mbunge wa kigoma mjini mh. peter shelukamba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya mawasiliano ya bunge akiongea na waandishi wa detsche welle walipotembelea juzi wakiwa katika ziara ya mafunzo hapa ujerumani juu ya namna ya kuanzisha postal code bongo.
mh. shelukamba alisema katika kikao hiki kifupi kwamba tumr ya mawasiliano imepania kuliimarisha shirika la posta kwa kuanzisha, pamoja na mambo mengine kibao, mfumo wa 'postal code' ambapo halmashauri zitalazimika kuwa n majina ya mitaa na namba za nyumba kila sehemu bongo ambapo itarahisisha sio tu usambazaji wa barua bali pia utoaji wa huduma mbalimbali tofauti na ilivyo sasa ambapo bado tu watu wanafuata barua ama vifurushi posta.
na ukimtaka mtu kama kule kwangu uswazi ni balaa. alisisitiza pia kuanza kwa zoezi la kumpatia kila mmbongo kitambulisho cha uraia kitasaidia kufanikisha maswala ya kimaendeleo kama hayo. wadau hii imekaaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. POST CODE??? itabidi nyumba zote tabata,sinza,nusu ya manzese na mwananyamala ivunjwe,huyu anajua anachoongea?

    ReplyDelete
  2. NA UAMINIFU PIA UNATAKIWA MAANA HUKO BONGO UKIJARIBU KUTUMA KITU KUTOKA UK AU NCHI NYENGINE YOYOTE ILE ZA UGHAIBUNI BASI IKIFIKA SHUKURU NA PIA UKITUM LEO HESABU MWEZI NDIO KIMFIKIA MTU LKN MTU AKITUMA MZIGO KUTOKA BONGO KUJA HUKU UK KAMA NI MONDAY BASI FRIDAY UNAUPATA.

    ReplyDelete
  3. Hii programme ni nzuri.

    Hata hivyo naona kuna tatizo hapa kwani kama tabia ya mipango mingi ya nchi yetu ni ya kuzima moto au kutatua tatizo moja moja. Hapa watu wa mipango miji wanahitajika kuhusika na kuona ni jinsi gani nyumba zote zinafikika kwa urahisi. Nina wasiwasi kua bila ya kuangalia mpango wa makazi na kuufanya uendane na program hii itakua ni sawa na watu wa barabara wanajenga barabara bila kuwasiliana na idara ya maji, then baada ya barabara kujengwa ndo utawaona watu wa maji wanabomoa vipande vya barabara kupitisha mabomba yao.

    Kwanini hatujifunzi kwa makosa?

    Ignorant,
    Jeremani

    ReplyDelete
  4. aisee mwambie atulize kitambi chini tutakuja tu posta kuchukua hizo barua, msambaze barua nyumbani itafika mwaka gani? bado sana hiyo kitu bongo, wekeni numba kila nyumba lakini barua tutaijia posta

    ReplyDelete
  5. Namuunga mkono anonymous wa kwanza hapo juu. Huyu jamaa hajui anachoongea. Nilikaa Temeke wakati nikisoma mlimani na hali bado haijabadilika tena inazidi kuwa mbaya. Unless kama serikali ina pesa za kuvunja nyumba zote zilizojengwa shaghalabaghala na kuzijenga upya kufuata hiyo misimbo? (codes) anazozisema basi hakuna kitu.

    Anonymous wa pili. Nilituma dawa (kwa FEDEX)za mama aliyekuwa mgonjwa wala hazikufika. Jamaa wanaiba mpaka dawa za mgonjwa pamoja na kwamba niliandika ki-meseji kabisa na kukizungushia kifurushi kizima kusema kwamba hizi ni dawa za mgonjwa na anazihitaji haraka. Hatari sana!

    ReplyDelete
  6. Muhidin,

    Kweli picha moja tafsiri elfu moja! Nimeitazama hii picha nikacheka. Muheshimiwa Shelukamba anatoa somo jamaa mmoja kashika tama akimsikiliza na mwingine kashika tama akiangalia nje. Mama kakunja mikono halafu tama limeangukia kifuani.

