HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI KWAMBA KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA NDONDI NCHINI (TBF) GATSON MLAY (PICHANI KULIA AKIMPOKEA RAIS WA TBF ALHAJ SHAABAN MWINTANGA) HATUNAYE TENA DUNIANI.

KWA MUJIBU WA HABARI HIZO MAREHEMU MLAY ALIKUTWA NA MAUTI USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA TATU HAPA JIJINI DAR KUTOKANA NA KUSUMBULIWA NA BP PAMOJA NA KISUKARI.
MAREHEMU MLAY ALIWAHI KUWA BINGWA WA TAIFA WA NDONDI UZITO WA JUU AKIWA NA KLABU YA UHAMIAJIA NA ALIWAHI KULIWAKILISHA TAIFA KATIKA MICHUANO MBALIMBALI NDANI NA NJE YA NCHI.

MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWAKE MANZESE FRIENDS CORNER NA HABARI ZAIDI TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA KADRI ZINAVYOKUJA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Wadau wataniwia radhi kwa kusema ivi...huyu mshua nilipomuona first time weight yake iliniogopesha sana, alikuwa mwanamichezo kwanini alijiachia namna hiyo??? RIP GATSON, mbele yako nyuma yetu

    ReplyDelete
  2. marehemu alinisaidia kupata paspotrt yangu ya kwanza,alikuwa mtu wa watu sana miaka ya 80-90 pale uhamiaji,michuzi nazani ujasahau kwanba alikuwa akija pia ymca enzi zako ukitupiga picha miaka ya 86...na wakati tukicheza volleball ymca na akina LiliAN alikuwanshabiki wetu sana. ampumzike kwa hamani...mdau st albano...00316

    ReplyDelete
  3. Michuzi hii blog yako sasa imekuwa Sehemu ya kutangaza vifo tuuu. Embu punguza matangazo ya huzuni. Hii si sehemu ya kutangaza vifo. Tupe mamboya furaha.

    ReplyDelete
  4. I wanted to offer my condolences on the passing of Gatson Mlay to all who know him and all members of Tanzania Boxing Federation(TBF), esp its President Mr Mwitanga and his family. I know that his passing is a big loss for you and Tanzania. I know the upcoming months will be difficult for all of you, but know that our thoughts are with you during this difficult time. Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi.Amina!

    ReplyDelete
  5. WE MDAU WA 2:17 UNAHITAJI MATIBABU YA AKILI, KWANI NANI KAKWAMBIA MAISHA SIKU ZOTE NI FURAHA BILA HUZUNI!!!!!!!, HIVI UMESHAWAHI KUFIWA NA MTU WAKO WA KARIBU WEWE/, AU HATA JIRANI TU SIO LAZIMA MTU UMJUE ANYWAY.....PUMBA KABISA WEWE. RIP MLAY....
    MDAU SCOTLAND

    ReplyDelete
  6. wanted to offer my condolences on the passing of Gatson Mlay to all who know him and all members of Tanzania Boxing Federation(TBF), esp its President Mr Mwitanga and his family. I know that his passing is a big loss for you and Tanzania. I know the upcoming months will be difficult for all of you, but know that our thoughts are with you during this difficult time. Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi.Amina!

    ReplyDelete
  7. Napenda kuwapa pole wafiwa. Ila jamani tuangalie afya zetu. Unene ni ugonjwa...mola alitoa na mola ametwaa jina la bwana lihimidiwe. Amen

    ReplyDelete
  8. Poleni sana wafiwa pamoja na wadau wote wapenda Ndondi ni msiba wetu sote Tunamwombea Mungu amuweke mahali panapo stahili kutokana na matendo yake AMINA

    (From B)

    ReplyDelete
  9. Michuzi naungana na mdau hapo juu , kwamba hii Blong imekuwa ya matangazo ya VIFO.. Kweli tunakubali binadamu tumeumbwa kuwa na Shida na raha, lakini tukisema hii blong igeuke ya matangazo ya misiba basi nadhani itakwa, haitoshi itabidi tuazime blog nyingine .. za kina MJENGWA..maana Redio nying za FM zimelenga burudani na kuelimisha ..na wewe tunaomba uendeshe BLOG .hii ki FM ..RADIO!!!

    ReplyDelete
  10. We Anony wa Sunday, March 16, 2008 2:17:00 Medula Obulangata yako nadhani Plug hazichomi zote au Firering Order imekosewa unahitaji marekebisho sio siri!! Maisha ni mchanganyiko wa Tamu na Chungu we unataka Utamu tuu eeeeh Baba?
    Anyway kwa wafiwa poleni sana nilimjua huyu bwana nilipokuwa Business Times those days... Jamaa alikuwa poa sana.
    R.I.P Kaka

    ReplyDelete
  11. Mungu amlaze mahali pema peponi.

    Mama lao
    UK

    ReplyDelete
  12. NAOMBA MANENO YA POPE YAKUGUSE NA WE ANONY WA 3:52:00
    mshindwe na mlegee hata sehemu zenu za sirikali.

    wafiwa Poleni

    ReplyDelete
  13. Pole sana wifi yangu carolyine kwa kuondokewa na mumeo.Pole sana watoto AUDAX NA HONEYSET kwa kuondokewa na baba yenu mkiwa bado wadogo na mtayamisi malezi yake.Hao wadau namba 2 na 9 nahisi wanatindio wa ubongo.Huwezi ukabeza mwenzio akifiwa hata siku moja ka kweli umetimia.Inavyoonyesha hawajafunzwa nidham za midomo toka utoto wao na hayo ndo matunda yake kuropoka tu..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...