nimeshatua dar na ile pyeee naripoti kijiwe cha empress ambapo mwenyekiti wake fundi mussa hakosekani. na leo nimekutana na watangazaji mahiri wa michezo wa redio one na ITV isaac muyenjwa gamba (shoto) na maulid baraka wa kitenge.
nimefurahi kumsikia kitenge akikanusha habari ambazo mdao mmoja kabandika humu kwamba anaoa mke wa tatu. hata mie nilistushwa na kutaka kuanza kumlaumu kwa kuninyima pilau. bahati nzuri kijiwe cha fundi mussa ambacho huwa hakina umbea wala kusema urongo kimenihakikishia kwamba si kweli kwamba kitenge anaoa mke wa tatu na kwamba yeye bado anaona raha ya maisha na wakeze eshe na rehema.
kitenge mwenyewe kaeleza masikitiko yake kwa uzushi huo kuwa anaoa mke wa tatu, akisema si kweli na wala ahajawahi hata kuota kufanya hivyo, na kawahakikishia wakeze kwamba mambo kama kawa - yeye na wao wawili tu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Issa Michuzi naona Umekwiva kwa ujerumani. Sasa Issa Michuzi Ukisikia umegongwa na gari usishangae mie ile mizigo nimekuomba Simu ya Camera,Jezi ya Bwawa la Maini na Kiatu cha Mpira mbona hujaniletea tena subiri sasa. Hahahaa! usijali mungu akunusuru, Namuona Fundi Musa bado anadai Toka Nipo La Kwanza Bunge Shule Ya Msingi mpaka Sasa Na Age 25. safi sana Fundi Musa Mwambie Fundi Musa Na MSalimia Sana.

    ReplyDelete
  2. mimi sioni tatizo kwa jamaa kuoa mke wa tatu kama anauwezo wa kuwatosheleza wote watatu basi poa tu mwachine aoe muhimi asizidishe zaidi ya wanne
    big up kitenge tuko pamoja kufuata nyayo zako

    ReplyDelete
  3. Hana hata haja ya kukanusha, kwani cha ajabu kipi?. Unajua Michuzi Mwalimu JK Nyerere alisema na namnukuu "Ukithubutu kula nyama ya mtu dhambi hiyo hutoachana nayo mpaka siku ya kufa". Hivyo basi as long Kitenge alithubutu kuoa mke wa pili ajue jinamizi hilo halitomtoka hadi siku ya kufa.Ataoa wa tatu mpaka wanne. Akae zake kimya tuu litakalokuwa na liwe na siyo kujiapiza. After all Wa Manyema wa Kigoma kama yeye kuoa wake wengi ni jadi yao tuu, hakuna cha ajabu.Kula kaka

    ReplyDelete
  4. Anashangaa watatu sas mbona wawili anao hakuna tofauti siuwamuzi tu

    ReplyDelete
  5. Sasa we maulid kwani kuoa wa tatu ni tatizo kinachokufanya ukane ni nini si afadhali uoe wa tatu kuliko kuwa na vibanda vya simu kila mahali acha kutuzuga mtu wangu

    katochi)

    ReplyDelete
  6. Na wewe Gamba acha kuuchuna hapo tueleze unao wangapi? achana na vile vibanda vya huko upitapo

    katochi)

    ReplyDelete
  7. Bro Michuzi karibu tena nyumbani. Pole na safari kaka.
    Sas najua wewe ni mtu muhimu sana naomba ongea na watu wa VODCOM wamsaidie huyo fundi Musa lile box lao la shoe shine na miamvuli. Tafadhali, inaelekea huyo mtu ni muhimu sana ati.

    ReplyDelete
  8. hivi kuna wanawake bado wanakubali kuolewa wawili, watatu ...
    karne hii??
    i dont praise westerners but i love their culture tutafika tu au siyo

    ReplyDelete
  9. WAACHIE WENYE MENO WATAFUNE..KITENGE..WEKA MABO YAKO WAZI KAMA KAWAIDA YAKO...ACHANA NA STAILI YA ISSA YA KUJIFICHA FICHA NA ..WAKEZAKE.., KWASABABU HUO NI UAMUZI WAKE YEYE MWENYEWE...

    ReplyDelete
  10. kwa waislamu, lakini culture ya wakristu hairuhusu, labda kwa wanaume wanaopenda wanawake na wasiotosheka na mmoja.

