huku ukifika sheli unajitilia mwenyewe mafuta, halafu unaenda ndani kulipa na hakuna anayekusimamia....
kupotea huku ughaibuni ni nadra sana hata kwa dereva mgeni kama mie kwani kuna kitu kinaitwa 'navigator' (kimatumbi chake sijui) ambayo unawek unakokwenda kinakuongoza sio kwa mishale tu, bali pia kwa sauti nyororo ya mama wa kitasha. mnaonaje hii nikija nayo bongo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. Masikini michuzi ulikuwa hujui vitu vingi hivyo?hata navigator kwako ilikuwa ndoto?namshukuru aliyemwezesha michuzi..mdau norway

    ReplyDelete
  2. michuzi hiyo siyo sheli aka SHELL kama ulimaanisha hivyo hizo rangi sio za shell lazima kungekuwa na yellow, huku tunaziita GAS STATION

    ReplyDelete
  3. Michuzi !! naomba nikusahihishe , hapo sio SHELL, ni kituo cha mafuta.GAS STATION,...SHELL, ni jina la kampuni ya mafuta kama ,CALTEX, BP ,AGIP,OILCOM au MICHUZI-OIL na vingine vingi.... unajua wakati Tanzania ,inaanza kuingia kwenye kwenye biashara ya vituo vya mafuta ,makampuni ya kwanza yalikuwa SHELL,Agip,na BP hivyo Vituo vingi vya mafuta vilikuwa chini ya SHELL,.. Kwa hiyo kuna misemo haitofutika kutokana na hali ya ukata na ukiritimba enzi hizo..mimi naishi MAREKANI. lakini nikienda BONGO wanasema katoka ULAYA..wakati ULAYA ni Bara .(EUROPE) lakini sababu zamani ukienda nje kimasomo.. mara nyingi ilikuwa ULAYA ..enzi hizo hakuna kubeba Boksi Kama jamaa zangu wa UK,kwa hiyo ilizoeleka hivyo mpaka leo..
    ...Vile vile hapo umetuacha hoi ..!!!!unajza mafuta kisha unaenda kulipia ndani? mh! mie najua unalipa kwanza kisha unakuja kujaza mwenyewe,au unaweza kutumia bank cards moja kwa moja kwenye mashine,..Michuzi dunia imani imekwisha hakuna ustarabu huo hata , huko ULAYA ...

    ReplyDelete
  4. Michuzi,
    Navigator kwa kimatumbi twaweza kukiita - ramanigeta. kifaa hiki hakitoweza kufanya kazi Bongo. Maana mpaka sasa ktk globefinder ya google hata jiji letu la DSM kunaonyeshwa barabara tatu tu, yaani Bagamoyo Road, Kilwa road na Morogoro Road.

    Hata mitaa yenye majina na ya zamani sana iliyopo DSM ktk vitongoji vya Oysterbay,Upanga, Ilala, Kariakoo, Magomeni pia huwezi kuipata ktk mtandao.

    Hivyo ili jiji la DSM liende na wakati angalao waitie mitaa hiyo ya vitongoji hivyo iliyobarikiwa kuwa na mitaa na ramani ya mipango miji ya jiji, ianze kuonekana ktk mitandao ya internet na setalaiti ndipo Navigator itaweza kutumika Bongo.

    ReplyDelete
  5. uk unatia mafuta halafu unakwenda kulipa.

    ReplyDelete
  6. ah hiyo navigator,hata ikiingia bongo bado madereva watapotea tu,maana hakuna ramani,

    ReplyDelete
  7. Navigator haitasaidia chochote Bongo kwa sasa kwani hatuna satelite itakayowasiliana na hio navigator, hio kitu inasaidiana na satelite nasijui kwamba Bongo tuna satelite ya taifa

    ReplyDelete
  8. Mdau POT,
    Michuzi hajadanganya kusema anaweka mafuta halafu anaenda kulipa. Hata huku US ilikua hivyo zamani (miaka ya nyuma)mpaka watu walivyoanza kuiba mafuta na kukimbia, ndio maana siku hizi unalipa kwanza, ndio unaweka mafuta. Hata kuna sehemu nyingine huku huku US bado wanajaza mafuta kwanza, then kulipa baadaye.

