Habari kaka Issa,
Pole sana kwa kazi nzito ya kuwaunganisha Watanzania, Waafrika Mashariki na Walimwengu wote duniani kupitia Blogu yetu hii. na pia hongera kwa kumaliza vakesheni yako salama usalimini, na sasa upo nyumbani bukheri khamsa wa ishirin. Nilitarajia kabla ya kurudi Kijiwe utatupitia na sisi wadau wa huku Scandinavia (DK) angalau tuasabahiane, naamini muda haukukuruhusu lakini inshaallah tutaonana tu.

Kaka Issa mi leo naomba msaada mmoja tu kutoka kwako binafsi na wadau kwa ujumla. Nikiwa nipo skuli hapa DK natakiwa nifanye masomo kwa vitendo (internship) katika moja ya jumuiya za kimataifa duniani kukamilisha shahada yangu ya uzamili katika Uhusiano wa Kimataifa na Maendeleo. Nimebahatika kupata ofisi moja mjini Geneva, lakini kwa taarifa nilizonazo ni kuwa maisha mjini pale ni ya juu sana. wenyeji wangu wamenitumia taarifa kuwa makaazi na malaji tu yanagharimu dola 1000 kwa mwezi, na natakiwa niwepo pale kwa muda wa miezi mitatu.

Ninachotaka kujua ni je wadau ambao walishawahi kufka au kuishi pale wana idea yoyote kuhusu upatikanaji wa kibarua (boksi, ufagio, n.k) ili kuweza kusaidia kukidhi mahitaji ya kila siku? na je kwa uzoefu wenu kuna makaazi (accommodation) ya bei ya chini ya dola 500 kwa mwezi? japo katika dakhalia za wanafunzi. kinachoweza kusaidia zaidi ni kujua kama kuna ndugu zetu pale ambao wanaweza kunipa miongozo zaidi, au hata wkanibeba na kugawana gharama (Mabibo Hostel style). Hata ughaibuni yapo hayo!

Kaka Issa nitafurahi sana nikipata ufumbuzi wa kizungumkuti hichi. ikishindikana basi naweza kujiunga na wewe katika libeneke lako.

Wassalaam,
Salam kwa wadau wote.

tafadhali anuani kapuni!
usiianike uwanjani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Wewe fala usituyeyushe haoa na dhiki zako. Wewe si unasoma kwa scholarship huko, inakuwaje huwezi kulipia chumba hapo Geneva. Acha ubahili wewe Mzanzibari lipa pesa hiyo usiwadhalilishe wenzio ambao wanajisomesha na bado wanakidhi gharama za maisha bila ya kuwa omba omba huko kwenye nchi za watu. Ukileta masihara nitakutaja na jina. Naanza kwa kukutambulisha humu kama Mzanzibari.

    ReplyDelete
  2. WEWE MDAU JUU VIPI MBONA UNA JAZBA? UZANZIBARI UNATOKEA WAPI SASA NA HUYU NI MWANAFUNZI ANAJARIBU KUANGALIA UNAFUU ? ACHA CHUKI BINAFSI KAMA HUNA USHAURI FUNGA DOMO LAKO .HAJASEMA KWAMBA ANATAKA KUKAA BURE ANAANGALIA UNAFUU KITU KINACHOELEWEKA KWA WANAFUNZI WA NG'AMBO.MDAU JARIBU KUANGALIA HOSTELBOOKERS.COM au JARIBU GOOGLE NA PIA MYSPACE UNAWEZA KUPATA WANAFUNZI WALIKUWA HUKO WAKAKUPA USHAURI MZURI ZAIDI.

    ReplyDelete
  3. mi nadhani kama ni mwanafunzi, wanafunzi wengi wanatafuta apartments wenyewe wakiwa nje ya nchi, za wanafunzi huku wakiwa wanasoma ndo maisha ya wanafunzi hayo.

    ReplyDelete
  4. Mkuu i nadhani ingia kwenye google. Tafuta cheap accomodation in Geneva. You will get one. Siku hizi Google imerahisisha mambo sana. wala usihangaike, labda kama unataka watanzania walio Geneva wakubebe makwao..Otherwise tafuta kwenye mtandao mkuu. Kama unasoma masters, basi hiyo ni kazi ndogo kwako unaiweza.

    Kila lakheri.

    Mdau

    ReplyDelete
  5. Mtoa maoni namba 1 acha unoko! kutafuta chumba cha bei nafuu siyo ubahiri, ukizingatia kwamba maisha ya uswisi ni ghali na scholarship nyingi hazitoi pesa kiasi kikubwa. Wewe unaelekea una chuki binfsi. umenyimwa uroda nini? acha kumfedhehesha mwenzako, kwani kama pesa za scholarship zingetosha watu wasingepiga fagio, kubeba maboksi, kusafisha wazee n.k.

    ReplyDelete
  6. michuzi zibiti nithamu katika blog,
    sijaona mantik ya uyo anony kumwita mwomba msaada fala,naamini fala ni yeye anayeyaangalia maisha katioka mtazamo wa leo na ajui kesho itakuwaje.kigezo cha kuwa na scholarship isiwe ndio kutokumbuka ni wapi umetoka, angalia ndugu zako nyumbani wanaishi kwa chini ya dola moja alafu unaona ni kawaida kutumia dola elfu 1000 kwa mwezi.kijana anataka kusave nawewe kama hauna msaada tambaaa sio unaona wenzio mafala.
    naamini kunawatakao jiutokeza umu kumpa msaada anao huitaji, na wewe utabaki fala na ubinafsi wako usiyekumbuka ndugu zako nyumbani wanaokula mlo mmoja kwa siku.

