
Haya wadau,
nimejaribu kutafakari niliyoyasikia kwenye vyombo vya habari hapa kwetu lakini bado nadhani moyo wangu haujapata jibu kamili…naomba na nyinyi wadau wangu mniambie vipi kuhusu hawa wasanii matajiri hapa kwetu Tanzania?
WASANII HAO NI HAWA HAPA NA THAMANI ZA RASILIMALI ZAO
WASANII HAO NI HAWA HAPA NA THAMANI ZA RASILIMALI ZAO
1; LADY JAY DEE - MILLION 500
2; JUMA NATURE – MILLION 300
3; BANANA ZORRO – MILLION 280
4; MATONYA - MILLION 180
5; FEROOZ - MILLION 140
6; PROFESA JAY - MILLION 130
7; STARA THOMAS -MILLION 80
8; AY -MILLON 60
9; KLYNN -MILLION 45
10; MWANA FA - MILLION 30
HAYA KAZI KWENU
Mdau Ngwega (pichani,mbele)
kulalalalalalalalalalalalambegeze michuzi unapenda ligi kweeeeeli kweeeli, unataka tuache box sasa tuje kuimba bongo flava si ndio???
ReplyDeleteJamani,ufisadi hata kwenye habari?
ReplyDeletelady jd ana worth 500 tsh millions??? kesho naenda kumtukana supervisor tena na beef nae ananibebesha box ka mtumwa, halafu naacha box najiunga na bongo flava
ReplyDeletemichuzi nihakikishie usilostishe maisha yangu babu nisije kikauvaa mkenge
Hiyo habari nahisi sio sahihi. Kama ni sahihi, je wametumia vigezo gani? Na kama wanazo kumbukumbu zao za mapato na matumizi, je wanalipa kodi? Pia kama kuna ukweli katika hilo basi nahisi watakuwa wanafanya na biashara nyingine zaidi ya usanii.
ReplyDeleteHakuna milionea hapo, wote tunawaona mbona wamechoka? lady jaydee angalau, naye si milionea bali anajiweza kimaisha
ReplyDeletesasa hiyo mil 500 ya jide kutokana na ile hiace ya kuchorwa au vipi lakini hiace si $4000 tuu dubai kama angekuwa na hizo si Gadne angekuwa na redio yake
ReplyDeleteHiyo Nature labda ni vipisi vya bangi vilivyoingia mwilini mwake
ReplyDeleteSamahani wadau!! hizo milioni zilizotajwa hapo juu zipo benki kwenye akaunti zao au ndiyo thamani za hiace, magitaa, computer zao, gari zao za kutemb elea, majeans yao pamoja na nyumba zao au kuna project kubwa ambao hawa wasanii wamawekeza? Niambieni vigezo vilivyotumika kupata hizo milioni walizo nazo.
ReplyDeleteDUH!
ReplyDeleteHuyo Klyn labda kama wamethaminisha private assets zake alizopewa na mungu atafikia 45Million. Mbona hana kitu jamani? Hana gari wala nyumba na anakaa kwa baba na mama mpaka leo. Hizo 45 Mil zimetokana na nini?
ReplyDeleteMauzo ya album yake ni kama milioni 16 hivi na distributor alichukua mmilioni 9 na studio iliyotengeneza ilikula milioni 4.
Embu tuambiane kama hili ni changa za macho?
Hizo millioni ziko kwenye account zao au? maana bado sijaelewa, kwasababu kuna wasanii wengine hapo bado wanaishi nyumba za kota na ukiwaangalia wengine hayo mabenzi wanayoendesha ni ya mwaka 47. Naomba Ufafanuzi TASAVALI.
ReplyDeletewamepata hizi hela kwa kuuza cd au wameiba wapi, kama masoko ya cd yangekuwa kam huku ughaibuni basi ningalikubali lakini mimi naangali kwa makini siyakatai lakini pia sikubaliani nayo
ReplyDeleteall the best
wewe unaishi zimbabwe? unachanganya
ReplyDeletemillion 500 za kusifiwa na sio za kweli msitishike jamani wala kuacha box,na ukiuliza ana invest vp pesa yake hakuna ni kuimba tu,poa sana naona ray c wamemuacha kisa anakatika sana na ananata sana eti ana 5m tu,sio kweli mgongo wake tu una bima ya 10m na mwili wake ni kama 100m sasa hatakosa vp si ndio shakira wa bongo na ana boutique,saloon,table dance club,na kama una 1m unapata one night stand,tz shwari jamani
ReplyDeleteWametumia vigezo gani kupata hizo thamani za hela?Watu kama Forbes magazine wana criteria zao zisizo na kwere... Huchelewi kukuta wamepiga evaluation ya hata magari. Anyway, looks muziki unaanza kulipa Bongo...
