Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2008

    mahali popote? Mbona huku bush kwetu not reachable kabisa hasahasa tbc televisheni

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2008

    Hapa Arusha kodi ya matangazo tunanyanyaswa sana wanapigia watu mahesabu ya juu alafu kampuni ya kuchukua kodi ya matangazo imebinafsishwa basi wanapia bei wanazotaka wao. watu wengi wanashindwa kutangaza unakuta wanafuta matangazo, hili nalo liangaliwe.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2008

    we anoni hapo juu mbona hueleweki? eti "Bush kwetu not reachable kabisa" Bush kwenu wapi, unafikiri kila mtu anaelewa unapokaa! ukitaka kujibiwa vizuri eleza bayana unapokaa, kama ni Tabora au Kasulu nk.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2008

    TBC ni mnyanyasaji mkubwa wa wafanyakazi kwa sababu ya kugomea kurusha moja kwa moja sherehe za wafanyakazi za mei mosi kitaifa kule Iringa wakati ndio wadau wao wakubwa wanalipa kodi za kuendesha TBC.

    Nimekuwa nikitafiti jinsi vyombo vya habari hasa Televisioni za mataifa makubwa duniani zisivyojali habari za mataifa madogo maskini duniani hata ziwe kubwa vipi hawazitoi.Jana nimethibitisha kuwa hata Tanzania hali ni hiyo hiyo.Hakuna tofauti.

    Nilifuatilia siku ya Mei Mosi taarifa za habari zote kupitia Sattelite TV na Internet kuhusu sherehe za Mei Mosi Iringa nikaona hakuna hata Television moja iliyokuwa Iringa kulionyesha lile tukio ambalo lilifanyika kitaifa kule na kurusha picha zake kuanzia maandamano hadi hotuba.

    Badala ya kuonyesha Lile Tukio kule Iringa Television zote zilijazana uwanja wa Taifa Dar es salaam Zikamwonyesha maandamano ya Mei Mosi pale na hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akihutubia kwa mbwembwe kubwa wakaacha kuonyesha Waziri picha za Waziri Mkuu Pinda aliyekuwa kule Iringa kama mgeni wa heshima kwenye sherehe zile.

    Television zote hazikuona umuhimu wa kuonyesha matukio ya sherehe hiyo ya kitaifa kwenye mkoa maskini wa Iringa.Wamegeuka na wao kuwa kama BBC,CNN,n.k ambao huwa ni vyombo vya kusemea matajiri hasa tu na miji yao ya kitajiri.Na televisheni zetu Tanzania zimekuwa midomo ya miji tajiri tu kama Dar es salaam,Arusha na Mwanza.

    Hata blog zote za watanzania nilipitia ikiwemo ya Majid Mjengwa ambaye yuko kule Iringa hakuna hata moja iliyotoa picha za mei mosi kule iringa wakati matukio hata ya mchawi kuanguka dare s salaam huchapishwa hapo hapo kwenye blog

    Hata Televisioni ya Taifa hawakwenda kurusha moja kwa moja matangazo yao kule wakati wanaishi kwa kutegemea kodi za watu wa Iringa.Walichokifanya badala ya kuonyesha picha za kule walionyesha picha moja ya Mgando ya kamera ambayo ni ya siku nyingi sana zilizopita ya Waziri Mkuu Pinda wakaanza kusema aliyosema Iringa!!!!

    Kama mkereketwa wa kujitegemea wa mikoa maskini Tanzania nalaani kitendo cha Televisheni zote za Tanzania ikiwemo Televisheni ya Taifa TBC kutorusha picha za sherehe za mei mosi kitaifa Iringa na badala yake kurusha picha za mei mosi kimkoa za Dar es salaam.

    Mkoa wa Iringa umeonewa kwa hili na naviomba vyombo ya habari uombeni samahani huo mkoa kama kweli mumepania kutokuwa kama BBC na CNN .Televisioni ya Taifa (TBC) mumewaonea walipa kodi wafanyakazi wenaolipa mishahara na marupurupu yenu kupitia kodi zao.Yaani hata kitu chao cha kitaifa mmeshindwa kuwarushia kweli?

    Na bloggers watanzania wenye blog mumekosa uzalendo kwa kutoonyesha kilichokuwa kinaendelea kitaifa kule Iringa siku ya Mei mosi mkashindwa kuleta kwenye blogs zenu picha live! Hamjui umuhimu wa vitu au sherehe za kitaifa mumekalia umbeya tu kuujaza kwenye blogs zenu!

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2008

    Umeme uko kwa mafisadi halafu wanaweka matangazo kwa walala hoi, sasa hizo tv au radio watazisikiliza/ziangaliaje kama hawana umeme?
    Bora TBC wangefanya kutengeneza matangazo kwenye muundo wa barua nakuwatumia wale wachache wenye umeme ili waone TBC.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2008

    Kama kawaida yenu waosha vinywa biashara matangazo babu kumbuka TBC kabla hijafikia hapo ilikuwa initwa TUT kwa iyo na uongozi nao ulikuwa tofauti wewe koloboi inshu yako hapo ni kuonyeshwa kwa kilele cha mei mosi tu au wewe ulikuwa mfanyakazi wa zamani wa TUT enzi zile mbona una maneneo mengi ivyo?
    Sasa nikumbie sherehe zionyeshwe wakati zimejee malalamiko kibao ya mishahara baada ya kiomba serikali iwaongezee mishahara walimu na askari wewe unawaza kuonyeshwa kwa ob ya mei mosi sio issue Tupo juu Shirika Kubwa hili ukitaka kuamini Kipindi kile baraza la mawaziri lilvyovunjwa kila mtu alikuwa anaulizia frequency za REDIO TANZANIA kwa sasa TBC-TAIFA asikilize watu walivyokuwa wanaachia ngazi na vijisent vyao.Wewe huoni kunoga waosha vinywa kama kawaida yenu nichambueni lakini nishawapa ukweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...