Michuzi,
Pole na kazi na mihangaiko ya kila siku, maana una kazi hasa hii ya kutuelimisha sie wanajamii kupitia blogu yako.
Nimefurahishwa sana na ujumbe maridhwa alaioutuma dada Mwajuma. Kiumri namzidi sana lakini kifikra naona tunalingana. Haya ndio matunda ya kumuelimisha mwanamke, na ule usemi kuwa ukimueilimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima hapa ndipo ushahidi wake unapoonekana.
Namuunga mkono Mwajuma kwa hayo aliyosema, kwamba umefika wakati sasa watanzania kuacha tabia zetu za vijiba vya roho na unafiki na kuishi kwa kupendana na kusaidiana.
Pole na kazi na mihangaiko ya kila siku, maana una kazi hasa hii ya kutuelimisha sie wanajamii kupitia blogu yako.
Nimefurahishwa sana na ujumbe maridhwa alaioutuma dada Mwajuma. Kiumri namzidi sana lakini kifikra naona tunalingana. Haya ndio matunda ya kumuelimisha mwanamke, na ule usemi kuwa ukimueilimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima hapa ndipo ushahidi wake unapoonekana.
Namuunga mkono Mwajuma kwa hayo aliyosema, kwamba umefika wakati sasa watanzania kuacha tabia zetu za vijiba vya roho na unafiki na kuishi kwa kupendana na kusaidiana.
Mtandao ni maisha ya pili, au second life wenzetu wanasema, na mahala ambako unaweza kutumia kama sokoni kwa manunuzi ya mahitaji mbali mbali vile vile ukakutana na watu ambao mnaweza kuwa na mawazo ya kufanana na mkafanya jambo la maana kwa jamii yenu.
Ni maisha kama yalivyo maisha mengine na haya yamerahisishwa na huu mtandao. Sasa linapokuja suala la kuanza kutukanana matusi eti midamu tu mtu unayemtukana hakuoni sioni mantiki yake kwani Mungu anakuona na dhamira yako itabaki na hiyo dhambi ya matusi mpaka siku unaingia kaburini.
Kuhusu unafiki ni kweli sie tunajulikana kwa watu wa mataifa mengine kama ni watu wapole, wapenda amani, tunapendana, tunawapenda wageni, lakini in reality hivyo sivyo tulivyo! Sisi ni watu wa ajabu sijawahi kuona hapa duniani, hatupendani wala hatuna solidarity, yaani kila mtu yuko against mwenzie kupata.
Afadhali ya walio nyumbani wanaweza hata kupeana vipisi vya sigara au kununuliana bia au kusaidiana hata kwa mawazo, lakini kwa sie tuliyo ughaibuni ni mambo ya aibu tupu hata kuyazungumzia, hakuna lolote ambalo watu wanasaidiana kwa kuwa ni watanzania, bali kwa kuwa tu wana urafiki au wanajuana tangu walivyotoka huko nyumbani. Wako watu waliowachoma (sio moto) wenzao, na huko South Afrika wako waliyowafanyiwa watanzania wenzao mambo ya kinyama kabisa. Huu ubazazi tuanofanyiana katika maisha ya kwanza tumeamua kuhamishia katika maisha ya pili haya ya kwenye mtandao.
Hakuna cha frustrations wala nini ni tabia na roho zetu za ufisadi kiwembe chenye makali kote kote na kuhusudu watu bila sababu za msingi.
Nawashauri wanawake wote tuungane katika hili la kuprotest matusi wanayotupiwa watu kwenye mtandao kwani sie wanawake ndio walezi wa jamii hii ni jamii ijayo, popote pale tulipo tuna jukumu la kuhakikisha tuna jamii yenye mwelekeo, kuwalea watoto wadogo na wakubwa pia!
Hakuna cha frustrations wala nini ni tabia na roho zetu za ufisadi kiwembe chenye makali kote kote na kuhusudu watu bila sababu za msingi.
Nawashauri wanawake wote tuungane katika hili la kuprotest matusi wanayotupiwa watu kwenye mtandao kwani sie wanawake ndio walezi wa jamii hii ni jamii ijayo, popote pale tulipo tuna jukumu la kuhakikisha tuna jamii yenye mwelekeo, kuwalea watoto wadogo na wakubwa pia!
Tusiunge mkono kabisa tukiona matusi yanamimwinwa kwa mwanamke mwenzetu tuwe mstari wa mbele kukemea tabia hiyo mbaya, mwishoe itafutika katika jamii yetu.
Tupambane na kila aina ya udhalilishaji wa wanawake na hata wale waliojariwa kwa kazi za usanii tunaweza kuwasaidia kuepuka kudhalilishwa na waajiri wao kwa kuwekwa uchi stejini wakati wanaume wakivikwa nguo!
Na wanaume wenye kupenda maendeleo na wenye busara jiungeni nasi katika hili kama vile ambavyo tuliweza kutokomeza matusi ya nguoni hasa yanayotamka sehemu za siri za mwanamke kipindi fulani huko siku za nyuma kwa kampeni kabambe iliyofanywa na gender rights activists.
Tunaweza humu kupeana ushauri wa maana na kufanya jambo kubwa la maana kwa kutumia mtandao mbali na kufurahi na kusalimiana.
Na wanaume wenye kupenda maendeleo na wenye busara jiungeni nasi katika hili kama vile ambavyo tuliweza kutokomeza matusi ya nguoni hasa yanayotamka sehemu za siri za mwanamke kipindi fulani huko siku za nyuma kwa kampeni kabambe iliyofanywa na gender rights activists.
Tunaweza humu kupeana ushauri wa maana na kufanya jambo kubwa la maana kwa kutumia mtandao mbali na kufurahi na kusalimiana.
Kwa wale ambao waliangalia the TRIBE, hawa ni watu ambao walikutana online na wakaanzisha wazo la kuwa na sustainable green tourism na walifanikiwa kuwa na hiyo project. Unaweza kusearch hicho kikundi ukaona jinsi watu wanavyoweza kutumia mtandao kuleta mabadiliko katika jamii. Sisemi kuwa hata hao wa mataifa mengine hawatukanani, lakini hatuja haja ya kuiga mambi ya kijinga wakati mambo yenye manufaa kwetu yako mengi.
