Shina jipya la Chama Cha Mapinduzi jijini Southampton, Uingereza lilizinduliwa rasmi tarehe 15 Machi 2008.

Shamra shamra za uzinduzi ziliongozwa na Mwenyekiti wa Tawi la CCM London Ndugu Maina Owino na Katibu wa Tawi Bi Susan Mzee, mgeni rasmi wa katika tukio hilo la kihistoria alikuwa Mhe Joyce Masunga (MB – Viti Maalum). Wageni wengine waalikwa walikuwa Mhe Martha Mlata (MB - Viti Maalumu, Singida) na mlezi wa Tawi la CCM London Ndugu Shariff Maajar.


Uchaguzi wa kutafuta viongozi wa shina hilo jipya ulifanyika ambapo Ndugu Kapinga Kangoma aliibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Shina na Ndugu Good Mrema alichaguliwa kuwa Katibu wa Shina la CCM la Southampton. Katika uchaguzi huo pia walichaguliwa wajumbe watatu ili kutimiza timu ya uongozi wa Shina, wajumbe hao wapya ni Bi Vicky Kamata, Salim Abji na Gomoka John.

Wakati huo huo, Katibu wa Tawi la CCM London Bi Susan Mzee anapenda kuwakaribisha Wana-CCM na Watanzania wote wakazi wa maeneo ya Kaskazini ya London, kuwa kutakuwa na mkutano wa ufunguzi wa Shina jipya la CCM la London ya Kaskazini siku ya Jumamosi, tarehe 22 Machi 2008.

Mkutano huo utafanyika katika anuani ifuatayo:
303-307 West Green Road,
N15 3PA.
Siku ya ufunguzi wa Shina hilo jipya kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Shina la London ya Kaskazini na pia kadi za CCM zitatolewa kwa wale watakaopenda kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Wote mnakaribishwa.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Ahsante.
Wako Katika Ujenzi wa Taifa
Soames Phares
Mkurugenzi wa Habari na Teknologia
Tawi la CCM London.
United Kingdom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. NAOMBA KUULIZA WENZANGU NA MIMI MNAOISHI NJE YA TANZANIA (OF COURSE NAMI NIKO NJE).

    SWALI: "HIVI KUNA HAJA YA KUUNDA TAWI LA CHAMA NJE YA NJE KWELI? LET'S BE VERY REALISTIC. MIMI NILIJUA KUNA MAMBO MENGI YA KUFIKIRIA, MFANO KUWA NA UMOJA WA KITAIFA WA WATU WANAOISHI NCHI FULANI NA KUFIKIRIA TAIFA NA SI 'UCHAMA'.

    MLIOSOMA DEVELOPMENT STUDIES MNAELEWA DHANA YA UKIBARAKA, NA KUJIPENDEKEZA KWA WATAWALA NA KUJIPATIA MASLAHI BINAFSI. WATU HAWA NAHISI NI WALE AMBAO MASLAHI YAO YANAPATIKANA KUTOKANA NA WALE WALIOKO MADARAKAI. HATA KUISHI HUKO NJE NI SABABU YA CHAMA WANACHOKITANGAZA.

    OTHERWISE, MIE BINAFSI SIONI HAJA YA KULETA SIASA ZA CHAMA TAWALA NCHINI TANZANIA NJE YA NCHI. LABDA TU KUFUATILIA NAMNA YA KUPIGA KURA KAMA RAIA.

    CHAMA NJE YA NCHI, MMEKUWA WAPIGANIA UHURU WA KUSINI MWA AFRIKA MIAKA YA 1980? HII NI DANGANYA TOTO YA WATU KUJIWEKEA NAFASI ZA KUTAWALA WATANZANIA MIONGONI MWAO ILI HATA WAKIRUDI TANZANIA MTAWAKUBALI WAKIDAI WAO WAMEKUWA WANACHAMA HATA HUKO NJE YA NCHI. ACHENI KABISA UTAPELI WATANZANIA WENZANGU!!!!!


    MWENYE MACHUNGU NA NCHI INAYOLIWA NA WAJANJA WACHACHE.....

