Wabunge wa Upinzani wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo baada tu ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu, ikiwa ni kupinga pendekezo la CCM kutaka kuwe na kura ya maoni juu ya mustakabali wa hali ya kisiasa Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Naona sasa watu wameamua kufanya kweli..HONGERA WABUNGE KWA KUSIMAMIA MASLAHI YA WANANCHI SIO PROPAGANDA ZA CHAMA CHA MAFISADI!!

    ReplyDelete
  2. Sasa nakubali lazima CCM waonyeshwe kuwa Tanzania watu wote sio CCM na kila kinachoamuliwa nao sio sheria. Kuna haja ya CCM kuheshimu lagislature kuliko kutaka kulitumia bunge kama rubber stamp kupitisha maovu na ufisadi wao.
    Vilevile ni wakati muafaka kwa baaadhi ya wabunge wa CCM kuonyesha ukomavu wa kisiasa na kuungana na wenzao wa upinzani katika kutetea hoja zenye maslahi kwa watanzania badala ya kuangalia personal interest zao.
    We gonna get there kwani wapo wengi ndani ya CCM hawakubaliani na kila jambo na kama wanavyosema kuna mpasuko wa kisiasa Zenji wabaki wakijua kuwa vilevile kuna MPASUKO MKUBWA WA KISIASA UNAKUJA NDANI YA CCM

    ReplyDelete
  3. kwa mwenendo huu hukumu ya ccm haiko mbali.

    ReplyDelete
  4. ...hongera wabunge wa vyama mbadala (mimi siviiti vya upinzani). mko wachache sana lakini kwa sababu yenu nchi itabadilika. msije choka hadi kieleweke.

    ReplyDelete
  5. Jamani hebu nisaiidieni kwani huenda sijaelewa! Hivi wapinzani wametoa sababu gani za kukataa suala la muafaka lisiende kwa wananchi ukiacha msemo wao kwamba ni mbinu ya CCM kukwamisha muafaka? Si wananchi ndiyo waliokuwa wanatka serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, sasa kwanini CUF hanaogopa? kuna sababu nyingine mnazijua wenzangu au ndiyo tabia yetu wTz kila lisemwalo na CCM ni baya ila ya wapinzani ni mazuri? Kitendo cha kususia vikao vya bunge hakina maana ukizingatia wanalipwa posho kubwa kwa siku. Kama hawatoingia bungeni inabidi tumshinikze spika asimamishe posho zao vinginevyo hii itakuwa Richmond ya kinamna yake kwani kuwa fisadi ni pamoja na kupata malipo ambayo kuyafanyia kazi. Mnalipwa ili muingie bungeni na siyo kuleta usanii! mbona hamkususia vikao vya kamati?

    ReplyDelete
  6. WAKUMBUKE KUWA NAO WAMEWEKWA NA WANANCHI HIVYO WAACHANE NA KUWAKOSESHA WANANCHI/WAPIGA KURA WAO UWAKILISHI BUNGENI PIA WAACHE CUF NAYO IWEKWE NA WANANCHI KULE ZANZIBAR HII NDOYO DEMOKRASIA KUTOKA BUNGENI HAKUNA MASLAHI YA WANANCH JE MASLAHI GANI WANAYOPIGANIA HAWA? JAMANIIIIIIIIIII

    ReplyDelete
  7. Waambieni hao wabunge wa CUF wanaotoka wasirudi tena bungeni kwani kuna cha maana gani wanachofanya bungeni? Michango mingi ya maana wanaoianzisha na kuishupalia wanatoka Chadema kuanzia EPA,RICHMOND n.k

    Wao leo wanatoka eti wanataka serikali ya mseto Zanzibar wapewe vyeo chap chap bila hata wananchi kupewa nafasi ya kura ya maoni.!

    .Kwanza kama kususia vikao vya bunge ilitakiwa wafanye hivyo kwenye Baraza lao la wawakilishi ambalo ni bunge la Zanzibar na siyo bunge la muungano kwa sababu wanachodai kinahusiana na kule Zanzibar ambako mgao wa vyeo hivyo wanavyolilia watanzania bara hatuna hisa.

    Hili la kukataa kura za maoni tunaomba na bunge lilishupalie.Bunge lihakikishe CUF HAWAPATII UONGOZI MEZANI BALI WAKAUPATIE KWENYE SANDUKU LA KURA ZA MAONI.Wasipate uongozi bila ridhaa ya wananchi kupitia kura za maoni.Wabunge mlisimamie kidete hilo pasipo kuyumbishwa kwa namna yoyote hata na mataifa ya nje au vitisho vya CUF.Bunge Simamieni demokrasia na mhakikishe wananchi wanapata haki yao ya kura ya maoni.Bunge na baraza la wawakilishi Zanzibar wasikubali kuburuzwa na vishinikizo vya kitoto kama maandamano na kutishia vurugu na kama vurugu wakazifanyie kwao Pemba na Unguja bara mtukome.

    Wallahi kama safari hii fujo zikisababishwa na wapemba na waunguja wakazifanyia Tanzania bara mali zetu zikaporwa na vibaka lazima tuvunje maduka na magodown ya wapemba na waunguja. Tumechoka nao, kufanyia vurugu za mambo yao ya ndani ya Zanzibar Tanzania bara tuishie kuvuta moshi wa mabomu ya machozi na kuporwa mali zetu wakati hatuko kwenye hayo maandamano.