    ReplyDelete
  7. Inshallah, wastaarabu na wenye roho za utu watakujibu na kukusaidia. Hili si jambo la kuingiza masikhara na matusi. Kuna globu nyingi mtandaoni zenye kutoa fursa za matusi na masihara lkn si kama hii. Tujifunze kuzimgatia muktadha.

    ReplyDelete
  8. Jamani huyu Anon wa kwanza si jazba tu, ila ndo vile vijitabia wanavyookoteza huko kwa wenzetu wanoitwa wametutangulia, hizo ndo zile athari tunazozisema zinachachua donge zima la unga. sasa wewe ndugu yetu uungwana wako na malezi ya kwenu yako wapi hapo tuseme umeyasahau au huyataki, kama huyo mwenyeshida ya kuelekezwa tu ndo mvua yote hiyo ya masika ya matusi? Hee kulikoni au kuna jengine, basi atakutumia dola 5 umuelekeze, ikiwa bure inaua si kihivyo ndugu yetu. Hata kama umembaini kua ni mzanzibar kwa lafudhi yake ila shida yake haishabihiani na ukabila wake hususan na pale mtu anaomba msaada tutani bro.

    ReplyDelete
  9. huyo jamaa wa kwanza niwale wenye frustration za maisha na yeye yuko bongo anaangaika kwenye ma cafe kutafuta vyuo bila mafanikio.

    ReplyDelete
  10. He makubwa jamani, ndivyo mnavyoishi hivi huko ughaibuni, hasa hapa namaanisha ndivyo watu wa Europe ndivyo mnavyoishi hivi under EU? Hapa si kwamba na stereotype kwani hii si kauli ya kwanza kuisikia kutoka kwa watu wa EU. Ndio maana waliopo Marekani wanawakandya.

    Wewe anon wa kwanza kama huwezi kumsaidia mtu kwa mawazo tu bila kutumia senti tano yako je unaweza kuwasadia nduguzo kwa kuwatumia pesa? Wakati mwingine maneno tuandikayo, yanaonyesha u mtu wa aina gani. Inaonyesha u mchoyo hasa tena hasa pengine mpaka unajifanyia choyo wewe mwenyewe kwa ulivyokubuhu kwa uchoyo.

    Unayetafuta mahala nafuu, cheki international youth hostel kwenye google kama wanayo hostel huko unakotaka kwenda. These hostels are very cheap, na hata kama umri umeenda hauko kwenye kundi la youth unaongeza hapo pesa kidogo. Na unajipikia mwenyewe which is cheaper kuliko kununua chakula kilichokuwa tayari. Na hizi youth hostel ziko all over the world I think.

    ReplyDelete
  11. Pole ndugu yangu watu wa huko watakupa idear. mi sijui mambo ya huko

    ReplyDelete
  12. Student,nenda Geneva mtafute mtz mmoja hapo Geneva anaitwa Daud ni alwatan wa hapo utapata chumba/nyumba bei mteremko kuna watu wanazo za bure.
    Ukitaka kumpata kwa urahisi nenda central Geneva kuna baa ya watz inaitwa TANZANITE hicho ndo kijiwe chake na utakutana na watz kibao watakusaidia na ishu yako.chakarika kijana.
    Cha chandu - UK

    ReplyDelete
  13. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  14. Huyo anoni wa kwanza nami nimemshitukia, atakuwa ni wa mitaa ya migombani tu mchaga! manake kwa matusi na kutokujua kishwahili wanaongoza.! Nimemgundua kwa kutumia neno "Fala" kwanza fala mwenyewe! Kwani mtu kuomba msaada ndio umtukane? Au kwa kuwa kaandika kiswahili khaswaaaa kizuri imekuuma? au ulitaka pale penye "ana" aandike "hana" au badala ya kutaja "r" na "l" kunakotakiwa ataje kinyume? Hiloo utabaki hivyo hivyo na uchaga wako! hilooo au umelewa nini?

    ReplyDelete
  15. sasa kama hutoi email inakuaje, dada email tu issue.

    ReplyDelete
  16. Mdau namba moja acha kutumia maneno makali sana kwenye blog kwa sababu mtu kuomba ushauri ni sawa tu na kumsaidia kwa ushauri si lazima kama huna la kumsaidia haina maana kumtukana chunia msg yake kama huna mpya ya kumsaidia na wewe mwanafunzi sasa mtu atakusaidiaje kama hutoi contacts zako kuwa makini kama kweli unataka ushauri

    Katochi)

    ReplyDelete
  17. I got 2 advice for you bro, check their local news paper in the area wer u gonna stay, luk for advert. about accomodation that way u will know the price for apartments and hostels. Second use google bro. If that won't help maybe this link will give u an idea.
    Mdau T-Dot.

    http://switzerland.isyours.com/e/guide/geneva/geneva-cheap-hotels.html

    PS:4get about the comment made by the 1st person, he/she doesn't know nothing about life outside TZ.

    ReplyDelete
  18. Mimi nawashukuru, walioonyesha moyo wa kumsaidia mwenzetu kwa ushauri mbalimbali.Mzidishiwe.

    ReplyDelete
  19. You 'brainless' skull commenter #1: Funga domo lako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...