    Hao anaowahutubia au siju kuwahubiria wanaijua nyanja ya mawasiliano kwa utalaam na uzoefu. Utaalam na uzoefu wao wa nyumbani na ughaibuni wanajua nini kinawezekana na kisichowezekana nyumbani katika nyanja ya mawasiliano. Wanajua nini hoja na nini porojo katika anayowahutubia au kuwahubiria juu ya kuboresha nyanja ya mawasiliano Tanzania.

    Shirika la Posta (TTCL) kwa lilivyo sasa hayo anayosema Muheshimiwa Mbunge ni porojo na wala si hoja wala sera wala mkakati. Ushauri wangu ni kwamba waheshimiwa wakija ughaibuni wakumbuke kwamba wanakutana na "wabeba maboksi smart" Kwa hiyo waangalie sana kauli zao.

    Kila la heri.

    ReplyDelete
  7. Seluuu kiboko ya Kaburu..!! ndani ya Bonn, kaaazi kweli kweli. Anatitwa Selukamba sio Shelukamba

    ReplyDelete
  8. Mh Mbunge, hizo postal code labda zianzie Ujiji Kigoma ambapo kuna mtaa mmoja tu. Lakini jiji kama la Mwanza, DSM, Mbeya n.k itakuwa kazi kubwa. Kwani mfanyakazi wa posta itabidi ajue vichochoro vyote vya miji hiyo kwani hakuna mitaa.
    Pia itabidi waajiriwa wa posta wawenawekwa maeneo ya vichochoro vyao ili kufanikisha zoezi hilo. Huyo mfanyakazi mwenyeji akiumwa au akipata udhuru basi atakayemshikia nafasi yake kama ni mgeni, barua siku, wiki, miezi hiyo hazitafikishwa majumbani.
    Mh.Mbunge hiyo ndoto ni kazi kuitimiza.

    ReplyDelete
  9. damn Serukamba unakula nini wewe siku hizi? umechana ile mbaya inabidi uanze mazoezi sasa,tulipokuwa IFM hukuwa hivyo...mazoezi sasa sio beer tuu na nyama za mbuzi dodoma
    Mdau USA

    ReplyDelete
  10. Huu mtizamo hasi uliotutawala ndio unaotunyima maendeleo. Utasemaje eti hii kitu haiwezekaniki? Kama bongo tumeweza kulipia bili za maji bila kupata maji,bili za juu za umeme bila kupata umeme wa uhakika,watu kujenga nyumba huku cement ikiwa bei juu(waziri kabariki ipande bei toka 11600 hadi sh.12400 bei ya viwandani,mtaani itafika 20,000 pengine!) hili litashindikana vipi? Kama kutuma mzigo kwa ems unafika within 3 working days. Ukiibiwa unaweza kuidai posta na wakakurudishia,hata mie kesi kama hiyo ilinitokea na nikalipwa changu.
    Mambo haya ni ya kufurahia sio mnapondea kila kitu

    ReplyDelete
  11. We Michuzi mbona umempa jina la kisambaa huyo Muha? Ni Serukamba na si Shelukamba. Manake nilivyomuona nikasema iso Serukamba huyu mara hii ameshakuwa Msambaa. Mwe Ubunge mzuri amenenepa mpaka amebadilika.

    ReplyDelete
  12. We Michuzi mbona umempa jina la kisambaa huyo Muha? Ni Serukamba na si Shelukamba. Manake nilivyomuona nikasema iso Serukamba huyu mara hii ameshakuwa Msambaa. Mwe Ubunge mzuri amenenepa mpaka amebadilika.

    ReplyDelete
  13. MHESHIMIWA SELUKAMBA SI UNASOMA HII BLOG? BASI TAFADHALI WAAMBIE POSTA VIFURUSHI ZAWADI KWA NDUGU NA WAZAZI WETU, VIKIWEMO VITABU, NGUO, VIATU, DAWA ZA WAZAZI WASITOZE KODI KWANI NI ZAWADI!!!. TENA HASA KODI AMBAZO ZIMEZIDI THAMANI. FIKIRIA MHESHIMIWA, WEWE UKO PALE IFM, MIMI NANUNUA KITABU EURO 50 NAKUTUMIA USOME, WEWE UNAFIKA PALE WANAKULIPISHA 50,000/=, YA NINI?

