JUMUIYA YA WATANZANIA WASHINGTON METROPOLITAN INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA NDUGU / RAFIKI KADUMA THOMAS MSUKA.
KILICHOTOKEA TAREHE 7 MWEZI WA TATU , SAA SABA MCHANA KATIKA HOSPTALI YA HOLLYCROSS MARYLAND USA.
MAREHEMU ALIZALIWA 23/01/1973 .
MAREHEMU AMEACHA MCHUMBA NA MTOTO WA MIAKA MITATU.
JITIHADA ZINAFANYIKA ILIKUWEZA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU KWENDA KUUPUMZISHA NYUMBANI DAR ES SALAAM, TANZANIA.
UNAWEZA KUTOA MSAADA WA MCHANGO ILIKUWEZA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU KUPITIA:
CITY BANK
ACC #6738216475
ROUTING # 254070116
ALBERT MATESO
UNAWEZA KUWASILIANA NA ;
RASHID MKAKILE # 301-675-8383
STEPHANO MHINA # 443-278-6119
ALBERT MATESO(COCHA) # 301-447-9367
KHALFAN LYIMO # 202-468-8312
KAUGA AARON # 240-988-2699
SALEH RHONDA # 240-273-8871
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHE PEMA PEPONI.
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 50 mpaka sasa

  1. JAMANI KUULIZA SIO UJINGA, NI NINI KILICHOMUUA MAREHEMU?

    ReplyDelete
  2. Bwana alitoa, na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Yesu libarikiwe. Amen.

    ReplyDelete
  3. raha ya milele umpe eeh bwana ,na mwanga wamilele umuangazie astarehe kwa amani . amina .. sema sala hii mara tatu..
    baba yetu ulie mbinguni jina lako litukuzwe ufalme wako ufike hapa duniani kama huko mbinguni , utupe leo mkate wetu wa kila siku ,utusamehe makosa yetu kama na sisi tunavyowasamehe waliotukosea ,usitutie majaribuni lakini utuokoe katika zambi kwakuwa ufalme ni wako na nguvu na utukufu hata milele amina.. mara tatu

    atukuzwe baba na mwana na roho mtakatifu kama mwanzo na sasa na siku zote na milele amina..mara 3.

    simfahamu marehemu but he seems alikuwa kijana mdogo sana.. mungu ametoa na mungu ametwaaa jina la bwana lihimidiwe...
    mdau wa ulaya...

    ReplyDelete
  4. Kilichomsibu ninini umri wote huo mdogo? R.I.P

    ReplyDelete
  5. POLENI SANA KWA MSIBA WA KIJANA WETU, MIMI SWALI LANGU NI KWAMBA HOW COME HIYO ACC INA JINA LA MTU BINAFSI KWANINI ISINGEANDIKWA JINA LA MAREHEMU AMA MCHUMBA WAKE THEN MEMORIAL FUND ILI IWE RAHISI KUTRACK HELA INAVYOINGIA KULIKO KUWEKA KWENYE ACC YA MTU WA NNJE.ITATUSAIDIA KUWA NA TRANSPARENCY NA INTERGRITY YA PESA YA MICHANGO...NI MAONI TU.GOD BLESS

    ReplyDelete
  6. Tumepokea kwa mshangao na masikitiko makubwa sana msiba wa ndugu yetu Kaduma Thoma (RIP)... Mungu amlaze pema peponi rafiki yetu.
    Ee Mwenyenzi uwape nguvu na ujasiri ndugu, jamaa na marafiki za Kaduma kipekee tunawaweka mikononi mwako Mchumba na Mtoto wa ndugu yetu....
    Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe!!!
    (Ilboru class of 1992!!!)

    ReplyDelete
  7. Rest in Peace my dear brother, we will always, always love you and remember you for your good sense of humor, love and kindness to everyone around you!! We love U so much, but God loves U more...

    ReplyDelete
  8. Mungu wangu ni kijana tena bado mdogo hata 40s bado. Kuna nini huko majuu mbona vijana wantutoka sana.

