JK akiwa na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh (India) na Mwenyekiti wa AU Commission Profesa. Alpha Konare wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika na India huko New Delhi, leo.
MKUTANO wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Afrika na India (India-Africa Forum Summit) umeanza leo (Jumanne, Aprili 8, 2008) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Vigyam Bhavan, mjini New Delhi, India.
Ufunguzi huo wa Mkutano huo umefanyika chini ya uenyekiti-wenza wa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete na mwenyeji wa mkutano huo, Waziri Mkuu wa India, Dk. Manmohan Singh.
Katika kikao hicho cha kwanza, mkutano huo umepisha Azimio la Delhi pamoja na Mpango wa Ushirikiano kati ya India na Bara la Afrika.
Chini ya Mpango wa Ushirikiano kati ya India na Bara la Afrika, masuala ambayo yatatiliwa mkazo ni ushirikiano wa uchumi ambako nguvu zitaelekezwa katika maendeleo ya kilimo; biashara, viwanda na uwekezaji; viwanda na shughuli za biashara ndogo na za kati (SME’s) na masuala ya fedha.
Mpango huo wa Ushirikiano pia utatilia mkazo uhusiano na ushirikiano wa kisiasa ambako masuala makubwa chini ya eneo hilo yatakuwa ni amani na usalama, na utawala bora, na uendelezaji wa taasisi zisizokuwa za kiserikali.
Mpango huo pia utatilia mkazo ushirikiano wa kisayansi, teknolojia, utafiti na maendeleo ambako nguvu zitaelekezwa katika masuala ya habari na mawasiliano kwa njia ya kompyuta (ICT).
Mpango huo pia unatilia mkazo ushirikiano katika maendeleo ya huduma za kijamii na ujenzi wa uwezo wa nchi za Afrika katika utoaji huduma kwa uwezo mkubwa zaidi kwa watu wa nchi hizo. Maeneo yakayolengwa katika nyanja hiyo ni elimu, afya, maji safi na majitaka, michezo na utamaduni, pamoja na juhudi za kumaliza umasikini.
Mpango huo pia utatilia mkazo uendelezaji wa shughuli za utalii kati ya pande hizo mbili, ujenzi wa miundombinu, upatikanaji wa umeme wa uhakika zaidi, mazingira, na mawasiliano na habari.
Nalo Azimio la Delhi limezungumzia mambo mengi ambayo wakuu hao wa nchi wamekubaliana, mengi yakiwa kuhusu ya kimataifa yakiwamo mabadiliko ya hali ya hewa duniani, na umuhimu wa kufikia majadiliano kuhusu hali ya biashara duniani chini ya majadiliano ya DOHA.
Akifungua mkutano huo, Dr. Singh ametangaza ongezeko la kiasi cha fedha ambazo zinaweza kukopwa na mataifa ya Afrika kutoka kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.15 kati ya mwaka wa fedha 2003/04 hadi 2008/09 hadi kufikia dola za Marekani bilioni 5.4 katika miaka mitano ijayo.
Amesema kuwa fedha hizo zitaelekezwa hasa katika ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo ya reli, mawasiliano ya simu, mawasiliano kwa njia ya kompyuta, uzalishaji wa umeme na miundombinu ya uunganishaji wa nchi za Afrika.
Dr. Singh pia ametangaza kuwa kiwango cha misaada kwa Afrika kitaongezeka katika miaka mitano hadi sita mpaka kufikia dola za Marekani milioni 500.
Waziri huyo wa India pia ametangaza kuwa nchi hiyo itafungua soko lake bila masharti yoyote na bila kodi yoyote kwa bidhaa kutoka nchi 50 masikini duniani, kati ya hizo 34 zikiwa za Afrika.
Baadhi ya bidhaa ambazo zinanufaika na soko la India chini ya mpango huo ni pamba, kakau, korosho, sukari ya miwa, mavazi yaliyokwisha kutengenezwa, minofu ya samaki, almasi zisizotumika viwandani, shaba na bati.
Viongozi wengine ambao wamezungumza katika ufunguzi huo ni Mwenyekiti wa Tume ya AU, Profesa Alpha Omar Konare ambaye katika siku 20 zijazo anamaliza utumishi wake wa AU, na Rais Joseph Kabange Kabila wa DRC kwa niaba ya Jumuia ya Uchumi ya Afrika Kati (ECCAS),
Wengine ni Rais John Kuffour wa Ghana ambaye ni mwenyekiti aliyepita wa AU, Rais Abdoulaye Wade wa Senegal, Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa niaba ya EAC, Makamu wa Rais wa Nigeria, Jonathan Goodluck na Makamu wa Rais wa Zambia, Rupia Banda kwa niaba ya SADC.
Mwenyekiti mwenza wa mkutano huo, Rais Kikwete ataufunga mkutano huo kesho (Jumatano, Aprili 9, 2008).

Wakati huho huo, Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana (Jumatatu, Aprili 7, 2008) usiku alikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Zambia, Bw. Rupia Banda.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika Hoteli ya Ashok, mjini New Delhi, ambako viongozi hao wawili wanahudhuria Mkutano wa Kwanza wa Viongozi wa India na Bara la Afrika. Mkutano huo umeanza leo (Jumanne, Aprili 8, 2008) na unamalizika kesho.
Mazungumzo kati ya viongozi hao yalihusu masuala ya uhusiano kati ya Tanzania na Zambia.
Viongozi hao wawili pia walijadili hali ya kisiasa katika eneo la Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ikiwamo ile ya Zimbabwe. Tanzania na Zambia ni wanachama wa SADC na Zambia ndiyo mwenyekiti wa sasa wa jumuia hiyo.
Zimbabwe ilifanya Uchaguzi Mkuu wake wa Rais, wabunge, maseneta na serikali za mitaa Machi 29 mwaka huu.
Ingawa matokeo ya chaguzi nyingine yametangazwa, bado nchi hiyo haijatangaza matokeo ya uchaguzi wa urais.
Nafasi hiyo ilikuwa na wagombea watatu ambao ni Rais Robert G Mugabe, ambaye alikuwa mgombea wa chama tawala cha ZANU-PF; Morgan Tsvangirai wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC), na Simba Makoni, Waziri wa zamani wa fedha wa nchi hiyo aliyesimama katika uchaguzi huo kama mgombea binafsi.
Baadaye leo, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) atakutana na kufanya mazungumzo na Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini.

Jk kanenepa kweli raisi una raha
ReplyDeleteDuu! Kikwete punguza hizo bullet proof. maana naona kifua kimevimba.
ReplyDeletemdau DC
Kijana katoka shavu kweli kweli
ReplyDeleteD