Hello Michuzi!

Naomba nitumie blog ya wananchi kuweza kuwafahamu na kujuliana na wabongo wanaopenda mawasiliano na waishio Nijmegen- The Netherlands. Tafadhali kwa yoyote atakayependa tuwasiliane kwa email kwanza. Napatikana jmosi na jpili tu, siku za kazi ni kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Teh Teh Teh!!watu wengine wajanja sanaa wameanza mbinu mpya ya kutafuta wachumba hongera sana kaka utawapata tuu..

    ReplyDelete
  2. Facebook, tumia facebook aah huko utakutana na WTZ wa dunia nzima ati ndio utachagua mwenyewe.

    ReplyDelete
  3. WATU WENGINE WANAMATATIZO SANA WEWE NDIO UNAWATAFUTA WATU ALAFU UNAJIFANYA~KWAMBA UNAPATIKA WEEKEND TU HIO SIO NAMBA YA SIMU KWAMBA WATU WATAKUSUMBUA KILA SAA HIO EMAIL ADRESS NA KAMA MTU AKIJISIKIA KUKUTUMIA ~UJUMBE WEWE UTAJIBU WAKATI WAKO WOWOTE UKIPATA NAFASI KILA MTU ANAFANYA KAZI SIO PEKE YAKO.acha ushamba wewe.

    ReplyDelete
  4. Umesema kweli anony at 4:07 ...watu wengine bwana kama wao tu ndio wanafanya kazi...

    teh teh eeeee lakini labda hata email anazicheck weekend tu ...labda hamna email kazini na nyumbani mambo ya mtandao ni kwa city library...

    ReplyDelete
  5. Eheeeeee said umeniacha hoi yaani mtu akose email home basi na arudi bongo maana najua hata single room kuna computer kaka kama hivyo basi bora arudi bongoland akale vumbi maana mtandao mpaka library ni soo bora hata bongo kuna net kila kona ni pesa yako na muda wako tuu tena zingine mpaka saa nne usiku.Kufanya kazi ya kuosha vyombo basi imekuwa dili, je ingekuwa naniiiiiiiiiiiii pole kazi unayo kama sikosi wewe ni kabila fulani..................wapenda kazi oyeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  6. Nimesoma comment za ndugu zangu walionijibu, nafikiri hao wote waliojibu ni watu wanaopenda marumbano. Watu wenye nia njema wameniandikia email na baadhi tunapanga kuonana weekend hii. Ningependa kuweka wazi kwamba napenda kukutana na watu na kuongea siku za weekend, haimanishi kwamba watu wengine hawafanyi kazi. Kwa anayetaka physical address anaweza kuniomba na nikampatia.

    ReplyDelete
  7. karibu sana uholanzi. mie nipo the hague. nitakutafuta siku hizo. lakini je unafanya shughuli zipi hizo hata upatikane week end tu?

    ReplyDelete
  8. Ni Malumbano sio marumbano acha kuharibu kiswahili lugha tamu. Na acha hulka ya kisukuma, kikurya na kiaskari okay?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...