Atakayenitukana shauri yake mwenyewe anajisumbua bure maana halitang'oa ngozi hilo tusi lakini ukweli lazima usemwe tunahitaji kubadilika and YES WE CAN CHANGE!
Ni mimi Bibi Maendeleo,
Masomoni UK
Atakayenitukana shauri yake mwenyewe anajisumbua bure maana halitang'oa ngozi hilo tusi lakini ukweli lazima usemwe tunahitaji kubadilika and YES WE CAN CHANGE!
Ni mimi Bibi Maendeleo,
Masomoni UK
Haya wewe ni bibi sikulaumu. Ushazeeka hujui unalosema. Naomba ongea na Jovi, si yupo Sudani or Dafur katika kambi ya wakimbizi? Atakueleza nini maana ya kutopendana na kuchukiana.
ReplyDeleteWanawake wa Kibongo acheni hizo muanze kuwaona wanamume zenu kuwa ni watu wa maana na wenye upendo kuliko. Tunajua hampendi kuambiwa ukweli na wengi pamoja na kuwa mmekwenda shule lakini hamkuelimika, si mbaya tutarekebishana humuhumu taratibu. Ninyi ndo wanafiki lakini mnawasingizia wabongo wote, jamani si wote tupo kama ninyi, hatukai kudahani wabongo wengine wanatutenga wakati hawatutengi.
Ninyi ndo mnao watenga watu wenu kwa kuona wa mataifa mengine nin bora kuliko. Wenzenu wanawake wa mataifa mengine wanaogopa kweli strangers yaani watu wasiowafahamu hasa wanaotoka nchi si za kwao. Ninyi mnaona ujiko kutembea na wapopo, wazungu, n.k. mnafagilia wanaume wa nchi zingine bila hata kuwajua vizuri na kudharau wa kitanzania.
Igeni mfano wa Waethiopia wanaweka mbele wanaume wa kwao kwanza.
Mama wahalifu hawapo tanzania tu na si watanzania tu, kwa choyo na husuda kila jamii wapo watu wa aina hiyo. Wamarekani wangapi wanauwa wenzao, wanawaibia wanawatapeli na kudhulumu? Wanigeria ndo usiseme wanajulikana dunia nzima, muulize michuzi anawajua vizuri, blogu hii walishaiteka na kuanza kuitumia kuwaliza watu fedha na mali zao.
ReplyDeleteHao wazungu ndo wabaguzi kupindukia na ni wanafiki kuliko mfano. Wakenya hawasemeki, juzi juzi tulikwenda kuwapatanisha jinsi walivyo na chuki tena bila simile.Wazimbabwe? Wakongo? Wahutu na watutsi? Waarabu kule kaskazini je? Wanawake wao hawaruhusiwi hata kuendesha magari. Wabongo tunachuki, mama chuki gani hiyo? Nakubali ulimbukeni kwa madada zetu nami hapo niwe muwazi wakiona watu wa mataifa mengine wakwanza kujibaraguza. Haya wewe huo umoja unautaka vipi? Nawe ndo wa kwanza kukandia wabongo? Mimi nasema sisi wabongo ni watu wema kuliko mfano na hatuna wa kufanana naye duniani ukizingatia ni masikini, maana hicho kingelikuwa kigezo kikubwa cha kutufanya tuwe wakatili, lakini wapi, tunakaa chini na kushirikiana. Hivi ushirikiano unaousema ni upi? Misibani tupo pamoja, harusini pamoja, kazini pamoja, na kadhalika nakadhalika. Umbea, majungu na fitina vipo kila jamii hapa duniani. Wabongo hatuna jazba, tunaongea kwa msisitizo. Jazba wanayo waarabu na si wote. usipokubaliana nao wanakulipua. Halafu hayo mambo ya watu kuvaa sijui nini nguo fupi uchi unajua wewe, kuna mtu anawalazimisha wanawake wa kibongo kufanya hivyo si ninyi wenyewe mnaona wenzenu nje mnawaiga. Na hili ni suala la mtu binafsi.
Halafu inaonesha upungufu fulani inapokuwa mtu unaomba watu watetee tu mtu kwa kuwa tu ni mwanamke na si kwa hoja.
Sina ubaya na mademu wa kibongo, ila ninasikitika wakikaa kukandia wanaume wa kibongo kwa kuwapa sifa wasizokuwa nazo.
Matusi wabongo hata hawajui, humu watu wanapashwa tu na kutoa maoni kwa mitazamo na njia tofauti. Tunajua wabongo hawajazoea kuambiwa spade ni spade na si watu wa kuzingatia hasa nini wanachoongea mbele za watu kwa kuwa hudhani kila mmoja atawachukulia vile wanavyodhani. Ukweli ni lazima tunapozungumza tuzingatie wenzetu watatuelewaje kabla ya kutamka maneno au kufanya mambo fulani, kwa kuwa hayo ndo hasa huleta mjadala.
WEWE UNAYEMUUNGA MKONO BI MWAJUMA KWA POINT GANI ALIYOTOA?????KUSEMA SISI WATANZANIA HATUNA UPENDO ILA WAPOPO NDIYO WANAUPENDO?????UA WAKENYA WANUPENDO KUZIDI WABONGO?????MSICHANGANYE MAPENZI NA UPENDO WA WANANCHI KAMA MBONGO KAKUTOSA SIO MEANS HAWANA MPANGO WOTE,,,NA UKAPATA MPOPO KAKUPA MAMBO MAZURI SIO MEANS KILA MNAIGERIA MTU MZURI,KUHUSU WATU KUFANYIANA MAMBO MABAYA TUKIWA HUKU MAMTONI,HUKU DADA YANGU TUNAKOISHI KUNAITWA SILI YA JANDONO AU KUMFUNDA MWALI,MAISHA MAGUMU NA HAKUNA MAMA WALA BABA AU MJOMBA WATU WAMECHANGANYIKIWA HIVYO SIO KAMA BONGO, KUKIWA NA UGOMVI MTAENDA KWA WAJOMBA HUKU DADA YANGU UKIZINGUA TUNAMAKIZANA HUKU HUKU....NJOONI NA POINT KINA DADA SIO HIZI...MDAU ULAYA 00316.
