Mstahiki Mkuu wa Wilaya ya Tegeta ambaye bado kuapishwa,
April 18 ni siku ya kumbukumbu ya nchi 'jirani' na rafiki wa Tz. Nayo ni Zimbabwe. Nchi hiyo iko ktk janga kubwa la kisiasa. Lakini anaweza akatokea mdau wa globu hii ya jamii akatupasha yaliyo ya neema nchini humo. Haizungumzwi, lakini kimiundo mbinu wenzetu wamepiga hatua.
Pia swala la elimu. Asilimia isiyopungua 85 kama sio 90 wanajua kusoma na kuandika. Lakini ambalo linanikuna zaidi ni jinsi wenzetu walivyofanikiwa kustawisha muziki ambao unawatambulisha kimataifa! Hapo sijataja michezo kama cricket na soka....
Akina Mutukudzi, Mapfumu...Tukumbushane, kuwa iwapo sisi waafrika wenyewe kamwe hatuoni mazuri uyafanyayo, kamwe wageni hawatatupamba. Tutabaki kulalama.
Majuu sikuzote wanatuchora vibaya kwenye magazeti na tv zao! Lets be positive, about ourselves, wanasema kwa kimombo.
Mdau
Khoti Mwana wa Liti Chilomba Kamanga
Jamani wadau sasa imetosha tafuteni kitu kingine cha kutokea sasa, Maana naona imekuwa kila siku ni kuungana mikono eti na kutuelimisha watanzania wenzenu tuache kukosoana,inamaana sasa mambo mengine hayaongelewi ni kuunga mikono tu.mngekuwa mnauchungu sana na maendeleo yetu mngemtumia hata penseli na madaftari kaka michuzi awapelekee watoto wanaosoma kwenye mazingira magumu hapa kwetu tanzania ili kusudi tupate tanzania ijayo yenye waelewa kama mnavyojiita nyie mnaojitokeza kila mara na majina yenu kuwaunga mikono waliopit,kwani si tumehshasikia,kaka michu alisema watoa maoni wakachangia sasa kila siku na majina jina yenu mnaunga mkono nini sasa.njooni basi likizo mfanye semina au mnataka tujue kuwa mko nje!!!1 haya tumeshasikia,heee tupeni break sasa haya tumeshawakikia.kaka michu tafadhali ikibidi hii iwekwe front page kabisa.
ReplyDeletemdau
Dar
Ujinga mtupu, miundo mbinu si ilijengwa na wakoloni? Hebu angalia tokea janga hili la kisiasa lianze niambie kama kuna kitu kimefanyika? Chakula kilikuwa bwerere leo hii mkate tu kupata noma. Zimbabwe haijitoshelezi kwa chakula wakati baadhi ya mashamba wamenyang'anywa hao wakulima wakubwa, mbona waliochukua hatuoni matokeo? Acheni ujinga hii tabia inabidi ikemewe kwa nguvu zote
ReplyDelete