ReplyDeleteHa,ha,ha Basi kachemsha maana box haachi mtu. Ila nimashaka na Ferooz maana nilisikia kuna siku za karibu alikosa hata Nauli ya kurudi bongo akitokea Uganda baada ya kutiwa mchanga wa macho na Promoter wa Onyesho aliloenda kutumbuiza huko. WASANII WENGI- NO COMMENT
ReplyDeletemmmmmmmmmmm ni kweli sikubali basi kesho naanza kuimba,Inabidi niache kazi ya kulea wazee.
ReplyDeleteRose Norway
Ni kigezo gani mmetumia kujua wana kiasi gani kwenye bank?
ReplyDeleteFirst of all nawapongeza hawa wanamuziki kwa kazi yao.Lakini these figures are so unreal,I mean how do they value their wealth,based on what:Album sales,Copy rights,Tour/Concert sales,Ringtones,Shares ama kitu gani?
ReplyDeleteHiyo sio kweli next hiyo hela ni ndogo sana.Mi namjua mtoto mwenye tsh 3bis anauza mawe na yuko 24yrs old
ReplyDeletehizo data umepata wapi? michu sometime post kama hizi unazipotezea, hao washkaji wengi wao life zao tunazijua, kutuambia mtu kama ferooz anautajiri wa 140m wakati anakaa kwa washua wake ni vichekesho istoshe jeep yenyewe kaiuza, data mnatoa wapi? na haya mambo ya kuitana matajiri wakati hata hamlipi kodi ni kuzinguana...2pac alisema i wanna pay rent when rent is due, lkn hao washkaji kazi kuombana biere tu club..siyo issue..haimake sense ferooz sijui kuhusu matonya awe juu zaidi wakati watu kama dady, ay na fa wapo juu sasa esp ay ambaye ana clothing line ambayo nasikia inafanya vema sokoni, vp kuhusu ray c, tid wenye mashow kibao mbele wapitwe na stara ambaye kitambo hatujasikia tungo zake??? ni mtizamo wazee lkn tuache kuzinguana, mkatutia mdadi wa kurudi huko na kuacha bata huku kwa joji kichaka teteteteeee
ReplyDeleteDoh!!,yaani T.I.D mbwembwe zote alizo nazo hata ktk top 10 ya wasanii matajiri hayumo!!!yaani stara yupo juu ya T.I.D,kweli noma.
ReplyDelete500m?????? MICHUZI HAUKO SERIUOS
ReplyDeleteMAISHA YAO MBONA TUNAYAONA HAWANA HATA VITEGA UCHUMI MFANO KUNUNUA SHARES(HISA) KUFUNGUA MIRADI MBALI MBALI KICHA WAKO BAAA HWANA HATA WANASHERIA,DOC,WASHAURI,HIYO 500M SI MCHEZO KWA BONGO
Issa Michuzi mie yangu macho. kama kweli vizuri kwao ila lady jaydee kidogo naweza kukubali yuko makini na market zake, Tanzania mauzo wanaibiwa na wahindi kama wanahesabu nyumba zao nam agari yao sawa. lakini unambie kwenye bank wanazo hizo ni uongo mtupu. T.I.D vipi hayupo na Ray-C mie naona wengine wanatumiwa kupitisha UNGA tu Airport zetu wanakatiwa mshiko na baazi ya ma MP jamani tuweni makini kabla kusifu uongo. anayeingiza pesa Producer na muuzaji CD's Tanzania.
ReplyDeletewabongo kwa chuki binafsi na wivu tunaweza kubeba kombe duniani kwani cha ajabu ni kipi mtu kuwa na 500m wenye wivu wajinyoke na kila mtu na bahati yake ala?
ReplyDeletewe kama huna umiza kichwa ufanye nini sio majungu na kama hutaki basi kaa hivyohivyo na mdomo wako
HIYO LIST MBONA R C HAYUMO???