ReplyDeleteSina nia ya kukutukana,
ReplyDeletelakin nachosema sometimes kutukanwa huwa mnatakaga wenyewe,
Sasa umetoa comment ndeeeeefuuuuuuu badala ya ku-summerize watu wakaelewa,
Then hata baada ya kuwachosha watu na li-comment lako lirefu kama hotuba ya Raisi then unamalizia na vijembe kuwa eti hata wakikutukana hujali,
Muwe makin mnapoweka maneno yenu, mnajitakiaga wenyewe kutukanwa
Nashukuru kusoma post mbili zenye akili na fikra za upeo kutoka kwa mwanajuma na huyu bibi maendeleo. Nashukuru that kuna watu wanapenda undugu wa kitanzania, I used to have same dream.
ReplyDeleteNadhani tunatakiwa kubadilisha tabia yetu yakutokuwa wawazi zaidi. nadhani inatokana na malezi na mila zetu kwamba sometimes hatusemi kile mioyo yetu inasema. sisi sio wapendanao ingawa tunaishi pamoja ndio maana mpaka leo kuna jamii mtu hawezi kuwa na rafiki wa jamii ingine. ndio maana hata maeneo ya kazi wameajiliana kimakabila huu ndio msingi wetu home. Mchaga akipata deal atamtafuta mchaga sio mmakonde. SO?
Pia kunasuala la jinsi ya kushirikiana pia, nipomasomoni UK nashukuru tupo watanzania kama kumi chuo kimoja na wakenya. But watanzania wenzangu ni mabinti. Inakuwa taabu kwa msichana kuelewa kwamba msaada ambao unampatia niwabure sio kama unamtaka and that ukikaanaye for sometime badaya ya kuchukulia kama brother anaanza kuona anapoteza muda sababu yeye alidhani utakuwa naye. Comeon let us trust each other. Kuna mtu mmoja anasema hataki mtu ajuwe anakaa wapi kwasababu sio kuzuri kwake. Mimi nimetoka kijijini najuwa maisha ni maisha hakuna suala la mtu kuwa muoga.
Let us believe that we can be friends no matter what and how we differ!
All the best,
G7
Sheffield
UK
toa na picha yako basi tumeshakuelewa...unaleta mambo ya manzese humu wala haupo uk
ReplyDeleteSalaam sana mama Maendeleo.Napenda kutoa pongezi nyingi na kukuunga mkono kwa dhati kwa hoja yako hapo juu.
ReplyDeleteKila la heri.
mama Sole.
Nakubaliana na maoni mazuri ya kwako na ya dada Mwajuma.Nakubali kwamba watanzania tunapenda kubaniana sana,na kuoeneana wivu ambao sio mzuri kwa maendeleo ya Jamii yetu ya kitanzania.Lakini natofautiana na wewe unaposema ukimuelimisha mwanamke umeilimisha jamii,je unamaanisha kwamba ukimuelisha mwanaume haujaielimisha jamii,Je utakuwa una maanisha kwamba watanzania wanaume walionje ndiyo wanabaniana tuu.Na dhani itakuwa siyo sahihi kama una maanisha hivyo.
ReplyDeleteHaya yote ni mapungufu yetu kama binadamu.Tunahitaji kuelimishana ilituondokane na matatizo haya.
duh Beijing all over .shusha hiyo agenda ya wanawake utafika mbali changanya jamii nzima.kuhusu matusi ya humu ni kwamba tunaendana na wakati. kumbuka good news is bad news huku watu wanashindana kwa ku hit front page. eg chibiritti manka jovinta na wengine wanajipandishia chati.amka karne ya 21 hii. mwangalie jade wa big brother uk. beckam brand na nyingine nyingi tu . ndo mwendo wakisasa. umaarufu ni vigumu kuja kwa masters au usamaria. ndo maana watu wanachukuwa shortcut.chibiriti akafungue duka kariakoo kesho atalamba dume na watu watasema kaloga kumbe wapi alivumilia matusi humu. haya jovinta anaweza kuuza email za vigogo kwa magazeti ya udaku na kama anakisomo kizuri watamfunika kwa ubunge wa vitu maalum chanzo? mithupu blog.mama maendeleo mtandao umetubadilisha sana wanajamii amka unga bogi.
ReplyDeletegas uk
Bana na si tumchoka na nyie mnayejifanya mna akili! kila mtu anajua anachokifanya sema basi tu! hasa nyie kila siku sera za km mna akiiili..km hupendi kitu shut the fk up anzisha blog yako!
ReplyDeletewe toka huko
ReplyDeleteeti samahani anti uan undugu na hadija kopa?au kikundi chochote cha tarabu?
ReplyDeletePoleni wana blog hii, kwa wote wapenda maendeleo wafikisha ujumbe kwa njia zote iwe kwa kuchafua hewa au kutumia lugha za majitaka au lugha za kumwaga upupu, utani ambao unawawasha wasikilizaji au kwa kutumia lugha murua au lungha ya kumtoa nyoka pangoni, lugha za kiungwana.
ReplyDeleteMimi napenda kutoa mawazo yangu hapa kuhusiana na hili. Kwanza tutambue kuwa hii blog inapitiwa na watu wa aina zote wenye mitazamo tofauti iwe kwa uwezo ufahamu au uumri, hivi vyote vinachangia sana kuleta maongezi ya aina hizo mbalimbali yawe ya busara, upuuzi utundu uongo na blah blah, hivyo basi tukielewa hilo kila mtu asimame kwenye zamu yake kujaribu kufundishana na kuelekezana kwa njia ya upole na upendo badala kutoa kasoro na kejeli kwa wale wanaoonyesha udhaifu mahali flani, naamini mimi na wewe msomaji na mtoa maoni ndio tutakaofanikiwa kulimaliza hili sio kuanza kupeana malawama na kuonyeshana makarama humu kwani vidole havilingani na hata kama kuna kidole kinauwezo mkubwa kuliko kingine, kuna usemi kidole kimoja hakivunji chawa,Kwa pamoja tupendane, tufundishane na kutaniana bila kuvuka mpaka.
