huyu ndiye athumani iddi 'chuji' aliyefunga bao muhimu jana taifa staaz ilipotoka 1-1 dhidi ya uganda huko kampala na kuisongesha mbele timu yetu kwenye michuano ya kwanza ya afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani. staaz imepita ngwe hiyo kwa mabao 3-1 baada ya kushinda katika mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa ccm kirumba kwa magoli 2-0, mabao yaliyofungwa na emmanuel gabriel na shabani nditi.
staaz imeweza kuweka rekodi ya kihistoria katika soka kwani hayo ni mafanikio ya kwanza katika ardhi ya waganda tangu mwaka 1984, ikiwa ni miaka 24 baada ya Stars kushinda kwenye uwanja wa Nakivubo.
katika mchezo huo staaz iliyoundwa na juma pondamali, mohamed bakari 'tall', jellah mtagwa, juma mkambi 'jenerali', makumbi juma 'homa ya jiji', charles boniface mkwasa 'master', zamoyoni mogella 'golden boy' iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, ikiwa ni baada ya kufungwa nyumbani bao 1-

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2008

    mimi sijui sana mpira, ila huyo Charles Bonifance Mkwasa bado anacheza soka kwani? mbona yeye ni kocha au sina memory,halafu si ni Mke wa Betty mkwasa? sasa kwenye mechi amehusikaje, sasa hapo Michuzi umemuweka Charles mkwasa kama nani? mbona binafsi sijaelewa, mwenye kujua naomba ufafanuzi.

    Dada T.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2008

    Staz imewezaje kuvunja record ya waganda kutofungwa nyumbani kwao na staz kwa miaka 24 kwa kutopa draw? Tumewafunga ndio lakini record yao ya kutofungwa uganda na staz bado hiko pale pale labda kama ulikuwa unamaanisha kwamba hatujawai kuwafunga toka miaka 24 iliyopita.unaweza kunieleza vizuri manake itakuwa noma kama hatujawahi kuwafunga toka miaka 24 iliopita/

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2008

    Issa michuzi nyuma kule kuna comment mtu kauliza kwanini umesema "UKWENI" najaribu kumfahamisha, Ukweni Bw Issa Michuzi ndio kwenye wakwe zake Uganda huko. Tanzania Inshaallah tutafika mbali kama tutajiamini, Waleteni wa Sudan tujifunze kushinda nje ya nchi si chini ya mabao 2.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2008

    Maximo alisema hachukuwi timu ya Taifa mchezaji mwenye umri zaidi ya miaka 24.

    jee MBona LAMPARD FRANK ANA 29.DROGBA ANA 30,MICHAEL BALLACK 32,MAKELELE 34,KOLE TOURE,GALAS WILLIAM 32,

    DAVID JAMES 35.ROBERT CARLOS 33,GILBERTO 30.

    JOHN TERRY 27, GARY NEVILLE 32,HENRY 30,KANU 31. YAKUB,GIGGS AMEJIUZULU AKIWA NA MIAKA ZAIDI YA 32.

    GATUSSO ,CANAVARRO,PILLO WOTE ZAIDI YA 30 NA WANACHEZA TIMU ZAO ZA TAIFA.

    NA HAMTAKI JUMA KASEJA ANASEMA NI MFUPI.INAONEKA HUYU KOCHA HAJUI ANACHOKIFANYA. KILA SIKU KIKOSI KINA WACHEZAJI WAPYA.

    TIMU HII INA SHINDA KWA KUDRA ZA Mwenyezi Mungu.

    Maximo hatufai jamani.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2008

    kweli wewe ni dada , umesoma haraka haraka, alikuwa nakuelezea timu ya taifa iliyocheza na uganda mwaka 84, rudia tena kusoma dada,

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2008

    anony unayesema MAXIMO HATUFAI, na pengine unataka watu wa kusaport, kwanza wewe inaelekea sio mwanamichezo na hufahamu kabisa soka la tanzania,

    1.kumbuka kuwa mbali ya kumwajiri Maximo bado jukumu la kutengeneza timu ya taifa liko mikononi mwetu, hivyo kasoro unazoziona ni sisi wa kulaumiwa!! usitegemee umwajiri mtu kazini au ofisini kwako aje kukufanyia kazi mpaka zisizostahili, kuna mambo anafanya mwajri na kuna mambo anafanya mwenye ofisi au kiwanda.