    Tujiulize labd akunatatizo kwani tulitarajia huko ndiko watu wanaishi miaka mingi kuliko huko bongo madongo kuinama. lakin trend inaonyesha tofauti. hili ni tatizo tusaidiane kulitatua. nawazungu vijana pia wanakufa hivyo au life style ni tofauti?

    Poleni waliofiwa. huu ni zaidi y amsiba binafsi ni tatizo lijadiliwe kuepuka vifo vy a vijana.

    ReplyDelete
  9. RIP
    HILDA

    ReplyDelete
  10. Mdau wa juu kabisa mbona umeuliza swali kwa jazba sana.yani umeshindwa kuanza kwa kutoa pole kwa wafiwa alafu ndio ukafuatia swali lako la kilicho muua marehemu? Tueni na moyo wa kibinadamu jamani.ndio kuliza sio ujinga lakini ungeanza vizuri " poleni wafiwa wote alafu ungefuatia swali lako lakutaka kujua kilichomchukua marehemu.
    R.I.P

    ReplyDelete
  11. My condolences to his fiancee, kid and hommies.

    Death has never been easy especially when it involves a very young person.

    RIP dude...

    ReplyDelete
  12. Wengi mmeuliza kilichomsibu marehemu ni kweli alikuwa ni kijana mdogo sana, tunasikitika sana kumpoteza marehemu mapema kiasi hiki.Alikuwa anasumbuliwa na tatizo la ini.
    We will miss you my dear brother/brother in law!!! we really do...upumzike kwa amani!

    ReplyDelete
  13. it is difficult to be separeted from the one we love so much and that some day the circle of life will be complete and we will all be together.thank you for all you have given us Please GOD give him internal PEACE AMIN.

    ReplyDelete
  14. MUNGU akuweke mahali pema peponi..
    Amen

    ReplyDelete
  15. POOR YOUNG SOUL!!!!!!

    EVERYBODY WANTS TO GO TO HEAVEN BUT NO BODY WANTS TO DIE.

    R.I.P MY BROTHER AND HAVE A SAFE JOURNEY TO HEAVEN. MAY THE ANGELS HOLD YOUR HAND ALONG THE WAY

    ReplyDelete
  16. Mungu wa rehema amekuandalia makao ya milele na sisi tuliobaki tunakuombea, siku moja tutakutana kule kwa Baba.Mbele yako Nyuma yetu.Mungu awape nguvu na matumaini familia ya marehemu,jamaa na marafiki. Mungu Mkubwa.AMEN.

    -Tx.

    ReplyDelete
  17. Take a minute,Muombee ndg yetu aliyetutangulia.Asante.

    ReplyDelete
  18. Jamani watu tulio hapa dc md va na wengine kwenye majimbo yambali tujitokeze katika kutoa michango ya kusafirisha mwili wa marehemu,huu sio wakati wa malumbano alikufa na nini ndiyo hivyo tena kaisha tangulia mbelle ya haki.Ila kwa kweli nasikitika pale kitabu cha rambirambi kinapoandikwa mchango kuanzia $100,sasa je kama mtu ana 20 au 50 asije? jaribuni kuwa wa staarabu kidogo nadhani hiyo pesa haitafutwi namna hiyo hata watu hamtawapata kwa mipigo hiyo pia tunaomba matokeo ya michango maana tunaona kuna ujanja mwingi wabongo hatuachi asili kweli kufa kufaana

    ReplyDelete
  19. Poleni sana wafiwa. Nafikiri nilimfahamu marehemu kipindi nilipotembelea Washington lakini sina uhakika. Huyu ndiye alikuwa anakaa kwa mtanzania mwingine ambaye alikuwa kama anamsaidia kumuuguza? Hii ilikuwa kama miezi sita au zaidi iliyopita au nimekosea? Siombehi mabaya kwa yoyote ila naona kama sura na jina ni familiar. Nakumbuka huyu kijana alikuwa ni mcheshi sana. wakati nimeonana naye ilikuwa pia ni kipindi cha matatizo pia lakni ingawa huyu kijana aliongelea kuwa anaumwa alikuwa anaonyesha kuwajibika, kuwakaribisha wageni na kuwa mcheshi sana kwa wafiwa wengine...Regardless, RIP. Ni kijana mdogo sana ni pigo kwa familia lakini wanafamilia farijikeni kwani Mungu amemchagua ndugu yetu kwenda kupumzika sehemu nzuri zaidi...huko hakuna uzuni, maumivu wala magonjwa...Jina la bwana litukuzwe.

