
Haya, juma hili aliyetinga kwenye jedwali la Foto la Wiki si mwingine bali mdau Elizabeth Munthali. Hadi tunakwenda hewani picha hii ilikuwa imeshatizamwa mara 67. Tunakupongeza dada Liz kwa picha yako kuwa picha ya wiki, mwili haujengwi kwa matofali, kanyaga twende.
Ndugu mdau,
Napenda kuchukua nafasi hii kukufahamisha kuwa picha zitakazokuwa zinakubalika zaidi katika FotoBaraza ni zile zilizopigwa na mdau mwenyewe au rafiki yake wa karibu ambaye amemruhusu kutumia picha hizo.
Hatutaweza kuruhusu picha zilizochukuliwa toka katika tovuti zingine bila ya kibali cha maandishi cha tovuti husika. Hii ni kukiuka sheria za hati miliki na inaweza kuchangia FotoBaraza kuondolewa mtandaoni.
Tarehe 12/4, mmoja wa wadau wetu alirusha picha za wanaume walio nusu uchi na ziliwakwaza wadau wengi, nilipata malalamiko kwa njia ya barua pepe. Naomba radhi kwa niaba yake.
Kuna wadau wameomba nimpe adhabu ya kumfungia udau wake, lakini kwa kuwa ni mara yake ya kwanza naomba tumstahi kwa sasa kwani ameniahidi kwa barua pepe kutorudia tena.
Kwa kila picha isiyofaa itaondolewa kwenye FotoBaraza.
Ni hayo tu kwa sasa.Pamoja katika ujenzi wa kijiji.
Babukadja
Mwanzilishi na Msimamizi wa FotoBaraza.
Visit FotoBaraza at: http://fotobaraza.ning.com
Hapa Dubai blog hiyo ya fotobaraza imekuwa BLOCKED, nilikuwa nastaajabu kwanini? sababu sijawahi kuhudhuria huko. Sasa nimefahamu itakuwa ni vitu vilivyomo humo kama hizo picha za nusu uchi.
ReplyDeleteNina hakika patakuwa ni pahala bomba sababu Bob Sankofa namuaminia!, lakini bahati mbaya watu wachache wanatunyima uhondo!
ANAUZA SURA!!!Wabongo kwa kuuza sura imekuwa dili.
ReplyDeleteHivi huwa mnafikiriaga watu wote wanaotoa picha zao kwenye blogu huko wamekaa wanawasubiria nyie mrudi mje muwaoe? Na TZ hakuna wanaume wa kuwatongoza na kuwa nao kama wapenzi kama si kuwaoa,I mean hawana relationship?
ReplyDeleteBasi wasichana wengi wangekuwa mabikira kwa kuwasubiri vidume mrudi! Acheni kuwa na mawazo ya kiwanga na kichawi, mkiona picha tu mnataka kuroga!
yaani wabongo kwa wivu???
ReplyDelete