hi bro michuzi,
Nimeamua kukudunga picha ya hotel mpya iliyofunguliwa na aliyekuwa mmiliki wa shelaton katika kambi ya wakimbizi Mtabila,hapa ni maarufu kwa aina ya nyama inayoitwa zingaloo,jamaa anamake sana labda ndiyo maana hana wazo la kurudi nyumbani.
Ahsante
Mdau gebo
kigoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Tanzania asili...yaani 'orojino'!!!

    ReplyDelete
  2. Ninafikiri ni 'Sheraton' na sio 'Shelaton'.
    Naona siku hizi kiswahili kimekufa na wale wazee wetu.

    ReplyDelete
  3. Jamani mbona hao watu wamechoka hivyo je ni Aboriginal People nini.He jamani kumbe box ni zuri, michu hebu wafanzie mambo hao waje huku wachangamke na box kidogo labda watapata ahueni.Kweli inaumiza hii ni asilimia ndogo tu ya jumuiya inayotuzunguka.

    ReplyDelete
  4. We mdau Gebo a.k.a Mr. Kigoma!!!
    Unataka arudi kwao, mbona wewe unazidi kwenda mbali huko uliko wakati hata alikotoka babu yako hupajui!!
    Muulize baba yako vizuri kuwa nyie mnatoka wapi!! maana hata mama yako hakuelezwa ukweli. Lasivyo utawamaliza ndugu zako hao...ni ndugu zako sema tu walikuwa ving'ang'anizi, hawakukimbia mapema kama babu yako aliyekimbia 50's kama siyo 60's.
    Achani ubaguzi...hao ni ndugu zenu! kumbuka ahadi ya kwanza ya mwana TANU..."binadamu wote ni ndugu na Africa ni moja"...fikiria maana yake..na ujumuisho huu wa "na Africa ni moja" halafu kamuombe baba yako akupe hiyo siri...nakueleza huyo mumiliki wa Sheratoni utampenda kuliko hata huyo jirani yako...kwani ndiye ndugu yako wa kweli huyo.
    Lakini sikushangai...mfano ndiyo maana hata ICTR Arusha imeshindwa kutofautisha nani "Victim" wa Genocide ya Rwanda, kwa kuanza kuhukumu watu bila kujali nani alianzisha 'genocide' na hivyo kuruka suala la msingi la kujua kilichosababisha mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 na kuendelea kuhukumu upande mmoja wa tatizo.

    Pole sana na kutojitambua!! hahahah

    ReplyDelete
  5. wabongo kwakuchapia hamjambo sasa ni Sheraton yenye r sio sheLaton jamani muwe wangaligu na spelling usiandike kama uongeavyo inaelekea wewe ni wale wale kwenye kundi la kuchapia maneno

    ReplyDelete
  6. bongo tambarare

    ReplyDelete
  7. shelaton ndio bab kubwa. hapa sio kuchapia, shelaton ni shelaton na sheraton ni sheraton. shelaton Kigoma ndio yenyewe hawakuwa na amaana ya sheraton unyoijua wewe. Kutetemekea Sheraton ni kuendekeza imperialism of powerful and capitalist countries who want to dominate the world economy. In my views I think these guys are very creative and all they need is an injection of more capital and some assistance in management and how to grow. They are good to go. I am very impressed by the activities of these guys in Kigoma and hope one day some one will find a way to inject more capital into their business model. I am studying in the US. and I think their case should deserve more research and attention. Michuzi please give me their contacts I can help these guys raise money more and win in their business. Sio mchezo manake hawa vijana kwa kweli wanastahili sifa. Wanatakiwa kuzingatia usafi na afya za watu. Other than that as entrepreneurs, they are set to go. I wish them goo luck. acheni kutazama nguo zao na kusema wamechoka. Utajiri ni mawazo na wazo lao la kutuma picha yao na kumuomba michuzi aiweke kwenye blog huko ndio kukomaa kiakili hata kama elimu yao ni ndogo sana si tatizo. Hili si tatizo lao ni tatizo letu na uchumi wetu na future ya nchi yetu kuwacheka hawa ni sawa na kumcheka babu yako kwa kutokuwa na degree.

    ReplyDelete
  8. Bongo kuna shelaton siku hizi, hiyo biashara ya shelaton itakuza utalii Kigoma. hata mkipata hela jengeni hivohivo shelaton kila mkoa, mtakuwa mamilionea nyie vijana wa nguvu kazi. Mtu kazi bwana usijali makunyanzi. Hamna kujidai cheki bobu. Mmependeza. Mtapata hela za kuvaa lakini hilo lisiwe ndio goal lenu. Goal liwe ni kufanya mapinduzi ya kiuchumi.

    ReplyDelete
  9. Hawa jamaa wameniacha hoi sana. nawaonea huruma lakini wanafurahisha kwa picha yao na bila shaka watapata msaada na kufanikiwa na shelaton yao. wamechagua jina zuri sana na hawatashtakiwa kwa kuchafua jina la Sheraton. Kwanza kwa wale mnaosoma Wall Street Journal, mwaka huu Bill Gates alikuwa anasikitishwa na malengo ya Ubepari na amekashifu ubepari na kusema kuwa ubepari si kitu kibaya lakini uwe unajali kuwasaidia wasio nacho. Ubepari mpya wa karne ya sasa ni ule wa kuchangia kupunguza tofatuti kubwa sana sana kat nchi tajiri na maskini na watu matajiri na watu maskini. Ukiwa maskini unakuwa huna internet, lakini hawa vijana wameonyesha kuwa hawajachacha na hivyo si ajabu msaada wao ukapatikana kwa kiwango kikubwa sana na hata makampuni makubwa yakapenda kujitolea kusaidia. Kinachotakiwa ni kupigiana debe kama vile anavyofanya Michuzi asiyebagua watu. Kitendo cha kuiweka picha ya hawa jamaa ni cha kishujaa kama kile alichofanya Mwakyembe cha kumuumbua waziri mkuu mbele ya Bunge. haya ndio mabadiliko tunayotaka katika kila level ya jamii na huu ni mwanzo tu. Biashara hainzii kwa Mwakyembe na kuishia Shelaton Kigoma vijana wanaofanya kuwasaidia Wakimbizi kupata nyama choma ni sawa na kuwa Sheraton. lakini yakwao si Sheraton five star bali ni dongo kuinama, no parking lot, you just walk in.
    Risk yake ni afya tu hivyo vijana ili msipigwe vita hakikisheni mnafanya usafi wa hali ya juu,osha nyama , nawa mikono na sabuni, fua kauka nikuvae yako. usimmind mchawi yoyote. Songa mbele tazama mbele. Hivyo ndivyo wote waliofika mbali walivyofanya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...