    INAUMA!

    ReplyDelete
  14. Michu kwenda Ujerumani ndio unasahau hata majina ya watu? Tangu lini Kigoma kuna Shelu

    ReplyDelete
  15. HUYU JAMAA AFAI KABISA, MBUNGE MTETEZI WA MAFISADI. LAZIMA NIMFANYIE KITU MBAYA. ANA FAIDA KWETU WANACHI WA TANZANIA. MWEU MKUBWA HUYO. MICHU UKIITOA HII COMMENT, LAZIMA NIKUPIGE PASTOLA SIKU UKIRUDI

    ReplyDelete
  16. Hiyo mikono Hapo Shelukamba alikuwa akiomba Dua SENTI ZIPATIKANE,si unajua tena mzee we are underdeveloped.Kuna jamaa mmoja alikuwa anawasilisha mada katika mkutano mmoja wa kimataifa.Mwenzake mmoja kutoka nchi moja jirani ya kiafrika akaliona neno 'developing countries' katika kuielezea hali ya Tanzania.Mwenziwe haraka haraka akamboyeza,wewe,wewe, badilisha hilo neno 'developing' weka 'UNDERDEVELOPED COUNTRY'.Vinginevyo hatupati kitu hapa tutaondoka watupu,hela zote zitakwenda Bangladesh na Benin.Jamaa haraka haraka akabadilisha.Nasikia walichota michuzi mingi sana.Come 2080 Tanzania will still be an underdeveloped country,mpaka line ya michuzi ikatwe,upo hapo mshikaji!

    ReplyDelete
  17. Huyu jamaa ndio kiboko ya WALID KABOUR!

    ReplyDelete
  18. watanzania tutabaki nyuma kila siku, mtu amekwenda kujifunza wenzetu iliwezekanaje wakafika hapo walipo, watu wanasagia!! tutabaki hivi hivi kila siku, ooh hajui anachoongea!!! inavunja moyo kwa kweli ndo mana watu wengine wanaamua kujichotea, wanawaacheni hivyo hivyo, maana hamna shukrani! Mtu hata awafanyie nini, hakuna mnachoridhika nacho!!
    watanzania tubadilike.
    haswa hao waliozamia kwy nchi za watu ndo weeeee, wao ndo wanajua kila kitu, c mrudi basi mfanye nyie, kazi kuponda tu wenzenu.

    ReplyDelete
  19. As with all other policies and strategies we acquire in
    TZ, COPY AND PASTE NEVER WORK!

    Hii haiwezekani!

    Thanks.

    ReplyDelete
  20. Ni kweli P.Serukamba anaongea tu maneno then arudi Tanzania baada ya porojo akaeleze alivyofurahia safari na ni kiasi gani ame-make.

    1.Hii ni kitu technical sana, na sio suala la kisiasa. Peter ni accountant na sio mtaalam wa mawasiliano.
    2.Hili ni suala lililopaswa kuongelewa na specialists wa field hii na sio ujinga huu wa kubishana tuu for the sake of ubishi.
    3. Badala ya kutafuta maoni Bonn, kwa nini wasingekwenda na model ya hicho wanachokitaka, yaani wawe wamejaribu mf. kinondoni au arusha au dodoma, kwa hiyo waseme kwamba wanaona jinsi hii project itakavyofanikiwa.Otherwise ni bullshit!
    Hivyo suala hapa si Peter kutaka maoni au kutueleza maoni ya wanachotaka kufanya TZ, jamani porojo tuu hadi lini. Kwanza siamini kama Peter au hata baadhi ya wanaosema haiwezekani, pamoja na ujumbe wa Peter wanaelewa jinsi hii kitu inavyofanya kazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...