    ReplyDelete
  11. Hivi ni moja ya vitu vinavyonifanya niupende uislamu pamoja na kwamba mimi ni mkristo na sababu ya kuwa mkristo sio nyingine ni kwa kuwa baba na mama yangu walikuwa wakristo. Nadhani na wadau wengi mnafuata dini zenu kwa sababu wazazi au walezi wenu walikuwa/wanafuata dini yenu. Ndoa za kikristo zinaitwa pingu za maisha na kwa mke mmoja tu. Kwanini iwe hivyo. Uislamu unaruhusu kuoa wake wengi pia unaruhusu talaka. Mwanamke akikukera unampa talaka yeye, akikukera zaidi una mpa talaka pamoja na uko wake wote basi ndoa kwisha. Kuhusu Maulidi owa upendavyo na wakileta shida acha na owa wengine, Jamani raha. Mimi nina mke mmoja lakini natamani kuoa mke mwingine lakini padri ananikatalia na ananiambia kanisa litanitenga nadhani nitahamia kwenye uislamu. Au mnasemaje wadau. Jamani kulingana na sensa iliyofanyika Tanganyika inaonyesha kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume kwa hiyo tusipokuwa na wawili wawili wanawake wengine waolewe na nani. Natoa wito kwa wanawake wa kikristo kuipinga sheria ya ndoa moja kupinga wengine kukosa wanaume. Najua kuna watu watapinga ambao huwa wanapenda kuongelea vitu vya kufikirika na sio halisi na namalizia kwa kusema huo ndio ukweli na utabakia kuwa ukweli. Asalamu alekumu.

    ReplyDelete
  12. Mimi kusema kweli ni dini tu inanikwaza, lakini ningeruhusiwa ningeoa mke wa pili hata wa tatu pia, alimradi iwe kitu halali yaani sio dhambi na taratibu zote zimefuatwa. Kuna wakati huwa natamani nimpe mke wangu angalau ka-breather ka siku 2 hivi, lakini kwa kuwa sina pengine pa kwenda kupumulia inabidi tu tubanane hivyohivyo!

    ReplyDelete
  13. Katochi halahala mti na macho huo, usijevunja miji-ngwa

    Anon mar 18, 9:02 jibu utalipata yakikukuta, haina haja ya kuyachungua, hivi sasa jibu lake litakua halina hakika sana.Nakushauri sasahivi tulizana tu.

    ReplyDelete
  14. Which culture anonym 9:02? Ya kuwa kama kipepeo kutua kwenye kila ua kwa tofauti tu ya nyakati? Mbona hata Bongo hiyo ipo?

    ReplyDelete
  15. jamani nyie wanaume mnajipendelea sana,nasisi wanawake tunatamani tubadilishe vilele ,sasa mtakubali KUSAIDIWA????maana asikudanganye mtu unajidai kuoa mke wapili ili ujiliwaze zaidi je NA MIMI NANI ANILIWAZA?NDIO MWANZO WA UKIMWAI ,MAANA HATA MIMI NITATAFUTA CHA PEMBENI,SIKUHIZI HATA WANAWAKE TUNATAFUTA HAMNA HAJA YA KUSOSONONEKA ETI MWANAUME ANA KIMADA OR MKE WAPILI,HIYO NAWATAADHARISHA TU NYIE WANAUME.WE OA TU MI NAGAWA VILELE,TENA VYA KUIBA VITAMU SANA NA HATA USIPONIGUSA WEEK MI SAWA TU,THATS IS FACT!!!!!

    MDAU

    ReplyDelete
  16. Michuzi kishavu hiki si cha bure inaonekana umekula sana ile nyama ya kikatoliki,haya bwana nani alikuona najua utakataa tu!oa na wewe mke mwingine maana watu wa pwani sie tukiwa na kipato kidogo tu basi tunaongeza mke kama huyo kijana mdogo anavyofurahia maisha ya nyumba mbili!

    ReplyDelete
  17. Fundi Musa huyo michu anapenda sana kukutoa kwenye blogo yake, nimekumaindi kishenzi nipe basi namba yako. wewe mndenge nini. nakufagilia wawaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  18. Tafadali salimu polepole aloo... usitutusi nduguzo, watu wa pwani ni samaki peke yao sisi ni watu wa mwambao, au watu wa kando ya bahari. jihadhari kidogo.

    Koplo sajent na wengine ni uamuzi wa mtu kwa raha zake, mnajitia namuogopa padre huku small house kwa kwenda mbele si useme tuu, usomuogopa mungu anaekuona ukamuogope padre.

    ReplyDelete
  19. Michu,naomba number ya simu ya Maulid wa Kitenge namie niombe kuolewa mke wa nne sinto jali
    Mdau

    ReplyDelete
  20. Ndugu yangu Michuzi siku chache ulizokuwa majuu umeng'ara hivyo, majirani hawakuonei donge?

    Msalimie sana fundi Musa, mwambie uzi huo huo. Nikija likizo bongo itanibidi nifike maskani kumsalimu ni miaka mingi imepita.

    Mdau
    UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...