ReplyDeleteJAMANI SIJAELEWA SASA KAMA UNATHAMANI YA HELA HIYO MBONA WANAISHI KWENYE UNFINISHED HOUSES MATOFALI YANACHUNGULIA NJE.MIMI NI WAZAZI WANGU WANAFIXED ASSETS ZA THAMINI KUBWA SANA NIKIPIGA HESABU NDIO LABDA KUKARIBIA HUKO HUKO NA SASA NASHINDWA KUELEWA HUYO JAYDEE ILE NYUMBA NA AU MLINZI AU GARI NDIO THAMANI YAKE AU
ReplyDeleteAh! Lakini tusishangae sana maana bongo ukivaa dhahabu ni tajiri, ukinunua gari ni tajiri, ukijenga nyumba ya kawaida ya kuishi ni tajiri hata nguo unazovaa ni pia ni utajiri. Hii ni ajabu sana. Inawezekana ndivyo walivyoviangalia. Halafu wanamziki wetu wanapenda sana kujilinganisha na na wanamuziki wa marekani. Hapa bongo musiki bado kabisa hayo tunayoimba ingekuwa kanisani ningesema mapambio. Hata zaire hatuwafikii, south ndo kabisa. Anyway kama tumeamua kupakana mafuta kwa migongo ya chupa ndo hapo sasa. Wacheni wavimbe mibichwa lakini mi naangalia hivi akina temba nao hawana kitu? Craz GK naye je?
ReplyDeletedata hizo si kweli kwani hata kwa data za prime time promotions ambao ndio humega sehemu kubwa ya mgao huu , bushoke aliuza kuliko jd.na hakuna mtu atakupa data za kweli kwa ajili ya ufisadi wa all the players, primetime wasambazaji ka GMC wote ni wa kwepa kodi wakubwa.Kama wanabisha wajitokeze watuambia true statistics
ReplyDeleteTHAMANI YA RASILIMALI ZAO = ardhi, nyumba, magari, fedha nk. Kwa Tz nadhani hata nguo na vipodozi wamehesabu.
ReplyDeleteWaaungwana huyu michuzi anawachongea hawa watu jamani si balaa hiii?
ReplyDeleteHongera zao hao wasanii mamilionea.
ReplyDeleteHaya na nyie ndugu zangu wabeba mabox wala msitishike sana na kutaka kukimbilia bongo. Kumbukeni hizo pesa za wasanii hapo juu ni madafu, sio US dollars au Pound Sterling. Kwa mfano hiyo million 30 ya Mwana Fa ni sawa na pound elfu kumi na mbili (12,000) za UK. Haswa nyie mlioko Uingereza endelezeni sana libeneke maana ukija na mshahara wako wa mwezi mmoja hapa bongo wewe ni milionea. Kitu nachowashauri ni kuwa bebeni sana hayo maboksi na ku-save kila mwezi huku mkikumbuka kujenga/kununua nyumba nyingi muwezavyo huku bongo. Si mnajua tena huku nyumba ni bei nyanya tofauti na UK. Na siku hizi nyumba Dar zinalipa kichizi, unavuta pesa kiulaini. Na nyie mlionunua nyumba za mortage miaka iliyopita huko mkiamua kuziuza sasa uongo maana hiyo profit ndogo mtayopata na kuamua kuileta bongo hata huyo Lady Jay Dee haoni ndani.
Asante sana kaka Michuzi, nakutakia weekend njema.
Mbeba maboksi mstaafu
Huo ndo uzushi haswa. ingekuwa baadhi ya hao madogo siwajui sawa. hapo naona ni mtu kaamua kutafuta attention tu. Yani kijana wa kiswazi awe na tuseme 300m halafu kuwe na amani uswahili,Haiwezekani. Hapo naona ni changa la macho hapo. Nafikiri huyo lady J walikuwa wanamaanisha 500K
ReplyDeletewenger
kiukweli hapa bongo ukiwa na njenge basi ww ni mkali na tunaamini tayari uchumi wako ni mzuri nimebatika kuona nyumba ya JD ambayo value yake inaweza kuwa 150 milioni Professor J 100 milion Banana zoro 80 milion kwahiyo ukiwa na nyumba ni heshima kubwa lakini ukweli awajaweza kuingia katika sector ya investment ambayo wao inaweza kuwatoa na wakafika mbali kwani pesa zao huwa kama za msimu lakini dada judith Wambura anakwenda vizuri na wengine wanafuatia lkn walio wengine wamewekeza kwenye pombe, mademu,na kubadili magari kwahiyo hizo juu data sio sahihi kabisa
ReplyDeleteTWAAAAAT!!!!!!!!!!!