    ReplyDelete
  2. mkutano utafanyika saa sita usiku

    ReplyDelete
  3. mama yangu muzazi walewale ma....di sasa wanaanza hukuhuku hamunipati ng`oooo ccm nahuku wapi na wapi kama si usamjo huo.na mchango munautaka ah!!!! wapi,nyie mandondocha.

    ReplyDelete
  4. Here we go again UK. I just don't know what favors CCM have done to yall. It's not suprising most of you folks are beneficiaries of the corrupt culprits back home. I thought folks who are outside the countries living in democratic societies should push and advocate on eliminating corruption in our country rather than being advocates of evil policies of CCM abroad.
    If yall in love with your country than CCM talk about the radar deal and help out the mwannachi.
    Shame on yall in UK.
    mkereketwa.

    ReplyDelete
  5. Haooo bwana JK sijui kawapa nini,manake wamekuwa mandondocha kabisa na ccm.mie nimesema nimechoka manake uchungu unaniingia moyoni.ngoja nipunguze jazba nisije nikapandisha presha bure.NATAKA NIFUATILIE SHERIA ZA UK KAMA INARUHUSU MATAIFA MENGINE KUENDESHA VYAMA VYA SIASA NDANI YA NCHI YAO.UNAJUA HII SAWA SAWA UNAMPA HIFADHI RAFIKI YAKO NYUMBANI KWAkO KWA MDA ALAFU BAADAE ANAMUAMISHIE GIRL FRIEND WAKE HUMO HUMO NDANI YA NYUMBA YAKO.WADAU IMEKAAJE HII? NA HIVI YA MASHINA HELA ZA KUENDESHEA INATOKA WAPI? Hawa watu kama kweli wanapenda ccm kwanini wasirudi nyumbani wakafanya hio siasa huku? Hakuna kosa kubwa kwa MUNGU kama unafiki.

    ReplyDelete
  6. huu utitiri wa matawi ya ccm uk siuelewi una maana gani.au ni mbinu ya watu walioamua kwenda kubeba boksi kwa muda wasitoke nje ya system,maelezo tafadhali.
    nadhani maana nzima ya chama cha siasa na malengo yake ama hayaeleweki au ni kwa makusudi watu wanafanya mambo katika namna ya wao kutengeneza mambo yao binafsi.

    ReplyDelete
  7. Where all the money Come FROM??? to fund the uniforms, rents, parties after parties and all the cost associated with these so called party branches across England.

    I wonder ???

    ReplyDelete
  8. kweli tunayo pesa ya kuchezea..
    Hao wabunge wamepelekwa kwa pesa ya chamaaa...........! au?

    GOD BLESS TANZANIA

    ReplyDelete
  9. hawa ni waganga njaa.sidhani kama wanakijua chama au katiba ya ccm.
    kama wanataka kugombea ubunge waende Tanzania wakawasaidie watu. sio kuzurura miji ya UK TU.
    JK jihadhari na hawa watu wanaitwa wana maslahi. siku ukikutana nao waulize wanamjua bibi TITI MOHAMED AU kura tatu za 1958.

    ReplyDelete
  10. Erooo...!! sheeeee! hii saa lako inasungumsa saa ya wapi? mwambie na ile mishus ingine irekebishe

    ReplyDelete
  11. Nyinyi watu acheni kutusanifu. Mnatukaribisha Watanzania wote kwenye ufunguzi wa tawi lenu la CCM, tuje kwa lengo lipi? Mnaanzisha vikundi, badala ya kujenga jumuia ya Watanzania wote. Je, Watanzania wenzenu wakianzisha matawi ya vyama vya upinzani, mtakwenda kuhudhuria ufunguzi wake? Acheni kutusanifu. Mmefilisika kimawazo kama ilivyofilisika CCM yenu, ambayo sasa inavuma si kwa kuiendeleza Tanzania, bali kwa kuhusishwa na ufisadi.

