Kwenye post yako ya dada anayetembelea kijiji cha makumbusho, maoni ya baadhi ya wadau yalihusu asili ya vyakula fulani.
Mimi kwa kweli nilijiuliza maswali kadhaa ambayo yamenifanya niombe msaada kwa wanakijiji wanielezee babu zetu walikuwa wakila nini kwani vyakula vingi tunaambiwa kuwa asili yake ni nje ya Tanzania, kwa mfano mahindi tunaambiwa yametoka Mexico, mihogo inatoka Amerika kusini, ndizi zinatoka asia na australia, mchele unatoka Asia, sasa babu zetu walikua wakila nini?
-Mdau Andy

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. mdau unaeuliza swali jawabu yake ni kuwa hivi vyakula ndivyo walivyokuwa wanakula babu zetu. hawa wazungu tatizo lao kila kizuri ni chao na kila kibaya ni cha waafrika.

    vyakula wanadai vinatoka kwao lakini maradhi yote mabaya wanasema yametoka afrika. ukimwi ebola nk ni mfano wa maradhi yanayodaiwa kuanzia afrika na kusambaa maeneo mengine ya dunia.

    hivyo naomba uondoe mashaka kuwa hivi ni vyakula vyetu na wala havijaletwa kutoa ulaya asia au marekani.

    ReplyDelete
  2. Walikuwa wakila SAMAKI NCHANGA na UBUYU, hahahahaaha

    ReplyDelete
  3. vilevile,kila mnyama au ndege anayefugika,yaani kama ngombe,kuku,mbwa etc,etc ametoka nje ya africa.tembo tulikuwa naye lakini tulishindwa kum-domesticate,wahindi waliweza.HII ni sababu kubwa why africa has lagged behind,we where wanderers for too long,looking for wild meat,instead of settling down and organising ourselves into divisions of labour

    ReplyDelete
  4. mdau kama ulisoma historia vizuri magrands wetu walikuwa wakila mizizi na matunda pori na nyama pori kwa sana tu. hope nimekusaidia.

    ReplyDelete
  5. sie wamasai tulikuwa tunakula nyama, asali, mizizi na maziwa kwa sana, walio maeneo ya pwani walikula samaki ila sijui wengineo walikula nini? hope hawatasema pia hivyo vililetwa na wakoloni

    ReplyDelete
  6. Babu zetu walikua wakila mizizi, matunda na nyama za porini. Kama utakumbuka historia ya shule za msingi inaeleza vizuri.

    ReplyDelete
  7. Andy , wewe si unaijua ile hadithi ya kwamba aliegundua ziwa tanganyika alikuwa ni Dr. Livingtone mzungu akitokea sijui wapi huko !! wewe hii ilikuingia akilini ? ina maana lile ziwa lilikuwa pale na wakazi wa pale walikuwa vipofu mpaka mzungu katoka alikotoka ndio akaja kugundua kuna ziwa !!! hii hadithi ya vyakula mimi naona ni hivyo hivyo in a sense kwamba sisi watanzania wenyewe ndio tunapenda utumwa na tunajitia utumwa mpaka kesho watu wengine watatutawala, wewe badala ya kuwafundisha watoto wetu mashuleni common sense tunaongea huu utumbo, sasa hiyo mihogo karne gani ilitolewa sijui wapi huko ilikoanzia na kuletwa bongo kwa mamabu zetu ???!! yaani mimi hapa nimeshakerekwa mana hii subject huwa inanichanganya kichwa na siimindishi kabisaaa ndio mana bora wazazi siku hizi tupeleke watoto wetu mainternational school wasijazwe uongo wa historia ta kiTZ !! Mimi niliiipenda sana history mana I love my coutry but tusipobadilisha hulka zetu tutaendelea kuwa watumwa maishani na sijui ni legacy gani tunaachia watoto. Huku Uingereza wana hiyo lesson kam ya historia husikii wakimpa sifa mjerumani ama mfaransa kwenye vitabu eti katoka huko alikotoka akaja hapa kugundua river!!!! Mimi naona hivi vitabu vya historia vifanyiwe review big time ....... kaka Andy sorry nimepandwa na jazba mno..... and by the way nyie wadau hapo juu mnaokubalian na suala la mababu zetu kula wanyama pori na mizizi jiulizeni swali moja hivo vitabu vya historia yetu kaandika nani wa kwanza ?? Mzungu !! so mlitegemea atawalisha babu zetu chakula sawa na alichokuwa anakula yeye ?? !!! Jamani eeh lets WAKE UP AND SMELL THE STINKY SMELL that is our History !!! And yet we call ourselves NATIONALIST!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. Son of Alaska,mmasai na anon 12:50pm nadhani you have been extremed brainwashed and never recovered.Hawa wazungu ndiyo walioandika historia yetu kwa hiyo waliandika yale mabaya waliohadithiwa na wazungu waliokuja Afrika mwanzoni.MKisema mababu zetu walikuwa wanakula mizizi ni uvivu wa kutofikiria.Mnashindwa kutambua kuwa Mihogo na Viazi ni Mizizi?Wazungu walipokuja kwetu na kukuta mababu zetu wakila mihogo na Viazi walitambua ni vyakula vya aina gani sema waliamua kupotosha ukweli ili kupaka matope waafrika.Ukiangalia kila kitu kilicholetwa toka kwa wazungu,waarabu kina jina litamkwalo tokana na asili ya litokalo.