    2.sababu alizotoa Maximo ni kuwa anataka kutengeneza timu ya kudumu ya taifa staz, yaani ile ambayo itadumu angalau muda mrefu, kwani hivi sasa hatuna timi za vijana wadogo amabo wanaweza kuchukua nafasi za wakubwa wakistaafu au likitokea lolote let say ajali kama ile ya Zambia.Maximo anatoka taifa amabalo wana uwezo wa kuunda timu 11 bora za taifa, sijui umenipata, yaani vikosi 11 tofauti vya timu ya taifa na vyote vikawa vizuri.

    3.Unaposema maximo hatufai, ni bora kwa ufahamu wako uka sema nani anafaa ili iwe rahisi watu wakayafanyia kazi maoni yako, hili si hapa tu popote pale atika maisha yako nibora ukalaumu huku ukiwa na ufumbuzi watatizo.

    mdau
    canada

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2008

    Wewe mtoa maoni wa Tarehe May 19, 2008 2:59 AM, Mtoa Maoni: Anonymous.

    Ninaamini wewe akili huna. Unasema timu inashinda kwa kudra za mwenyezi mungu mbona hapo kabla ya kuja kwa huyu kocha,hizo kudra zenu hazikusaidia?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 19, 2008

    we dada T kama hujui soka kalale tu issa kakwambia kuwa hiyo ni stars ya mwaka 84 na Charles Boniface Mkwasa Master enzi hizo alikuwa mmoja wa wachezaji na ni mume sio mke wa mkuu wa wilaya sijui ya wapi Mama Betty Mkwasa Zamani alikuwa mtangazaji wa radio Tanzania

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 19, 2008

    haya mkubwa, anon wa 2:59am tushajua kuwa unayemtaka wewe ni KASEJA....!!! kwani kaseja asipodaka kuna kosa gani? yale yale ya simba na yanga hapa...hatutaki, kama kocha hamtaki basi...subiri utakapopewa wewe taifa stars ndo umpange uyo kaseja wako

    maximo anafanya kazi yake

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 19, 2008

    Anony wa Tarehe May 19, 2008 2:59 AM, kuna article moja michuzi aliiandika nadhani kwenye daily noize akimhoji Maximo na humo ndani ameweka bayana kwa nini timu ya taifa inaonekana hivyo. Alisema kuwa lengo lake ni kutengeneza pool ya wachezaji wanaoweza kuchezea taifa na kwenye pool hii ndipo atakuwa anachagua wangapi wa kuwaita kambini. Alisema kuwa nchi nyingi zinafanya hivyo kwa mfano RSA, Portugal, Brazil, USA etc - ukiangalia nchi hizo tatu za kwanza zina makocha wa kiBrazil, wao na kama USA wana wachezaji mathlani 40 ambao wanaweza kucheza timu zao za taifa. Kwenye article hiyohiyo amesema kwamba ameshachagua na kuona wachezaji wa kutosha na tutegemee kuona timu iliyotokana na wachezaji wooooote aliyewachagua tangu amechukua taifa stars.

    Vilevile, record ya taifa stars inajibu maswali yoote kuhusiana na kocha - 10 wins,5 losses, 9 draws (or something like that)Tena siku hizi tunafunga magoli ugenini!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 19, 2008

    We Anon wa 2:59 ndiye huna hata idea na mpira,au labda hujui timu ya TZ.kama huna la kuchangia changia huko ktk miss TZ EU.Maximo alisema anapendelea wachezaji wenye umri mdogo,lakini sio kwamba hachukui zaidi ya miaka 24. Kwa taarifa yako,kuna wachezaji wengi tu ktk timu hii wamezidi miaka 24,kwa uchache ni Emmanuel Gabriel,Ivo Mapunda,Shadrack Nsajigwa,Haruna Moshi na hata huyo Athuman Iddi mfungaji wa goli.Mi nadhani ulitaka kutuonesha kuwa unajua umri wa wachezaji wa Ulaya,lakini ni unajiabisha tu.Eti ushindi wa kibahati,unataka ushindi gani sasa ndio kwako sio wa bahati?ingekuwa tumefungwa ungesema Uganda wanajua sana,tukishinda sisi eti bahati,kweli cha mtu ..vi.acha ushamba