Mungu ibariki Tanzania
THE SILENT STALKER SAYS........Amen Dada !!! ujumbe well presented, as a MAN u got all my support in this issue.
ReplyDeleteHongera bibi maendeleo, nakupongeza kwa mchango wako.
ReplyDeleteHata hivyo napenda nitoe maelezo kidogo kuhusu ugumu uliopo katika suala unalodhani ni udhalilishaji wa mwanamke. Kwa mawazo yako, unadhani wanawake wanaojihusisha na usanii (pengine ulimaanisha wachezaji muziki jukwaani) wanadhalilishwa. Pengine ungetoa maelezo zaidi hapa.
Kwa taarifa yako hili suala limekua linajadiliwa sana lakini suluhisho ni gumu kwani kwa upande mwingine ni wanawake wenyewe wanaokubali kufanya hivyo. Pamoja kua ni chanzo cha kipato, kwa upande mwingine mwanamke huwa anajisikia fahari sana kua pambo la dunia. Hebu jiulize kwanini wanawake wanapoteza pesa nyingi kubadili mavazi kila wakati? Kwanini unapoteza muda mrefu kujipamba na kujiangalia mbele ya kioo? Sisemi kua kufanya hivyo ni vibaya ila haya ni baadhi tu ya maswali ambayo unapaswa kujiuliza kabla haujalaumu na kulalama kua wanawake wananyanyaswa kwa kucheza muziki wakiwa nusu au pengine 95% uchi.
Nasita kutoamini kua mawazo yako yameathiriwa sana na juhudi za wanawake duniani kupambana na mfumo dume. Kuna makosa mengi sana yanafanyika katika juhudi hizi. Kuna upotoshaji mkubwa kuhusu dhumuni hasa la juhudi hizi.
Kwa faida yako na wengine, naomba tujiulize ni faida gani tunataka kupata katika kutokomeza hali hizi tunazoita unyanyasaji? Je hizi juhudi ni kipaumbele chetu kwa wakati uliopo? Haya ni baadhi tu.
Ujerumani ni nchi yenye idadi kubwa ya divorce... (40% mwaka 2002). Kwa sasa limeonekana ni tatizo na kushawishi mijadala. Moja kati ya sababu zinazotolewa ni hali ya wanawake kudhani kunyanyaswa katika kufuata taratibu fulani ndani ya ndoa. Sidhani kama hili ni baya, ila ninachotaka kuonyesha ni tafakari tunazopaswa kuzifanya kabla ya kutoa majumuisho au misimamo.
Ningependa kutoa tahadhari kua tuwe makini pale tunapotaka kueleza jambo ambalo pengine linaathiri au ni mawazo ya wachache na sie kutaka kulifanya liwe general.
Mwisho kabisa, inaaminika na kuthibitishwa kua wanawake wenye uwezo mkubwa kiuchumi wana nafasi kubwa ya kutoathirika na unyanyasaji kuliko wanawake wanyonge kiuchumi. Hivyo moja ya juhudi za kumtoa mwanamke katika wimbi la unyanyasaji ni kumpa uwezo wa kiuchumi na mengine yanafuata.
Ignorant,
Jeremani
Kweli kabisa Bibi Maendeleo umesema... unafiki umezidi baina yetu, hatupendani tunaoneana wivu kwa vitu vidogo tu!! je tutafika kweli.. ushirikiano hatuna kabisa.. umaskini wa roho!!!!! Kama ulivyosema ukweli nilazima usemwe, wache watakaosema waseme...
ReplyDeleteNapenda nikupongeze Bibi Maendeleo kama ulivyojiita, ni kweli kwamba watu wamekuwa wakitumia lugha ambazo si za kiungwana.
ReplyDeleteKatika mjadala wowote si lazima mchangia maada ukubaliane na mtoa maada na wala si ajabu mawazo yako mchangiaji yakawa sawa na mtoa maada. Kwa kifupi ni kwamba haingii akilini kwa kuanza kumkashifu mtu anayetoa mawazo yake, iwe unamjua au haumjui.Muungwana yoyote usikiliza na kupima yanayoongelewa. Kwa mtu makini hasipokubaliana na jambo anataoa sababu zake, kwamba mie ili jambo silikubali kwa sababu a,be,na che! Na kwa mtazamo wangu naona ingekuwa de,fe na ge!! Lakini utakuta mtu anaanza hooo gauni ulilovaa ni la valentine na mie ninae valentine wangu! Nani kakuuliza? Kwani maada ilikuwa gauni au mahusiano ya wabongo ndani na nje ya tanzania!
Maisha ni mtazamo kuna walio bahatika kukutana na wabongo wenye roho nzuri ya utu na wakafurahia kukutana nao katika maisha yao, na vile vile kuna waliokutana na wabongo ambao kukubalika kwamba ni binadamu ni jambo gumu! Napenda kukubali kuwa tupo nyuma katika maendeleo nawala nchi yetu si ya kwanza kuwa masikini, lakini kama kila mtu atachukua jukumu la kufanya kazi nina uhakika tutafika pahala kizazi kijacho kitafurahia kuitwa mtanzania. Achilia mbali mambo ya kifasadi na mengineo yanayo endelea. Lakini ipo nafasi ya mtu mmoja mmoja kubadilika na kubadili jamii inayomzunguka.
Hongera Dada Mwajuma, Bibi Maendeleo na wengine wenye mtazamo kama wenu.
Naomba niwakumbushe msome makala ya Padri Karugendo (Raia Mwema ya wiki iliyopita)..http://www.raiamwema.co.tz/08/04/09/karugendo.php
Huna kazi wewe! Unatuandikia utenzi suo navina wala maana, si urudi kwenu ukaimbe taarab, hovyoo kama mchuzi wa magozi, ungeweka sura lako hapa...!
