bondia wa zamani wa kimataifa isaac mabushi (shoto) akiwa na katibu mkuu wa boxing federation of tanzania (bft) godrefy msengi walipogongana leo katikati ya jiji. jina la mabushi si geni kwa wapenzi wa ndondi wa zamani wakaati wa enzi za kina habibu kinyogoli, gerald isaac, emmanuel mlundwa, abdallah mgeni, titus simba, flavian bitegeko, ahmed tesha na wengineo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. DUU KWELI BONDIA AMESHACHUKUA USHINDI HUYU KWELI? BASI NAONA ATA SHEMEJI TRINDAD AND TOBBEGO ANGEKUWA MWANA MASUMBI USHAURI WA BURE KWA NKEYEKU

    Mawifu

    ReplyDelete
  2. Duu hawa jamaa wako choka mbaya!!viatu vinavumbi na sidhani kama walikuwa wamepata lunch kweli!!maana wanaonekana wana njaa sana

    ReplyDelete
  3. Na bila kumsahau mwanaMbeya mwenzangu yaani Lucas Msomba!

    ReplyDelete
  4. mngepangusa viatu hivyo basi kabla hamjapiga picha mbona mnatisha na hilo vumbi kwenye viatu,kweli bongo mnakula vumbi.

    ReplyDelete
  5. Ustaadh Michuzi umenikumbusha mbali sana, huyo Issac Mabushi ni mtu muhimu sana! Walipeperusha bendera ya Tanzania nje ya mipaka kwa moyo mmoja bila kujali pesa wala umaarufu. Nilibahatika kuonana naye mwaka 1978 Musoma-Biafra wakati tunaishi na mzee wake Elias Mabushi na wadogoze Sweet, David, Azimio na Fany.
    Ustaadh watafute mabingwa wengine kama Lucas Msomba, Habib Kinyogoli nk kwani wanastahili pongezi nyingi. Natoa maoni kwamba, vyombo vyetu vya habari nchini viwe na taratibu za matamasha ya kuwaenzi mashujaa hawa, kwani ni mapema mno kusahaulika kutokana na mchango wao madhubuti kwa taifa letu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...