    ReplyDelete
  9. weye POT vipi? huku civilised world,unajaza mafuta alaafu unaenda kulipa,huwezi kimbia cause you will be risking a criminal record just for petrol.criminal record huku ni hatari,everywhere you go,unakwama

    ReplyDelete
  10. WEWE UNAEJIITA POT WACHA USHAMBA MWENZIO MICHUZI YUKO UJERUMANI NA WEWE UKO UNYAMWEZINI HUONI TOFAUTI HIYO?HUKO BASTOLA MTU HATA DIRISHANI KUCHUNGULIA UNAOGOPA LKN HUKO UJERUMANI NA HAPA UKEREWE AAH MAMBO SAFI TU...HUKU U.K MTU UNATIA MAFUTA KISHAUNAKWENDA KULIPA MWENYEWE HAKUNA KUINGIA MITINI WALA NINI WATU WOTE HUKU WAAMINIFU HATA UKISAHAU WALET YAKO SEHEMU BASI UTALETEWA TUMEKINAI SISI HUKU TUNAKULA KKU KWA MRIJA WEWE BEBA BOX TU HUKO NA UKIRUDI NYUMBANI FIKIRIA UKAMSHIKIE NANI LEO BASTOLA.KUDADADEKI WEEEEE

    ReplyDelete
  11. MJOMBA MICHU HIYO NAVIGATOR INAKWENDA NA POST CODE IKIWA BONGO SIKU HIZI WATU WOTE WANTUMIA POST CODE BASI ITAKUFAA HIYO WAKATI WA MGAO WA UMEME USIJE UKAPOTEA BURE

    ReplyDelete
  12. Yaani wabeba mabox wanadhani Michuzi mshambaaaaaa, kwamba hajui tofauti ya Shell na Petro station, kwamba eti hajui navigator. Poleni na ulimbukeni wenu wa mabox.

    ReplyDelete
  13. Mdau Pot"Thursday , March 13, 7.24pm" Mimi pia naishi USA, huku tunakoishi tunajaza gas kwenye gari kwanza, halafu tunakwenda kulipa. Na miji mingi tu bada wanafanya hivyo. Hata hivyo nafahamu kwamba kuna baadhi ya miji kama unaoishi wewe huwa mnalipa kabla ya kutia mafuta kwenye gari.

    ReplyDelete
  14. Huyo navigator ni kama mke wa pili,
    anakuambia kule unakwenda, eti kata kulia, kushoto, punguza speed.
    Alishataka kumuua mkongo mmoja kamwambia next kata kushoto, kukata tu kakutana na bwawa la maji, kadumbukia na gari lake.
    Mpaka mapolizai na Falck kuja, mwenyewe alishaipata.
    Alimdivorce mwenyewe!!!
    Huyo anaitwa second bitch

    ReplyDelete
  15. hata france unatia kwanza mafuta ndo unalipa!kwa hiyo wewe mdau pot said usifikiri sehemu zote zipo sawa yaani kulipa kwanza ndo utie mafuta!

    ReplyDelete
  16. Michuzi tumia neno sheli tunajua inazungumzia nini achana na hao jamaa kabla ya kwenda nje kwani walikuwa wanatumia neno gas station? Sema hio navigator yako ukija nayo huku itakuja kukupeleka kigamboni badala ya kibaha shauri yako. NAKITU KIMOJA MICHUZI UNANISHANGAZA VACATION ZAKO ZOTE UNAENDA BILA MKEO KULIKONI?

    ReplyDelete
  17. Michuzi wee andika vyovyote vile ili mradi wameelewa ukiandika SHELL,BP STATOIL..YOTE MAFUTA,,,kibanda cha mafuta wee poa tuu

    ReplyDelete
  18. Bongo huwezi kutumia navigator kwa vile barabara zetu hazijawa digitised na kutengenezewa software ya ku run hizo navigators. Hata huku ughaibuni kama ukiwa katika barabara ambayo haiko digitised hiyo navigator haikupeleki popote. Nimeona Tomtom wana ramani za sehemu tu ya South Africa.

    ReplyDelete
  19. Watu kama nyie kina POT ndio ma haters of UK people,tumesha choka kusikia habari za boksi na chuki zenu mlizo nazo na watu UK.Watanzania kwa ujumla wanatumia UK English,they therefore dont call it Gas Station they call it Petrol Station,na kwa taarifa yako UK unatia petrol yako kwanza then unaenda kulipa ndani,nyie wamarekani majambazi na kutiana risasi kila siku,eti imani imekwisha hamna ustaarabu tena,ustaarabu bado upo na imani bado ina exist.Ikitokea mtu kaiba mafuta ana shikwa na camera tu!kuiba is very unlikely(rare).
    Ushauri hangaikia hizo karatasi ulizozing'ang'ania huko US atleast utembee nchi za watu ushamba hauto kutoka kwa kuwekwa jela marekani.Michuzi mtoto wa mjini,anatumia lugha kutokana na watu anao communicate nao,he knows all the different names you've mentioned,but the majority of Tanzanians call it SHELL,what's the fuss?

    ReplyDelete
  20. Mdau POT, ni kweli kuwa unajaza halafu ndio unaenda kulipia, in case km unalipa na cash, kama unalipa na kadi ndio unaweka kadi kwanza.

