Kaka Michuzi,
napenda kuanza kwa kutakia heri ya sikukuu wewe pamoja na wadau wote popote pale walipo. Kwa ufupi nimehamia mji wa Bellevue, Seattle karibuni na bado sijaimaster mitaa vizuri.
Nilikuwa ninaomba wadau wanaoishi mitaa hii wanielekeze lilipo kanisa la kilutheri katika maeneo haya au hata seattle ambalo wabongo huwa wanajumuika ile niweze kusali nao misa ya pasaka.
Ahsante,
Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Unaweza ku-google kanisa la Lutherani hapo, pata address yake kisha nenda kwenye goole earth/google map to get the exact location of the church.

    ReplyDelete
  2. I just past the baptist church around the corner.Do you want the address?
    Btw there aren't many lutheran churches in Usagara.
    Why dont you relocate to German?

    ReplyDelete
  3. kwani aki-google ndiyo inamwambia wabongo wanasali hapo?
    jamani mtu anapohitajika msaada ni bora kumpa mawazo wanayosaidia na kama huna hayo mawazo ni heri kukaa kimya. Jamani wabongo mnaokaa karibu na huko alikosema huyu bwana msaidieni

    ReplyDelete
  4. Kuna kanisa linaitwa Calvary Lutheran Church ni watu wazuri sana.
    Tena leo ijumaa kuna misaa saa moja jioni na pia jumapili kuna misa pia. Address hii hapa chini.
    16231 Ne 6th St
    Bellevue, WA 98008
    (425) 401-1595
    All the best.
    Pia Kuna chama cha Watanzania kinaitwa Tanza-Seattle. Unaweza kutembelea hii web site www.tanzaseattle.org.

    ReplyDelete
  5. Ndugu yangu wewe ingia kanisa lolote la ki protestant hapo Seattle siku ya ibada mradi wasali mungu huyo huyo mmoja. Je ungekuwa Uchina au Japan kuliko nadra makanisa?

    ReplyDelete
  6. Nenda kaulize polisi, watakuelekeza mtu wangu..

    ReplyDelete
  7. Naungana na huyo mdau wa kwanza aliye comment hapo juu.
    Mie kwa ku-search kwenye google na kuangalia on google earth naona kuna makanisa mengi tu ya Lutheran. Southeast ya Bellevue kuna St Andrew's Lutheran Church, northeast kuna All Saints Lutheran church, pia mjini hapo kuna Piligrim Lutheran Church na mengine mengi tu. Tungejua waishi upande gani wa Bellevue (address) ingekuwa rahisi kwambia wapi liko kanisa karibu nawe.

    Fungua hii link labda kwa kuona address na zip code za hizo Lutheran churches humo waweza jua kanisa lipi liko karibu nawe.
    http://www.google.com/search?q=Lutheran+church+in+Bellevue%2C+Seattle&rls=com.microsoft:en-gb:IE-SearchBox&ie=UTF-8&oe=UTF-8&sourceid=ie7&rlz=1I7SNYG

    Bongo tambalale.....

    Mdau toka Kyela
    Mbeya

    ReplyDelete
  8. WABEBA MABOX WENGINE MNABOA..INA MAANA YOU CAN NOT ASK ANYBODY AT YOUR NEW ARE MPAKA UJE UTUJUZE HUKU KWAMBA NA WEWE UMELAMBA KARATA DUME..OK LIPO MKUNANZINI


    kachaa

    ReplyDelete
  9. Kuna watu wengine wana roho mbaya kama nini

    Wewe anonymous hapo juu kwani yeye hajui kuwa ukigoogle utapata hizo information? Anaulizia watu kama wapo wabongo sehemu hizo wakasali pamoja....

    Acheni roho mbaya na pelekeni frustration zenu kwingine

    Back to your question Lutheran Church yapo mengi na different varieties kwenye middle west states. East Coast na West Coast yapo machache na sehemu niliyoko miye mengi yanafungwa kwa kukosa waumini. Na pia huku nilipo yaliyopo ni ELCA. Kama huko uliko kuna ya karibu yaliyo chini ya Missouri Synod ni bora uende huko kwa vile wao wanasali kama Lutherani tuliyozoea bongo. ELCA ya huku wanasali na kufanya mambo mengi kama RC na ndio yapo mengi huku ninakoishi.

    Good luck

    ReplyDelete
  10. Kaa chonjo Marekani Makanisa ya Kilutheri yako mengi na tofauti.Yako ya kilutheri kama ya Tanzania kimfumo na taratibu za ibada,yako ya Kilutheri kikatoliki,kilutheri kiangilikana,Kilutheri Kipentekoste,Kilutheri Kikarismatiki,Kilutheri kibaptisti na Kilutheri huru ambayo hata hayana uhusiano na makanisa mengine ya kilutheri popote iwe Tanzania au Duniani.Kwa ufupi marekani ni kazi kuchagua kanisa la kusali.Mara ingine hata likiwepo linakuwa mbali sana na linaweza kuwa na matatizo mfano ya ubaguzi wa rangi.

    Hivyo unapochagua kanisa la kuabudu uangalie vitu vingi si ujirani peke yake au jina la kanisa kama linaitwa Lutheran au la.

    ReplyDelete
  11. Concemptual... Mwenzetu anataka kujua walipo wabongo huko Seatle, akasali nao, na wafahamiane. Pasaka itakuwa muda mzuri kujuana. Ni utamaduni mzuri sana, ambao nauunga mkono 100% as there are many to share, and for 'security' and social ...
    SEV

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...