Jk akingalia vitalu vya zao la pilipili aina ya paprica kwenye shamba la vikundi vya wananchi wa kijiji cha Hoyoyo katika wilaya ya Mkulanga,Mkoa wa Pwani jana. Jk aliwasisitizia wanakijiji hao kulima kwa wingi zao hilo ambalo lina soko zuri nchini Hispania ili liwe mkombozi wa kuinua hali zao zamaisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Naona JK kaamua kumuunga Mama Salma ziara za kipande hicho. Vipip lakini Mkweo hajambo?
    Jitahidini bwana kuinua nchi sio ziara tu na kufanya kwa maneno badala ya vitendo.
    Kila la heri.

    ReplyDelete
  2. Samahani sana wanablogu najua labda kuna watakoudhika lakini nimevumilia hadi nimeshindwa, hivyo naomba kuuliza. Hivi mama yetu huwa ahisi joto? Maana kila wakati huwa amejitundika miguo mingi sana na mizito mno nikizingatia hali ya hewa ilivyo nchini mwetu.

    ReplyDelete
  3. wewe, kama huwezi kujifunza kiswahili fungu hii blog bwana utaandikaje Mkulanga?????ni MKURANGA kaka

    ReplyDelete
  4. zao la paprica linalipa sana ktk nchi za nje,hasa nje ya africa.
    kama tanzania ingezingatia uwekezaji ktk sekta ya kilimo,ikandaa miundombinu yakuaminika ktk kilimo haswa cha umwagiliaji.ikaepuka kuagiza hata vyakula kutoka nje baadhi ya nyakati,nabadala yake ndio iuze nje, wananchi wasio na kazi za offisini wengi wange jinusuru kupitia kilimo.maana nguvu kazi ipo tena yakutosha tu!machangu,vibaka,wazururaji,na irresponsible parents wange kuwa wanakamatwa na kupelekwa huko kama ilivyokuwa JKT,lakini wakimaliza kutumikia wanakabidhiwa walichozalisha na tayari inakuwa ni mtaji na mfano wa kuonyesha pia kuwa endapo watawekeza nguvuzao kwa hiari ktk shughuli hiyo[mazingira yakiwa yanaridhisha] basi inalipa.
    napia hataelimu fulanfulani zingeweza kutolewa ktk kambihizo na kuwa affect watu positively. nchi nyingine wana msimu mfupi sana wakulima kutokana na haliyahewa kuwa barafu kwa robotatu ya mwaka.lakini njaa kwao ni ndoto!nikweli kuwa technologia yao nikubwa hatujilinganishi nao lakini nasisi muda umefika tuanze na tunalo weza!

    ReplyDelete
  5. haya wasomi wetu wa kilimo na agro-mechanics pamoja na mechanical engineering mnasubiri nini kubuni na kuzalisha zana na kuwasaidia hawa? au ni jembe la mkono na plau tu!hahahaaa!
    msiniambie habari za ghara za kuvizalisha, wenzenu walio endelea wangewaza gharama wasinge anzia waliko anzia wakafika walipo sasa!
    acheni uzembe wa kufikiri mnaishia kujua ku solve mahesabu vitabuni tu na physics za nadharia za kina newton, lakini kufanya ziwe applicable ktk mazingira yetu hamuwezi nyambafff! mnacho hitaji nini? wafadhili sio?hahaaaa ,je wao nani aliwafadhili wakafika huko?
    mtaji wenu ni huu hapa:-
    1.ujuzi mlionao wa theory na practicals.
    2.malighafi zilizomo ardhini.
    haya tuanze kazi[rigwaride] acheni kuleta kiswahili kirefu mara mmmhh unajua tunahitaji heavy plants,wafadhiliiii!!!
    engineering ya tanzania hovyoooooo[sio wote lakini]!nyambafff!

    ReplyDelete
  6. kilimo juu!ndio uti wa mgongo wa taifa letu!?what?unabisha.
    nchi yetu sio maskini wa mali, bali ni maskini wa kufikiri, na ikitokea akapatikana mtu anaye fikiri basi atadunishwa hadi adumae. atashambuliwa na kupingwa vikali maana watu wanataka kula vilivyo tengamaa mezani!
    mi yangu macho,ooh shule zawenye vipaji maalum[mzumbe, ilboru] nakubali lakini vipaji hivyo je nivya kufikiri ideas na kuzifanya real au ndo yaleyale ya kukariri facts usiku mzima hadi wanatoboa?
    haya serikali anzisheni basi sehemu ya kufadhili idea zinazoweza kuwa realised!!
    njooni muone nchi zawatu,vyuo vikuu vinaongoza kwa kuendesha research halisi na kurealise dreams za vijana wenye vipaji! lakini vya kwetu kazi kukusanya data na kuwatumia nje kisha wanazitumia kuwaponda baada ya kuwa wamewapa chenu.
    leo nilikuwa nasoma habari, eti kilasiku africa watoto milioni tatu[3,000,000] wanakufa kwa malaria, na watu milioni saba[7,000,000] wanakufa daily kwa HIV. je kwa haraka tu hayo we unayaona ya kweli?mtoto huzaliwa baada ya 9 months,inamaana hadi hapo watakuwa wamekufa watu [3,000,000x270]+[7,000,000x270]=milioni 250.
    africa nadhani ina nchi 52, tuki asume kila inchi inawatu milioni 20 tunapata almost 1040[wakiwemo wato wasitayari kwa umri wakuzaa, na wazee waliovuka umri huo, je kwa miaka mitano tu 250x5=1250 watakuwa wamekufa, je africa ingekuwepo kweli?
    tuamkeni jamani tufikiri tuanze kufanya vituvyetu wenyewe tuache kubezwa kwa maradhi,umaskini, na ujinga.
    eti tanzania inaongoza kwa ukimwi, na kwa mara yakwanza nikashangaa kusikia eti ugongwa wa kaswende[syphilis] ulianzia tanzania toka kwa nyani!hapa patamu!
    yaani mngelijuwa picha wazungu waliyo nayo kuhusu tanzania kama wakivua nishai waka kwambia utachoka! nyingine hii, eti tanzania chanjo a polio anachanjwa mtoto mmoja ktk familia ilikubana matumizi, kisha kwa kuwa hali ya usafi yaani vyoo hakuna anajisaidia hovyo, nawengine wote wanapata zile weakened strain za wadudu wa polio na wanapata kinga! je hapo mpo wa Tz?ka!!eti kuna buibui wakubwa kama zile beatle[vikobe],na mamba wanatembea mjini!
    msije mkaona watalii wanakuja huko mkadhani wakuja kuona nini! na wamasai wawatu mmewafanya kionyesho!ka!
    mi yangu majicho!!wakati kwao ukitaka kupiga picha ombaomba unaweza ishia jela au kufukuzwa nchini.wakati nyie kwanza ndo mnakusanya familia yote watoto vifua nje matumbo makubwa na kamasi mnapigwa picha, naziona huku!kujisifia oooh sie maskini tupeni misaada!makubwa haya!

