nimefurahi kumsikia kitenge akikanusha habari ambazo mdao mmoja kabandika humu kwamba anaoa mke wa tatu. hata mie nilistushwa na kutaka kuanza kumlaumu kwa kuninyima pilau. bahati nzuri kijiwe cha fundi mussa ambacho huwa hakina umbea wala kusema urongo kimenihakikishia kwamba si kweli kwamba kitenge anaoa mke wa tatu na kwamba yeye bado anaona raha ya maisha na wakeze eshe na rehema.
kitenge mwenyewe kaeleza masikitiko yake kwa uzushi huo kuwa anaoa mke wa tatu, akisema si kweli na wala ahajawahi hata kuota kufanya hivyo, na kawahakikishia wakeze kwamba mambo kama kawa - yeye na wao wawili tu...
Issa Michuzi naona Umekwiva kwa ujerumani. Sasa Issa Michuzi Ukisikia umegongwa na gari usishangae mie ile mizigo nimekuomba Simu ya Camera,Jezi ya Bwawa la Maini na Kiatu cha Mpira mbona hujaniletea tena subiri sasa. Hahahaa! usijali mungu akunusuru, Namuona Fundi Musa bado anadai Toka Nipo La Kwanza Bunge Shule Ya Msingi mpaka Sasa Na Age 25. safi sana Fundi Musa Mwambie Fundi Musa Na MSalimia Sana.
ReplyDeletemimi sioni tatizo kwa jamaa kuoa mke wa tatu kama anauwezo wa kuwatosheleza wote watatu basi poa tu mwachine aoe muhimi asizidishe zaidi ya wanne
ReplyDeletebig up kitenge tuko pamoja kufuata nyayo zako
Hana hata haja ya kukanusha, kwani cha ajabu kipi?. Unajua Michuzi Mwalimu JK Nyerere alisema na namnukuu "Ukithubutu kula nyama ya mtu dhambi hiyo hutoachana nayo mpaka siku ya kufa". Hivyo basi as long Kitenge alithubutu kuoa mke wa pili ajue jinamizi hilo halitomtoka hadi siku ya kufa.Ataoa wa tatu mpaka wanne. Akae zake kimya tuu litakalokuwa na liwe na siyo kujiapiza. After all Wa Manyema wa Kigoma kama yeye kuoa wake wengi ni jadi yao tuu, hakuna cha ajabu.Kula kaka
ReplyDeleteAnashangaa watatu sas mbona wawili anao hakuna tofauti siuwamuzi tu
ReplyDeleteSasa we maulid kwani kuoa wa tatu ni tatizo kinachokufanya ukane ni nini si afadhali uoe wa tatu kuliko kuwa na vibanda vya simu kila mahali acha kutuzuga mtu wangu
ReplyDeletekatochi)
Na wewe Gamba acha kuuchuna hapo tueleze unao wangapi? achana na vile vibanda vya huko upitapo
ReplyDeletekatochi)
Bro Michuzi karibu tena nyumbani. Pole na safari kaka.
ReplyDeleteSas najua wewe ni mtu muhimu sana naomba ongea na watu wa VODCOM wamsaidie huyo fundi Musa lile box lao la shoe shine na miamvuli. Tafadhali, inaelekea huyo mtu ni muhimu sana ati.
hivi kuna wanawake bado wanakubali kuolewa wawili, watatu ...
ReplyDeletekarne hii??
i dont praise westerners but i love their culture tutafika tu au siyo
WAACHIE WENYE MENO WATAFUNE..KITENGE..WEKA MABO YAKO WAZI KAMA KAWAIDA YAKO...ACHANA NA STAILI YA ISSA YA KUJIFICHA FICHA NA ..WAKEZAKE.., KWASABABU HUO NI UAMUZI WAKE YEYE MWENYEWE...
ReplyDeletekwa waislamu, lakini culture ya wakristu hairuhusu, labda kwa wanaume wanaopenda wanawake na wasiotosheka na mmoja.