ReplyDeleteHivi huwa nikutafuta publicity, kutafuta u celebrity au ndo ilimradi net ya bure unadike tu! Sababu naona kuanzia sentsnsi ya mwanzo mpaka ya mwisho, pumba tupu, unaongea vapour tu, au tuseme unaongea virai!'
You better go straight to the point kama unatafuta bwana au vipi? Na mtakufa na utaula na chuwa, karne hii kama ulishindwa kujitunza, utakufa na utamu wako kama muwa, wanaume wako very focus! We sasa utaishia kunuma numa kwenye blog kutafuta umarufu au kumalizia ma frastrution yako!
Humpati mtu hapa kikojozi we! Hivi mwanamke mwenye kazi, busara na heshima yake anapata wapi muda wakukaa akaandika upuuzi kama huu!
Maana hata hajui anaongea nini, utafkiri kuku mpapúro mwenye vifaranga (alotoka kuanguka muda si mrefu), anachachawika tu hajui hata asema nini!
Nendeni shule kwanza mkasome, mpate elimu ya psychology ndo utaweza kujua umuhimu wa mgongano wa mawazo!
Hem ni sign off niwahi kumsaidia wife kufua nguo...
OYAAAAAAAAA. BIG UP MZEE JOHN SAMUEL MALECELA KWA MTAZAMO WAKO WA UZEENI WA KUTAKA SERIKALI IHALALISHE GONGO NA ITENGEZWE KWA KIWANGO KILICHO BORA ZAIDI.
ReplyDeleteNADHANI KAMA UNGEKUWA NA MTAZAMO HUU WAKATI ULE ULIVYOKUWA WAZIRI MKUU, MAMBO YANGEKUWA MSWANO MGOGO MWENZANGU. TATIZO UMECHELEWA NA SASA HUNA TENA YALE MAKALI YA PM!
LAKINI KWA KUTOA SWALI LA NYONGEZA HUKO BUNGENI, UMEONA MBALI NA ITASAIDIA KUWAPA KIPATO WAJASIRIMALI. POMBE ZA KIENYEJI ZOTE HALALI KWA NINI GONGO ISIWE HALALI KAMA DENGERUA, CHIMPUMU, ULANZI, ULAKA (MNAZI), MBEGE, KANGARA NA NYINGINE JAMANI NISAIDIZENI WANYWAJI WENZANGU.
KWA MTAZAMO WANGU MIMI, NADHANI GONGO INATENGENEZWA KWA KIWANGO CHA JUU KULIKO POMBE ZOTE ZA KIENYEJI KWANI UKIKOSEA KUCHANGANYA MADAWA, MZEE WANGU INAKUWA MAJI YA KUNYWA BADALA YA GONGO!
HILI LITAKUWA PIGO KALI KWA KIWANDA CHA BIA, KONYAGI NA HATA CHIBUKU(KIBUKU) KWANI HAKUNA ATAKAYEKUBALI KUPOTEZA ELFU KUMI AU ZAIDI WAKATI ULEVI WA HARAKA WA GONGO HAUGHARIMU ZAIDI YA ELFU TATU. HIYO NA SODA YA COCA JUU.
HAYA WADAU WA KONYAGI KAENI MKAO WA KULA HASARA SASA KWANI MAMBO YANAONEKANA MSWAAAAANO KWA WAPENZI WA GONGOOOOOO. LIT IT UP
Bibi maendeleo,Point kwakweli umeziweka vizuri. Mimi ninaku-support.Kwa upande wangu naamini kwamba atakaye kutukana kwa haya uliyoyaongea au kwa mengine then FOR SURE atakuwa ana "psychiatric problems".Anyway tuone ingawa huwaga hawakosekani..
ReplyDeleteUwezi kutushauri mambo yako wakati wewe mwenyewe hauna confidence, we ni anon. and we are not sure who you are!!! endeleeni kulea mimba za west africans ana wazungu alafu mseme maendeleo sawa eh! Ukiweza kwenda kuwaambia wazee wenu kule kijiji ulitoka ingekuwa bora labda utapata unachotaka si umekuja UK ukakuta mtandao bue ndio unaanza oh! bla bla zako na essay zako sioni mpya we are the one tumesaidia all southern african countries warundi na wakongo uganda and the like leo uje kuanika ujinga wako atii hatuna...sikubaliani na wewe kama uwezi kuvalue kwako kwanza na kupenda ndugu zako na wanaume wa kwenu bado mwaya Upendi maendeleo wewe bibi
ReplyDeleteBADO TU MNAANGAIKA KUMPIGIA MBUZI GITA?
ReplyDeleteinasikitisha kuona wanawake wa kitanzania kuona sisi watanzania kuwa ni wabinafsi na kashfa nyingine nyingi tu na kuwaona watu wa mataifa mengine kuwa wapo safi wa kuigwa kitabia, wakati ni kinyume kabisa cha mambo, sisi ndo tunafaa kuigwa kitabia.
ReplyDeleteNatambua kuna baadhi ya watu, si wabongo tu, bali hata mataifa mengine wanudhaifu wa kujiona hawafai na hivyo kuwaona wenzao wa taifa moja kuwa matatizo. Na kuamini kuwa watu wa mataifa mengine hawana kabisa shida na ni perferct. Huku ni kujidanganya na ni ulimbukeni ulotusababisha mpaka tukawa watumwa kwa wageni walipokuja africa mara ya kwanza.
Isingelikuwa baadhi ya watu wetu kuwaona waarabu na wazungu kuwa bora kuliko sisi wala wasingeliwakaribisha na wengina hata kuwauza watu wao utumwani.
Mtu yeyote anayedhani kuwa wabongo hatufai, hatushirikiani, hatuna maendeleo, huyo ni mnafiki na ni mtumwa katika karne hii ya 21.
Wabongo wangapi wanamaendeleo? Na wala si wabongo wote maskini, ingawa wengi ni maskini wa elimu na hivyo fikra.
