Shirika linalojishughulisha na utoaji wa mikopo ya biashara nchini la Easy Finance limetoa msaada wa vyandarua na dawa za kutibu maji kwa waathirika wa bomoa bomoa ya Tabata Dampo jijini Dar es Salaam.

Msaada uliotolewa ni wa vyandarua vyenye viuatilifu 400 na vidonge vya dawa ya kutibu maji vya WaterGuard catoni 16 vyote vikiwa na thamani ya karibu shilingi millioni tatu.

Msaada huo umetolewa ili kusaidia kuwalinda waathirika hao wapatao 400, ambao kwa sasa hawana makazi, dhidi ya magonjwa ya matumbo kama vile kipindupindu na ugonjwa hatari wa malaria.

Wananchi hao wa Tabata Dampo kwa sasa hawana makazi ya kudumu baada ya Manispaa ya Ilala kubomoa nyumba zao kwa madai kuwa zilijengwa katika eneo hilo kimakosa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Easy Finance, Isaack Kasanga alisema kuwa shirika lake limeguswa na matatizo yaliyowakuta wakazi hao ndiyo maana limeamua kutoa msaada huo ili kulinda afya zao.

“Matatizo mliyoyapata ndugu zetu yametugusa sana, ndiyo maana shirika letu kwa kushirikiana na PSI-Tanzania tukaona tukae pamoja na kujadiliana jinsi ya kuweza kusaidia walau katika kuwakinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na hata ugonjwa hatari wa malaria,” alisema.

Aliwaeleza waathirika hao kuwa vyandarua vilivyotolewa vitatosha kumpatia kila mmoja kimoja na kuwa kama vitatumika vizuri basi vitaweza kuwakinga dhidi ya kuumwa na mbu waambukizao ugonjwa wa malaria.

“Ni imani yetu pia kuwa sasa mtaweza kutibu maji kabla ya kuyatumia kwa dawa hii ya WaterGuard na jambo hilo litaweza kuwalinda na magonjwa ya milipoko ya matumbo ambayo mara nyingi hutokea katika mazingira kama haya ya watu kutokuwa na sehemu maalumu na za uhakika wa vyanzo vya maji na maeneo ya kujisaidia.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Congratulations Easy Finance!! Thats wot we call CSR (Corporate Social Responsibility) plus its a great marketing campaign for your company..we hope other companies will follow suit..since serikali yetu imeshindwa majukumu siku hizi...
    Mdau kutoka Warwick Uni.

    ReplyDelete
  2. HAO NIWATANZANIA WENZETU HAWAKO MWANZA WALA KIGOMA TUKASINGIZIA NI WAKIMBIZI,WAPO DAR ES SALAAM KILICHOWAKUTA HAO KUSEMA KWELI INASIKITISHA KWANI UZEMBE WA SERIKALI KUTOFANYA KAZI KWA MAKINI/NAJUA HABARI ZILICHELEWA KUWEKWA KWAMICHUZI LAKINI NEWS MEDIA ZOTE ZILIAONESHA NA SERIKALI YETU INMESHINDWA KUDILI NA SWALA DOGO KAMA HILI KWA WATU WACHACHE/JE ENEO KUBWA LIKIJA KUATHIRIKA SERIKALI IMEJIANDAAJE? HAWA WATU SERIKALI NDIO ILITAKIWA KUWAPA VYANDARUA SI KUSUBIRI MAKAMPUNI BINAFSI.SI NI JUZI TU HAPA BUSH KATOA MSAADA NA VYANDARUA NDIO SEHEMU YA MSAADA ULIKUWA? AU BADO HELA ZIJAFIKA ZA KUTOA MSAADA BALI HELA ZA KUIBA ZIPO TAYARI? IMEFIKA WAKATI WATANZANIA TUAMKENI.
    Mdau mzawa

    ReplyDelete
  3. Isaack, umeanza diet nini? Au picha, naona umependeza... keep it up guyz

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli serikali ya Tanzania nimeamini kuwa haina mpango kazi ni ufisadi tu ktk ngazi zake zote.
    Munahitajia raia wakati wa kampeni zenu za kugombania madaraka, tukishakuwekeni kwenye nyadhifa inakua basi, tunaonekana kama kuku ni wakuchinjwa nakuliwa supu.Nyie viongozi wa Bongo tuseme ndio mnaonesha dharau aina gani kwa wananchi, haiwezekani serikali ishindwe kuwasaidi hawa wananchi waliokumbwa na janga hili la bomoa bomoa. Ingelikua kuiba mali ya umma
    ingelikuwa tayari mumeshagawana.
    Angalia vile hata aibu hawana, kazi uonevu na rushwa ndio ibada zenu.
    kumbukeni "You can fool some people
    sometimes, but you can not fool all the people all the time"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...