    ReplyDelete
  12. Hi MICHUZI,
    KAZI YAKO NZURI SANA NA TUNAIPENDA SANA WANA BLOGG, MI NI MSOMAJI SANA WA HII BLOGG LAKINI HUWA NATOA MAONI PALE INAPOBIDI TU!
    KWA KWELI SASA NIMECHOKA NA UCCM ULIONAO,
    JARIBU KUWA MAKINI SANA KWA SABABU
    UCCM NI MAKUNDI,HULETA MAKUNDI KWENYE BLOGG NA PIA KWA WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI,
    MIMI SIO CUF ILA NIMECHOKA KUONA UCCM HUMU NDANI,
    HATA KAMA UKIIBANIA COMMENT HII BUT UJUMBE UMEKUFIKIA!!

    ReplyDelete
  13. Ndugu zangu wa UK kama karatasi zimegomba.. mnatafuta GEA!! ya kurudi nyumbani ..nyie endeleeni kubeba BOKSI tu..wala msijidanganye hiyo GEA ya CCM kwamba itawasaidia.. mje kuwa kwenye SYSTEM BONGO..mh!!! sahau!

    ReplyDelete
  14. Nasikitika sana. Tanzania imeanza kusambaratishwa na mafisadi kiuchumi nyumbani. Sasa chama cha CCM kimeanza waziwazi kutugawa Watanzania. Iweje balozi aliye kiongozi wa nchi ya Tanzania bila j=kujali itikadi awe mlezi wa Tawi la CCM nje ya nchi??? Mheshimiwa JK.JK.JK.JK kwa msisitizo! Hizo hela za walipa kodi Tanzania umeruhusu zichezewe hivo kupitia ubalozi wako UK? Tunauliza wenye nchi, tafadhali. Kwakweli, kuna siku mtatulipa tu. Hiyo siku inakuja, walahi. Siyo leo, lakini nawaambieni wezangu, Tanzania kuna siku itafika tuanze kushikishana adabu sisi kwa sisi. Tumechoka sana kuchezewa kidalipo!

    THIS IS A SHAME. FOR THOSE WHO THINK THAT ARE IN THE UK BY ACCIDENT, PLEASE GO BACK HOME TO DEAL WITH CCM POLITICS. THE GOAL OF BEING ABROAD SHOULD, AND IS ESSENTIALLY TO FULFILL SOME DUTIES IN THE FOREGN COUNTRY, WHICH OTHERWISE COULD NOT HAPPEN IN TANZANIA. oR ESLE SOMEONE IS ABROAD IN A FOREIGN MISSION. OTHER THAN THAT, YOU GUYS ARE FOOLING US.

    JAMANI, MNAUDHI SANA. ENDELEZENI TU HASIRA KWETU. MNAGAWA WATANZANIA HATA NJE????

    ANZANIA KUIBADILI NI KUSAMBARATISHA CCM KWA GHARAMA ZOTE SIKU SI NYINGI. HATA KAMA ITACHUKUA MIAKA 10 SIYO MBAYA.

    ReplyDelete
  15. MKUTANO UTAANZA SAA 8 MCHANA NA KUISHA SAA 12 JIONI.

    WOTE MNAKARIBISHWA.

    ReplyDelete
  16. OTHERWISE, MIE BINAFSI SIONI HAJA YA KULETA SIASA ZA CHAMA TAWALA NCHINI TANZANIA NJE YA NCHI. LABDA TU KUFUATILIA NAMNA YA KUPIGA KURA KAMA RAIA.

    Hii ni sababu mojawapo, ila itawezekana iwapo Watanzania wote bila kujali wao ni ccm, cuf, chadema etc wakishirikiana kwa nafasi zao pale walipo kusukuma hoja.

    MAISHA MEMA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA; TIMIZA WAJIBU WAKO PALE ULIPO KWA KADRI YA UWEZO WAKO.

    ReplyDelete
  17. Huku hamuoni haja ya kutoa maoni kwenye tukio hili muhimu la kihistoria..??

