mwalimu akiwa ameongozana na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa kigoma enzi hizo marehemu ukiwaona ditopile mzuzuri, wakati alipokwenda huko kutembelea kambi za wakimbizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Inna Lilahi wa ina ilahi Rajiuun.

    ReplyDelete
  2. Duh wakimbizi wa enzi hizo, cheki kambi yao ilivyokuwa muruwa

    ReplyDelete
  3. anon hapo juu 2:32 nafikiri hiyo picha hujaifahamu umeambiwa walipotembelea kambi ya wakimbizi lakini hapo inaonesha hao viongozi walikua hoteli na sio kambi kama ulnavyofikiria.

    ReplyDelete
  4. Du! anony wa 2:32pm umenifurahisha kweli, kuiita hiyo hotel ya kitalii kambi ya wakimbizi, kwa ufupi tu mimi ni mwenyeji wa huko na hiyo ni moja kati ya hotel za kitalii mkoani hapo inaitwa Hilltop Hotel na inamilikiwa na Raia mwenye asili ya Kihindi.

    ReplyDelete
  5. Ditopile alikuwa superstar. Mpaka Nyerere alim-trust na kumkubali. Si mchezo.

    ReplyDelete
  6. Nasema hongera sana na asante kwa kutuwekea picha ya mtu muhimu hapa TZ na Ulimwenguni, ni mtu ambaye hakupenda viongozi wake kuhusika na UFISADI.

    ReplyDelete
  7. asante kwa mumweka baba wa taifa

    ReplyDelete
  8. Mwalimu bado na anaonekana kama bado yupo hai, kweli mtu mwema akifariki anakuwa bado anaishi kwenye fikra za watu, Tumuombe Mungu atokee mtu kama yeye awaondoe mafisadi kama yeye alivyowaondoa wakoloni na kujenga nchi ya watu wote tofauti na sasa ni ya mafisadi wachache, From Michael Laiser - Dar

    ReplyDelete
  9. Yes!!!!
    Hatimaye nimeona nishiriki kwenye makala hizi baada ya kumuona mwalimu.
    Aliipenda nchi yetu sana
    Hakuwa na mijitamaa na mali ya uma
    Aliona mtu aliyekuwa bado anatawaliwa na wakoloni kama kaka au dada yake aliyekuwa akiteswa na alisaidia kwa njia zote.

    Please endeleeni kuweka picha zake maana nikiziona nashukudia responsible leadership

    Nchi yetu itahitaji revolution ya viongozi kama ile ya Africanism ya wakati wa kugombea uhuru ili kupambana na Wizi wa mali ya uma na rushwa maana rushwa inatuchafulia sifa sana tena sana kuku ughaibuni.
    Inawezekana rushwa kuisha ingawa itachukuwa muda mrefu
    Nchi iwe na database ya kumjua kila raia wake na kila raia na aichukue namba yake,itunzwe kwenye database.(Huku inaitwa social Security Number)
    Pia mtoto anapozaliwa tu apewe

    Ukiibia nchi au kula rushwa basi maisha yako yaathirike kweli kwa kufukuzwa kazi, kufungwa na kutoaminiwa tena (Felon)

    Sasa hivi rushwa imejaa na kunuka mno kila kwamba kila mtu lazima ahusike ktk rushwa unapenda au hupendi, watu wanaokula rushwa wanajiona mafahali na kama ndio wenye akili kwa kuiba na kujitajirisha mno kwa magari na ,majumba ya kifahari.

    Wanawaona baba zetu na mama zetu wanaolima kwa jembe la mkono kama watumwa wanaoishi nchi nyingine inayoitwa nchi ya umaskini ndani ya nchi yao ya Tanzania

    Na labda, nasema nasema mwalimu alikosea mambo machache tu
    Hakuchukua sera za uchumi ambazo zilikuwa realistic kwa hiyo ikakaribisha viongozi wake mwenyewe kuwa mabingwa wa kuongopa tena mbele ya macho yake huku wakiwaibia wananchi, mwalimu alijua lakini hakujua tatizo hilo litazaa balaa la rusaha kukomaa zaidi, akawahamisha hamisha kidogo.

    Nitatoa baadaye maoni yangu ya jinsi rushwa inaweza kutokomezwa Tanzania na Afrika nzima kama Rushwa ikaingizwa katika sera za vyama ktk chaguzi kuu.

