafahamiana zaidi ya asilimia 50.
    Salakana C, kama unawafahamu/una undugu na mapacha Gilbert na Alfred wasalimu na dada yao Angela.

    Mdau wa Mawenzi Sec, Form 1c7 - 2c6 (1991 - 1992), Session B.

    ReplyDelete
  6. wadau mimi nilisomaga huko tulitesekaga sana na hiyo barabara mpaka kuna siku mvua ilinyesha tukalala njiani tulikuwa tunaelekea shuleni afadhali wameikazia kamba. Ben86

    ReplyDelete
  7. Rombo, ah Rombo!! Kiraeni Girls(I remember you ....nanhii..mto Ngwasi sunday afternoon unakumbuka?), Mashati, (nanhii uliolewa kumbe na .....yule jamaa?)Namfua na baba lao of course ni Kili Boys!!

    Remember Kilimanjaro Boys!!Enzi zetu wakati wa mvua na tunafunga shule unaondoka saa 12 asubuhi na unafika downtown Moshi saa 6 na mabasi yote mazuri ya kwenda Dar tiketi zao zimeisha!! Unapanda Star unaingia Dar saa moja wakati wenzako wameingia saa 11 alfajiri(inawa basi moja machachari kutoka Iringa Kwacha "Navalonge Swela" limeingia zamaaaaanii!)

    Rombo Investments "Umeme", Rombo Safari "Manta Line" & "Msambweni" & "Bondei Warden", Rombo Mwelekeo "Ziggy Munta", Inter City, TTBS (eti Twende Tukafe Bila Sababu Lakini Tusiruke Dirishani), Yero Mbasai "Super Masai Coach", Kindokyakombe, Rundugai, "Umsolopogas" Safina (moja lao lilitumbukia mto Karanga mwaka fulani). Eniwei, bila kusahau gogo (treni) na wengine masafa ya KIA.

    ReplyDelete
  8. wadau wa mawenzi naona mmekumbukana hapa amini ni clasmoniotr 1c1 and 2c1 1991/1992.TUMAINI GEOFREY

    ReplyDelete
  9. Si mchezo, juzi weekend nimetoka Rombo, barabara inatanuliwa halafu jamaa wanaua kona kibao, si unajua barabara ilivyokuwa na kona nyingi??(wajenzi wa mwanzo nasikia walikuwa wakiona mti wanaukwepa, ndo maana kona zikawa nyingi). Ila nimeanza kusikia ujenzi muda mrefu, ila Mramba atlast akafanya mambo......Hongera sana mzee, wewe ni kidume, achana na hao wanaochukua hela wanazipeleka Dubai na RSA...hela zijenge home bwana...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...