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 19, 2008

    NAOMBA NISEME ROHO INANIUMA
    JUMAMIOSI KATI YA MECHI YA UGANDA NA TAIFA STARZ KUNAVURUGU ZIMETOKEA NA WATANZANIA WAMEPINGWA NA KUUMIZWA VIBAYA MBELE YA VIONGOZI WA SOKA WA UGANDA NA WANAUSALAMA BILA YA MSAADA WOWOTE.
    KINACHO NIUMA NI KWAMBA HAWA JAMAA WA UGANDA TUMEWAKARIMU SANA HAPA KWETU, LAKINI WAMEFIKA KWAO WAMEKUWA WAKATIRI SANA KAMA WANYAMA.
    OMBI LANGU KWA VIONGOZI WA TFF NA VIONGOZI WA SERIKALI NIKUFUATILIA SWALA HILI;-
    1. INABIDI BALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA ACHUKUE HATUA KUFUATILIA KILICHOTOKEA NA KUOMBA MAELEZO TOKA SERIKALI YA UGANDA “KWANINI IMESHINDWA KUTOA ULINZI KWA WATANZANIA WALIOKUWEPO UWANJANI?”

    2. PIA INABIDI SERIKALI KUPITIA BALOZI WAKE NCHINI UGANDA WAIAMBIE SERIKALI YA UGANDA KUOMBA RADHI KWA WATANZANIA KWA VITENDO VYA KIHUNI VULIVYOFANYWA NA WANANCHI WAKE.

    3. SERIKALI YA TANZANIA KWA KUPITIA BAROZI WAKE NCHINI UGANDA YABIDI KUHAKIKISHA INAFUATILIA WALE WOTE WALIOFANYA MATENDO YA KIHUINI WANAFIKISHWA MBELE SHERIA NCHINI UGANDA.
    NOTE
    NACHOONA MIMI NI KWAMBA TABIA YA MATENDO YA KIHUNI TIMU ZETU KUFANYIWA LIMEKUWA LIKIJITIOKEZA MARA KWA MARA. NA SISI WATANZANIA TUMEKUWA KIMYA NA WAPOLE SANA PIA NIWEPESI WA KUSAHAU.IMEFIKA WAKATIKA SASA TUTUMIE TARATIBU ZILIZOPO KULINDA HADHI NA WATU WETU.

    na Rtuz

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 19, 2008

    Kwangu mimi au kwa mtazamo wangu naona kuchukua wachezaji wadogo au kuchukua wakubwa wote ni sawa ila kuna baadhi ya wadau wanasema kwamba anataka kujenga timu naona ni sawa kama anachukua wachezaji wadogo kwa ajili ya hapo baadae hata kwa sasa hivi pia ni vizuri kabisa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 19, 2008

    NAWAPONGEZA WADAU WALIOKUWA MAKINI KUCHANGIA,HAPA MIMI SIUNGANI NA WATU WANAOMPA LAWAMA MAXIMO,LAZIMA TUELEWE KUWA MSINGI MKUU WA SOKA KOKOTE DUNIANI NI SOKA LA VIJANA KUWA NA SHULE ZA SOKA LA VIJANA,KUWA NA TIMU YA UNDER 17,UNDER 21KUWA NA MISINGI MIZURI YA CLUB ZETU ZA SOKA:
    -KUWALIPA VYEMA WACHEZAJI,KUWA NA MAKOCHA BORA,KUTOKUWA NA MIGOGORO NDANI YA VILABU,VILABU VIWE NA WAFADHILI NA WAZAMINI WA UHAKIKA,KWA MISINGI HII TUNAWEZA KUZALISHA WACHEZAJI WAZURI KTK TIMU YA TAIFA,LAKINI KWA SASA INABIDI TUMSIFU HUYU MBRAZIL MAAMNA AMEKUTANA NA WACHEZAJI WASIO NA MISINGI MIZURI LAKINI AMWJITAHIDI WALAU NASI TUMESOGEA TULIPO KUWEPO HAPO MWANZO.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 19, 2008

    Anon wa 8:02 umenichekesha sana.
    Nilikuwa na hasira zangu, kusoma comment yako, nikabaki kucheka.. safi!

