Waheshimiwa,
Naomba msaada wengu kwani kuficha haya maradhi sasa imefika mwisho, yanaumbua, wahenga walishaonya.
Naomba msaada wengu kwani kuficha haya maradhi sasa imefika mwisho, yanaumbua, wahenga walishaonya.
Ninajua mpo watu mtakaosema tulizembea kumlea ndugu yetu ama hatujui malezi, mtatushurutisha kuwa tumelikoroga basi na tulinywe, mimi nakubali yote, rusheni mawe, pigeni vijembe, malizeni matusi na kejeli zote, lakini ukweli unabakia pale pale, hili halinyweki!
Mimi ndiyo hivyo tena maji nshayavulia nguo, kuyaoga sina budi. Tafadhali rejezeni roho zenu za huruma, ninakuombeni ushauri.
Shida yangu hii:
Ninaye ndugu aliyekumbwa na tatizo la utumiaji madawa ya kulevya.
Juhudi binafsi tulizoafanya hadi sasa ni kumfanyia sala, dua na maombi, pamoja na kumfikisha ndugu yetu huyu katika hospitali mbalimbali kwa matibabu zaidi. Hospitali na vituo tulivyovitumia ni pamoja na: Mawenzi Hospitali Moshi, KCMC Hospitali Moshi, Mirembe Hospitali Dodoma na Lutindi Hospitali Tanga.
Tatizo hili limemvuruga yeye, sasa hasikizi suala la mhadhini wala la mteka maji kisimani. Sasa wanandugu tunavurugana na kuchukizana.
Ndiyo maana ninaomba ushauri kutoka kwenu.
Ikiwa umewahi kukumbwa na mkasa kama huu, Je, ni hatua gani ume/mnachukua kumsaidia ndugu yenu huyo?
Ikiwa hujakumbwa na mkasa kama huu, Je, unao ufahamu wowote wa jinsi ya kuwasaidia wanaoathirika kutokana na vitendo vya muathirika ili waweze kuchukuliana na tatizo hilo?
Je, unafahamu kituo chochote nchini Tanzania ambacho kinashughulika na watu walioathirika na madawa ya kulevya?
Natanguliza shukrani za dhati!
Ndimi
Mdau Sudi
huyo jamaa sio adcore mpeleke magereza miezi sita na natumaini hata onja tena hayo mambo,au sio magereza tu tena magereza apelekwe butimba mwanza au segelea akitoka sijui kama ataonja tena
ReplyDeletePole sana. Nenda kwenye vituo vyaushauri nasaha watakusaidia zaidi. kama unaishi kinondoni kuna kikundi fulani kilisaidia wavuta unga. waoshwa vinywa naomba msimtukane
ReplyDeleteNiandikie mona40ly@yahoo.co.uk au weka email yako
ReplyDeletePole sana ndugu yetu.mimi kwa kweli sina uzoefu kabisa wa haya wether drugs,alcoholic addictive umejaribu kuingia kwenye link za watu wenye hayo matatizo mfano
ReplyDeletedrug addiction treatment,stop drug aadiction nadhani ukijaribu utafaidika na kimoja au kingine. nadhani wadau wenzangu wenye uzoefu watakusaidia zaidi
kila heri
DADA HILDA
Pole kwa matatizo yaliowajiri kwani hauko pekee katika tatizo hilo kwani ni vijana wengi wa kitanzania ni wateja wa madawa ya kulevya. La kwanza kabisa bado Tanzania hatujui jinsi gani ya ku deal na drug addicts na vilevile every drug addiction has its own treatment strategy. Kwa kusema hivyo basi huu ni ushauri wangu.
