Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohammed Shein leo anatarajiwa kuwaongoza mamia ya wakaazi wa Jiji la Dar es salaam katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Olimpiki utakaokimbizwa kwa siku moja katika jiji la Dar es salaam.

Sherehe za uzinduzi huo ambazo zitafanyika katika viwanja vya stesheni ya Reli ya TAZARA iliyopo katika barabara ya Nyerere zitahudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo mawaziri,Meya wa jiji na viongozi wa michezo wakiwemo wa Kamati ya Olimpiki nchini.

Mara baada ya kutoa nasaha zake kuhusiana na mwenge huo na michezo ya Olimpiki Makamu wa Rais ataanzisha mbio hizo kwa kuukabidhi mwenge huo kwa Mh Mohammed Sief Khatib ambaye ni mmoja kati ya wakimbiza mwenge huo kitaifa.

Mwenge huo ambao uliwashwa rasmi huko katika mji wa kihistoria wa Olimpia nchini Ugiriki Machi 24 na kutembezwa kwa siku tano nchini humo utawasili leo usiku ukitokea Buenos Aires Argentina na kupokelewa rasmi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Kapteni Mstaafu George Mkuchika.

Mwenge wa Olimpiki ulipelekwa mjini Beijing China mji utakaofanyika mashindano ya Olimpiki mwaka huu Machi 31 ukitokea Ugiriki kuanza mbio zake za kilomita zipatazo 137,000 katika nchi 20 safari itakayochukua siku 130.

Tayari mwenge huo unaobeba ujumbe amsha shauku yako timiza ndoto yako umeshatembezwa katika miji sita ambayo ni Almaty katika Jamhuri ya Kazakhstan, Istambul Uturuki, St. Petersburg wa Russia, London Uinrgereza, Paris Ufaransa na San Franscisco Marekani na Buenos Aires nchini Argentina..

Baada ya kumaliza mbio zake humu nchini mwenge huo utapelekwa Muscat Oman kuendelea na mbio zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mbona sijasikia wabongo kupanga maandamano kupinga mwenge wa olimpiki??

    ReplyDelete
  2. Acha kabisa kutuzingua na hiyo mienge yenu. Barabara za Dar tayari zishakuwa kero na bado mnatuletea mienge na kutuzibia barabara ili tuzidi kuchelewa makazini. Hivi hiyo mienge yenu mnayoshabikia ina manufaa gani kwa mtanzania au ni ulimbukeni tu wa kuiga kila upuuzi unachoanzishwa na mzungu? Acheni hizo msituzingue kihivyo! Au kama kuna mtu anayejua manufaa ya hiyo mimwengu yenu kwa mtanzania na ajitokeze atueleze.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...