    ReplyDelete
  21. Pot utakuwa unakaa kwenye high crime areas, maeneo ya Ghetto au kwenye trailer parks ambapo ndio wana tabia ya kuiba mafuta. Mimi niko USA na siku zote hujaza mafuta kwanza halafu ndio naenda kulipia ndani bila ya matatizo.

    Halafu wakati mwingine hata hivyo vigari vyenu vibovu mnavyoviendesha mnawafanya wahudumu wa Gas Station wa disable kuweka Gas kwanza ba kulipia baadae. Mtu unapaki kiHonda Civic kimechoka ile kishenzi yaani kigari kina tetanus.

    Mimi nikipaki mashine yangu kali tu kwenye Gas Station hadi surveillance Camera Systems zinajizima maana zinajua gari kali na zinaona ni safe na hazina haja ya kurekodi kitu chochote tehtehtehtehtehteh.

    ReplyDelete
  22. Acheni na huyu mvuta bangi POT labda kaja huku juzi.Sio wewe peke yako upo U.S kama walivyokueleza hata hapa USagara hiyo system ya gas/petrol station kama za Ulaya bado zipo.Na kwa taarifa yako kuna hata system ya kujaziwa mafuta kama bongo hapa hapa Usagara,nenda N.J utaona haya.

    ReplyDelete
  23. hili swala la michuzi kutokwenda vacation na mke wake itabidi atupe jibu kwanza

    ReplyDelete
  24. Welcome majuu bongo tambarare saba nilizania navigator zimeshafika...ila bongo hata ramani hamna sijui utanavigate wapi....

    I watch out zisije zikakupeleka baharini...ikikwambia turn right bora uchungulie kwanza huko right kukoje?? Kuna mtu anasue hicho kimsichana kilimpeleka kwenye njia ya rail... nusu train imkanyage....teh teh teh

    Well, kujisave gas sio fun especially during the winter time...I am glad ninaishi state ambayo siye bado wanatujazia na kukuletea credit card machine kwenye gari wee ni signature yako tu....Nachukia state za jirani gas yao vey expensive na bado unafill mwenyewe.....

    ReplyDelete
  25. Michuzi that "navigator" won't work in bongo, but i m NOT happy with the comment made by Anony wa saa 7:41pm about "u ken only c barabara tatu tu on google earth. I m not sure which google earth is she/he is lukin at,koz u ken c more streets in Dar. Mdau T-Dot

    ReplyDelete
  26. We Pot usilete zako. kuna watu wanaobeba boksi kama wa US? nimeishi US na sasa naishi Ukerewe na kote wabongo wanabeba boksi kwa kwenda mbele. fanya research kabla ya kukurupuka na kuandika mambo usiyoyajua.

    ReplyDelete
  27. Bongo tunahitaji "physical address" kwanza ndio navigator ifuatie, haya mambo yetu ya kupeana direction kwamba nakaa karibu na nyumba ya balozi....kuna mbuyu mkubwa na mtaro pembeni...hatutafika na teknolojia ya "navigator"!!! Chuo cha ardhi mnafanya nini huko?? Internship yenu angalau mtutengenezee "physical address"....maana google inapata shida kutafuta mitaa Bongo!!

    ReplyDelete
  28. Geographical Position System(GPS)Tanzania!! Mhh!!.(House No.,Street Name,Post Code/Zip Code)
    Michu,hivi ni vitu basic kabisa na nnaelekea kufikiri umuhimu wake tunauona. Sasa hebu niambiye hata kama tukasema tuanze kukusanya Data ili Tuzi-'Code'ktk Satellite,tutaanzia wapi:?? Mtoni kijichi/Mtongani?,Keko Machungwa/Magurumbasi/Malapa/kwa mfuga mbwa?,Uwanja wa Fisi?,Kaskazini Unguja,Makunduchi?halafu Dar kila kukicha Bomoa bomoa haiishi.
    **Angalau Keenja Alitubandikia Vibao vyenye majina ya Mitaa hapo Dar.

    ReplyDelete
  29. Kaka michuzi sikuwezi. Haya naona wawaingiza watu kichwa kichwa kuhusu shell. Wabongo bwana kujifanya wajua kukosoa watu? Kwa utaalamu wangu wa mambo ya ramani hiyo navigator usilete bongo kwani bado hatujafikia hiyo hatua kwani hata serikali yenyewe hiyo pesa ya kugharamia project nzima ile nasi tuweze tumia navigator ni sawa na ndoto. Labda tuombe mungu wafadhili watusaidie, lakini sidhani kama tutafadhiliwa kwani bado twahangaika na basic things like water, electricity, etc.

    ReplyDelete
  30. We Michuzi nimekustukia.
    Usitufunge kamba wala nini.
    Hilo gari sio wewe unae liendesha bali wewe ni abiria tu umepakiwa kiti cha mbele cha abiria.
    Kwa nini nasema hivyo?
    1 Huwezi kuwa na Leseni ya kuendesha gari Ujerumani wewe au international driving licence.