    ReplyDelete
  20. Naungana na wenzangu wote katika kutoa pole kwa wafiwa.
    Mimi nilisoma mzumbe miaka ya 94-96 A-level, sura ya marehemu sio ngeni, je huyu ni mtoto wa Mz. Msuka aliyekuwa head master wa Mzumbe miaka hiyo?

    ReplyDelete
  21. R.I.P!

    Max (Class of 92. Ilboru)

    ReplyDelete
  22. RIP Bro,

    Kila nafsi itaonja mauti, bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

    NAULIZA. Jina lake na sura ni kama namfananisha na mtoto wa headmaster wa Mzumbe, mzee Msuka. Nakumbuka kuiona hii sura miaka ya 96-98 , wadau wenye details nisaidieni. kama ndie basi, Mzee Msuka (wa Peace Corp) pole sana.

    ReplyDelete
  23. Mko sahihi kabisa..huyu ni mtoto wa kwanza wa mzee TDK Msuka, aliyekuwa Headmaster wa Mzumbe Secondary na sasa yuko pale Peacecorps. Wale wote waliosoma mzumbe secondary mida hiyo pamoja na waliosoma IDM mzumbe wakati huo watakuwa wanamfaham vizuri sana KD. Msiba uko pale nyumbani kwa mzee Msuka Mabibo, Dar es salaam na mazishi yanategemewa kufanyika weekend hii Mzumbe morogoro. lakini mipango hii yote inategemea tarehe ambayo mwili wa marehemu utaingia Dar.

    We will surely miss you brother! RIP

    ReplyDelete
  24. Pole nyingi kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa na marafiki popote pale mlipo.
    Bwana ametoa na bwana ametwaa. Mwenyeze Mungu ailaze roho ya Marehemu kaka "KADUMA THOMA MSUKA" mahali pema peponi, Amen. ROHO ZA MAREHEMU WAPATE REHEMA KWA MUNGU WAPUMZIKE KWA AMANI, AMINA.
    Njia ile ni nyembaba iendayo uzimani..... ewe kaka kaza mwendo uipite njia ileee..... nawe kijana kaza mwendo uipite njia ileeeee............
    MWENYEZI MUNGU ATUBARIKI SANA

    ReplyDelete
  25. Tunaomba updates za utaratibu uliopo hadi kumsafirisha marehemu, like schedule ya leo, kesho, etc ikoje?

    Thanks,

    ReplyDelete
  26. Pumzika kwa Amani.

    NM

    ReplyDelete
  27. Our Father......,
    Hail Mary.......,
    R.I.P Kaduma we met last year(2007) in NC.

    ReplyDelete
  28. Mungu akulaze mahali pema peponi Amen
    Oh

    ReplyDelete
  29. Poleni wandugu marafiki na jamaa. Jamani katika misiba ni utaratibu kuwa account inafunguliwa kwa familia ya marehemu au jina la marehemu. Na hii inaleta ustaarabu na heshima siyo tu hapa hata huko Tanzania. Sasa michango itawezaje kutofautishwa na activities nyingine za hii account? Inachukua muda gani kufungua account ya kuwezesha kufanikisha hii shughuli na kuwapa watu moyo wa kuchangia. Maana ni kweli kuwa hii account inaleta mashaka na michango mingi inaweza ikakosekana kwa ajili ya hali ya mashaka. Haya ni maoni ya watu zaidi ya watano nilioongea nao. Siyo kama watu hawaaminiki lakini community inavyokuwa kubwa inabidi tufanye mambo kistaarabu na siyo kilocal.