ReplyDeleteHivi ni moja ya vitu vinavyonifanya niupende uislamu pamoja na kwamba mimi ni mkristo na sababu ya kuwa mkristo sio nyingine ni kwa kuwa baba na mama yangu walikuwa wakristo. Nadhani na wadau wengi mnafuata dini zenu kwa sababu wazazi au walezi wenu walikuwa/wanafuata dini yenu. Ndoa za kikristo zinaitwa pingu za maisha na kwa mke mmoja tu. Kwanini iwe hivyo. Uislamu unaruhusu kuoa wake wengi pia unaruhusu talaka. Mwanamke akikukera unampa talaka yeye, akikukera zaidi una mpa talaka pamoja na uko wake wote basi ndoa kwisha. Kuhusu Maulidi owa upendavyo na wakileta shida acha na owa wengine, Jamani raha. Mimi nina mke mmoja lakini natamani kuoa mke mwingine lakini padri ananikatalia na ananiambia kanisa litanitenga nadhani nitahamia kwenye uislamu. Au mnasemaje wadau. Jamani kulingana na sensa iliyofanyika Tanganyika inaonyesha kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume kwa hiyo tusipokuwa na wawili wawili wanawake wengine waolewe na nani. Natoa wito kwa wanawake wa kikristo kuipinga sheria ya ndoa moja kupinga wengine kukosa wanaume. Najua kuna watu watapinga ambao huwa wanapenda kuongelea vitu vya kufikirika na sio halisi na namalizia kwa kusema huo ndio ukweli na utabakia kuwa ukweli. Asalamu alekumu.
ReplyDeleteMimi kusema kweli ni dini tu inanikwaza, lakini ningeruhusiwa ningeoa mke wa pili hata wa tatu pia, alimradi iwe kitu halali yaani sio dhambi na taratibu zote zimefuatwa. Kuna wakati huwa natamani nimpe mke wangu angalau ka-breather ka siku 2 hivi, lakini kwa kuwa sina pengine pa kwenda kupumulia inabidi tu tubanane hivyohivyo!
ReplyDeleteKatochi halahala mti na macho huo, usijevunja miji-ngwa
ReplyDeleteAnon mar 18, 9:02 jibu utalipata yakikukuta, haina haja ya kuyachungua, hivi sasa jibu lake litakua halina hakika sana.Nakushauri sasahivi tulizana tu.
Which culture anonym 9:02? Ya kuwa kama kipepeo kutua kwenye kila ua kwa tofauti tu ya nyakati? Mbona hata Bongo hiyo ipo?
ReplyDeletejamani nyie wanaume mnajipendelea sana,nasisi wanawake tunatamani tubadilishe vilele ,sasa mtakubali KUSAIDIWA????maana asikudanganye mtu unajidai kuoa mke wapili ili ujiliwaze zaidi je NA MIMI NANI ANILIWAZA?NDIO MWANZO WA UKIMWAI ,MAANA HATA MIMI NITATAFUTA CHA PEMBENI,SIKUHIZI HATA WANAWAKE TUNATAFUTA HAMNA HAJA YA KUSOSONONEKA ETI MWANAUME ANA KIMADA OR MKE WAPILI,HIYO NAWATAADHARISHA TU NYIE WANAUME.WE OA TU MI NAGAWA VILELE,TENA VYA KUIBA VITAMU SANA NA HATA USIPONIGUSA WEEK MI SAWA TU,THATS IS FACT!!!!!
ReplyDeleteMDAU
Michuzi kishavu hiki si cha bure inaonekana umekula sana ile nyama ya kikatoliki,haya bwana nani alikuona najua utakataa tu!oa na wewe mke mwingine maana watu wa pwani sie tukiwa na kipato kidogo tu basi tunaongeza mke kama huyo kijana mdogo anavyofurahia maisha ya nyumba mbili!
ReplyDeleteFundi Musa huyo michu anapenda sana kukutoa kwenye blogo yake, nimekumaindi kishenzi nipe basi namba yako. wewe mndenge nini. nakufagilia wawaaaaaaaaaaaaaa
ReplyDeleteTafadali salimu polepole aloo... usitutusi nduguzo, watu wa pwani ni samaki peke yao sisi ni watu wa mwambao, au watu wa kando ya bahari. jihadhari kidogo.
ReplyDeleteKoplo sajent na wengine ni uamuzi wa mtu kwa raha zake, mnajitia namuogopa padre huku small house kwa kwenda mbele si useme tuu, usomuogopa mungu anaekuona ukamuogope padre.
Michu,naomba number ya simu ya Maulid wa Kitenge namie niombe kuolewa mke wa nne sinto jali
ReplyDeleteMdau
Ndugu yangu Michuzi siku chache ulizokuwa majuu umeng'ara hivyo, majirani hawakuonei donge?
ReplyDeleteMsalimie sana fundi Musa, mwambie uzi huo huo. Nikija likizo bongo itanibidi nifike maskani kumsalimu ni miaka mingi imepita.
Mdau
UK