Mbali na kuwa na utajiri wa asili wa aina yake,Tanzania ni nchi ambayo inajivunia kuwa na wasomi maarufu ambao wametapakaa kote ulimwenguni wakifundisha katika mashule na vyuo mbalimbali au kuongoza vitengo nyeti katika idara za kimataifa na zenye uzito wa ki-dunia nzima.

Miongoni mwa wasomi hao ni Prof. Joseph Mbele (pichani), Mtanzania anayefundisha katika Chuo cha St. Olaf kilichopo Northfield jimboni Minnesotta, nchini Marekani.


Miongoni mwa wasomi na wafuatiliaji wa mambo mbalimbali ya kitaaluma jina la Prof. Mbele sio geni hata kidogo. Yeye ni mtunzi wa kitabu maarufu sana kiitwacho ''Africans and Americans:Embracing The Cultural Differences''.


Kitabu hicho ndicho kinachotumika zaidi hivi leo mashuleni na katika taasisi mbalimbali(zikiwemo balozi mbalimbali) wanapokuwa wanawaandaa watu wao kuja kusoma, kutembea tu, kufanya kazi au tafiti mbalimbali barani Afrika.
Mengine mengi zaidi ya msomi huyu nenda www.bongocelebrity.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hivi maprofesa Marekani huwa hawachani nywele wala kunyoa ndevu?

    ReplyDelete
  2. Hivi maprofesa Marekani huwa hawachani nywele wala kunyoa ndevu?

    ReplyDelete
  3. Yafuatayo ni mahojiano ya Profesa Mbele na BONGO CELEBRITY (BC)
    yasomwe kwa manufaa ya wana blog maana yana uzito mkubwa.

    BC: Kumekuwepo na mijadala mbalimbali kuhusiana na suala la mila,tamaduni na desturi za mtanzania.Kuna ambao wanasema hakuna kitu kama mila,utamaduni na desturi za kitanzania ingawa wanakubali kwamba inawezekana kukawa na mila,tamaduni na desturi za makabila fulani fulani. Nini maoni yako kuhusu dhana kama hizi? Unadhani kuna mila,tamaduni na desturi zinazoweza kuitwa “za kitanzania”?



    PROF.MBELE: Pamoja na tofauti zote baina ya makabila,kuna pia mambo ya msingi ambayo yamo miongoni mwetu sote. Mifano ni kama kuheshimu wazee, kupenda kuwa na watoto, kushirikiana kwenye shughuli kama mazishi na sherehe. Mambo hayo yamo miongoni mwa Waafrika kwa ujumla. Kuna mengine ambayo tunaweza kusema ni ya kiTanzania. Kwa mfano, Mtanzania ana utamaduni wa kutotilia maanani ukabila katika mahusiano na Watanzania wengine. Anazingatia utaifa kwanza. Huu ni utamaduni wa Mtanzania. Lugha ni nguzo muhimu ya utamaduni, na Mtanzania anathibitisha kuwepo kwa huu utamaduni wa kiTanzania kwa kuongea kiSwahili anapokuwa na Watanzania wa makabila mengine. Kwa kiasi kikubwa, hayo ni matokeo ya juhudi ya Mwalimu Nyerere.



    BC: Vijana wengi wa hivi leo wanapenda(pengine hata kuabudu) tamaduni za kimarekani.Hii sio kwa vijana wa kitanzania peke yao bali dunia nzima.Unadhani hii inatokana na nini? Nini faida au madhara ya mapokeo haya ya tamaduni za kigeni au kimarekani?



    PROF.MBELE: Hao watu wanaoiga namna hiyo wana matatizo.Tatizo moja ni kuwa wanayoiga ni yale yenye mushkeli hata huko Marekani kwenyewe. Marekani, kama sehemu yoyote duniani, ina watu wanaokiuka maadili ya jamii. Vijana wetu wanaiga mambo hayo yenye walakini, iwe ni katika mitindo, lugha, na kadhalika.