    ReplyDelete
  30. Na michango ya kwenye state nyingine itangazwe pia wamezowea kula pesa za misiba rip

    ReplyDelete
  31. POLENI SANA JAMANI - Je huyu mtoto ni wa Mzee Msuka (PEACE CORPS) kwa kweli inasikitisha sana ni kijana mdogo mno na familia yake ilikuwa inamtegemea - RIP

    ReplyDelete
  32. INALILLAH WAINA ILLAH RAJIUN.
    Simfahamu marehemu ila nainamisha kichwa kila nafsi inaporidi ilikotoka na kumtukuza mungu.
    Poleni wafiwa mungu awape subira na uvumilivu kwa uchungu mlioupata kuondokewa na kipenzi wenu. alhamdulilah rabil allamin.

    ReplyDelete
  33. Poleni sana famili ya mzee Msuka naifahamu sana familia hii ya msuka tumeishi nao mabibo maziwa kwa kweli ni watu ambao wamenisaidia sana kimawazo na ushauri. Mke wake ni mfipa jamii ya wabende Mpanda huko karema. Anawatoto wengine Rose , Rita na Robart. Mungu awape moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Mungu ametoa na yeye ametwaa Jina lake libarikiwe. Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu apumzike kwa Amani. Amina

    Hilda Pembe

    ReplyDelete
  34. Nachukua fursa hii kuishukuru kamati ya maombolezo kwa kufanikisha majukumu yake ,kamati inaongozwa na ndugu Rashidi Mkakile,Stephano Mhina na Khalfan Lyimo kamati imefanya kazi kwa jitihada za hali ya juu, pia watanzania wanoishi maeneo ya DC wameonyesha mshikamano mkubwa sana,ushirikiano wanaoendelea kuutoa hauna kifani,tunatoa shukrani za dhati,nachukua fursa hii kujaribu kuwaelewesha baadhi ya wadau waliohoji kiwango cha $ 100,sijui mdau upo nyumbani TZ au upo US,michango yote ilipokelewa bila kujali kiwango utashangaa kuona idadi ya watu wengi wamevuka kiwango kilichowekwa,kutoa ni moyo,pesa zote zilizokusanywa hakuna hata senti moja ambayo imetumika visivyo,kama upo US usisite kuiona kamati.Maandalizi ya mwisho yanafanyika,taarifa rasmi itatolewa kesho.Shukrani

    ReplyDelete
  35. Poleni wafiwa na msiba, mchumba wa marehemu na mtoto wanaitwa nani? kwani kuna jamaa wengine wanaweza kuwawanamfahamu na wangependa kumpa pole lakini hawajui kama amefiwa.

    ReplyDelete
  36. Duh Kaduma mshkaji!anyway kama Mungu amependa ndio basi tena tangulia tu!tutafanyaje sasa?

    Rest in Peace Brother.

    ReplyDelete
  37. Michuzi hapa DC wabongo sijui vipi, mara wamejichagua macelebrity wakakutana Safari Club kwa ajili ya harambee wakati wengine habari hatuna. Huyu mtanzania mwenzangu jamani hata kama simjui tujulishane, you never know kesho itakuwa ishu yangu hii na nitahitaji msaada.

    ReplyDelete
  38. Poleni jamaani kwa msiba kwa watu waliobahatika kumjua Kaduma watawasifu wazee wake na familia yake kwa kumlea vyema na kumfanya kuwa mtu wa watu toka kule Iliboru kwenda Minaki baadaye IDM ni kijana aliyekuwa hana makuu. Ni mmoja wa watu wa kwanza kuwa wanapenda RAP kwenye mwanzo wa miaka ya 90 na alikuwa always anawapenda ile time ya Washington REDSKIN. Unakumbuka hili wewe mtu mfupi Mwanyoka, Stephen na Brown bila kumsahau mzee wa mijadala Otieno ni pigo kubwa sana ambalo hatuwezi kuziba lakini tunaweza kujifuza kuwa watu wazuri zaidi bila kujali familia tulizotoka kama mnakumbuka wale waliokuwa kwenye class ya vigogo na wakulima tuliweza kuchanganyana bila shida hata zile heater za vitanda tulitumia kuanzia pale Ujamaa to Makangoro tu Mirambo kwa mabishano zaidi hizi zote sasa ni story mwezetu katangulia bila kusahau upenzi wake waa Basketi ball na hapo hapo kupiga PCB na kwenda PUGU kwa biology na sisi siku moja tutamuunga huko. Wazee poleni, Mchumba pole mno maana Kaduma alikuwa mtu wa Vision sana hope nimekuwa dash lakini ni Imani yangu kuwa Mungu atakusaidia, Mtoto pole mno mambo mazuri ya ndugu Kaduma. Poleni Sana na Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  39. Taarifa ya fund raising Safari club ilikuwa wazi mdau kama upo dc na hukupata taarifa samahani sana hakukuwa na suala la ucelebrity inawezekena kabisa labda si mtu wa kujichanganya,mwili wa marehemu tutauga jumamosi kuanzia saa tisa tutatoa taarifa rasmi,leo baada ya kamati kukutana na familia.