ReplyDelete1. Ushauri nasaha/councelling ni jambo la kwanza katika kumtoa mtu katika addiction. familia na wana ndugu inabidi mkae chini na mtumiaji kumweleza ni jinsi gani mnavyomthamni/ mnavyompenda na jinsi gani utumiaji wake wa madawa unamweka mbali na familia zake pamoja na wandugu. Kwani mtumiaji yeyote wa madawa, kama wanavyosema wao wenyewe ni kwamba they beleive no one give a shit on them and its just the drug that difines their world. Kumbuka ya kuwa utumiaji wa drugs ni kama ndoa na mtu yuko tayari kwa kila njia kuficha addictin yake na vilevile sometimes they get violent and dont want anyone to tell them what to do. Na mara nyingi huwa welevu na kutoa ahadi ambazo huwa hawazitimizi. Counselling ni jambo la muhimu sana kwani ni kawaida yetu watanzania kuona mtu kuwa huo ni msalaba wako mwenyewe na ni yeye mwenyewe ata deal na consequences zake.
2. Rehabilitation is the next stage. Katika kipindi hiki katika kumuondoa mtu katika addiction ni lazima kuwepo na transition point. Lazima kumpeleka katika hospitali inayojua jinsi gani ya kumhudumia mtu mwenye drug addiction. Hospitali zinazofahamu jinsi gani ya kumhudumia mtu mwenye matatizo hayo watamweka katika dose ya madawa wakati wanapunguza matumizi yake hadi hapo itakapofikia kiwango ambocho daktari ataona hakuna haja tena ya kumpa dose za kilevi. Kumbuka ya kuwa kuacha ghafla utumiaji bila ya kupitia rehabilitaion may cause stroke or even death kwani hata organs za mtumiaji may shut off kwani mara zote huwa wanatetemeka na kusikia baridi kali pale ambapo hawana drugs in their sysstem.
3. Ingia kwenye mtandao na tafuta more information katika kumhudumia mtumiaji wa madawa ya kulevya. Hizi chini ni baadhi tuu ya website zinazoweza kukusaidi:
http://www.lapalomatreatment.com
http://www.nida.nih.gov
http://www.cocaine-effects.com/
Mwisho nakutakia kila la kheri katika jitihada zako za kumsaidia huyu kijana na tafadhali jaribu ku share information na wengine. Its always a great thing to reach for somebody else with an addiction. Save another soul thats should be the motto.
Msaada kwenye tutaz walipewa Liverpool jana...Haya Muhidin...anakuja Essien...kazi kwako. Watu mnatakiwa muwe huru kama mimi ninayependa Mara Spurs
ReplyDeletePole kwa tatizo hili,mimi niliwai kuwa na ndugu yangu with the same problem,but thatnks God amepona.
ReplyDeletewasiliana na Dr Agustine Godman,GODAPET Tabata Segerea Migombani Tel +255732924439
Aww duh Sudi kaka. Kwanza poleni kwa yalio wakuta. Duniani hakuna wa kumlaumu istoshe yeye mwenyewe aloanza tabia hiyo kwani wahenga walisema "Mtoto akililia wembe mpe akijikata shauriake" sasa nategemea huyo si mtoto na nyie hamuwezi kuacha shughuli zenu kila siku kuangalia maisha yake. I cant stand "I know what your going through" But i can "Imagine"...Ila la msingi ni kwamba mchukueni huyo ndugu yenu kama kuna watu wa rehab basi mpelekeni akakae hata kama mwaka ili aweze kupona kwani utumiaji wa drugs ina vitu viwili JAIL ama DEATH. Na pia msikate tamaa kwake endeleeni kumuombea mungu kwani mwenyezi mungu hakupi mitihani usoiweza. Endeleeni kumuomba Allah basi atawafikisha na Inshallah ndugu yenu atapona, msikate nae tamaa, dondokeni nae na pia nyanyukeni nae kwani anafanya yoote hayo lakini anaitaji ndugu zake na ndugu zake ni nyie tuu hakuna mwenginewe. It's NEVER TOO LATE. Na pia usife moyo muombee mungu, kama doctor anasema vitu basi fuateni doctor jinsi anavyo sema. Prayers from Allah can heal someone is heart. So believe in Allah pray for ur brother and he will be fine. Hakuna zaidi ya mola believe dat.