ReplyDeletemh, hamna kitu kam hicho labda biashara haramu pia
ReplyDeleteBOLA MIMI SIJASEMA
ReplyDeleteHabari za masiku wana blog! Hongera Lady JD kwa kuweza kuwa na hiyo fortune ya 5oom.Lakini kwa upande wa pili bado na hoji kuhusu Gadna,NAELEWA NI SUALA BINAFSI ZAIDI, inakuwa aje anaendelea kuwajibishwa kwa kazi ya 80,000/=pm.Kwanini asijikite na mke wake wakafanya mambo yao zaidi hasa ktk fani hiyo ya Music.kwani hata Gadna ana knowledge kubwa sana ktk masuala ya music kwani hata huko nyuma alisha wahi kumiliki KIBANDA CHA KUUZA CDs.Au Marriage Contract terms haziruhusu FINANCIAL ENGAGEMENT.
ReplyDeleteSasa kama na $ laki tano mbona ana nyumba ya $30,000? ...mtu mwenye hela kama hiyo bongo angetakiwa awe na vitega uchumi vingi tu na nyumba i we na vitu vya maana...makochi tuliyaona ya $2000...na ile nyumba kama yangu nimejenga bongo na mimi ni mbeba boz nimetoka shule mika minne na nusu iliyopita....sasa kama kweli ana hizo hela something is wrong with her....bongo hela kama yake angekua hata na usafiri mzuri....Maybe I am wrong lakini it sound a little fishy...
ReplyDeleteMichuzi baab kubwa,
ReplyDeleteHii taarifa imetulia sana,
Please tupatie list zingine kama za wanamuziki wa 'jazz band' matajiri.
pia utuletee na list ya wachezaji mpira matajiri.
Mbona kwenye hiyo list Fresh Jumbe hayumo?
Michuzi na wewe pia ni milionea kwani hata kule kwa Mugabe kila mtu ni milionea.
Weeeeeeeeeeee haiwezekani...Kylnn worth more than Ray C na T.ID na AY??...PLZ gimme a break. Michuzi fanya utatisi mzuri kisha tuletee data manake siamini hata moja hapa..
ReplyDeletesasa wanalipa kodi hizo
ReplyDeletewabongo utawajua tu! always negative mind, sina hakika na hiyo statistic ya kiwango cha fedha cha wasanii waliotajwa hapo juu...lkn napenda tu tujue jamani kuwa sio kwamba kwa kuwa wao ni wanamuziki basi wabweteke na hela ya mauzo ya music bila ku invest na kufikiria activities nyingine. naweza kuona jinsi jitihada za AY katika kujijasilia mali na sitashangaa kusikia kama ana worth ya that amount.....Hlf kitu kingine cha kushangaza, mbona wabongo hamuhoji wanamuziki wa mamtoni wanaothaminishwa utajiri wao kwa kuangalia assets walizo nazo plus hela ya bank? tufikie wakati sasa tukienda ulaya tusome na utafute kazi za maana, hizi za kupiga BOX zinatufanya tuwe na negative minds kwa kila kitu kwa sababu ya Inferiority complex..tunakuwa wazembe wa kufikiri mpaka tunaona kila kitu hakiwezekaniki....bongo ya sasa sio ile ya kukusanya vijipaund kwa miaka miwili baada ya box la ASDA na kuja kutesa bongo kwa wiki mbili..muamke otherwise kila siku mtakuwa mnakuja bongo hlf mnakimbia baada ya siku 2...bongo ya sasa si ya kumuogopa mtu anaeongea kizungu..tunavalishwa na wachina sawa lkn at least tunaishi maisha yenye dignit..sitaki kuwalaumu sana maana wengi wenu kutokana na knowledge ndogo hamuwezi kupambana bongo...niwapongeze wote walio mamtoni na wanaojua maana ya shule na wale wanaofanya kazi intelectual na professional....muwaamshe watanzania wenzenu waliolala huko na kuamka kila siku kwenye blog ku critisize
ReplyDeleteNyumba ya Lady Jay Dee tumeonyeshwa na sasa twaambiwa ana hizo pesa. Ama kweli pesa za madafu....
