


Timu hiyo ilifanikiwa kuingia fainali baada ya kuifunga timu ya Jamaica FC. 8-3 katika mchezo wa nusu fainali. Katika fainali mabingwa hao waliisambaratisha Argentino bao 8-4.
Huku ikiwapeleka mchaka mchaka,vijana hao waliweza kupata ushindi kiduchu wa 1-0 hadi karibu ya mapumziko! Ndipo Benchi la Ufundi lilipomwinua "Super Sub' Hadji Helper ambaye alibadilisha kabisa sura ya mchezo! Magoli yalianza kumiminika kupitia kwa Nyota wa mchezo huo Muzi Mswazi hukuakisindikizwa na magoli mwaili mazuri ya Helper!
Mchezo wa leo ulikuwa burudani tosha hasa ukizingatia Kwamba Tanzanite iliwashusha uwanjani wachezaji wake wa kulipwa Elvis "Gaza' Mnyamuru(maximo unaua kipaji hiki) na Amani Kombo( Former Tanzania U-20).
Kwa hakika ushindi wa leo umeleta hamasa kubwa sana miongoni mwa wachezaji, wapenzi na viongozi wa timu hii. Kwa kunyakua ubingwa huu Tanzanite Fc imejishindia seti nzima ya jersey (adidas) na hundi ya kiasi maalum.
NB: Weekend ijayo timu itakuwa ziarani BerminghamAlabama kwa mchezo wa kirafiki.
lazima mshinde, mazoezi kubeba maboksi guess misuri ndo siri ya ushindi! so mbaya wazee baada ya maboksi michezo kuondoa mawazo.
ReplyDeleteHongereni sana Vijana wa TanzaniteFC, naona mmeshinda mpaka mkachukua mashabiki kutoka mataifa mbalimbali hasa yule dada wa Mexico, kweli game lenu kali.
ReplyDeleteKila laheri na safari njema huko Alabama.
Pole na maisha mtoa maoni wa kwanza, hongera kwa vijana wa Atlanta .
ReplyDeleteHongereni vijana kwa kupeperusha vyema bendera ya nchi yetu huko ughaibuni. Ningependa kujua how serious you guys are in football. Tungependa mje kutembelea nyumbani siku moja. Good job!
ReplyDeleteDuh ! tuje nyumbani kutembelea kimichezo au kuona familia zao .
ReplyDelete...wengi mambo hayatulia kiivyo .
We si unaona hata timu ya taifa kusafiri inahitaji msaada wa wafadhili ?
ukipata mfadhili tutakuja, yawezekana baadhi yetu tukashindwa kwa sababu ya makaratasi, alkini timu itakuja kali sana(tutachomeakea majeshi toka Stae zingine) .
Hii timu sasa ni moto wa kuotea mbali-karibu watatuthibitishia kuwa timu bora ya wa-TZ nje ya TZ.
ReplyDeleteKwa picha zaidi please pitia mitandao ya timu:
ReplyDeletewww.tanzanitefc.blogspot.com
www.tanzanitefc.com.
Ahsanteni!!
hongera vijana wa Tanzanite F.C..siku zote mwanzo ni mgumu,lkn kama nia mnayo na uwezo mnao basi mtafika mnakokwenda..msianze kubweteka na huo ushindi wa indoor maana tunajua waTZ wanavyopenda kuvimba vichwa kila wanapoonja mafanikio kiduchu then wanaishia kwenda mbele hatua mbili na kurudi nyumba hatua 30..kama walivyofanya Simba na Yanga..and STARZ next up..msikose kutupa habari kuhusu matokeo ya huko Alabama next weekend hata kama mkikung'utwa 11-0 kama Shelisheli.sio mtuletee habari mkishinda tu alafu mkifungwa mnaingia mitini..you live u learn and peeps learn thru mistakes.
ReplyDeleteMkiwa tayari kiuchumi mje walau hapa Mexico.
ni hayo tu!!