Hili la umaskini wa elimu na fikra si kosa letu ni kosa la serikali na uongozi ulopita huko mwanzo, wangelizingatia elimu hasa tungelielimika na kuona vile tulivyo watu safi, wema na matajiri.
Mimi sishangai kuona mtanzania mwenye masters kuwa na fikra hizo kwa wabongo ukizingatia kuwa tangu shule ya msingi hakuona waalimu madarasani kuja kufundisha na vitabu hakuna na hata maabara hazipo. hiyo Jiografia angeijuaje? maarifa ya nyumbani je? Historia na siasa ya nje, mahusiano ya jamii na
saikolojia. TV zenyewe na video tumeanza kuziona baada ya Nyerere kufa na tumekuwa busy kutazama michezo ya kina bishanga na sinema za kipopo na mtoni pamoja na tamthilia zao. Huyu mtu sasa yupo busy pia na kazi huo muda wa kujifunza mambo ya uhusiano na mataifa mengine atautoa wapi? Ila kwa kuwa alisomea kufaulu mitihania na kashakuwa mwanataaluma na pengine hata hiyo taaluma yake hawezi ifanyia kazi ipasavyo, hivi niambieni ni wangapi wamesoma taaluma fulani hapa bongo halafu baada ya mahafali wanashindwa kabisa kuitumia taaluma hiyo kazini na ni kazi hizohizo walosomea?
Wabongo wengi wanaamini kuwa kila wanachokiona katika tv na sinema na tamtjilia za nje kiko hivyo hivyo. Hawaijui hali halisi na si wa kuwalaumu kwa kuwa ndo upeo wa elimu walonao, ingawa wengine twawaita wasomi, wanafanya mambo tofauti kabisa na madarasa yao, wakikemewa, oohho tunatukanwa, wanawake tunadhalilishwa. UPUUZI MTUPU.
Wote mnaopiga makelele ya kuhusu kubadilika. Kwanza nyie inabidi m-badilishe mitazamo yenu. Mkumbuke hata vidole havilingani ingawa viko katika mkono mmoja. na shilingi ina pande mbili. Kusemwa ovyo na kusemwa vizuri yote sawa. Na wewe Mkuu wa wilaya tumia busara sio kutuwekea hoja hizo hizo kila siku.
ReplyDeleteAngalia huyu dwanzi,hii style ya kuzunguka mbuyu sijui mnaitoa wapi,si useme tuu unamtaka huyo bibie...kwanza kishasema kaolewa sijui unataka nini,mwandikie email kisiri siri sio kutupa lecture zisizoeleweka hapa
ReplyDeleteHi,
ReplyDelete!!!Tumekuelewa mama maendeleo lakini picha picha,contact na cv jamani viko wapi....??!!!
Baba Maendeleo,
USA/MN.
CAN WE DROP THIS TOPIC ALREADY?DAMN,AM SICK OF THIS,WATU UMESHATOA MAONI YENU,WHY DO WE HAVE TO BACK TO SQUIRE ONE?
ReplyDeleteKAKA MICHUZI WEKA TOPICS NYINGINE PLIZZZ,HII INABOA SASA!
i bet everyone has the eyes to see n ears to hear,...and u don't be a genius or even hold a PHd. to understand this kind of trends,Just work on ur own to have enough to help even the NEEDY,always never dream to be a RECEIVER,...better give than receive,ushirikiano unakuja just by default usipokuwepo it is alrighty u can force or try make people understand that they already know that WHY people get frustrated when needing people to act accordingly while they NEVER act,....!!ya all Be blessed and have my best LOVE YOU ALL
ReplyDeleteHALAFU JAMANI JIFUNZENI KUSAMARAIZI maana watu wanaandika sana Hivi kuna mtu wa kukaa na kusoma hiyo NOTE ndefu kwenye hii moving fast busy WORLD?? atasoma moja nyingine ataacha!!
Mdau....India!!
Unajua saa nyingine mi naona hawa wanawake hawajui wanataka kitu gani katika jamii.kama huyu anaeungwa mkono nimeona kasema eti watanzania hatupendani alaf kataja mataifa kama naijeria na kenya.Hivi alifanya research akaangalia tabia za hawa watu for really au kakurupuka baada ya kukosa bwana wa kibongo?Inshort kawaulize hata hao watu wa nchi nyingine walizotaja kuwa wanapendana watakueleza ukweli kuhusu tabia zao..Woote ni crap, especially wakenya ni wabinafsi.
ReplyDeleteNa kuhusu swala la matusi kwenye blog, Hivi hii ndo blog yenu ya kwanza kutembelea?Mimi ni mpenzi wa sports na ni mchangiaji mkubwa wa comment kwenye BBC 606 sports page, pale ikija comment yenye akili unakuta kuna watu karibu 10,000 wamechangia kwa siku na ukifatilia kati ya hizo karibu 75% zitakuwa zinakwenda against na mada iliyotolewa.Lakini huwezi kukuta moderator wa pale ambae ni Alan Hansen (mchezaji wa zamani wa Liverpool) anazifuta kwa sababu wanaamini kuwa unapomruhusu mtu kuongea kwa kupinga inakufanya upate msimamo wa watu, hata kama imeongelewa kwa njia mbaya.Watanzania Tatizo letu hatupendi kuelezwa ukweli, nadhani tunaponzwa na zile sera za "Ndio mwalimu" au "zidumu fikra za mwenyekiti". Kubali au kataa katika jamii huwezi kuwafanya watu wote wafikirie sawa, lazima kuna positive na negative, jifunze kukubaliana na hayo matabaka mawili.
Na kwa nyie dada zangu, acheni ulimbukeni kuona kama wanaume wa kibongo hawafai au vipi...kabla hamjakimbilia kwenye conclusion za kijinga fanyeni kuchunguza, walinganishe hao wanaume mnaowasifia na hawa wa kibongo (wa UK mnaelewa namaanisha nini).Kila siku wanaijeria wanwatungua mimba na kuwaacha mnahangaika alaf eti leo unakuja kusifia..wat the fuzle?
