Amani, Heshima na Upendo kwako na wadau wote
Huyo mkongwe wa muziki wa Reggae ulimwenguni Gregory "The Cool Ruler" Isaacs yuko kwenye tour ya kuadhimisha miaka 35 tangu ajiingize kwenye muziki wa Reggae ambao umempatia heshima kubwa kote ulimwenguni.
Hapo ni usiku wa kuamkia Jumapili alipo-perfom ndani ya Zanzibar on the Waterfront Club jijini Washington DC.
Japo umri umemuacha, lakini aliweza kutumbuiza veeema saana na kukonga nyoyo za wengi.
Blessings
Ras Nas
Naam Michuzi huyo namkumbuka sana hata vibao vyake tulivyo vicheza nyakati hizo, cool down, night nurse,money in the pocket, the magic dragon etc. hata zikipigwa leo nitakumbuka neno kwa neno!!wasela wa Tambaza mnakumbuka 'Idles corner'
ReplyDeleteDaah!! Ningekuwa nimejua mapema ningefunga safari kumwona... Hebu kwanza nikatafute collection ya CD zake niwe nazo.. Mkali sana huyu jamaa. Halafu inabidi upandishe volume ampifaya ya Sansui mpaka at least half wei....Night Nurse, Objection Overruled, Stranger in town, Red Rose for Gregory..
ReplyDeleteMdau - Boston,US
duh jamani mi bado sijamuelewa aliyeleta hii habari amesema alipo peform ndani ya zanzibar on the waterfront club jijini washington DC..naombeni msaada au misupu umemuelewa na kiinglishi chako cha ugoko?
ReplyDeleteKwa mdau uliyeomba ufafanuzi,Gregory alitumbuiza Zanzibar Club.... iliyopo eneo linaloitwa Water Front(kuna mkondo wa maji ya mto Potomac/Anacostia) kule Washington,DC upande wa South West.
ReplyDeleteAha! Wanna know just little about the club Zanzibar; ni ya mpemba au muunguja? Au mzanzibara? Ama ni muwekezaji aliamua kutufwagilia kimtindo... alipendezwa nasi vile.
ReplyDeleteIngekuwa Zanzibar ya hapa Tanzania tungechupia usafiri wa baharini nakwenda kujionea wenyewe huko ni mbali na wengi wetu imebaki kuwa ni ndoto tu Hongera mliokuwa karibu nae .Hivi hizi ZANZIBAR zipo ngapi hapa ulimwenguni na ipi original naomba msada wa majibu
ReplyDeletenilipoona jina zanzibar nilidhani kule nyumbani kumbe ni jina la club marekani,naomba kumjibu anon 10:40 hapo juu kwamba zanzibar original ni kule kisiwani unguja nyengine yeyote ni feki wako katika utiifu.
ReplyDelete