    ReplyDelete
  9. Walikula asali, nyama na matunda. Pia mizizi, maji n.k.

    Ukichimba sana asili ya nyuki, swala, maji etc utakuwa unambipu Mungu kwa praiveti namba; evolution and origin of life!
    SEV

    ReplyDelete
  10. Babu zetu kule Majita walikuwa wanakula mizizi mbalimbali na kupozea matunda kama sungwa,obhunyunywa,obhukomakoma.Mboga zao kuu zilikuwa samaki kama ngere aka gogogo,jimome,jimbofu,nyingu na jimamba

    ReplyDelete
  11. WAZUNGU WAMECHANGANYA UBONGO WETU WAAFRIKA NA KUTUFANYA TUFUATE MAMBO YAO KWA KUTULETEA ELIMU YAO.FIKIRIA VITABU VYA HISTORIA YA AFRIKA VIMEANDIKWA NA WAZUNGU. Lakini Africa ni Paradise, hatuna natural disaster kama za mataifa mengine. HATA MTUME ALIWAAMBIA WAISLAM WAKIMBILIE HABESH (Ethiopia)ili waokoke.YESU ALIKIMBILIA MISRI (Afrika)ili kuokoka kuuwawa na Herode. JAMANI TUNAPATA SHIDA SABABU YA KUIGA MAMBO YA WAZUNGU.

    ReplyDelete
  12. WAZUNGU WAMECHANGANYA UBONGO WETU WAAFRIKA NA KUTUFANYA TUFUATE MAMBO YAO KWA KUTULETEA ELIMU YAO.FIKIRIA VITABU VYA HISTORIA YA AFRIKA VIMEANDIKWA NA WAZUNGU. Lakini Africa ni Paradise, hatuna natural disaster kama za mataifa mengine. HATA MTUME ALIWAAMBIA WAISLAM WAKIMBILIE HABESH (Ethiopia)ili waokoke.YESU ALIKIMBILIA MISRI (Afrika)ili kuokoka kuuwawa na Herode. JAMANI TUNAPATA SHIDA SABABU YA KUIGA MAMBO YA WAZUNGU.

    ReplyDelete
  13. Waachie hao wazungu waseme wanavyotaka...Siku hizi inabidi tuandike vitabu vyetu vya kufundisha

    Hukumbuki tunavyoambia muzungu wa kwanza kuuvumbua mlima KILIMANJARO sijui alikua nani vile...Kam vile babu zetu walikua vipofu hawaoni kuwa huo ni mlima...au wangesema mzungu wa kwanza kufika uchagani na kuuona huo mlima alikua ni fulani

    ReplyDelete
  14. KWA SISI WATU WA TANGA MABABU ZETU WALIKUA WAKILA MIHOGO YA NAZI AU YA KUCHOMA NA YA KUKAANGA HABARI YA KUSEMA MUHOGO UNATOKA AMERIKA UNAEZA KUNIAMBIA HILO SHAMBA LA MUHOGO LIKO WAPI HUKO AMERIKA?NA MUHOGO ASILI YAKE NI TANGA HASWA HUKO GOMBERO KIRARE NA MTIMBWANI NA MAHINDI YANATOKA MUHEZA HAYATOKI MEXICO WAMECHUKUA U MBEGU ZETU WALE NA MCHELE UNATOKEA MBEYA TENA UKIUPATA ULE MCHELE MPYA HALAFU UKIUPIKA KWA NAZI WEEE HATA NYUMBA YA ISHIRINI WATAPATA HABARI

    ReplyDelete
  15. matunda yetu ya kiasili ni masasati na mbura,na kwa nyama katika sherehe maalum ilikuwa ni binadamu mwenzie na haswa akiwa wa kike!!!kweli historia tambarare!!!!!