    Diaspora investment and skills forum

    Watanzania mliochangia hapo juu hasa mliopo UK jiangalieni mlivyo wanafiki. Huu mkutano wa Diaspora umewekwa kwa faida ya Watanzania wote wa UK...lakini hakuna aliyeenda kuchangia lolote kule japo kuwasadia walioandaa wapate mawazo ya wengi. Halafu wakati huo huo mnakuja kwenye habari hii ya CCM na kusema mnataka Umoja wa Watanzania, kana kwamba CCM huko UK ni ya watu wachache tu waliopewa nafasi ya kujiunga na CCM.

    Sitoshangaa nikisikia hawa wanaojitokeza na kushiriki kwenye kufungua mashina CCM ni ndio wale wale wanaojitokeza kwa moyo mmoja kusukuma na kujitolea kuona Umoja wa Watanzania UK unasimama kwa namna moja au nyingine.

    NI AINA YA WATU WANAOTAKA MABADILIKO YA KWELI PALE WALIPO kwa kadri ya uwezo wao...Inasikisha kuona wengi wetu humu tuchangia kinafiki.

    ReplyDelete
  18. hawa wote wana chembechembe za ufisadi tu,haiwezekani mtu aliyekwenda huko kwa nguvu zake mwenyewe aanze kufikiria mambo ya kufungua matawi,

    ReplyDelete
  19. Ndio Maana Watu Wanadai UK kama Manzese tu Nimeamini....CCM hadi Kiwanja mmh si kikuku Ila Huwezi Jua Kuna Sofa Maalum Zinatokaga( Ubunge Wa Viti Maalum) Inaweza Kuwaangukia Maana Siasa Mtaji..Angalieni Msije Sema Mnagombea Na Ubunge Jimbo La Southampto tu Tutakufa kwa Kucheka...Michu Niweke

    ReplyDelete
  20. Kudumu chama cha Mapinjduzi! Idumu siasa ya ujamaa na kujitegemea! Maji ya bendera, bora gongo!

    ReplyDelete
  21. Hawa Londoners na Michuzi ikibidi nawe tutakuunga humo kwenye hilo kundi la kijinga....need a medical attention... Si bure, kila siku ni ujinga tu CCM CCM.... matawi matawi... anzisheni na kajimbo kenu basi huko London na muwe na Mbunge na Raisi wenu ikibidi... Mnakera.... mnaleta ufisadi hadi nchi za watu..... Unafikiri UK hawajui kama CCM ni chama cha mafisadi?

    ReplyDelete
  22. Haya mambo ndio maana yanasababisha tulio Usagaa tuwapige madongo wabongo wa Ukerewe.
    N-way si mbali tutaona wabongo wa DC(washington) tri-state wanakuja na upumbavu kama huu.Maana DC nako kuna ujinga-ujinga wa Mwananyamala.

    ReplyDelete
  23. Jamani mbona sisi ambao tupo nje tusifikirie kuanzisha vyama vya charity ili visaidie ndugu zetu nyumbani wanaoishi vijijini? Vitu kama maji, mahospitali, mashule yaani huku ulaya kuna watu wapo tayari kuchangia pesa, computers, printers n.k kwa watu kule nyumbani. Si lazima tungojee wazungu wafanye hivi. Surely, hii ni jambo la msingi kuliko haya mashina ya vyama vya kisiasa ambayo hayamsadii mlala hoi yoyote kule nyumbani haswa vijijini.

    WaTZ naomba tufungue macho!!

    ReplyDelete
  24. WENZENU WA UK WANA UHAKIKA NA MAISHA YAO HAPO WALIPO NDIO MAANA WANAFUNGUA MATAWI YA CCM KILA MJI. NYIE WENGINE MUDA WA KUFUNGUA MATAWI MTAUPATA WAPI WAKATI NJAA NA VIWANDANI WANAWAHITAJI?

    NJAA HAIWEZI KUWARUHUSU KUSHUGHLIKA NA SIASA ZA TANZANIA, WAACHENI WENZETU WAENDELEZE CCM. HAPO UK KUNA HAZINA KUBWA SANA YA WATANZANIA WATAKAOWEZA KUJA KUPELEKA CHAMA CHA MAPINDUZI KARNE 21 BILA KIWUNGU CHA MAFISADI WALA WATU WENYE NJAA NYIE.

