Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kilwa wakati alipokuwa katika zara ya kikazi Mkoani Lindi iliyomalizika hiv karibuni.Mama Kikwete alikuwa mkoani Lindi kuzindua Kampeni ya upimaji saratani ya matiti na kuzungumza na wanafunzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. sarakani ya matiti kwa watoto wa kiumme???au lindi hamna wasichana??

    ReplyDelete
  2. WE MDAU ULIEKOMENT HAPO JUU(09:17) UWE UNASOMA KWA MAKINI, UMEAMBIWA YUKO LINDI KWA UZINDUZI WA SAKARANI YA MATITI KWA AKINA MAMA, PIA KUONGEA NA WANAFUNZI!!!!!!!!!!!LOH! KAAAZI KWELIKWELI AKIMAANISHA WANAFUNZI WA JINSIA ZOTE NA SIO WASICHANA PEKE YAO UPO, FUNGUA MIMACHO HIYO AU ANATUMIA KOMPYUTA YA MBAO WEWE.
    MDAU SCOTLAND

    ReplyDelete
  3. hivi salma, hamalizi safari za uko lindi mbona kila wakati yuko lindi, na hiyo wama ina watu wangapi??

    ReplyDelete
  4. Mama wa kwanza kwenu ng,apa kule lindi vijijini hakuna usafiri na sisi ndugu zako tukitaka kuleta magari ya zamani shemeji anazuia inakuwaje sasa??na ukija unaona sasa tusaidie kuongea nae ili tulete tu pick up twa kutusaidia basi.

    ReplyDelete
  5. Lindi ni kati ya mikoa masikini sana tanzania na kuna viogozi wengi maarufu wa tanzania wametokea huko,kuna wakina mama salma,mh membe,mh Hawa ghasia,magani,simba wa vita kawawa mzee mwenyewe yaani wako wengi ila mkoo huu uko nyuma sana mpaka utatisha maana maendeleo hakuna na watu wapo tu,kama wabunge wake ndio usiseme wako tu na wamejaha ufisadi wa ajabu mara wawe na band na wengine,hotel zisizo na kiwango basi shida tu ilimradi.Ipo siku tutafika lakini

    ReplyDelete
  6. Mkoa ambao hauna kiwanda hata kimoja,wala university au college ya maana ni shida tupu,umeme wenyewe shida ingawa gas ya songo songo iko mkoa huo ila kwenyewe hali ni choka mbaya sana

    ReplyDelete
  7. Halafu yupo katika ziara ya kikazi toka serikalini ama...?Michu,tatizo ndo hivo tena sijui hao nao wadhamini!Hii biashara ya udhamini mwisho italeta ufisadi!

    ReplyDelete
  8. Duh...suruali na pantaluni kama wachezaji wa kuigiza!!!

    ReplyDelete
  9. siyo ajabu kwani hujasikia kuwa kuna saratani ya matiti kwa wanaume pia

    ReplyDelete
  10. Kabla hujatuma comment hebu soma uilewe habari sio unakurupuka tu!!! hata watoto wa kiume wanaweza elimishwa juu ya saratani ya matiti kwani muhimu ujumbe ufike kwa walengwa, ni imani yangu kuwa hata watoto wa kiume wakiwa na uelewa wa hayo wanauwezo mkubwa wa kusambaza ujumbe kwa wazazi na ndugu zao na hata majirani!!!

    Mama Salma alikuwa huko katika ufumbuzi wa kampeni ya upimaji wa saratani ya matiti, lakini pia alienda zungumza na hao watoto wa kiume.

    Ingeandikwa English labda uengeelewa, ndio maana huwa tunafeli shuleni kwa kukurupuka kujibu tu!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. VIONGOZI WA NCHI WANAOSHIKA CHATI KATIKA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA:

    1. SALMA KIKWETE.- huonekana kila siku.
    2. M. PINDA.- huonekana kila baada ya siku moja.
    3. J. KIKWETE. - huonekana mara chache.

    ReplyDelete
  12. wewe anon wa 9:17PM ungekuwa uko shule na huu ni mtihani ungepata ziro, 0 au yai. Soma maelezo ya hiyo picha vizuri uone kwanini ungefeli.

    ReplyDelete
  13. Wewe uliyeweka post hapo juu huna akili kweli!!kwani wanaumme hawawezi kuwa na sarakani???au baadae wakiowa je?elimu ni elimu tuu inasaidia kwa wote..Mama wa kwanza pole na mizunguko mama..kwa kweli mama unajitahidi sna kwa kazi.HONGERA

    ReplyDelete
  14. Anon wa 9:17 PM Soma maelelzo vizuri ndipo uposti comments zako. Mama alikuwa Lindi Kuzindua kampeni ya upimaji wa saratani ya matiti na KUZUNGUMZA NA WANAFUNZI. Hii ina maana alikuwa na shughuli mbili uko Lindi na hapo yuko kwenye shughuli ya pili-KUZUNGUMZA NA WANAFUNZI.

    ReplyDelete
  15. Mhhh!! Matiti tena? au Michuzi Ulimaanisha Pu.....? Angalia!Unyanyasaji wa Kijinsia huo!

    ReplyDelete
  16. Mama wa kwanza pole kwa safari ndefu ya kikazi ila tunaomba kwa sasa ugeukia kwenye mikoa yetu kusini inatosha hivyo

    ReplyDelete
  17. Sasa wewe mtoa mada wa kwanza unashangaa nini kwani hakuna saratani kwa wanaume au umesahau kama huo ni moja kati ya mikoa ya pwani

    Nawakilisha mada

    ReplyDelete
  18. Kipindi cha Mzee wa milima ya usambaa(MKAPA) Moshi walineemeka kwa shinikizo la mkibosho-Kikarara(ANNA) sasa tuangalie mtoto wa mjini bagamoyo-pwani(Kikwete) kama wakusini wataneemeka nao kwa shinikizo la mrufiji(mama salma)

    Nawakilisha maada

    ReplyDelete
  19. ukweli ni kwamba safari za huyu salma lindi ni nyingi mno, hmna neno ila je na mikoa mingine jamani, pametosha uko lindi.

    ReplyDelete
  20. tangia ameanza lindi ameenda mara nyingi mno, tunaomba basi asonge na mikoa mingine kuchangia maendeleo ya watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...