Kwa style hii wallahi mtazidi kubaki kuwa chini.
Ukarimu wetu wabongo ndo umasikini wetu. Hivi fikiria ni kiasi gani cha muda na mali tumetumia kuikomboa afrika, kutatua migogoro, kuwafundisha upendo waafrika wenzetu na nini maana ya kushirikiana, kuwahifadhi na kuwapa misaada mbalimbali.
ReplyDeleteJamani, halafu bado twaitwa tusiopendana, tena na watanzania wenzetu? Hivi ninyi kina mama na wa baba mnaowafagilia hao mwaishi wapi? Mmesoma kweli historia yetu ninyi? Mwaijua dunia hata kiduchu tu, acha ile mtu unaletewa tiketi panda ndege nenda mahala fulani, kaa kula bure, sanifu wabongo.
Niambie nchi kubwa kama South Africa, ni siye tumeikomboa na kuwafundisha hao makaburu faida ya kuacha ubaguzi na wazuru na wenzao jinsi gani wanaweza kuishi wote katika nchi hiyohiyo. Lakini wabongo leo wakienda huko wauawa ka kuku. Zimabbwe tumeipa uhuru na leo hii tunazungumzia jinsi ya kuwafundisha kuvumiliana na kushirikiana.
Ninyi watu wapotoshaji na msojua maana, wanafiki, wambeya hamna lolote na ni watanzania wenzetu, leo hii mwakaa kutupaka matope na kuona eti wakenya, wadosi, wapopo na kadhalika kuwa bora zaidi?
WANGA WAKUBWA NINYI na mnamifadhaiko yenu binafsi msituletee humu. Wabongo tunajua kupashana na kurekebishana na mwisho wa siku tupo mpamoja, na huu ndo huitwa UBINADAMU.
Blaza misupu hongera kwa kuanzisha blogu hii, maana bila hiyo wengine tusingelijua kuwa wanawake wetu wenyewe ndo wasaliti wetu wakishirikiana na baadhi wa wavaa suruali.
MNATISHA KAMA NJAA
Hayo yaliyosemwa hapo yana ukweli fulani, hasa huko Ukerewe, utakuta Watanzania wanaishi katika makundi, wabara na wazanzibari, na hata hao wazanzibari nao wamegawanyika, wapemba na waunguja. Kusaidiana ni kwa kujuana, hata hao wanaojuana hawana msaada na wenzao, hasa hao wapemba kina Bablii ndio usiseme kabisa tena midamu wao wanakula pesa ya 'bibi' basi hawataki hata kuwasadia jamaa zao. Kuna watoto wametoka kwenda kusoma huko UK na wamewakuta jamaa zao wakimbizi, jinsi walivyochuniwa wengine wameshindwa hata kuwapa msaada wa mahali pa kuishi japo kwa muda jamaa zao wakati wao wanaishi nyumba za 'bibi' na wanakula pesa ya 'bibi'. Na hao wanaokula pesa za 'bibi' wengine kwa upemba au urundi au unyarwanda au usomali ndio wanaongoza kwa kuchomeana.
ReplyDeleteNgoja niishie hapa kesho nitamwaga mtama zaidi hasa kuhusu hilo kundi la kina Bablii, na wenziwao. Maana watu wanabisha wakati vitu vipo ukweli na ugonjwa huu umeenea sana huko UK.
jamani humu kijijini kumeingiliwa na pepo mbaya sana naona kinadada wanapagawa. misupu inabidi ufanye tambiko hali inakua mbaya kabla hajatokea mwengine kesho akatoa hotuba,
ReplyDeletewewe sio bibi wa maendeleo wala nini. wewe ni MWAJUMA umeamua kuja na style nyengine, HAHAHAHAHAAAA tumekushtukia
ReplyDeletena tabia ya kuja na hoja zenu zisizokua na mpango muache leteni ishu za maana, kama mtu amekukera mueleze sio unatumia hii blog kumfumbia mafumbo, hatutaki shari humu wala kuchochea ugomvi kwenye kijiji chetu NO.
Mbona watu ni kulalamika tuuuuuuuuuuuuuuu...Mimi nafikiri watu wanaolalamika ndio wenye majungu wenyewe...
ReplyDeleteWanaolalamika kila siku ...hivi wivu au majungu ya mtu yatakufanya usifanye mambo yako unayotaka kufanya katika maisha yako? Wivu wa mtu utakufanya usisaidie watu na jamii yenu nyumbani...
Majungu yanakuaffect nini katika kusaidia maendeleo ya nchi yako?
Mimi naishi na watanzania wenzangu hapa USA...ring yetu ni nzuri sana...Na watu tunasaidiana sana kimawazo, raha na shida.....
Hapa tupo kwenye hii community yetu tupo ambao tunaishi karibu sana...(naongelea dakika kumi au ishirini)...na kuna wengine wengi wanakaa umbali wa saa moja hadi masaa matatu.....na kila mtu ana maisha yake. Always uwezo haulingani hata siku moja hata mtu ukiwa unaishi nje ya nchi....Kwa group letu kuna watu wanaendesha magari ya nguvu sana tu na kuna watu wengine wanaendesha magari ya kawaida sana tu na wengine hawana hata magari.....Kuna watu wamejenga huku na kuna watu bado wanaishi nyumba za kupangisha. Kuna watu wanaoenda Tanzania kila summer na kuna wanaoenda baada ya miaka miwili or so na kuna watu wengine hawajaenda Tanzania toka wameondoka huko....Kuna waliooa na kuolewa, kuna singles na kuna wengine wana watoto wala hawajaolewa au kuoa......lakini hamna anayemdhau au kumsema mwenzake....manake kila kitu kinaeleweka huku....
Kama nikusaidiana kimawazo, michango au hata kutafutiana kazi tunasaidiana sana tu......na wala hatusemani kuwa huyu ni doctor, au huyu ni mwalimu au huyu anafanya kazi nursing home...tunaheshimiana vizuri sana tu ....