ReplyDeletekwanza kabisa napenda kusema kuwa sina imani kuwa habari hii ina usahihu wa 100%. Lakini pamoja na hayo kuna vitu vichache nataka kusema.
ReplyDelete1. Unapozungumzia kipimo cha utajiri iwe Bongo au mtoni, huzungumizii hela katika akaunti. hela iliyokaa tu katika akaunti haina maana, faida ya utajiri ni kuwekeza utakapokuwa na kuongezeka. Hivyo suala la mtu kuponda eti wamehesabia nyumba/magari, n.k. ni upuuzi, kwani hizo mali zote ni sehemu ya utajiri.
Mtu kama Nature najua kuna kipindi alipoibuka akapata hela zake aliwekeza katika viwanja/nyumba kadhaa na thamani ya viwanja sehemu nyingi Bongo imepanda sana katika miaka michache iliyopita.
2. Wasanii wa Bongo utajiri hawapati katika mauzo ya CD maana wanaibiwa sio na wahindi tu, hata na sisi wengine tunaoendeleza libeneke ya kunakili CD na kuweka MP3 zao katika mtandao bila ridhaa yao na kulipia. Hivyo wengi wanategemea kupata mapato kutokana na show. Jide najua kuwa anakamata bingo ndefu kwa gig yake Peacock hotel.
3. Umaarufu wa msanii haumaanishi utajiri. Inategemea mauzo yako ya CD na show,, n.k. Inategemea hela zako ulizopata umetunza au umetanulia zote. Na inategemea una vitega uchumi gani nje ya kuimba. Mfano P-Didy, Jay Z na Master P Marekani amabao wamewekeza hela zao katika biashara nyingine nje ya muziki. Hivyo suala la fulani mbona hayupo katika list hii wakati ni maarufu sio hoja, inawezekana anazidiwa ujanja na hao walio juu yake.
4. Inanisikitisha sana kuona tabia ya kuchukiana na kupondana tuliyo nayo wabongo. Wanamuziki waliotajwa hapo hawajiandika wao, habari kaandika mtu mwingine. Kama una mashaka na usahihi wa habari hiyo mkosoe mwandishi sio unaanza kuwaponda hao wanamuziki kuwa fulani yuko hivi, fulani yuko vile.
5. Bongo flava imepiga hatua kubwa katika miaka ya karibuni na wasanii wengi (lakini sio wote) ambao uongo mbaya kwa maisha yetu ya Kibongobongo wanajiweza angalau. Sisemi kuwa wana mamilioni ya hela zilizotajwa hapo juu; ila angalau mtu ana kibanda somewhere, maybe kausafiri kidogo na hela ya pamba, n.k.
6. Sidhani kama takwimu zilizotolewa hapo juu ni sahihi (angalau kwa baadhi ya wanamuziki), lakini sina ushahidi wa kubisha. Lakini sidhani kama ni busara kuanza kupondana na kuiponda Bongo yetu na umaskini, n.k.
Mwisho nawatakia mema wasanii waliotajwa na kama bado hawajafikisha thamani ya fedha zilizotajwa hapo juu, basi wafanye itihada inshallah siku 1 labda watafika. Kama sauti ndio kipaji chako kwanini kisikutoe basi
wewe wa pili kutoka chini acha kuwa na akili finyu km unakula funza wa kuwa na mil 300 kwa hapa bongo hasa hawa wasanii wetu nani?unafanya masihara nn na huyo muhindi?katoa hela ningi kwenye album yako mil 30 ss hiyo 500 mbali na asset zako unafanya mchezo
ReplyDeletejamani hiyo taarifa si kutoka kwa michuzi kuna gazeti moja hapa bongo linaitwa BAB KUBWA ni la udaku ndio wamefanya research yao wameona hao ndio wasanii wao.vigezo vilivyotumika ni kujuana kwa hiyo sishangai,limetawaliwa na masifa kwanza gazeti lenyewe so don believe everything u read in the papers
ReplyDeleteM500? Kwa hile nyumba ya bati na ambayo iko ka Xmas tree ama? Usitutanie Michuzi! Angekua na hizo m500 asingekimbilia Kimara kwenye viwanja vya bei rahisi.