    ReplyDelete
  16. Hiyo mizizi wanayosema wazungu, ni pamoja na mihogo, viazi mbatata, viazi vitamu n.k. Kule kwetu Shambalai tunaita ugali wa mhogo "bada' lakini sijasikia mzungu akitaka kula bada. Kama mhogo ulitoka kwao, jina la ugali wa mhogo kwa kiingereza ni nini? au hata ugali wa mahindi ni nini? Jamani wazungu walikuwa wanajifagilia ili tuonenkane kutoka Afrika ( Black Continent) hatujui kitu. Labda tulikuwa hatujui, lakini wao wenyewe wametuonyesha kuwa walichoandika sio kweli. Kilimanjaro, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyanza (Victoria) haya yote yalikuwepo kabla hata Jesus kuzaliwa. Tubadilike.

    ReplyDelete
  17. WALA USIJIULIZE NDUGU YANGU HAO WAZUNGU WA ASIA NDIO ZAO HATA MLIMA KILIMANJARO,ZIWA TANGANYIKA WAMEVUMBU WAO WAKATI SISI SIKU ZOTE TUNAOGA.TUNAFUA NAWALIPO KUJA WAO WAKASEMA WAMEVUMBUA WAO.

    ReplyDelete
  18. MIHOGO, VIAZI, VITUNGUU NI MIZIZI, MAEMBE, NDIZI, MACHUNGWA, MANANASI, MACHENZA NI MATUNDA YA PORINI. KWA HIYO WAZUNGU WALIPOKIMBIA NJAA NA VITA HUKO KWAO WAKAJA AFRIKA WAKAKUTA NEEMA YA VYOTE HIVYO. VYAKULA AMBAVYO KWAO HAVIOTI KWASABABU HALI YA HEWA HAIRUHUSU, AMBAVYO HAWAVIJUI WALA HAWAJAWAHI KUVIONA, WAKAVIKUTA KWETU, KWA HIYO KWA WAO NI "VYA PORINI".

    NDIO MAANA WALE WALIOKUWA WANAKWENDA AUSTRALIA(KUKIMBIA SHIDA KWAO, NA WENGINE WAMEFUKUZWA HAWAFAI KWENYE JAMII)WALIPOPUMZIKA AFRIKA KUSINI MACHO YAKAWATOKA, HAWAKUAMINI KUONA HALI YA HEWA NZURI HIVYO, MATUNDA KWA WINGI NA MAZURI AMBAYO YANAOTA NATURALLY HATA BILA KUYAPANDA, WAKAPAITA "CAPE OF GOOD HOPE", WAKASHINDWA KUONDOKA, WAKABAKI MPAKA LEO WAMENG'ANG'ANIA KUANZIA CAPE TOWN MPAKA HARARE MPAKA KENYA.

    HIVYO HAYO MATUNDA NA MIZIZI HAWAKUYAFAHAMU, TUANDIKE VITABU KWAMBA TULIWAFUNDISHA HAYO.

    TENA WALIKUWA WAGOMVI KWELI. WALIPOONA NCHI NZURI WAKAANZA KULETA SILAHA, KUPIGANA NA WENYEJI KUWANYANG'ANYA ARDHI. MPAKA LEO WEUPE WACHACHE AFRIKA KUSINI WANA ADHI KUBWA KULIKO WEUSI WENYEJI WALIO WENGI! NDIO HUKO HIZO WINES ZINATOKA, HAYO MATUNDA MNAONUNUA HUKO SHOPRITE NDIPO YANAPOTOKA! HAYO AMBAYO HAWAKUYAJUA TUKAWAFAHAMISHA, LEO WANAYAUZA DUNIA NZIMA!

