mwanasheria wa kampuni ya tanzania standard newspapers Ltd. (wachapishaji wa dailynews na habari leo) mh. emmanuel tamilla (shoto) akipokea kompyuta toka kwa meneja wa tawi la univesrity of dar es salaam computing centre daniel methuse ambayo itatolewa kama zawadi kwa shule ya sekondari ya iringa kwa kuibuka washindi wa mdahalo wa mashule. shule hiyo pia itapatiwa mipira mitatu iliyotolewa na kampuni ya digitouch, wa pili kulia ni bosi wa masoko wa ucc samwel mwamasamali na pili shoto ni afisa masoko wa tsn furaha pallangyo. katika kuhamasisha elimu mashuleni tsn imekuwa ikiandaa mashindano mbalimbali kwa wanafunzi wa shule mbalimbali kushiriki na kujipatia zawadi kama hizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Sekondari ya Iringa ipi specific?Maana zipo nyingi Iringa!All the same wish to congratulate wholeheartedly WHOEVER IS THE WINNER for restoring fame and dignity to Iringa for the outstanding achievement.Iringa ilikuwa moto katika academics mze,sijui siku hizi vipi,ulanzi umezidi nini mashuleni?

    ReplyDelete
  2. Ebwanaeee! Furaha siku hizi ni afisa??? sio mchezo, babu hilo ni bonge la make-over, kweli people change. I remember those dayz at SRSS. Congratulations!

    ReplyDelete
  3. Kweli Dunia Hadaa ulimwengu shujaa

    ReplyDelete
  4. Mh. Tamila, duh big up man, naona mambo si mabaya kwani ki-frigde hakiongopi, it has been long time really.
    Gervas.

    ReplyDelete
  5. Doh Daniel kumbe ni meneja! Hiyo baada ya kumaliza MBA au? Hongera chapa kazi.
    Mdau,
    USA.

    ReplyDelete
  6. zawadi ni computer moja tu? shule ina wanafunzi wangapi?
    kama ni moja tu bora ingetolewa zawadi ambayo ingeinufaisha shule nzima vitabu etc

    ReplyDelete
  7. Tamila hongera, tafadhali tuwasiliane kaka. Ila hako ka fridge jitahidi kukadhibiti maana kakizidi ni tatizo kaka. All in all Hongera sana. www.kipimautu.wetpaint.com

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2008

    Yes Tamira,

    I salute u, bro! Keep it real... lakini huto tuzawadi tuko unga hakika tunahitaji improvement, kama kweli tumeamua kuboresha elimu kwa kiwango kinachotakiwa. We should be serious, aisey. Ingekuwa ni mtu binafsi, poa. Lakini si mwakilishi wa kampuni anakuja na ka-computer kamoja, tena tunaonyeshwa ka-screen tu, huenda CPU yenyewe ina mgogoro.

    Wakati ambapo serikali imeazimia kukuza uingizaji wa wanafunzi sekondari kwa kujenga sekondari nyingi. Wadau wengine inabidi ku-complement kwa kutoa vitu vya maana na kwa idadi/uwiano unaokubalika. Hiyo ndo maana halisi ya PPP!

    Mwanasheria wa kampuni ni mtu mkubwa na nyeti sana (No wonder, kakitambi kanakunyemelea). Hizi mbwembwe za kukunyanyua kuja kupokea ka-computer na tumipira tutatu (tena tumipira twenyewe ni tule twa bei nafuu, na yawezekana ikawa ahadi hewa, maanake hata kwenye picha hatujaonyeshwa). Kengele ya tahadhari inaendelea kugonga!

    Tukaze buti jamani...

    Mlinzikimenyi, Korea Kusini!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...