    ReplyDelete
  40. Rest in peace Kaduma Mungu akulaze mahali pema peponi.Maisha ni mafupi ila maisha ya binadamu ni kama maua.Kwa familia yake tunawaweka kwenye maombi mwenyenzi Mungu awape nguvu na awatulize roho zenu, na awa fute machozi.Uchungu mnao hakuna yeyote anayeweza kusema anaelewa ni Maulana pekee anaye jua.Mwenyenzi Mungu awahifadhi na awape imani na ukakamavu.Tuko pamoja na nanyi.

    ReplyDelete
  41. Natoa pole kwa wafiwa. Inabidi tubadilike tunapopatwa na tatizo tujifunze jinsi ya kukabili yanayo fuata. Nyinyi wabeba boxi hatutaki aibu huko mliko. Anzisheni vyama vya kufa na kuzikana ili mtu akifa huko mununue tickect na kumleta nyumbani kuliko kuanza kukamatana wakati wa shida kwani siku hiyo usipopata box la kubeba marehemu hataletwa Tz. Kwa wale ambao hamuwezi kuchangia mifuko hiyo rudini nyumbani haraka kuna mashamba mtalima na mkifa huku hatutakuwa na gharama za kuchangishana. Pesa ya kumleta mbeba box ni mtaji mkubwa sana kwa shughuli za kimachinga. Pesa yote hiyo Masawe wamepoteza kwa kumsafirisha maerehu tuu-naitamani na amekufa kabla ya kulipa deni langu kweli.
    Pili tuwe wawazi nini kimemuua marehemu. Kuna mtu amesema ugonjwa uliomuua ni INIi. Kama ni kwelii hivi marehemu alikuwa anakunywa gongo? . Ni bora tujue ili watu wengine waache tabia ya kunywa gongo kwa kuangalia mfano wa marehemu. Vilevile kama ni ukimwi ni bora tuseme ili watu waache ngono uzembe kwa kuangalia makosa ya marehemu. Dawa ya jipu ni kilipasua. Nimemaliza na sitaki malumbano message sent and delivered.

    ReplyDelete
  42. REST IN PEACE THOMAS KADUMA.
    STAFFORD(ILBORU 92/94).

    ReplyDelete
  43. Mimi nakuunga mkono hapo juu ni kweli inabidi tuwe wakweli ili tuweze kusaidiana, kama wanavyosema marehemu alikua anaumwa ini ni sababu gani ilisababisha matatizo yake ya ini? kwani kwakuambiana ukweli inaiweka jamii yyetu katika hali ya uangalifu na nini cha kufanya kwa watu wengine ilikujikinga na matatizo kama hayo na hata kama ni AIDS pia ni vizuri kusema kwani siku hizi hata kama ni HIV positive hiyo siyo death sentence lakini ukijua mtu uliyekuwa inajiusisha naye kimapenzi mape kufa kwaajili hiyo ni raisi wewe kwenda kupima na kuanza matibabu napia kuto ambukiza wengine bila kujua, naamini hii jamii ya watanzania hapa marekani wengi ni waerevu na wana upeo wa kimawazo kwa hiyo basi shime naomba tuelimishane.