    KUKAA KWENU KOTE NJE HAMUONI UMUHIMU WA KUWA NA WANASIASA WENU WA KUJIVUNIA MNAWAJUA KAMA NI MAFISADI AU LA HAPO HAPO UK?

    MNATIA AIBU, NINYI SUBIRINI MUAMBIWE TU FULANI KAMA WAZIRI AU FULANI KAMA MBUNGE HALAFU MUANZE KUULIZA ALIMETOKEA WAPI HUYU?!!, NI AFADHALI MKISIKIA FULANI AMEPEWA CHEO KWENYE SERIKALI YENU AWE NI MTU MNAYEMJUA, MLISOTA WOTE HUKO UGENINI.

    ACHENI USHAMBA HAKIKISHENI MNAPATA VIONGOZI SAFI WA HAYO MASHINA, HAO NDIO MAWAZIRI NA WABUNGE WENU MIAKA IJAYO. MNATIA AIBU

    ReplyDelete
  25. Kweli kabisa hakuna haja ya kufungua haya matawi ya CCM huko nje. Tatizo letu waTZ ni kujipendekeza kwa viongozi, akija mbunge tu tunataka tujifanye tunakipenda sana chama hadi tunafungua tawi na mashina. Kimsingi kabisa hayana maana hayo, fanyeni mambo ya maana huko sio mnabakia kufungua matawi na mashina ya CCM kilasiku, ni kwa faida ya nani? AMA!!

    ReplyDelete
  26. NJAA ZITAWAUWA. TATFUTENI MAISHA KWA SHUGHULI ZINGINE. SIASA NI MCHEZO MCHAFU

    ReplyDelete
  27. Mimi ni mmoja wa Watanzania wanaoishi UK lakini napingana kabisa na hii hoja ya kuunda matawi ya vyama nje ya nchi.

    Kama kuna wanaofuatilia safari za rais JK watakumbuka kuwa alikutana na watanzania pale London cha kusikitisha hata Mke wake Rais (First Lady) alijisahau akidhani kuwa wote ni wana CCM akasalimia kwa KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.Hivi watu wote naona wana dhana hiyo hiyo ya kutaka kuweka Tawi la CCM kwa maslahi.

    Sasa tutajilinda wenyewe mpaka lini? Hivi huu ujinga wa CCM tutaumaliza lini? Ama bado tunaamini zidumu fikra za JK?

    Wajinga ndio waliwao, na nina wasi wasi hawa wanaojifanya wanachama wa ccm London wanataka kurahisisha kufungua account ili wawe wanahifadhi hela za wezi wenzao walio Bongo.

    Tuache unafiki ndugu zangu mbona hakuna Labour ama Consevartive ama democratic wala republican branches nje ya Marekani/UK ambako kuna demokrasia imekomaa kuliko bongo?

    Mungu Ibarikia Tanzania
    Mungu Ibariki Afrika

    Mdau

    Mtanganyika UK

    ReplyDelete
  28. HIVI NYIE AMBAO MNATOA COMMENTS ZA UNAFIKI KATIKA MATANGAZO YA CCM - UK MNABORE, HAMZIJUI HATA PERSONAL PROFILES ZA HAO WANACCM, NI WATU WA NAMNA GANI NA PIA WANA KAZI GANI NA VIPATO VIPI.

    HAWANA HAJA YA KUJITANGAZA NI MISAADA MINGAPI WAMETOA KWA WATANZANIA NYUMBANI.

    MNAOTOA COMMENTS HATA BARUA KWA NDUGU/WAZAZI WENU TANZANIA HAMUANDIKI,LAKINI MNA MUDA WA KUTOSHA KUSHINDA KWENYE MABLOG NA KUTOA COMMENTS ZA UNAFIKI

    "SHAME ON YOU" FAHAMU VIPATO/MISHAHARA YAO HUKU UGHAIBUNI HALAFU ULINGANISHE NA MISHAHARA YENU YA PESA ZA MADAFU HUKO BONGO, "DON'T EVEN GO DOWN THOSE ROADS"