    ReplyDelete
  7. Track-suit na shati la drafti... Wapi na wapi?

    ReplyDelete
  8. Waspanish hawawezi nunua bongo wakati majirani zao wa portugese wanazlisha zao hilo hilo tena masaa machache tu wanaingiza Spain.

    ReplyDelete
  9. Huyu jamaa hakai ofisini! Khaaaaah!!

    ReplyDelete
  10. We kipofu hapo juu..hiyo sio track suit ni jiti linasupport hilo zao la paprica...

    ReplyDelete
  11. Hey!!! Anon hapo juu!!
    Unamatatizo ya macho? Kuna track-suit hapo!!
    Wabongo mnachoniacha hoi..nikujua kukosoa tu...na mnajitahidi kutafuta makosa kila siku kwa watu.

    Jitahidi kuwa 'postive', kutoa hongera kwa vitu vya maana na siyo kupenda kuangalia penye kasoro tu maana matokeo yake ndiyo haya ya kukosoa hata vitu ambavyo havipo.

    Hiyo ni 'darkbleu trouser' hicho kilichokufanya uiite 'tack-suit' ni huo mti iliosimikwa na kuonekana kama msitari kwenye suluali hiyo. Na kwasababu ya utafuta kwenye makosa tu ndiyo maana utang'ang'ana kuwa ni 'track-suit'.

    ReplyDelete
  12. Mimi nadhani tatizo kubwa la umasikini linachangiwa kwa kiasi kikubwa na sisi wananchi wenyewe. Kwa sasa kilimo kinalipa sana, mfano mzuri ni kupanda kwa bei za mazao mwaka hadi mwaka na kinachowanyima ubora wa maisha wananchi wengi wa vijijini ni ukosefu wa umeme. Nasema wananchi tunajitafutia umasikini kwa sababu kwa sasa vijana wengi wanakimbilia mijini kwa kudhani kwamba huko ndiko kila kitu na kuwaacha wazee vijijini, athari zake ni kwamba watu wenye pesa wanaenda vijjini kununua ardhi kutoka kwa wazee kwa bei nafuu na hawa wazee wanasahau kwamba wana watoto wanahitaji ardhi na ardhi sasa ni bidhaa adimu kuliko kitu chochote Tanzania. Hawa vijana wanaokimbilia mijini wanaishia kuwa wamachinga, wezi, machanguduoa n.k. Watanzani tufikiri mbali tusifikiri ya leo na kesho tu, ardhi inayouzwa kiholela na wanavijiji na kuwasahau watoto wao wanaokimbilia mijini itakuja kusababisha yanayotokea kenya kwa sasa. Vijana tufiriri mbele

    ReplyDelete
  13. Tanzania bwana!,kweli mnyonge mnyonge tu aisee.
    Yaani sisi tuendelee kulima Paprika,Nyeye mwaendelea kulima Dhahabu,haya ndo-kuhimiza maendeleo tena huko!!

    ReplyDelete
  14. nakubaliana na kilimo kamanjia pekee iliyo wazi ya kumkomboa mtanzania,lakini sio kilimo cha staili hii.
    anzisheni pia na viwanda vidogovidogo vya kusindika baadhi ya vyakula yakiwemo matunda, kisha viuzwe ndani na nje ya tanzania.
    hamuoni msauzi alivyo mjanja?ana wekeza bongo kakiwanda, analeta mazao anayozalisha kwake,nafasi za juu kiwandani anawapa watu wake,soko unampatia wewe kwa kununua product alizozalisha hapo.[juice,kuku,nk ktk shoprite zake] kisha anakulipa tax baada ya kupata faida kwanza!
    je nasisi serikali si iwawezeshe watu[maana tuna promote capitalism] kwa njia ya morgages ili waproduce juices na kuziuza hapo ikiwezekana na nje kwa jirani zetu maana itakuwa dili, na tax walipe kama msauzi ila faida ibaki hapo?
    nimtizamo tu!subiri dhahabu ziishe ardhini tuone forex zitatoka wapi. soko la ndani na kilimo vipeni umuhimu vinginevyo hatufiki mbali!bepari ni rafiki yako wakati ukiwa tu na kile anachotaka, kikimalizika hamjuani,kafe kivyako!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...