kampuni ya bia tanzania TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, kimetoa misaada mbalimbali kwa akina mama waliojifungua usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya agakhan jiji dar,ambapo wanawake wote duniani wanaadhimisha siku hii.Pichani ni balozi wa kinywaji cha redds Victoria Martin akimkabidhi zawadi mama Zena Hussein ambaye amejifungua leo asubuhi mtoto wa kike

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. kimaadili haturusiwi kunywa,kuuza,kupokea au kuhusika na chochote kuhusiana na pombe.mashekhe jitahidini kuangalia family zenu kuepuka dhambi zinazowezekana kabisa kuepukika.kwa wema kabisa bila ya lugha mbaya sema "ahsante,siwezi kupokea zawadi hii kufuatana na maadili ya imani yangu"

    ReplyDelete
  2. Mtu anayeweza kulipa gharama za Agakhan sidhani kama anahitaji msaada kama mtu anayejifungua hosp kama mwanayamala,temeke.

    Angalieni nani kweli wa kumsaidia na si ili mradi mtoka kwenye magazeti mmetoa misaada.

    ReplyDelete
  3. Jamani mbona misaada hamkupeleka muhimbili,temeke?au kusaidia wamama waliojifungulia nyumbani je ambao hawakuwa na uwezo wa kwenda hospitali kutokana na utaka wa maisha?mie sidhani kama kweli huyo dada aliyetoa hiyo misaada alifikiria kwanza...

    ReplyDelete
  4. Msemaji wa juu hapo umetoa point nzuri sana(maoni ya pili)
    Najua kwamba kutoka magazetini ni mojawapo ya kujitangaza lakini waheshimiwa inabidi muangalie jinsi gani mnataka kutoka.

    ReplyDelete
  5. Unakwenda kumsaidia mtu aliyejilipia zaidi ya laki 2 kwa ajili ya kujifungua au kalipiwa na shirika analofanyia yeye kazi au mumewe au unakwenda kumpa zawadi? Hebu tufahamisheni vizuri. Mie naona hapo wameenda tu kutoa zawadi lakini kama ni msaada wangeenda kutoa huko Mwananyamala, Temeke, na Amana wagonjwa wanakochangia vitanda. Au 'kamsaada' kenyewe kalikuwa kachache manake mwanawane unaenda na tu msaada twako uankuta wadi imejaa mpaka watu wanalala mzungu wa nne na wengine wanalala chini kwa nini usikimbilie Aghakhan ambako wadi nzima unakuta kuna wagonjwa wawili au watatu! Sana sana wamejaa ni watano ha haahaaa! lol!

    Au wameogopa kuambukizwa maradhi hizo hospitali zetu za uswahilini? Maana huwezi jua kwa nini wameenda huko!

    Mdaku

    ReplyDelete
  6. Naungana na mtoa maoni hapo juu kwamba msaada unatolewa kwa wale wanaouhitaji. Sasa kama mtu anaweza kulipia gharama za hiyo hospitali, weli huyo anahitaji hako kazawadi? Kwa nini msiwafikirie wale akina mama wa manzese, temeke, gongolamboto nk ambao kweli wanahitaji msaada? Kitendo cha huyo anayeitwa balozi wa hiyo kampuni iliyotoa msaada cha kukubali kwenda hapo hospitalini kutoa misaada hiyo kinatuambia ni kwa jinsi gani kichwani mwake ni patupu! Hata kama ana-degree kumi, basi hajaelimika. Na kama mimi ningekuwa mkurugenzi wa kampuni kama hiyo, basi huyo 'balozi' angefungasha virago muda huo huo alipokubali kwenda huko.

    ReplyDelete
  7. Yani mi mwenyewe nimeshangaa nilitegemea misaada itolewe mwananyamala,amana na pengine of the kind.lakini ndo hivyo..haya bwana.

