Ndugu Wanachama, Wapenzi na Watanzania wote waishio jiji la Southampton, UK.
Mnakaribishwa katika Sherehe ndogo ya Uzinduzi wa Shina la CCM Southampton, itakaofanyika siku ya Jumamosi Tarehe: 15/03/2008, katika ukumbi wa:
Slug and Lettuce
103-105 Above
Bar Street
Southampton
SO14 7FG.
Kuanzia Saa 9:00 Mchana mpaka saa 12:00 Jioni.
Baada ya ufunguzi wa Shina kukamilika jijini Sothampton, kutakuwa na Nyama Choma, Reading kuanzia saa 12:00 Jioni.
Anuani ni: 79 London Road, Reading, RG1 5BY.
Wote Mnakaribishwa.
Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali wasiliana na Ndugu Moses Katega kwenye namba 07791584289.
--
Moses Katega
Katibu wa Siasa na Uenezi
CCM - Tawi La London
Uingereza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mmebakisha kuvaa mapakacha tu huko UK
    Kweli UK imekwisha sasa. Ulaya ninayoishi mimi ina watanzania wengi lakini hawana ukereketwa, wao wanajivunia kuwa watanzania nakuwa na umoja lakini huko UK, duh nasikia hata vitumbua wanapika huko.

    ReplyDelete
  2. naona benefiti haziwatoshi sasa mmeshaanza shina tawi mwishowe mti mnataka kula pesa za watu kiulaini

    ReplyDelete
  3. Wengine hawa... Ama kweli UK wamelosti kifikra. Duh!!!! Of all the deals... mnaona kufungua mashina ya CCM ndio ujanja?

    Mwanangu simpeleki kusoma uko UK, maana na yeye ataharibikiwa tu.

    ReplyDelete
  4. UK tambarare kama bongo tu...yaani kukomushy mushy..uswahiliiii umewajaaa...tokeni hapo muone ulimwengu wa majuu ulivo...

    I was there macho yaninitoka watu wanaishi kiswahili kama bongo...yaani hamna tofauti kabisa na bongo mambo yao...na huko reading ...mh mh mhmmhhhhh mmmm

    Yaani mtu akienda London akarudi enzi hizo nilikua naona ameenda kufungua macho laini nilipofika nikashangaa...Ndio maana mashina ya CCM hayaishi kila siku kufunguliwa na bado.... leo reading, kwesho itakua west berkshire...tafuteni overtime sio kutaka kula kiulani na nyie mko nje ya nchi waachieni bongo wasio na njia ya kufanya overtimes hayo

    ReplyDelete
  5. Hongereni Sana Watanzania wenzetu kwa kuimarisha chama chetu.Wana-CCM mlio nje ya nchi tusaidieni kukuza uchumi, utalii na kupambana na mafisadi, wahujumu wa uchumi na Mabwenyenye ndani ya chama.

    Aman, +255756059481 DSM, anyekele@yahoo.com

    ReplyDelete
  6. Asante sana Ndugu Aman, ujumbe ulioutoa ni mzuri sana, na sisi tuko pamoja nanyi Watanzania wenzetu popote walipo wakati wote.

    ReplyDelete
  7. Maneno mazito hayo ndugu Amani, tuko pamoja. Tanzania ni nchi yetu wote; watoa maoni wengi hapa wamekata tamaa na Tanzania, lakini wapo wachache ambao wako tayari kudhalilishwa humu ili mradi wanafanya wanaloweza kujenga misingi ya haki, demokrasia na maendeleo nchini mwetu.

    Safari ni Ndefu lakini tuko pamoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...