    HUKU UK KUNA VIONGOZI/WANASIASA KUTOKA KATIKA JUMUIYA MBALIMBALI ZA WAHINDI, JEWIS,CARIBBEANS GHANANIANS, NIGERIAN ETC, AMBAO WAKO KATIKA COUNCIL/BOROUGH/WARDS MBALIMBALI AMBAO WANA INFLUENCE KUBWA KWENYE UK PARLIAMNENT, WANASAIDIA JUMUIYA ZAO KWA KARIBU SANA, HIVYO BASI KUPITIA CCM NI "KUJIFUNZA TU KATIKA SIASA" SIO LAZIMA KUJA BONGO NA KUONGOZA.

    NA NUKUU HOJA YA ALIYETOA KUHUSU
    "Diaspora investment and skills forum" HII NDIO ISSUE YA KUIONGOLEA, CONTRIBUTE CONSTRUCTIVE COMMENTS, WAHAMASISHENI WATU WAJITOKEZE KWA WINGI NA KUTOA MADUKUDUKU YAO KUHUSU SERIKALI YAO YA TANZANIA.

    ETI KUNA MTU ANAULIZA KUHUSU UHALALI WA KUFUNGUA TAWI LA CCM LONDON - KWANZA KAMUULIZE David Millband - (UK)FOREIGN SECRETARY PILI, TEMBELEA OFISI ZA FOREIGN & COMMONWEALTH,TATU INGIA KWENYE WEB SITE HII http://www.labour.org.uk/international_projects.

    HATA NYIE WAPINZANI (CHADEMA)MUULIZENI DR. WILLBROD PETER SLAA - "WHISTLEBLOWER - TUUKATAE UFISADI" ALIANZIA WAPI KATIKA HARAKATI ZAKE KATIKA SIASA, NANUKUU "Nimekuwa Katibu wa Shina la CCM, Tawi la Mambo ya Nje - ROME Italy wakati nasoma Rome, 1980 - 1981"
    Tembelea hapa: http:/bongocelebrity.com/2008/01/27/tuukatae-ufisadi-drslaa/

    "Mdau Mtanganyika UK" Nafikiri unahitaji PASSPORT MPYA, UNAONEKANA WEWE NI MBAGUZI WA ZANZIBAR, SISI NI "WATANZANIA" NA SIO "WATANGANYIKA"

    "JAMANI TUJENGE NCHI YETU TUSILETE UNAFIKI TUTABOMOA" NI MIMI "HARUFU MBAYA" KATIKA UJENZI WA TAIFA - UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA.

    ReplyDelete
  29. MDAU HAPO JUU,

    HOJA ZAKO ZINA MSINGI. WATANZANIA TUMEZIDI KULAUMU. CCM INAWAPA NAFASI HAPO WALIOPO UK KUINGIA KATIKA MCHAKATO WA KUJENGA NCHI WAO BADALA YA KUJIUNGA NA KUWEKA JUHUDI ZAO, WAMEKALIA KULALAMIKA BADALA YA KWENDA KWENDA KWENYE HIVYO VIKAO NA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KAMA WATANZANIA.

    MANENO MATUPU HAYAVUNJI MFUPA CHUKUENI UONGOZI KWENYE HAYO MASHINA ILI MPATE NAFASI YA KUHARAKISHA HAYO MABADILIKO MNAYOYATAKA.

    KALAGHABAHO..!!

    ReplyDelete
  30. Kwenu wenye wasi wasi ju ya matawi ya vyama nchi za nje naomba kumjibu mtanganyika. soma hapa:http://www.brusselslabour.org/membership07.htm

    na nitanukuu:Although Labour International now has branch status with the Labour Party, overseas branches do not receive funding from the national party and we rely on additional subscriptions from members. The Party has decided that Labour International Branches can require an additional payment to the national subscription, to meet costs including those for room hire for our meetings, funding social events, sending out mailings, and paying the running costs of our website.

    The Brussels Labour subscription rate is currently 25 euros, with a reduced rate of 5 euros. You can pay by making a transfer to the Group's account 001- 1128765- 52: (please put your name and '2007 subs' in the communication). The easiest way is to become a member is to complete the membership form.