    2. Pili Ujerumani magari yao madereva wanakuwa upande wa kushoto. Ukiangalia hiyo picha uliyopiga toka ndani ya gari, imepigwa toka upande wa kulia wa gari-yaani kiti cha abiria.

    Wacha kamaba hizo Michuzi!

    ReplyDelete
  31. Mi naona mnachanganya tu mada,

    Sulala la kutia kwanza ndio ulipe au ulipe kwanza ndio utie ni utashi tu wa mtu,

    Inategemea na unaepatana nae hayo makubaliano ya kutiana (mafuta)

    Wengine huwa hawaaminigi kabisa hao watiaji (wa mafuta) kwani wanaweza wakatia mpaka watosheke then wasilipe, au walipe kinyume na makubaliano.

    Ingekua kila anaetia (mafuta) anakuja kulipa kulingana na kile alichotia, basi haya mambo yasingekuwepo.

    hata huku kwwetu bongo kwenye Petro station zilizo maeneo ya Mitaa ya ohio, kinondoni makaburini na kwengineko yanakopatikana hayo "mafuta", mara znyingi hata kama mtiaji wa mafuta halipi kwanza lakin lazima apatane kwanza bei ya hayo mafuta ndio atie.

    ni hulka baadhi ya binadamu kusubiri kwanza action ndio walipe, mfano kuna jamaa flani ambao wao hua hawalipagi maji au umeme mpaka wakatiwe hiyo huduma.

    Nimewasilisha

    ReplyDelete
  32. kaka Michudhi,
    hicho ki-navigator kinafanya kazi kwenye BAJAJI???.

    ReplyDelete
  33. We,Anon Mtoa maoni,FRIDAY, MARCH 14,2008 2:26:00 AM EAT...wacha kamba hizo US kazi zinatafuta watu sio watu wanatafuta kazi,hizo kazi unazofanya wewe za kuchuma matunda na kupanga Mabox super Market kama mnavyoita huko.. UK..kwa taarifa yako huku USA watu waliisha achana nazo siku nyingi toka miaka waliyoKUDIPOTI..BONGO..Asilimia ya WABONGO ambao waliishi huku na kuamia UK either walifanya SO!! Wakarudishwa home . au walikimbia kuepuka so! au karatasi zimegomba Kwa hiyo seumu ya afueni kidogo ni UK ,sasa inawezekana na wewe ni mmoja wa hao , ...sasa kwa taarifa yako hao wenzako wa UK ,wanatusumbua kila siku tuwatafutie mipango ya kuhamia huku..

    ReplyDelete
  34. MICHU OYEEEEEEEEE! BABA NIMEKUKUBALI, UPO ULAYA NA BAADA YA MIAKA KUMI IJAYO, UTAKUWA UMEIMALIZA NUSU YA ULAYA YOTE. SIFA KWAKO MKUBWA. ILA MTASHA AKIJILENGESHA, AKIBABAIKA NA NGOZI NA MAVITU YA KIBONGO, MALIZA BABA

    ReplyDelete
  35. wewe uliedai kuwa ulikuwa unaishi US na sasa uko UK, sizani kama kuondoka kwako huku( US) kulikuwa kwa hiyari, kama hukufukuzwa basi uliikimbia segerea kwani nafahamu kwa makini sana kuwa ukerewe juwa linawaka kwa kuelekea kulia yani si kichezo

    ReplyDelete
  36. halafu hizi navigator zina bei kali, ziko za aina nyingi, sio bei rahisi.

    ReplyDelete
  37. hizo sheli hapa ukerewe zinaitwa petrol station na usa zinaitwa gas station

    ReplyDelete
  38. Kwa kuchangia kuhusu kama Navigator itafanya kazi kwenye Bajaj?
    Jibu ni Ndio ni ndio kwenye Bajaj, navigator inafanya kazi ktk injini kiuno(baisikeli), ngalawa na pia hata kama unatwanga mguu hii navigator pia inatoa maelekezo wapi upite ili ufike kwenye postal code ulioingiza ktk navigator kabla hujaanza safari yako.

    ReplyDelete
  39. Kaka Michuzi huku kwetu kuna automat filling pia huna haja kwenda lipa weka kadi lako la benki tu utajaza mafuta. Hivi hiyo navigator vip? mbona kuna bonge la waya waninginia?

    ReplyDelete
  40. we michuzi endelea kusema shelli, my wife wangu na dina ya mchana sie wenyewe lugha hiyo tunaielewa na tunaipenda. na hao wanakukosoa wanafiki hawajui wewe hapa unatupa kazi na dawa. huku unatubwagia habari na huku unatuchekesha. wewe umesoma na umetembea karibu half of the world, u r so exposed.

    Ash

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...