    Mdau, UK

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 19, 2008

    KITU AMBACHO KINAWEZA KUOKOA SOCCER LA TANZANIA Ni KWA KUUZA CLUB KWA~MAKAMPUNI HILI WAZIENDESHE KWANI VILABU VYETU VINGI VINAONGOZWA NA MIGOGOLO AMBAYO HAYILETI MAFANIKIO KWANI VIONGOZI WENGI WANA NJAAA NA HAWAJALI MASLAHI YA WACHEZAJI.MFUMO UNAOTUMIKA NA VIONGOZI WA CLUB SASA HIVI BADO NI HULE WA TIMU ZA MTAANI AMBAZO WACHEZAJI WENGI UCHEZA KWA MOYO KWA AJILI YA MAPENZI YA KLABU YAO YA MTAANI.HUWEZI KUONGOZA KLABU KUBWA KAMA SIMBA KWA MFUMO HUO KWANI WACHEZAJI HAO SOCCER NI AJIRA KWAO,SASA UNAPOMNYIMA~MTU MSHAHARA WAKE KAZINI UEGEMEE MENGI SANA KUTOKA KWA HUYO MFANYAKAZI AMBAYO HAYATAKULETEA FAIDA MUAJIRI.kwahio kuna umuhimu sana wa kuachana na hawa viongozi wanao kuja kuangamiza soka hili tupate makampuni yatakayo weza kendesha soka kama biashara.tuna vipaji vingi sana sema umaskini wa vilabu vyetu ndio vinaangamiza soka.
    Alafu kwa wale wachezaji wetu waliopata nafasi ya kuitwa timu ya taifa nendeni mkacheze kwa moyo mmoja kwani nchi nyingi wanaangalia na unaweza kkupata bahati ya kununuliwa na timu za nchi nyingine ukaangalia maslahi zaidi kwako binafsi.
    Huyo anayelinganisha na wachezaji wa ulaya kwa miaka ni wazi hajui soka la nyumbani vizuri.
    Na pia timu za vijana ni muhimu sana na kwa njia ya timu kuuzwa kwa makampuni mfumo ukiweza kubadilika na soka likiwa la kuvutia nina huakika wapenzi wa soka watarudi kutazama uwanjani hili vilabu vipate mapato mengi ya kuweza kuaqnzisha club za vijana wa kusaidia baadae.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 19, 2008

    Mtoa Maoni wa Tarehe May 19, 2008 2:59 AM unayesema Maximo hawafai unapaswa ushukuru kwamba Maximo amekuja nchini na kuleta kitu ulichokiita wewe Kudra za Mungu. Kwa kudra hizi, sasa hivi kuna wachezaji pengine hamsini waliopata kufanya mazoezi na kupata uzoefu wa kuwa wachezaji wa Taifa Stars. Kwa mfano, sasa hivi golini anaweza kusimama Ivo, Farouk, Ally Mustapha au Juma Kaseja bila kuwa na wasiwasi wowote na bado Shaaban Dihile anaandaliwa. Kudra alizoleta zimetupa chipukizi kama Kigi Makasi, Jerry Tegete, Uhuru Selemani na Amir Maftah ambao uwezo wao unapanda siku hadi siku. Kudra hizo hizo zimetuwezesha kwenda kuiangalia timu yetu uwanjani tukiwa na matumaini ya ushindi, mambo yakiwa magumu basi sare. Kudra hizo zimewatoa wachezaji Danny Mrwanda na Nizar Khalfan kwenda Kuwait. Waliporudi kwa ajili ya mashindano ya Afrika Mashariki na kati walionekana kuwa na viwango vya juu zaidi kuliko walipoondoka. Said Maulid naye ameenda Angola. Kudra hizi zimeunda timu yenye mchanganyiko wa chipukizi niliowataja na wazoefu kama Emmanuel Gabriel, ambapo Maximo anawatumia wazoefu wake kuwapa mbinu chipukizi wake vilevile.
    Mtoa maoni hiki kitu unachokiita wewe kudra, wenzio tunakiita utaalamu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 20, 2008

    Watanzania siwalaumu kwani ni siku nyingi mmekosa ushindi na baada ya mafanikio kidogo mnaanza kukimbia bungeni. mpira TZ bado. Mnakumbuka timu yetu ilvyofanya na Senegal-Goli tano. Mnakumbuka timu yetu ilivyofanya pale Mwanza mbele ya Kikwete. Mnakumbuka yalioikuta Simba kwa Enyimba na Yanga kwa Walibia. Jamani Aibu. Mpira TZ ZIIIIIIIIIIIII.Na TZ itatolewa katika na wasudan pamoja na kwamba wanapigana huko Darfur. Sisi tumezidisha uzalendo na tunashindwa kutumia uwanja wa nyumbani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...