    ReplyDelete
  8. utaweza kutuhabarisha bomoa bomoa ya ilala maana imenisikitisha sana kama utaweza sio lazima ni hiari yako

    ReplyDelete
  9. Yaan kweli mwenye nacho huongezewa kwa sababu kwa ufahamu wangu nilio kuwa nao ni kwamba Agha khan ni hospital ya watu ambao wanajiweza sasa msaada wa nini badala yake si mngepeleka huko Temeke,mwananyamala au hata muhimbili .jaman

    ReplyDelete
  10. Hivi jamani kweli mtu unatoka kwa akili yako na unajiita mtoa msaada unakwenda Hospital ya Aghakhan or Mikocheni or TMJ kutoa msaada kweli huo sio Msaada wala sio utu, Mungu anasema tusihukumu lakini hapo Dada hujafanya vyema kwani kuna wale watu Ambao hata Mungu anaona kweli wanahitaji msaada wako, Na dhawabu pia ungeipokea iwapo ungefika tu Pale Mwananyamala Hospital, Or Amana Hospital, Or Temeke hospital, Muhimbili na hospital nyingine yoyote ya serikali ambayo Kwakweli watu hawana hata jinsi ya kupata Kipande cha kanga kama Nepi ya kumfunga mtoto na ukapeleka hapo walau sabuni miche miwili na poda au mafuta tu ukawapatia wale akina mama wangekuombea Dua kwa Mungu na ungezidi kufanikiwa sana.

    Mwanamama aliyekwenda kujifungua Aghakhani ni Tajiri mzuri tu na anajiweza so sio vyema kwenda kumwongezea tena kumpatia mauwa na pempas ambazo anauwezo wa kuzinunua kwanini usiwapelekee ambao hawajawahi kuona hiyo pempas au Mauwa kwa macho yao?

    Kweli aliye nacho ataongezewa mara dufu na asiyenacho hata kile kidogo alichonacho atanyang'anywa.

    Mbarikiwe.

    ReplyDelete
  11. MNAJUAJE NYIE LABDA WAMETOA HOSPITALI ZOTE ILA PICHA HII NDO IMETOKEA

    ReplyDelete
  12. wewe unatoa misaada na wewe mwenyewe inabidi uanze kula sababu ujui kama model wenye ANAEREXIA wamekuwa burned

    ReplyDelete
  13. Hawa watu wa Redds wanatafuta cheap and meaningless popularity! wanawake wanaohitaji msaada wapo tele hospitali za umma ambako kuna walala hoi wanaohitaji zaidi huo msaada. Wahusika wajaribu kutulia na kutathmini maana ya msaada kabla ya uanza kutoa.

    ReplyDelete
  14. Hawawezi kutoa hospitali zote, ni upungufu wa mawazo na hekima wa mtoaji.

    ReplyDelete
  15. Huyu Mrembo aliona kinyaa kwenda amana, mwananyamala na Temeke ndio mana akakimbilia Aghakan kwa walionazo.lakini hajatenda haki kabisa na kama kweli ni Mtanzania Halisi Pasaka inakuja aende kwenye hizo Hosp za watanzania halisi mana hawa wengine ni walewale Rich........na picha tuzione.

    ReplyDelete
  16. kama kweli muko serious na kusaida, nendeni hospitali za vijijini, sio Aga khan hospital, ama munadhani media huko haifiki huko???????, acheni kututia changa la macho kuonyesha kuwa muna play role ktk COPRORATE SOCIAL RESPONSIBILITY!!!, wenye shida kweli hamuwaisaidii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. NDIYO MAANA MNATASEKA SANA HUKO BONGO,KWANI HAMNA HURUMA,KWANINI MSAADA UPELEKWE AGHKAN NA SIO MUHIMBILI AU MWANANYAMALA????MNAJUA KILA ANYEJIFUNGUA HAPO HANA UWEZO WAKE...WASHAMBA WOTE HAPO.MDAU 00316.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...