    ReplyDelete
  19. LABDA NIKUSAIDIE KIDOGO NDUGU YANGU NA HIZI ZINAZOITWA HISTORIA.
    KAMA WAZUNGU WANADAI ETI BABU ZETU WALIKUWA WANAKULA MIZIZI, NDIYO.
    NI MIHOGO WALIOKUWA WANACHIMBA AMBAO WAO WALIGEUZA NA KUITA MZIZI. UNACHIMBWA KAMA UNAVYOCHIMBA MZIZI.
    KWA VILE WAZUNGU WALIONA HIVYO, WAKAITA MZIZI, SISI TUNADHANI KWAMBA MZIZI NI WA MTI MKUBWA. TUNASAHAU KWAMBA HATA MUHOGO, VIAZI, KAROTI VYOTE NI JAMII YA MIZIZI.
    KAMA WALIDAI ETI BABU ZETU WALIKUWA WANAKULA MAJANI, SAWA KABISAA. USIKATAE.
    WAPE MFANO WA KISAMVU, MATEMBELE, MAJANI YA BOGA, MCHUNGA, YOTE HAYO NI MAJANI. YALIPONDWA KWA MAWE NA KUWA ROJO(PUREE) NA KUPIKA AU KULIWA BILA KUPIKWA. NI JAMII YA MAJANI HAYO.
    UKITAKA KUJUA ASILI YA KISAMVU, TEMBELE AU MCHUNGA NI AFRIKA, KARIBU NCHI ZOTE ZA AFRIKA WANATUMIA JINA MOJA LA KISAMVU, TEMBELE AU CHUNGA.
    NA KISAMVU LAZIMA KITWANGWE NDIYO KIPIKWE.IWE GHANA, NIGERIA, MALI, CONGO, DR CONGO, KENYA AU MALAWI, LAZIMA WAKITWANGE NDIYO KIPIKWE.
    KAMA JAMAA WALIDAI BABU ZETU WALIKUWA WANAKULA NYAMA MWITU, SAWA KABISA. NYAMA NI NYAMA HATA KAMA NI NYANI NI NYAMA. HUKO CAMEROUN NA CONGO VIJIJINI, WANANCHI WANAKULA HAO WADUDU KAMA KAWAIDA.
    KAMA JAMAA WALIDAI ETI MAHINDI NA MIHOGO VIMETOKA HUKO MEHICO AU MCHELE INDIA, KUBALI.
    MBEGU ZA MAZAO HAYO ZILIPELEKWA NA MABABU ZETU WALIOKUWA WATUMWA. KWA VILE HAWAKUTAKA KUFA NJAA HUKO WAENDAKO, WAZUNGU WALIBEBA BAADHI YA VITU KWA NIA YA KUHAKIKISHA SAFARI ZAO ZA BIASHARA HAZIKWAMI KWA KUKOSA CHAKULA IKIWA NI PAMOJA NA KUPOTEZA WATUMWA KWA VIFO.
    NA KWA TAARIFA, HAO JAMAA HISTORIA INASEMA WALIKUWA WANACHUKUA MAZAO HAYO NA KWENDA KUBADILISHA NA BIDHAA ZA THAMANI KAMA VILE DHAHABU, SHANGA, SHABA NA VITU VINGINE.
    KWA KUONGEZEA UTAMU HUU WA HISTORIA, JAMAA WALIOKUJA MWANZO, WENGI WAO WALIONDOKA NA BAADHI YA MAZAO NA KUPELEKA KWAO (ULAYA) AMBAKO WALIGEUZA NA KUWA KATANI (TOKANA MKONGE), NGUO (TOKANA NA PAMBA), SUKARI (TOKANA NA MIWA) ETC, ETC, ETC.
    NINA HISTORIA NDEFU KUHUSU AFRIKA WADAU NA JINSI INAVYONYWA SIYO HUKO NYUMA. HATA SASA KILA KUKICHA. JAMAA HAWANA KITU. HAWANA ARDHI YA KUPAMBA CHOCHOTE ZAIDI YA KULAZIMISHA UYOGA KWENYE MATENT.

    ReplyDelete
  20. yego majita kutiki go umenifurahisha sana na kumbukumbu za samaki wetu km gogogo jimbofu jimamba jimome ngere ila nyigu jitah kweli sijaisikia kabisa au umeongezea nini?mdau vmabamba
    kuala lumpur

    ReplyDelete
  21. Jamani jamani.... Kumbukeni kuwa vyakula vingi vimeanzia hapa kwetu na kupelekwa kwa hao wazungu wanaojifanya waligundua. Mahindi yalikuwa yakilimwa hapo Misri na Sudan miaka elfu nne (4,000) iliyopita. Sasa iweje waseme yametoka Mexico. Jirani zetu wakenya wameanza kufuga wanyama majumbani karibu miaka elfu mbili (2,000) sasa.

    Hiyo south America yenyewe ilikuwa ikitembelewa na watu weusi waliotawala Africa Magharibi miaka 2,000 iliyopita, bado mzungu Christopher Columbus kaenda karibuni na kusema yeye kagundua south America. Msiwasikilize hao kwanza washukuru sana African civilization imewasaidia kufumbua macho. Mji wa Timbuktu unasifiwa kuwa na ma scholars wa kizungu kwa kuwa na university karne 7 zilizopita. Huyo Galileo mwenyewe kakopi science iliyoanzishwa na mtu mweusi. Jamani tafuteni vitabu msome historia ya mtu mweusi. Kwa wenye internet uki-search kwenye google: Ancient and Medieval history of Black people, mtapata site kibao na hata nyingine zinakwambia vitabu vipi ununue na na utavipata wapi. Vitabu vingine vinavyouzwa vimetolewa copies ambazo ziligunduliwa na archeologists vimeandikwa karibu miaka 600 na babu zentu wa Ashanti huko Timbuktu. Hata hizo hesabu za algebra utashangaa kuona kuwa mtu aliyeanza ni mweusi.