ReplyDeleteWatanzania bwana sijui tupo vipi sasa kama ww huna pesa na huna deal ya kupata pesa hiyo basi kaa kimya kwa sababu hayo mambo ni yanawezekana kabisa. Halafu na hili swala la kubeba mabox jamani kazi ni kazi kwa hao wenzetu huku ndio maana walipata maendeleo angalia wenzetu China, Singapore, Korea, Japan nk watu huku hawachagui kazi ndio maana wanapata maendeleo. Mimi nimeshuhudia kwa macho yangu nilipokuwa Singapore jamaa ana degree ya utawala lakini anafanya training ya kuwa konda wa train na ana part job ya kufanya usafi katika hiyo station. nilipo muuliza aliniambia hawezi kukaa kusubiri kazi aliyosemea life hamsubiri kazi ikipatika poa. Nchi hizo zote nimefanya kazi kwa hiyo najua na nimebeba sana mabox nilipokuwa Wiingereza, nilikwa sichagui kazi labda ndio maana leo hii nipo hapa nilipo. Tufanye kazi kwa bidii Watanzania wanzangu tuache majungu.
ReplyDeleteMdau kwa sasa nipo Cameroon
ahahah samahanini sana kwa watu ambao hamjanielewa swala langu bado lipo palepale mimi nimepata habari hizi kwenye kituo kimoja cha radio ambacho ni maharufu sana hapa bongo...ndio maana nikaamua kuwajulisha na kupata maoni yenu..ila kwa imani yangu inaweza ikawa kweli..kwani hao wasanii kwa kwa mfano matonya ni msanii ambaye anafanya shoo nyingi sana ndani na baadhi ya nnchi za hapa afrika mara nyingi na vilevile nimeona maendeleo yake binafsi ambayo ameyapata kwenye kwenye music na anamiliki baadhi ya nyumba na magari na hata vitega uchumi....huyu tid kwa kweli huku nyumbani mi bado sijaona kitega uchumi chake chochote zaidi ya kung'aa tu na kuzulula huko ughaibuni.....kwa upande mwingine bongo kwa sasa ipo juu angalau baadhi yenu mnasema hata kama wanazo lakini sio ela ahahah kibongobongo sisi tunaona ni ela....kwa upande mwingine nashangaa sana kuona nyie baadhi ya watu wa uko ughaibuni kujiona mshayapatia....kumbukeni uku ni nyumbani na mnahitaji kupaheshimu....nadhani tumeelewana ....ni mimi mtoa maada ngwega
ReplyDeleteWatanzania kweli sie watu wa michapo yaani mtu na akili yako unaweza kuamini habari kama hizi...wanamuziki mashuhuri dunia ndiyo wenye thamani za 500m kama P.Diddy , JAY-Z , 50cent,Phatfarm ,JLO ....e.t.c hao watu wahapati hizo hela kwa kuuza album au concept... wana blend siyo chini ya tatu...sasa hao wabongo hizi milioni wamezipata wapi kwa kupiga muziki kwenye ukumbi wa ukonga bar halafu utegemea kukusanya milioni nyie watu mnacheza na hizo namba..
ReplyDeletein general income ya wanamuziki inategemea pato la wananchi sasa Tanzania ambayo mtu anaishi kwa dollar moja kwa siku hizi ni details za world bank leo hii huyu mtu akalipe kiingilio cha dollar 50 haya mahesabu sijuhi mmeyapigaji..mtu unaweza ukawa na dolar 500m ukajenga kimara uswahilini...kwanza ukiwa na hela hiyo uwezi kukaa Africa... ndiyo maana bara zima hakuna milionia hata mmoja mwafrica ikifanikiwa anahamia overseas.. hacheni michapo jadili vitu vinavyoendana na maisha ya kwetu andikeni habari kama ...ongezeko la vifo vya watoto wachanga au kupungua kwa uwezo wa kununua(purchasing power)kwa watanzania walio wengi for last two years hizo ndiyo thesis zilizo karibu na jamii kulikoni haya mambo ya michapo......
Doctor..
