MTAALAMU wa Kiswahili nchini, Hamis Akida amefariki dunia na kuzikwa Dar es Salaam jana. Mzee Akida alifia nyumbani kwake Mkwajuni katika Manispaa ya Kinondoni. Alikuwa na umri wa miaka 94.
Ofisa Uhusiano wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Mohamed Mwinyi aliliambia HabariLeo kuwa Akida alikuwa kiungo kikubwa cha lugha hiyo.
Alisema kutokana na mchango wake katika lugha hiyo, mwaka 1999 Baraza liliamua kumtunuku Nishani ya Utetezi wa Kiswahili.
Miongoni mwa michango yake ni pamoja na kutunga Kamusi ndogo ya Kiingereza kwa kushirikiana na Profesa Abdallah Safari, kusahihisha lugha, kutafsiri miswada mbalimbali na uandishi wa makala mbalimbali.
Kwa mujibu wa wasifu wa Akida uliopatikana Bakwata, alizaliwa Novemba 22, 1914 mkoani Tanga. Miongoni mwa nafasi alizowahi kushikilia ni pamoja na ile ya Mchunguzi au Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI).
Alianza masomo mwaka 1923 kwa kusoma Kiarabu na kisha alianza shule ya msingi mwaka 1925 hadi 1932 alipomaliza. Kati ya mwaka 1933 na 1934, alikuwa katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Tabora.
Alijiunga na Shirika la Posta na Mawasiliano ya Anga mkoani Tanga, mwaka 1935. Mwaka 1939 alihamishiwa Dar es Salaam ambako pamoja na mambo mengine aliyoyafanya, anakumbukwa kwa kuwa mchezaji mzuri wa mpira wa miguu na pia mwamuzi. Wasifu unaonyesha pia kuwa aliwahi kujiunga na Klabu ya Old Boys Sunderland (Simba) na baadaye alijiunga na klabu ya Yanga.
Alikuwa pia mpenzi wa muziki wa taarabu na aliwahi kuwa kiongozi wa The Egyptian Musical Club wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika.
Nathamini sana mchango wake! I salute him! Mungu amlaze mahali pema peponi Amen!
ReplyDeleteMdau,
Gotheburg, Sweden.
OOOOOOOH, MUNGU AILAZE MAHALI PEMA ROHO YA MZEE WETU
ReplyDeleteAMEN!
rip mzee akida nakumbuka vipindi vyako redioni ukisahihisha kiswahili.mungu akulaze pema.
ReplyDeleteRIP
ReplyDeleteInna lillah wainna ilaihi rajiuun
ReplyDeleteMzee lala salama na ulijitahidi katika masuala ya kiswahili pamoja na kwamba naweza KISWAHILI IS NON PROFIT LANGUAGE na nawalani wazee wangu ambao walibadilisha na shule za msingi tukawa tunafundishwa kwa lugha ya kiswahili. Hiyo imenikosti sana katika kutafuta kazi internationally japo sasa nimepata ila ni kwa mbinde. Ndio maana asilimia kubwa ya watu wenye pesa hawapeleke watoto wao kwa shule za serikali ambazo zinafundisha kwa kiswahili na wanawapeleka English medium. Inabidi niseme ukweli wale wanaowapeleka watoto wao katika shule za msingi za kiswahili sio kwamba wanapenda ila hawana uwezo. Nawashauri wazee mliobaki punguzeeni kiswahili na kazanieni English kwa faida ya vizazi vyetu.
ReplyDeleteDu mzee ameishi mpaka amepitisha muda wa kufa. Nadhani alikuwa anaanikwa. Vizee vingi vichawi huwa havifii haraka.
we anon hapo juu chunga mdomo wako, unaweza ukaongea ujinga lakini sio kiasi hicho, wewe inaelekea kwenu ni wachawi,ndio maana una mawazo ya kuwa eti mtu akiishi sana ni mchawi, mchawi mama yako na baba yako. RIP mzee wetu.
ReplyDeleteMpenzi wangu michuzi ukiwa safarini usiwaachie blog yako watoto wadogo, ambao hawayachambui maoni ya kipumbavu kama ya huyu anon hapo juu, inaelekea anon ni mtoto ambae BIBI BABU MAMA NA BABA zake walikufa kwa ukimwi, kazaliwa hakukuta wazazi, hana heshima wala taadhima, sio mstaarabu wa kuwapa faraja wafiwa,miaka 94 hata ulaya watu wanafikisha na wazungu wanakuwa wachawi?
ReplyDeleteDooo mwanaharamu hapo juu ni mtoto wa beach uliyetupwa mara baaba ya kuzaliwa namama yako, unakimbilia kuongea kingereza kabla yakukijua kiswahihili ambayo ni lugha yako mbumbumbu we!!!!!!!!!!!!!!. pumzika vizuri mzee wetu.
ReplyDeletePoleni sana watoto na wajukuu wa marehemu kaka Akida, kaka Husseni, dada Salama na wajukuu zake wa UK Lugha, Abuu na Kassim. Innalilah wailahi rajuun. Ndugu Amsterdam.