    Lazima pia kuwepo mabadiliko katka tume ya uchaguzi na sio tu tanzania lakini Africa nzima kuondoa viongozi mabingwa wa kuongopa kwa kuingiza Electoral voting system, badala ya popular votes.
    Kwenye Electoral votes
    Basi mikoa mikuu kama mitano mikubwa kwa mchango wake wa uchumi kwa nchi itaamua uchaguzi maana lazima uishinde hiyo pia
    mfano:-
    Dar es salaam
    Arusha
    Mwanza
    Zanzibar
    Mbeya
    Au iwe kwamba pamoja na ushindi wowote ukishindwa kushinda dar es salaam na Zanzibar huwezi kushika uongozi wa taifa kwa sababu dar es salaam inajumuisha watu kutoka nchi nzima na kila kabila na zanzibar ambapo watu wanaelewa mno nini maana ya kura wanayoipiga.

    Ndiyo maana huoni chama kimoja kinakaa uongozini hapa Marekani kwa miaka 25

    Dar es salaam na zanzibar zikikujua wewe ni mra rushwa hutashinda ! hiyo nakuhakikishia.

    Viongozi na vyama vitaogopa kula rushwa maana wanajua watakosa electoral votes hata kama wakishinda popular votes

    Natamani sana Africa ingebadilisha sheria za uchaguzi na kufanya kama hivi lakini ni vigumu kufanya maana vyama vingine vina tamaa ya kubaki madarakani milele na sio maslahi ya wananchi wao wanaoteseka kwa umaskini wa uktoweza kununua dawa hata za malaria au wanaokufa na njaa wakati kuna viongozi wa nchi au wanafanyakazi wote TRA wakiiba kila siku na kuonekana kama hao ndio waliofanikiwa (just kwa kuiibia nchi na watu wetu)

    Tazama wizi ulivyo TRA!!
    Tazama wizi ulivyo maliasili!!
    Tazama wizi ulivyo uhamiaji!!
    tazama wizi ulivyo kila ofisi utakakoenda!!!!
    Tuatakubalije mtu kusifika au kuonekana wa maana eti kwa vile yuko TRA wakati ni jitu jizi tu?

    Please Brother michuzi weka picha zaidi za mwalimu maana wengine tukimuona inakuwa kama tunapata nafuu mioyoni

    Mkereketwa,
    Kalamazoo,Michigan,USA

    ReplyDelete
  10. Yep
    Kaka hapo juu umenena
    Kama wakileta electoral voting system shida zote za rushwa zitakwisha

    Lakini wajua tena hakuna ila wachache tu wajuao electoral na popular voting systems

    Nani atajaribu hata kusema? wakati wanafahamu hawatakaa kwenye madaraka?

    Mambo ni kwamba chama kitaendelea kushika utamu(hatamu) mpaka doomsday

    Na actually huu utitiri wa akina mrema labda uungane wote watengeneze chama kimoja kitakachochalenge chama kilicho kwenye utamu

    Kumbe nchi yetu ina wakereketwa bado,
    tunashukuru kwa maoni bora kama hayo

    wenu
    Mpiga rushwa,Bongo

    ReplyDelete
  11. Hey
    The way i see coruption in Tanzania and Africa, i then see the following
    I see no responsible leadership
    i see death sentences to our own people(Due to diseases and poverty)
    While the greedy ones are enjoying first class and royal lives in a poor country like ours
    I see instability everywhere as the gap of the haves and the not haves is too far to be bridged

    I just see trouble along the way unless corruption issue is correctly adressed

    Yep people its not that much pretty to be clasified as corrupt ones,its a big shame.
    Ndimi Mchapakazi halali,
    Ohio,USA

    ReplyDelete
  12. jamani jamani mnanipa uchungu sana kuweka hii picha namkumbuka baba yani utazani yuko hai jamani inapendeza.MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA AMEN.

    Sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 20, 2008

    reason why we have corruption today, is because of this guy nyerere he killed democracy in in its infancy. wakoloni walituachia vyama viwili, hiyo tanu na congress, kulikuwa kuna mtu anaitwa zuberi mtemvu alikuwa mpinzani, nyerere alianza kama waziri mkuu sio rais, jamaa (nyerere)akajiuzulu na baadae kuwahaini wananchi na kuanzisha jamhuri ili awe rais, halafu akaendelea kupiga marufuku congress ili tanu iwe chama pekee, thats why people like oscar kambona were forced into exile,uongozi wake ulivumilia sana rushwa na ufisadi ili ashikilie hatamu, ruling class plundered the BOT at will and then were forced to resign, balali and all these scumbags did not start after nyerere died but they were there during nyereres administration, all he could do is talk and nothing else, kama mafisadi wangekuwa wanapigwa risasi hadharani leo nchi ingekuwa tofauti for better or for worse.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...