ReplyDeletepole sana, nakubaliana na wadau na naomba niongezee kuwa mpeleke muhimbili kitengo cha vichaa kule karibu na makuti utapata daktari kwani wanauzoefu na hao watu na wanajua kuongea nao ninauhakika watakusaidia
ReplyDeleteBw Sudi,
ReplyDeletePole kwa yanayokusibu. Tembelea http://drfaustine.blogspot.com/
Nimepost maelezo kuhusu matibabu ya madawa ya kulevya.
Mdau
Faustine
Pamoja na ushauri nasaha, huyo mtu anatakiwa apatiwe dawa mbadala ya hiyo ilimfanya awe adict ambayo siyo kali sana kama aliyotumia na kwa dose ambayo inapunguzwa kila baada ya muda fulani. Tunajua hizo dawa ni ghali kutegemea na addiction aliyonayo. Ni hatari na vigumu sana kama mtaamua kumuachisha mara moja kwani mwili wake kwa sasa umeshazoe hiyo hali. Nawashauri ongeeni na watalaam ili waone namna ya kumsaidia huyu jamaa. Jambo la muhimu ni kujua alitumia dawa gani ili aweze kufanyiwa hiyo rehabilitation
ReplyDeleteMpelekeni kwa Kakobe huyo, ataombewa atapona mara moja.
ReplyDeleteMhhh mimi bwana hapa sina la kusema maana nikisema itaonekana naongea au naponda sana haya bwana mkuu mimi ushauri wangu wewe unaweza kuwasiliana na mshikaji mkapanga mfanye nini ili muweze kufanikiwa au sio.
ReplyDeleteni muhimu kujua huyo ndugu yako ni dawa gani anazotumia kwasababu illicit substances ziko za aina nyingi na zina tiba tofauti. Zile za aina ya opiates kama vile heroine ndio unaweza kupata substitutes yake kama vile methadone ambayo inaweza kuwa prescribed na madaktari kwa ajili ya kumsaidia asisumbuliwe na withdrawal symptoms pale atakapoacha hayo madawa. Ila kama anatumia madawa tofauti kama cocaine mara nyingi tiba huwa hakuna zaidi ya kupata counceling na aina nyingine za pychotherapy. Sina uhakika kama hizi services zinaweza kupatikana Tanzania lakini unaweza kutafuta ofisi ya Tanzania Drug Control Commission hapo Dar watakupa ushauri zaidi. Ila kumbuka kwamba family support kama unayoonyesha ni muhimu pia katika kumsaidia huyo nduguyo
ReplyDeleteNinakushukuruni nyote kwa moyo wa dhati kwa yote mliyoshauri.
ReplyDeleteNimeyachukua mashauri yote na tutayafanyia kazi kadiri tutakavyoweza.
Mwenye kutoa Baraka awape heri na baraka maishani kwa moyo wenu wa kujali na kusaidia.
Asanteni sana!
Kutokana na uzoefu mdogo nilionao, kikubwa hata kama utampeleka kwenye vituo husika ni yeye binafsi kuwa tayari kuacha, unaweza kumpeleka akatibiwa na kupona lakini akirejea akaanza tena.
ReplyDeleteKAMA UPO TANZANIA.
Mahala pa kwanza ni kituo cha LUTINDI kiko Korogwe mkoani Tanga, taratibu zake ni kwenda katika hospitali za serikali mkoani kwako kisha wanapanga namna ya kumpeleka, kama ni mtu wa vurugu wanajua la kufanya na wana siku maalum za kupokea watu wa aina hiyo.
Mimi nilikuwa na tatizo kama hilo kwa mdogo wangu alikuwa hata kula hali lakini baada ya kukaa miezi mitatu alibadilika sana.