    ReplyDelete
  44. Michuzi !!! naomba niwaelimishe hao wanaojiita wanakamati .wawe na ustarabu kidogo , maana akiingia mtu wakijua kama jina lako halimo kwenye orodha ya waliotoa michango!! kabla hata ujakaa chini kuwapa pole wafiwa, unaona kitabu cha michango kipo usoni kwako..huku ukishindikizwa na maneno , dolaa miaaaaa!!!.."hee!! jamani subiri kwanza basi nifute hata hayo machozi "

    ReplyDelete
  45. POLE KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI.M'MUNGU AWAPE MOYO WA SUBIRA KATIKA WAKATI MGUMU KAMA HUU.
    ANON WA 5:36am UMETUMIA LUGHA KWA MAONI YANGU MIMI NAFIKIRI IT'S NOT APPROPRIATE,NI KWELI NI ISSUES AMBAZO ZINAHITAJI KUZUNGUMZIWA,LAKINI UNGESUBIRI WAFIWA WAKAMALIZA MSIBA WAO KWANZA HALAFU UKA MAIL KWA MICHUZI HILO DONGE LAKO AKAKUTUNDIKIA,WATU WAJADILI.
    M'MUNGU HUTUPA MSIBA KUSHTUA ROHO ZETU,BINADAMU HUJISAHAU,TUKAANZA KUFANYA MAMBO KAMA TUPENDAVYO KIFO HUTUFANYA WATU TUSIMAME TUFIKIRI NINI TUMEFANYA,NINI TUNAFANYA NA NINI TUTAFANYA ILI TUSIWE KATIKA WATU WA MOTONI, SASA KUANZA KUULIZA WATU MAREHEMU KAFA NA NINI AU KAMA SABABU NI INI ALIKUA AKINYWA GONGO? IT'S VERY INSENSITIVE,WAPENI WATU BREAK WAMLILIE MTOTO WAO,KAKA YAO,BABA YAO,RAFIKI YAO IT'S BEEN ONLY 7 DAYS SINCE HIS PASSING,HAYA MENGINE ULIZENI BAADAE.NAFIKIRI HUJAPATA KUFIWA,KAMA UMEFIWA QUESTIONS AND ANSWERS ABOUT WHAT KILLED YOUR LOVED ONE IS NOT A PRIORITY.
    Hutaki malumbano but your message was read,replied and now it's been sent back to you insensitive git.

    ReplyDelete
  46. Wewe anonymous uliyeuliza kwa kashfa na kejeli kubwa ugonjwa uliomuua marehemu umesababishwa na nini,,, kweli umenishangaza na kunikumbusha kuwa katika hii dunia kuna watu na vijitu. U'r such a shameless human being who doesn't care just for a moment and keep your stupid curiosity aside for the time being!! who are u to Kaduma and his family?? U'r nothing so kinakuwasha nini hata kama kafa na ngoma??? kitakusaidia nini kujua kwamba alikuwa anaagiza gongo kutoka huko madongo kuinama TZ anakunywa??? what is bothering you man?ehee, u such a s--n of B. to me, to write such a stupid comment in this situation! Shame on you, and I hope U'll live forever if not,I hope U'll learn b4 u get out of this world( if u'll ever get a chance to learn)
    Just remember to wash u'r mouth and brain b4 u start a new day!

    ReplyDelete
  47. watu wengine wana upeo mdogo kimawazo unashangaa watu kubeba box hebu nenda kipunguni uone watu wavyobebe box sasa ni ajabu gani sisi hapa US tukibeba box?isitoshe tunalipwa dola ndio maana tumeweza kupata fedha zote hizo,ndugu acha hasira za maisha nadhani unatamani kuja mtoni basi tu,lingine nataka kukuhakikishia hakuna mtu hapa DC atayezikwa hapa labda kama ametaka,box linalipa huku, nimesahau kidogo tunao maprofesa madokta na watu wa profession mbali mbali hapa DC,MICHUZI tafuta safari ya DC mzushi aone.RIP Kaduma

    ReplyDelete
  48. Mwili wa marehemu Kaduma utaingia Dar ijumaa saa nne na nusu usiku(10:30p)
    march 21st 08

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...