ReplyDeleteWewe ni mbuzi kama walivyo mbuzi wengine mkubwa jinga uchawi unaujua ukiuona badala ya kukazana kujifunza kiingereza chako mwenyewe kazi kujitetea umaskini ..mshenzi mkubwa ulojaa laana hivi unadhani we umezaliwa marekani mshamba mmoja ina lillah waina ilaihi rajun its me hatinafsi mjukuu
DeleteR.I.P mzee wetu.
ReplyDeleteBinadamu hatuna maamuzi juu siku zetu za kuishi hapa duniani, ni Mungu pekee huamua,Si vizuri kuongea maneno mabaya mtu anapotutoka.Muogopeni Mungu jamani, Huu ni Msiba,inawezekana wewe hakuhusu lakini ndugu wa merehemu,jamaa na marafiki,wanasoma hii blog, haitakuwa busara wao kukutana na maneno ya ajabu ajabu kuhusu ndugu au rafiki yao. please jamani.
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mzee wetu Mzee Hamis Akida.
ReplyDeleteMbali yakuwa ni mtaalam aliyetukuka katika lugha ya kiswahili, alikuwa pia ni mtu makini, mtulivu na mwenye subira wakati wote. Alikuwa ni Mzee aliyejaliwa hekima na busara za hali ya juu kabisa.
Ninatoa pole kwa familia ya Marehemu na kumwombea Mzee wetu ajaaliwe kila jema alilolifanya hapa duniani.
Mimi namshtumu huyo Anon aliyongea
ReplyDeleteutumbo hapo juu, lakini alianza kwa point..nzuri kuhusu kiswahili,kilivyoturudisha nyuma katika elimu ya kimataifa .......Wabongo wengi hata tulio University..bado english yetu mbovu , hata kama tunajua lakini ni waoga na hutuna mazoea ya kuzungumza,tulitakiwa tuzoeshwe kuzungumza ,kwani English .. ni moja ya lugha ngumu kuliko zote duniani,Leo hii nenda Sweden,Germany ,Netherlands na nchi nyingi zisizotumia lugha ya kingereza,... wabongo huko wanaongea lugha za huko, utafikiri walizaliwa nazo,,lakini njoo America na kwa wabeba ......nanihii..nini vile BOKSI..England ..kingereza bado kibovu kwa sisi WABONGO, najua mtaCRUSH.. lakini huu ndio ukweli...
Na kwataarifa yetu Tanzania ndio nchi ya MWISHO.. AFRICA..KUZUNGUMZA LUGHA YA TAIFA
LILILOTUTAWALA..(WAKOLONI)
Mungu amlaze pema ..Mzee wetu,
Wewe anon hapo juu una laana. Ina maana huna jamaa wa karibu au wa mbali aliyefikia umri huo? Nashindwa sijui nikuiteje? Sidhani hata kama unafanya kazi international. Hivi babu yako angefikisha umri huu ungesema mchawi? Chunga mdomo wako
ReplyDeleteRIP mzee Hamis Akiba
pole kina kassim ndio mipango ya mungu,innalilah waina ilahy rajiuni.mohd sweden
ReplyDeleteSikutegemea kama bado kuna washamba kama nyinyi duniani, Netherland wanaongea Kidachi na unawakuta wadachi wengi hawajuio kingereza Ujerumani wanaogea kijeru, muulize michu alikuwa huko juzi, Ufaransa wanaongea kifaransa, na nchi zote ulizo zitaja wana lugha zao, na utakuta kuna nchi nyingi hazizungumzi kabisa kingereza.pia kuna wabongo kibao wana zungumza English nzuri tu kama wewe una kichwa kizito ni wewe sasa hivi watu watunazungumza lugha tatu mpaka tano, kama wewe bado maimuna wewe.
ReplyDeleteLakini Jamani hivi kifo cha mtu na wewe kutokujua kingereza inatokana na nini haswa. Pumzika vyema Mzee wetu.
ReplyDeleteUlitowa mchango mkubwa sana katika kuikuza lugha yetu, RIP.
ReplyDeleteNilivyo mimi Michuzi ameandika ; mtaalam wa Kiswahili hatunae; sentesi haikusema aliyekataza Kiswahili hatunae,kweli nakubali una kichwa kizito hata Lugha wako inakusumbua sembuse hizo za kigeni Beach boy huna kichwa pole. RIP bwana Hamisi Akida.
ReplyDeleteNani kakwambia kingereza kigumu, niko Holland mwaka wa tisa sasa, nilipokuja nilikuwa najua kiswahili tu, lakini sasa nazungumza kingereza vizuri kushinda kidachi, kingereza sio lugha ngumu duniani ila wewe ni mzito wa lugha, poleni watoto wangu. Mama yenu Holland.
ReplyDeleteAbuu Uk mbona kimya, upooooooooooo. Poleni sana mwambie dada Salama pole.RIP mzee Akida.
ReplyDeleteAnon hapo juu! Please don't speak ill of my dad! Bwana Issa Michuzi tafadhali nipe contacts za mtu wa hii familia ya Mzee Akida. Mimi ni mtoto wake huku Kenya na nataka kuwaona watu wangu kule Dar! Nitashukuru sana ukinisaidia na hizi contacts. my email is ibnakida@yahoo.com
ReplyDelete