    ReplyDelete
  8. Wakisusia vikao, wanyimwe allowances za siku!

    ReplyDelete
  9. Cuf wanataka madakara ndani ya CCM kwanini wasisubiri muda wao ufike na wao wakatawala kwa ridhaa ya wananchi? Mimi naona CUF ni wasanii sana hasa huyo Katibu mkuu wao Maalim Seif, kila mwaka anataka kugombea yeye tu kwani hakuna watu wengine wa kusimama katika kugombea hicho kiti cha Urais zaidi yake,naona yeye anaweza akawa ni moja ya sababu ya kukosa ushindi katika chaguzi zilizopita na unaokuja.CUF kaeni chini mjipange vizuri kama kweli mna nia ya kuingoza Zanzibar na sio kulazimisha uongozi.Ni ushauri tu

    ReplyDelete
  10. wamechoka na vituko vyao, lakini wengi wanaopinga kitendo hichi, wana agenda za siri ndani ya mioyo yao! kubali tu.. UDINI UMEWATAWALA.... sioni sababu watu kwa nini wasisusie BUNGE linaloeendeshwa kiusanii sanii na CCM.

    Makubaliano yalipitishwa, sasa wanachosema irudi kwa wananchi wapitishe ufanisi wao.

    ReplyDelete
  11. me nawapongeza wabunge kwa hilo lakini bado sio solution kwa swala hili wala sio dawa dawa ni kusema tu lakini tayari dunia imepata meseji kwahiyo sasa wanaweza hata kuendelea na bunge letu.

    me naona katika swala hili ni upuuza wa ccm kurudi nyumba atua miamoja wakati wazo wa serikali ya umoja lilitoka kwao katika kamati ta muafaka wa ccm na cuf pia swala hili ni zito kwani wapemba ukweli wamechoka kwa kuonewa hata kubaguliwa na waunguja sasa kitakachokomboa swali hili serikali ya umoja kuliko vyovyote sasa ukichambua kablasha ya muafaka kuna matatzio ya daftali la kupiga kura maana sio shwari katika kupiga kura sasa tukisema kura ya maoni tutarudi kule kule kwahiyo ccm hawajatumia busara kwa maamuzi yao

    ReplyDelete
  12. mm nadhani CUF HAWAJAWAFANYIA HAKI WANANCHI WAO WANAOWAWAKILISHA KWA KITENDO HIKO! kwani BUNGE SI la CCM PEKEE NI LA VYAMA VYOTE ie HALINA CHAMA
    nadhani CUF MNGEKUA MNAFIKIRI KABLA YA KUTENDA!
    mlishajaribu kususia bunge mara baada ya uchaguzi mkidai nyie ndo washindi na mnataka mtambulike mmeshinda plz... nijulisheni mliishia wapi vileeee hadi mkaamua kurudi MJENGONI??
    viongozi wenu wanawapotosha!!muwe makini
    mdau XXXL

    ReplyDelete
  13. Wewe Mpemba Dunia unaposema walichofanya eti sawa maana Dunia Nzima imepata meseji kwa kuwaona wanapotoka.Kwani Dunia huwa wanaangalia hilo bunge la Tanzania linaloendeshwa kwa lugha ya Kiswahili?

    Kweli mpemba Dunia Una akili finyu kama na hao waliotoka walikuwa na mawazo kama yako kuwa dunia inawaona wanapotoka bungeni kazi ipo.

    ReplyDelete
  14. Nimezisoma comments za Anonyms wa April 08, 7:21,10:19,11:06,na 11:56 hakika ni za Makada wa CCM Typical!Mbumbumbu Mzungu wa Reli,Bendera Fuata Upepo!Iwapo hao ni vijana kwa kweli nawasikitikia sana.Nchi hii tukiiachia tuongozwe na Majinga kweli watatutumbukiza shimoni.Na hili halitatokea.Ndiyo hivyo tena,mkono ukipatwa na Kansa dawa ni kuukata ule mkono ili sehemu zingine za mwili zinusurike.Ukiuonea huruma ule mkono wenye Kansa basi ujue hata maisha yako pia yatakuwa hatarini.Nawashauri hao vijana wanao wabeza wabunge wa upinzani kutoka nje ya Bunge,watafakari mambo wasifuate mkumbo!Tamko la Butiama halikwenda Shule!Wapo wanaodhani watafanana na Mbuni kuzamisha shingo mchangani ili kukwepa matatizo yaliyopo.Huo ni Ujinga ulioje!Huwezi kuyatatua matatizo kwa kuyakwepa bali kwa kukabiliana nayo kwa umakini wa hali ya juu.Sisi wengine hatutachoka kuelimisha wajinga ili nao watambue kwamba walichokuwa wakikifanya kilikuwa siyo sahihi.Nafarijika tu kutambua kwamba kupitia Blog hii ya Michuuuz Dunia nzima itakuwa mashuhuda kwamba siyo kweli kwamba nchini Tanzania kila mtu ni mjinga!Wapo wenye akili zao.AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE!

    ReplyDelete
  15. Hawakususia mazungumzo/muafaka kupelekwa kwa wananchi, bali wamesusia mwendo wa kusuasua unaosababishwa na CCM.

    Inaonekana wapinzani wanataka mambo yaende kwa kasi zaidi wakati CCM inataka mambo yasuesue muda wa uchaguzi ufike>>kila mtu afe lwake!

    Vijana kwa mabadiliko. Anza, wengine watafuata.

    Sev

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...