Na Eline Shaidi, Morogoro
MLINDA Mlango mahiri wa timu ya Polisi Morogoro, Godfrey Shuruche ( 22) amefariki dunia baada ya kuungua kwa muda mrefu homa ya malaria kali na kutarajiwa kuzikwa Aprili 9, mwaka huu katika Kijijini Mang'ula , Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.
Mchezaji huo alisajiliwa na timu ya Polisi Moro kutokea timu ya Roling Stone ya Mjini Arusha Mwaka jana ndiye aliyekuwa nguzo kubwa wakati wa kipa namba moja Amani Simba alipokuwa akitumikia adhabu ya kufungiwa kucheza michezo sita na TFF.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana mjini hapa wakati wa kuuaga mwili wa mchezaji huo ambaye ni raia, Mwenyekiti wa timu ya Polisi Moro, Ahmed Msangi, alisema mchezaji huo alifariki dunia Aprili 7, mwaka huu majira ya saa 12: 30 jioni eneo la Uwanja wa Ndege ambako alikuwa amepanga.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa timu ya Polisi Moro ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Mkoa wa Morogoro, alisema awali mchezaji huyo alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kuanzia Machi 26 hadi Aprili 6, mwaka huu kutokana na kusumbuliwa na Malaria kali.
Alisema Mchezaji huo licha ya kupatiwa matibabu bado hali yake ilikuwa ilibadilika badilika na hivyo Madaktari kuamua kuruhusu kurudi nyumbani Aprili 6, mwaka huu hata hivyo alifariki dunia siku moja baadaye.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, Uongozi wa Polisi baada ya kutokea kifo hicho uligharamia usafiri wa kusafirisha mwili wa marahemu kwenda kijijini kwake Taraja ya Mang'ula , Wilayani Kilombero kwa ajili ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyika Aprili 9, mwaka huu kijijini hapo.
Alisema pamoja na kutoa gharama nyingine pia Uongozi huo umetoa fedha kiasi cha sh: 300,000 kwa ajili ya kufanikisha shughuli za mazishi sambamba na kutuma viongozi kushiriki kikamilifu katika mazishi
Poleni sana ndugu zetu wa Morogoro.Tupo nanyi katika kipindi hiki cha majonzi makubwa!Mweyezi Mungu awafariji ndugu na marafiki wa karibu wa marehemu.
ReplyDeleteMungu ailaze roho ya marehemu mahali pema Peponi. Amina- bube
ReplyDelete