    Wazungu waliandika African history kwa ajili ya manufaa yao. Nina kitabu kimoja kizuri sana kimeandikwa na Robin Walker, title yake: When we ruled.

    Mama Malaika

    ReplyDelete
  22. Chakula cha waafrika kilitegemea mahali walipo, kuna tofauti kubwa kati ya chakula cha waafrika wa kaskazini na kusini. Wakaskazini ambao walihama hama kuambaa na mto nile chakula chao kikubwa kilikuwa kinachoota juu, sio mizizi, hizi ni aina zote za nafaka, kama mtama wa aian mbali mbali, mahindi na vyinginevyo, lakini hasa hasa mtama. Na kwa kuwa mtama hauna wanga mwingi na walikuwa wakila protini sana kutokana na mifugo yao (walianza kufuga kabla ya ujio wa wazungu na wageni kwenye bara hili) miili yao ni slender. Lakini waafrika ambao walikuwa wakila mazao yanayotokana na mizizi, kama viazi (fufu) mihogo, magimbi, viazi vikuu, na hawa ni walaji wazuri wa mboga za majani na samaki wana miili mikubwa, waangalie watu wanaotoka ukanda wanaokula mihogo na jamii yake, kama wakongo, wanajeria, wakurya, na wengine wote ambao asili yao ni kula mizizi walivyo na maumbo makubwa kutokana na wanga uliomo kwenye mizizi ni mwingi kuliko kwenye nafaka.
    Tukija kwenye asili ya kuanza kulima, si kweli kuwa wazungu ndio wakulima wa kwanza. Wakulima wa mwanzo duniani ni wamisri (hata Sudan walikuwa wanalima kwa umwagiliaji mto nile) ambako ni Afrika, hata vitabu vya dini vinatuambia hivyo wakati Nabii Yusufu alipomshauri mfalme wa Misri kuhifadhi mazao kwa ajili ya miaka ya ukame hawa walikuwa wanalima nafaka. Kuhusu ustaarabu, usafi, utabibu, na hata elimu ya hesabu vilianzia Afrika huko Misri na Mali ambako kuna Chuo kikuu cha kwanza kina miaka mingi unaweza kuserach kwenye web ukaona hayo yote. Chuo hiki kwa sasa serikali ya Afrika Kusini ina program ya kuhifadhi kilichobaki hapo kwa ajili ya kumbukumbu ya vizazi vyetu. Wazungu hawakuwakuta Waafrika wajinga wasio na elimu.

    Wakati huko Ulaya kukiwa na shida na kuchafu na maradhi mbali mbali, wazungu walitoka kutafuta maisha bora, ndipo walipokuta bara lilijoaa utajiri wa ajabu na waakaanza kuusomba wakisaidiana na na waafrika wasaliti ambao walaiwasaidia wazungu kubeba rasilimali mali na rasilimali watu (nguvukazi kwa mtindo wa watumwa) kwenda kufanya kazi ulaya na Amerika. Mali iliyojenga Ulaya na Amerika chimbuko na asili yake ni Afrika. Rasilimali sio madini tu hata kuwafanyisha watu kwenye mashamba kama manamba ili kupata malighafi za viwanda vyao wakati wa industrial revolution.

    Tuje swala la chakula, walikiletaje wakati wao walikuwa wanakuja na shanga za kuuza na kauri huku na kiliwezaje kusambaa kutoka kusini mwa Afirka mpaka magharibi na kaskazini (hasa hiyo mizizi wanayodai walileta) mbona haioti huko kwao sasa hivi, hata kwenye maeneo yenye baridi mihogo kazi kuota inataka hali ya hewa ya Savana. Na wale mababu zetu waliochukuliwa utumwa walikuwa akisafiri na mbegu zao ili wasife njaa huko waendako na walipofika utumwani walipanda hizo mbegu ili wapate chakula. Historia inasema WaIrish walikimbia njaa kwao wakahamia Amerika na Canada na njaa hiyo ilikuwa ya viazi ambacho ndio chakula chao kikuu. Walipofika Amerika walikuta kuna chakula cha kumwaga.

    Kuna haja ya kuandika upya historia ya bara hili kwa kutumia hizo hizo contradictory stories zao.

    Subira

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...