Mbunifu wa mavazi Angelo Elly Mlaki chini ya udhamini wa kampuni ya Compass Communications ambao pia ndio waratibu wa Miss Universe Tanzania anatarajia kuonesha mitindo ya mavazi katika show itakayofanyika jumatano hii ukumbi wa kituo cha utamaduni wa Ufaransa (Alliance Francaise Cultural Center)

Show hiyo itazinduliwa rasmi na mrembo wa Miss Universe Tanzania Flaviana Matata ambaye kwa mara ya kwanza tangu apate taji hilo atapanda jukwaani kuonyesha moja ya mavazi ya mbunifu huyo.

Kama ilivyo kwa Flaviana vilevile Elly Mlaki itakuwa ndio show yake ya kwanza kuifanya peke yake yani bila kushirikishwa na wabunifu wenzake kama ilivyozoeleka. Onesho lake lililopewa jina la ‘Muonekano wa Mwanamke au “Discovery of a Woman” litahusisha mavazi yaliyotengenezwa na khanga na vitenge vilivyoshonwa katika mishono ya kisasa.

Huu ni utaratibu wa kituo hiki cha Ufaransa kuandaa matamasha mbalimbali kila mwezi katika ukumbi huu ikiwa pia ni njia mojawapo ya kukitangaza kituo hiki pamoja na ukumbi wao maarufu unaojulikana kama ‘Barazani’.

Mbali na fashion show ya Elly Mlaki pia kutakuwa na burudani mbalimbali ambazo zimeandaliwa na kituo hiki ikiwamo Walewale band ya hapahapa Dar es salaam, sarakasi, mashairi kutoka kundi la Parapanda, nyimbo za kifaransa na burudani nyingine nyingi.


Kwa maelezo zaidi kuhusu onyesho la mavazi la Neith Fashion unaweza kuwasiliana zaidi na wadhamini wa onyesho hili:
kampuni ya Compass Communications,
kwa namba zifuatazo: (022) 2182596
au 0748 305122.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hivi neno "KISASA" kwa kizungu cha england ni nini?

    ReplyDelete
  2. Asante kaka michuzi kwa kuniwekea mrembo wangu .nampenda sana huyu dada hata umueke mwanamke gani duniani unayemjua wewe.

    ReplyDelete
  3. yaani wewe flaviana mpaka natamani kuwa wewe nimebeba mabox mwenzio mpka mgongo unataka kupinda. All the best gal

    ReplyDelete
  4. wow! mtoto amependeza...

    hivi muonekano ni discovery???? Mimimaimuna

    ReplyDelete
  5. U mzuri saaaana mdogo wangu! Nionapo viumbe kama wewe, huwa nasifu kazi ya Muumba wetu. Nimevutiwa zaidi na kipara hicho, yaani inavutia mno! Unawakilisha vyema mabinti wa kitanzania. Utafika mbali dear, just keep it up. Ubarikiwe.

    ReplyDelete
  6. ni kweli! huyu demu ni bomba. Lakini toka mashindano ya miss universe bado sijaona progress. Huyu manager wake anafanya nini, vilevile lazma nigusie kidogo mavazi mengine anayovaa hayamfai kabsaa

    Manager fanya kazi, gal needs to look good 24/7, she is on the spotlight.

    ReplyDelete
  7. Huyu binti ndio anatakiwa awe anavaa mavazi haya, sio yale mavazi ya ajabu mliokuwa mnampatia!!!

    ReplyDelete
  8. Michuzi mambo kama haya huwe unatuwekea hata mara moja kwa wiki sio mbaya.yani huyu mdada ni mrembo yani siku nitayokuona uso kwa uso.kazuri kanavutia na kipara chako hicho nakupakaza asali mwili mzima.nitakulamba kuanzia kipara hicho mpaka kwenye nyayo zako.kwanini hufanyi mpango utokee kwenye tayra banks show unaweza kupata madili mengi wakati ni huu mchumba.asante kaka michu kwa kumuweka mrembo wetu mwenyewe wa kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...