    Kwa mfano,badala ya kujifunza kiIngereza sanifu, ambacho kingewawezesha kusonga mbele kielimu na kimaisha, vijana wetu wanaiga kiingereza kibovu na cha matusi ambacho wanakisikia kutoka kwa baadhi ya wanamuziki wa kiMarekani.Vijana wetu wanaiga mitindo ambayo hata huku Marekani inawabughudhi wengi. Kuna miji hapa Marekani imeshaanza kupiga marufuku aina ya mavazi wanayoiga hao vijana wetu.


    Filamu nyingi za Hollywood zinawapotosha watu.Wanadhani mambo ya Hollywood ndio hali halisi ya Marekani. Hollywood kwa ujumla inapotosha ukweli wa Marekani, kama vile inavyopotosha ukweli kuhusu Arabuni, Afrika, Asia, na kwingineko.Hollywood au inatia chumvi au inadhalilisha. Hollywood inatafuta biashara, sio kuelimisha watu, na hata kama kinachouzwa ni pofotu, wao wanauza tu. Ukweli ni kuwa Wamarekani kwa

    ujumla ni watu wenye heshima zao, kwa mujibu wa utamaduni wao, kama ilivyo katika nchi nyingine yoyote, na wanavaa na kutumia lugha ya kawaida na ya heshima kama vile wanavyofanya Watanzania walio wengi.



    BC: Utamaduni wa “kimarekani” ambao kila kukicha unazidi kuenea dunia nzima sio jambo linalotokea kama ajali.Ni mipango madhubuti ya kiserikali ya Marekani katika kuhakikisha inaendelea kuwa “super power’ wa dunia. Je unakubaliana na dhana hii? Kama ndio,unadhani serikali za nchi kama yetu ya Tanzania ina wajibu gani katika sio tu kujaribu kukabiliana na hali hii bali pia kuhakikisha mila,tamaduni na desturi za kitanzania zinalindwa,kutunzwa na kuheshimiwa?



    PROF.MBELE: Kinachoenea duniani kutoka Marekani ni utamaduni wa kibepari, ambao unageuza kila kitu kuwa bidhaa, kama alivyotueleza Karl Marx kwenye kitabu chake cha Communist Manifesto. Mabepari wanasambaza mitindo na vishawishi, ili kuwafanya watu wapende kununua bidhaa au huduma mbali mbali hata kama hazina maana katika maisha. Wao wanatafuta pesa. Wamarekani wa kawaida hawana uwezo wa kufanya hayo yote, wala hawahusiki.


    Serikali ya Marekani ni mshiriki na pia wakala wa hao mabepari, na inachofanya ni kuweka mazingira ya kuuwezesha ubepari kustawi duniani kote.Serikali ya Marekani inazishinikiza nchi kama yetu ziweke mazingira muafaka ya kuuwezesha ubepari kufaidika, pamoja na kwamba wananchi walio wengi wanaathirika. Serikali ya nchi kama Tanzania ingepaswa kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala hayo, kama alivyokuwa anafanya Mwalimu Nyerere.


    Lakini, leo tumekwama;viongozi wenyewe sidhani kama wana upeo unaohitajika,wala dhamira inayohitajika.Hakuna juhudi inayofanywa na serikali kuhimiza elimu kuhusu ubepari, badala yake kinachofanyika ni kuupigia debe ubepari na utamaduni wake. Hatutafika mbali, bali tutaanza kuona matatizo makubwa katika jamii yetu. Kujenga utamaduni wa kujifahamu,kujiamini, kujithamini, kujitegemea, na kujiheshimu kutatusaidia kuepuka kuwa jalala la kila kinachotoka kwa hao mabepari.

    ReplyDelete
  4. kachoka mno! wee michuzi umenistua, nilipoona picha nilijua tanzia maana jamaa ana sura kama anaumwa depression!

    ReplyDelete
  5. Jamani Maprofessa huwa vipi mbona wanajiachia na uchafu hivyo? Madevu na nywele bila kuchana?

    ReplyDelete
  6. Profesor halafu anaendeleza taifa ambalo limeshaendelea, kwanini hio elimu yake akawagaia walala hoi wenzake ili nao wakafunguka macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...