ISSA ACHA UFISADI
ReplyDeleteInavyoonekana wanaokandia ni wale waliondoka nyumbani sikunyingi wakiwa na mategemeo ya kufanikiwa majuu ilahadisasa hata shule hawawezikulipia na hela zote za mabox wanalipia bills.Jamani Tz imebadilika,mtakalia kupiga makalele ya ufisadi wakati wengine wanaendelea kula!nawatakia mafanikio vijana wote wahangaikaji!msiwasikilize wapiga domo
ReplyDeleteJamani huyo aliyetoa habari hii hawatakii mema hao wasanii. Anataka hao vijana watafutwe roho zao na majambawazi buree!!!.
ReplyDeleteanony wa Mar 9, 10:56, haijatajwa kuwa currency inayozungumziwa hapo ni USD. Kilichoandikwa ni thamani ya mali tu, inaweza ikawa ni TZS
ReplyDeleteTANZANIA REVENUE AUTHORITY TUTHIBITISHIENI KUHUSU MADAI YA UTAJIRI WA WASANII HAWA, KAMA HAWALIPI KODI KAMA INAVYOTAKIWA BASI WAWEKENI KATIKA ORODHA YA UFISADI.
ReplyDeletemaharufu (badala ya "maarufu")
ReplyDeleteWiingereza (badala ya "Uingereza")
hile (badala ya "ile")
hacheni (badala ya "acheni")
blend (badala ya "brand")
---
Makosa ya kiuchapaji yanayotokana na vidole (na sio "vidore") kuteleza mfano "wahapati" badala ya "hawapati" nimeyachunia.
Tuangalie lugha pia. Michapio hii nimeiona kwenye baadhi ya comments hapo juu:
ReplyDelete(1) maharufu (badala ya "maarufu")
(2) Wiingereza (badala ya "Uingereza")
(3) hile (badala ya "ile")
(4) hacheni (badala ya "acheni")
(5) blend (badala ya "brand")
---
Makosa ya kiuchapaji yanayotokana na vidole (na sio "vidore") kuteleza mfano "wahapati" badala ya "hawapati" nimeyachunia.
wabongo tuache dharau.
ReplyDeleteTutafanye utafiti wa kitaalamu na kuweza kujua ukweli, ili nasisi tuwe angalau kama wao.
Kuna maajabu gani kwa hao kuwa na fedha hizo, na tukumbuke kuwa sio kama wanazo chini ya mto au ziko benki, maana yake wanafikia hapo kwa hesabu za vitabu.
Robert B. Mujuni
HEBU FIKIRIENI, WASANII HUPATA KATI YA SILIMIA 5 NA 7 YA MAUZO HAPA TANZANIA, SWALI LA KIZUSHI....HAWA WADOSI WANAOBAKIA NA ASILIMIA 80, WANALIPA KODI?
ReplyDeletewe ngwega funga domo lako kwanza umetuma hii na lipicha lako kutafta umaarufu tu...uongo mtupu wewe na huko uliposkia
ReplyDeleteHapo imetajwa tu 500Mil,
ReplyDeletefedha inawezwa kuwakilishwa kwa njia nyingi.
Yaweza ikawa katika makumi, mamia, maelfu, malaki n.k
Sasa inawezekana hizo figure ziko katika Zimbabwean Money au pia Zambian Kwacha.
Pia kuna vigezo vingi vya kupata data,
Inawezekana alieleta hizo data hapo juu kajumuisha nyumba, magari na mali zote ambazo ye kaziona wasanii wakiigiza nazo kwenye video.
Yaan kama JD katumia nyumba flani basi inawekwa kwenye mahesabu.
Kama ndivyo basi hakunaga msanii maskin
Inawezekana hizo takwimu zinajumuisha mali (magari, nyumba etc) ambazo wasanii hao wametumia kwnye video zao kama mdau alivyopendekeza.
ReplyDeleteHabari kama hizi zitawaweka baadhi ya vijana hapo juu katika mazingira magumu. Imagine mtu unaishi kwa wazee halafu wanasoma magazetini eti una wealth ya 500M! Hapatatosha.
Bado tuna safari ndefu. Mwaka 1990 Michael Jackson alikuwa ana worth Millioni 350 US dollars...hizo ni sawa na Billioni 35 za Tanzania..he he he....tuna safari ndefu....!!