Kituo hicho kinasaidia wenye matatizo ya dawa za kulevya na hata ulevi wa kupindukia wa pombe za kawaida.
Unaweza kuweka namna nitakavyowasiliana na wewe, naweza kukupa namba ya simu ya daktari mmoja wa Lutindi.
Daktari mwingine wa Godapet tabata segerea nimemsikia sana watu wanamsifia na kituo chake nimewahi kukiona kipo njiani tu.
kazi njema
Asante
pole sana kaka mi nilikuwa na rafiki yangu wa hali kama hiyo yaani ikafikia namuogopa kabisa na alikuwa ananipenda yaani alikuja kubadilika akawa kichaa si kichaa yaani ilimradi siku ipite huwezi kuamini ameponea milembe DODOMA alikaa huko mwaka mzima sasa hivi yuko poa na nimsanii jina kapuni.
ReplyDeletesweet
Arusha
Pole sana ndugu,
ReplyDeleteKuna NGO flani iko pale kinondoni maeneo ya shentemba karibu na nyumba ya Tarimba, kuna geti jekundu na nje kuna maandishi kama JISAIDIE ADICTION REHABILITATION. Jaribu pale ndugu yangu! Pole sana
ZNZ KUNA WANAWAKE NA WANAUME WALIOACHA KABISA NA KUWAELIMISHA WENGINE, MIMI NAWAJUA, PIA KUNA MTU SASA HIVI AMEANZA KUACHA NA ANAENDELEA VYEMA, UNAWEZA KUNIPIGIA 024 2234897 [SAA 3-11] KWA MAELEZO ZAIDI
ReplyDeleteHaya sasa jamani kumbe watu mnaponda sana mkiona kitu hakina faida ni sawa kabisa kumbe mnavyoponda ni sawa na hii mada watu hawajaponda hata kidogo hivi ndio inatakiwa wabongo wote.
ReplyDeleteBig up sana wachangiaji!No wapondaji kabisa ktk hii mada,ni discussion yenye akili!Sasa ndugu pole sana,but tatizo hili si geni sana!ktkt masuala kama haya ya "Pschoactive substance abuse"kupona inategemeana sana na wliingness ya mgonjwa mwenyewe,;lazima naye awe na nia ya kuacha vinginevyo awe amerukwa na akili kiasi hawezi kuwa na Insight.
ReplyDeleteSo kama ana anakisasi flani ktkt kichwa yake lazima mjadiliane naye kwanza analichukuliaje suala hilo,pengine ye hajawa tayari kuacha nyie mnamlazimisha!pengine hana Insight kabisa na hajui analolifanya yaani amepoteza ufahamu wa kawida!
Nafahamu kuna vituovingi sana na taasisi mbalimbali zinazoshughulika na madawa ya kulevya!na baadhi zimefanikiwa sana huko Zanzibar ambako tatizo hili lilikuwa sugu,hivyo jaribu ku trace huko ikiwezekana pia yapo makundi ya vijana ambao wamefanikiwa kuacha kabisa Matumizi ya madawa ya kulevya pengine wanaweza kutoa uzoefu,na siri iliyo fanikisha wao kuacha!!
msisahau kuna tiba za Asili pia"SIO ZA KUPIGA RAMLI LAKINI"Maana hapo hukawii kuambiwa flani kahusika kumbe ni Ujinga wa mtumiaji mwenyewe halafu ukajukuta unapoteza muda wako bure!
Luse Dar.
kwanza kaka yangu poleni, pili nimefurahi sana na wadau walivyo toa ushauli,jaribu kufata ushauli ulio pewa na wadau,jitahidini kumuonyesha upendo na kumwambia anapotea, mwenyezi mungu atamsaidia ataacha na kurudi kwenye maisha ya kawaida, jambo hili ni zito famili nyingi linawakuta. Asante wadau kwa ushauri wenu.
ReplyDelete