Mimi naona charity starts from home ...Ukimwonyesha wenzako upendo nao watarudisha upendo kwako...Ukiwasema wenzako nao watakusema....Ukiwa mnafiki na mmbea utapata marafiki wanafiki na wambea....
Mnosema watanzania hatupendani tuna majungu ...mna vigezo gani? Mnaosema watanzania tumejisahau huku nchi za nje mna maana gani? Mimi nadhani hao watu wanaoona hivi waanze kujichunguza wao kwanza kabla ya kuja kulalamika huku.....
Nyie manaolalamika kuwa watu wanaparty...hivi mlienda mara ya mwisho lini Tanzania? ...Baa na sehemu za kustarehe zimefunguliwa nyingi tu kila mahali kuliko zamani na zote zinajaa sana tu hata weekdays...
Lets be serious now....
Manaosema tuongelee maendeleo ya nchi yetu and then what????? Kama kungekua kinaongelewa kitu na action, michango au kitu fulani kinafuata kweli hapo ningeelewa...yaani kuongea tu halafu watu wa nyumbani wazidi kuteseka and then hapo muone kweli mnachangia maendeleo ya nyumbani.....kama ni maendeleo ya nyumbani binafsi najua watu wengi wanaoishi nje ya nchi wanasaidia sana tu familia zao huko kwao kwa njia moja au nyingine.....Kama ni maendeleo ya nchi kwa ujumla hilo ni la raisi au mabalozi wetu wa nchi za nje kushirikisha wananchi wote wanaish nje ya nchi kusaidia...Mimi mtu wa kaskazini hivi leo nitatuma hela yangu kweli ziende Mtwara kusaidia maendeleao ya nchi from nowhere? Hapo hamna cha uongo...kama nina hela nahitaji kusaidida kitu ....100% ni huko huko nilikokulia....
Mwaka huu tumeanzisha kitu ambacho naona ni kizuri sana. Tumeamua kila miezi miwilli tuwe tunachangisha hela halafu tunampa mmoja wetu ....yeye anawapa watu wa kijijini kwao kufanya project moja... Tunamake sure wamefanya kilicho hitajika.... February tumeshasaidia mwenzetu kumaliza paa la kinisa lao...Mimi nadhani ingawaje mambo hayo tutakua tanasaidia sio makubwa ...lakini ni towards maendeleo ya nchi yetu.....
Kama kila comminity itafanya kitu chao kusaidia Tanzania tutafika tu...Kwavile tukisema watu wote tulioko USA tuanze kuchangishana ili kupeleka hela Tanzania bila usimamizi wa kiongozi yeyote wa nchi...itakua uongo.....Na kusema kudiscuss huku kwenye blog maendeleo ya nchi yetu tu ...haita wasaidia chochote wanachi nyumbani....
Kama picha za sehemu za nchi zikionyeshwa kila mara ni vizuri sana ili wanaotoka kwenye hizo sehemu tujue nini cha kufanya kuhelp out....kwa vile huku tuliko hatumjui hata balozi wetu ni nani.....Na pia hizo picha zinasaidia kuonyesha hali halisi kuna wengine wamekulia mijini, wengine wamekulia kwenye utajiri na wengine wameondoka Tanzania muda mrefu....haya mambo hawajui au wameshasahau...hizi picha zinawaelimisha wengi sana na kionyesha hali jalisi na kufanya tusisahau tulikotoka....
Mjue kuwa ingawaje tuko mbali na nchi yetu na wengine tumeshaishi huku miaka mingi sana lakini wote tunaipenda nchi yetu sana tu.....
Hey.... nyie mliopo huko Cabada na UK karibuni mjoin community yetu hapa....hamna majungu wala nini...mkija na majungu mtaishia kujisema wenyewe, kama ni umbea utaishia kuweka kwenye blog manake hamna mtu mwenye muda wakusikiliza majungu...na wengi tunawadharau....
Wewe kibibi na mwenzako mwajuma kaeni kwanza chini alafu anzeni upya ndio maana ukaitwa kibibi umezeeka sana ok asante.
ReplyDeleteWewe kibibi usitufanye sisi watoto wadogo kwannza KAKA MISUPU NAOMBA HII COMMENT USIIBANIE NIMPE KWANZA UKWELI HUYU KIBIBI kwanza hata wewe kaka MISUPU angalia kwa makini hii habari nani kaandika kwa mtazamo wako?asitake kutufanya watoto wadogo unatuzungusha vichwa kama hatuna akili kwenda zako wewe huna dili ni wewe ndio umeandika hii messeg usitake kujifanya eti wewe ni KIBIBI huna dili kabisa kwanza umekosa kazi za kufanya unakuja kufanya bia.....ra online kweli kizuri cha jiuza kibaya chajitembeza sisi kama sehemu ipo sawa tutasema kama sehemu ipo sio sawa lazima tuponde kwa sana maana mmezidi sasa maana mnataka kutuharibia blong yetu acheni mambo ya kifara na usiludie tena maana unatuma mada alafu unajijibu mwenyewe unajifanya eti wewe KIBIBI kwanza ustake kutuchafuria jina la U.K wewe U.K unasomea nini unasomea cleaning au nini maana mtu mzima na akili zake hawezi kukaa chini na kuweza kuandika hizo habari alafu anajijibu mwenyewe kwenda zako huko huna dili sisi tunabadilisha ngozi nyeupe kwenda mbele sasa wewe utaishia hapa hapa online huoni hata haibu alaaaaaaa.
ReplyDeleteWatanzania Tuna sifa moja kubwa hata kama tutatukanana baadae tukaa pamoja na kunywa pamoja au kucheka pamoja.
ReplyDeleteUndugu wetu upo tu na hii inathibitika hata hapa watu wanatukana kwenye comments lakini bado hatuchukiani tunapendana kwa hiyo.
Napendekeza kuwa watu wawe huru kutoa maoni yao hata kama wengine wataona ni matusi ila uhuru wa kutoa maoni udumu.
Mwaushe Ohiwa
Kaaaziii kweli kweli
ReplyDelete