ReplyDeletedoctor sunday 10 56 si dollar hiyo baba ni madafu (Tshs). halafu mamilionea wapo africa na wanaishi africa angalia fobes tajiri wa 336 ulimwenguni anatokea wake na anishi wapi (Nigeria) wa mia moja na sabini na mbili au tatu antokea africa ila sina uhakika ni wapi. na wengine wengi tu waakina SSB LTD Salim Said Bakhresa tunao bongo na wengine wengi tu siwezi kuwataja hapa wote. ninachokushauri usitoe comment kama huna uhakika nazo
ReplyDeleteahaahaa! i like that, nadhani wengi wetu tulio Nje ya nchi ni mamilionea basi Bongo. duuh hii kali ok.
ReplyDeleteIs that TZ currency or Mugabe's currency?????kama ni Mugabe then i believe but if its TZ currency, i m NOT convinced. Mdau T-Dot
ReplyDeleteUnajua nini??? watu hawashangai kuwa kapataje hizo hela. Ila kama ana hizo hela basi angeishi vizuri zaidi...
ReplyDeleteWengi tuko huku kama mini nimemaliza shule sio mda mrefu na nimejenga nyumba. Na nyumba kaka Michuzi aliyotuonyesha honesty sio najisifia lakini yangu iko much better. Na mimi sina hata hela za kutanua na nimejenga hiyo nyumba yeye mwenye laki tano basi angekua na nyumba nzuri zaidi.
Msianze kusema ana malengo yake au ana save...Bwana hata vitu ulivyonavyo ndani kama una laki tano hutaenda na vile alivyonavyo
Hela alizonazo ni zake na mimi nampongeza sana kwa kupata hela kupitia usanii mgumu wa africa usio na copyright ila waliotoa habari ndio wawe makini na data zao.
You can fool some all the time but you can't fool all the people all the time. Hata kama hatuishi bongo value ya dollar tunaijua.
I have only one big question: Assume the numbers are true, are these guys TAXED (I mean TRA friendly)?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
ReplyDeleteJafar
KAKA MICHUZI
ReplyDeleteMIMI NAOMBA SOURCE(CHANZO CHA HIZI TAKWIMU)HILI TUWEZE KUZIFUATILIA,KUZIHAKIKI KUWASHAURI NA KUWAPONGEZA!
KAMA HUNA
I HAVE NO COMMENT.
mimi nasema kama watoto wana Wealth those amount ni safiiiii sana it shows how Tz arts inavyo kubalika lakini to be honest I doubt with that dataz kwa kuwa nazani kama kweli muziki wa bongo ungekuwa unauza hivyo master J na P. Funky wasinge pumzika na wangekuwa mbali sana labda wange kuwa na ela kama mengi kwa kuwa hao wote hakuna mwenye Track 10 ambazo amerikodi nje ya MJ na Bongo record .....lakini kama kweli mzuka
ReplyDeleteJamani hivyo ni vijisenti tu, hao mabwana wadogo hawna kitu bado na ndio wanajitafutia rizki, kwahiyo msiwaghasi na kuwaongelea saana. Tuna mambo mengi ya kuongelea zaidi ya hivyo vijisenti vya hao mabwana wadogo, lakini wanajitahidi,wanaonesha juhudi. Ni mwanzo mzuri tu
ReplyDeleteHaw wasaani wote ni choka mbaya tuu, 500m za jay dee ni ile nyumba ya rangi rangi nyekundu au nini. na mbona Ray c hayupo, TID naye hao wote si wasanii wa bongo?? hizo infor niza udaku na masifu ya buree, mamilionea wenyewe wametulia hapo hapo bongo hawaitaji kujulikana habari zao.
ReplyDeleteinawezekana ikawa ukweli ila mdau atuiambie amatumia njia ipi kupata hizo data
ReplyDeletekwa kweli hakuna msanii bongo mwenye utajiri huo hata kidogo wote hao wanajitahidi kufika katika maisha mazuri zaidi.
ReplyDeleteWOTE HAO CHOKA MBAYA HAMNA MWENYE HIZO THAMANI..........BABU ACHA KUTUYEYUSHA HATUPENDI HIZOOOO....EBOOOOOOH!!
ReplyDeleteKAMA WANA THAMANI HIYO AU WANA FEDHA HIZO MBONA WAMECHOKA SANA! MAANA WAKO CHOKA MBAYAAAAAAAAAAA.
ReplyDeleteDUUUH KWELI KAMA KUPEANA MAUJIKO BASI HAPA BABU UMEZIDISHA. HATAAAAA!