    Full membership of the Branch is only open to Labour Party International members but Labour supporters living in Belgium can have associate membership, without voting rights.


    Asante

    Mtanganyizanzibar

    ReplyDelete
  31. HAMNA COMMENT YOYOTE YA UNAFIKI NYINYI WANA CCM NDIO WANAFIKI NA WATU WAMECHOKA KUFANYWA WAPUMBAVU/WATU HAWATAKI MABILIONI MNAYOCHOTA ZA WALIPA KODI TUNACHOTAKA BASIC NEEDS ZITAKAZOWEZA KUENDESHA MAISHA YETU KWA USALAMA ZAIDI MAJI SAFI,UMEME NA BARABARA MPAK MIKOANI ZIWE NZURI HILI WAKULIMA WAWEZE KUSAFIRISHA MAZAO YAO/ACHENI KUTETEA UJINGA WA VIONGOZI/

    ReplyDelete
  32. niko transit jamani,hivyo hiyo west green rd,whats the nearest underground station? na which train from piccadily circus

    ReplyDelete
  33. Congrats Wa TZ wote huko UK.
    Pamoja na kuanzisha matawi hayo na Binafsi nawaunga mkono! LAKINI HILI JINAMIZI LA HAWA VIGOGO wa CCM Miungu watu mbona hamuwapigii kelele. Vipi kuhusu taratibu za upigaji kura wakati wa uchaguzi! MTZ ukishakuwa tu nje ya mahali ulipojiandikishia huwezi piga kura hata ya RAIS, Mmaanishe yale mnayoyafanya! ONYESHENI TOFAUTI. La sivyo hamtakuwa na MAANA.
    Amani

    ReplyDelete
  34. FUNGUENI HUKO HUKO UK..SIO U.S.A.

    ReplyDelete
  35. ANON Wednesday, March 19, 2008 2:11:00 AM EAT
    nani yuko kwenye corparate world mwenye muda na chama cha mapinduzi ughaibuni? hao ni waganga njaa wa kulea wazee na kupiga box wanaangalia watoke vipi na ccm
    toka lini siasa ukapatia uzoefu ughaibuni ukaitekeleze bongo? way two different grounds
    msiogope umande ndugu zangu fungua fungua hizo kurasa kuna ukurasa mmoja bado hujaufikia ukiufikia huo utaiangalia ccm kwa mtazamo mwingine kabisa
    mind you, ccm is looking several steps ahead of you and probably cracking up for fooling you if you really dont know what their deal is(wanakula na vipofu)
    And ofcourse they have expectations, the dont just establish a center in UK for no reason
    i feel sorry for your parents if they incurred any cost to bring you where you are

    ReplyDelete
  36. Me naendelea kuwashangaa hao wakereketwa na wafurukutwa watanzania wenzangu wanaopoteza muda mwingi kufungua matawi ya CCM huko UK badala ya kukusanya michango mbali mbali kwajili ya ndugu zenu ambao hawana makazi, hawana pa kulala baada ya manispaa ya Ilala kubomoa nyumba zao kwa sababu ua ufisadi ambao umeota mizizi mikubwa hapa nchini kwanini tusitumia muda mwingi kuongelea uozo wa Tanzania ulio mkubwa kiasi hiki kuliko kukesha kwenye session za CCM tufanye mambo ya kukemea CCM waache kulindana walituingiza katika mikataba mibovu wafikishwe mahakamani waliotafuna pesa za EPA nao wakamatwe CCM jamani tuache kulindani au nyinyi ndugu zao hajuwi kinachoendelea huko. Tanzania hali sio nzuri kwa Taifa letu me naamini baba wa taifa akifufuka leo hii atakufa kwa stroko kwa hali hii mbaya zaidi, pesa karibu zote za EPA amerudisha mtu mmoja kwanini asikamatwe au kwa vile ni swahiba wa Kikwete na Mbunge Tajiri hii akubaliki.
    Aliingia madarakani kwa kalamu atatoka kwa kalamu aliingia kwa risasi atatoka kwa risasi na aliingia kwa ufisadi atatoka kwa ufisadi nchi imeharibika kuliko kawaida kwahiyo ndugu zangu ni bora tusiwe wanafaki kwa kuifagilia CCM wakati imeoza penye ukweli usemwe kuliko kupalilia tumieni muda wetu kuwa na makongamano na misimamo yenu.

    Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania

    naomba kuwakilisha hoja....

    ReplyDelete
  37. HAMNA COMMENT YOYOTE YA UNAFIKI NYINYI WANA CCM NDIO WANAFIKI NA WATU WAMECHOKA KUFANYWA WAPUMBAVU/WATU HAWATAKI MABILIONI MNAYOCHOTA ZA WALIPA KODI TUNACHOTAKA BASIC NEEDS ZITAKAZOWEZA KUENDESHA MAISHA YETU KWA USALAMA ZAIDI MAJI SAFI,UMEME NA BARABARA MPAK MIKOANI ZIWE NZURI HILI WAKULIMA WAWEZE KUSAFIRISHA MAZAO YAO/ACHENI KUTETEA UJINGA WA VIONGOZI/

    Mdau ulitoa huo ujumbe hapo juu.

    Soma ulichoandika, halafu jiulize wewe mchango wako ni upi katika KUHAKIKISHA hao viongozi unaowataka WAKULETEE maendeleo wanayaleta kweli KAMA WALIVYO AHIDI.

    Halafu jiulize kama kuandika kwenye blog peke yake kunatosha?

    Ukipata jibu, nina imani utaenda kutekeleza wajibu wako kwa makini zaidi.

    ReplyDelete
  38. MDAU

    ANON Wednesday, March 19, 2008 2:11:00 AM EAT

    nani yuko kwenye corparate world mwenye muda na chama cha mapinduzi ughaibuni? hao ni waganga njaa wa kulea wazee na kupiga box wanaangalia watoke vipi na ccm
    toka lini siasa ukapatia uzoefu ughaibuni ukaitekeleze bongo? way two different grounds
    msiogope umande ndugu zangu fungua fungua hizo kurasa kuna ukurasa mmoja bado hujaufikia ukiufikia huo utaiangalia ccm kwa mtazamo mwingine kabisa
    mind you, ccm is looking several steps ahead of you and probably cracking up for fooling you if you really dont know what their deal is(wanakula na vipofu)
    And ofcourse they have expectations, the dont just establish a center in UK for no reason
    i feel sorry for your parents if they incurred any cost to bring you where you are.



    Unasema CCM wanaangalia several steps ahead of you. Wewe kama mwananchi kwa nini usihahakishe hizo steps zinakuwa kwa manufaa ya jamii nzima ya Mtanzania popote pale alipo. Hivi kweli, unafikiri kukaa kwako pembeni ndio kutawazuia CCM kutimiza malengo hayo maovu unayohisi wanayo? Watanzania wenye akili kama wewe wamekaa pembeni miaka zaidi ya 40 tangu uhuru na ndio maana ufisadi umeshamiri. Wazungu wenye busara walisema "Evil Flourish when Good Men & Women Do Nothing".

    Ingia humo, hakikisha malengo hayo maovu kama yapo hayatekelezwi, hakikisha unajua nia yao ya kufungu matawi ughaibuni; hakikisha hizo chaguzi za viongozi vinachagua viongozi safi na wachapa kazi; hapo utakuwa umetimiza wajibu wako kama raia mwema. Isitoshe, ni nini kinawafanya muogope, maana hao wanaofungua hayo mashina ni watanzania wenzenu kama nyie, walisota hapo UK, mlisoma wote hapo UK, mlikuwa nao huko viwandani kwenye mahome ya wazee au maofisini. Iwapo mtashindwa kuwasimima hao mlisota nao hapo UK na mnaowaju vyema ili watende mambo mema kwa jamii ya watanzania wote hapo mlipo. Kweli unadhani utaweza kumsimamia fisadi anayetumia shs milioni 400 kugombea ubunge kule vijijini walipo ndugu zetu kwa wingi? Tafakari...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...