ndege ya airbus A320 atc lilitotua dar wikiendi hii tayari kwa kuboressha huduma za shirika hilo. ndege hiyo ambalo limekodishwa kutoka kampuni ya wallice trading company ya ufaransa ian uwezo wa kubeba abiria 150. ofisa mtendaji mkuu wa atc mh. david mataka amesema ndege hiyo itaanza na safari za dar-johannesburg kila siku kukidhi mahitaji ya njia hiyo na kwamba baada ya muda mfupi itaanza safari ya dubai


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2008

    Big up naona twiga karudi, yaani huyo twiga huwa anapendeza sana anapotua sehemu.I hope mambo yatakuwa mazuri sasa na sisi tuweze kujidai kiana
    Londoner

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2008

    hiyo airport ni wapi, i wish tanzania tunge-upgrade uwanja wetu uwe angalau kama huo.

    jamani hata nyasi zinazoota kwa asili pale kwetu utadhani kichaka.anyway, makongoro mahanga anawachimba mkwara wafayakazi waache umbea, kwa maana kwamba anataka ufisadi usifichuliwe?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2008

    Hey Michuzi, Kwani wewe Week end huwa inaanza lini kwako? "Lililotua wkend hii!!!!!!!"

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2008

    kwa nini imekodishwa na haijanunuliwa???
    Wanalipa dola ngapi au euro ngapi kila mwaka kwa kukodi hiyo ndege. natumaini Michuzi maswali hayo umeyauliza

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 02, 2008

    eee MUNGU SIMAMA KATIKATI YA UFISADI NA ATC YASIJE YAKAJIRUDIA YA HOTELI YA ATC KWA KULIPWA KONTRAKTA HEWA, YA GEORGE HALLACK NA NDEGE ISIYOKUWA NA MABAWA NA YA NDOA YA SAA NA ATC.

    amina

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 02, 2008

    Mdau uliyetaka kujua kiasi kinacholipwa kwa kukodi hiyo ndege ni dola 370,000 (zaidi ya milioni 380Tsh) kwa mwezi. nimesoma kwenye gazeti

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 02, 2008

    Michuzi nahisi una kale kaugonjwa ka wikiendi...

    Sasa hautapita muda utasikia ununuzi/ukodishwaji wa hii ndege una mkono wa RUSHWA!
    tena wizara yenyewe chenge aka mzee wa vijisenti ndio alikuwa waziri wake, yangu macho na masikio!

    Pongezi Mataka na team yako kwa kurudisha heshima angani...

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2008

    Mbona ndogo kama Boeing 737-300!
    Si bora wangechukua hiyohiyo mi-boeing tu waliyoizoea kuliko kuchukua hizi aina mpya halafu waje WATUBWAGE bure!
    Mweeh!

    ReplyDelete
  9. ETHIOPIA NJAA KALI LAKINI WAMETUPIGA BAO KWENYE HAYA MASWALA YA ANGA. SIJUI KIZAZI GANI KITATUKOMBOA. BABUU SAMBEKE TUANZISHIE KAVETA CHETU CHAKUSERVICE NDENGE NDOGO HAPA MOSHI.

    TUMAINI GEOFREY

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 02, 2008

    Tumaini Geofrey nakubaliana na wewe tena sana!
    Na siyo Ethiopia tu!Nchi nyingine inayotupiga bao sana katika masuala yaanga ni Angola wana ndege nzuri sana tena nyingi tuu!wakati wamekuwa vitani miaka kibao lakini bado wamekaa sawa kwa mambo kama haya.Hata watani wetu wa jadi wanatupiga bao na Kenya Airways.
    Anyway ATC wamejitahidi ingawa ingekuwa bora kununua zetu maana vitu vya kukodi havina profit nzuri .Kinachosikitisha ni kushangilia ukodishaji wa ndege bila kuuliza kuwa inalipiwa kiasi gani maana unaweza kuta ingekuwa cheaper kuinunua on installments.
    Anyway serikali na system choka mbaya hatuna cha kujivunia apart from great people ukiacha mafisadi.
    mdau sweden

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2008

    Air Tanzania kama mna masikio na mnajua kusoma someni hizo comments juu you will find something in common.Wanablog wengi inaonekana wanasafiri sana na ndege za nchi zingine na roho inawauma sana kuona wenzetu wanachukua dola zetuza nauli badalaa ya kurudi ATCL(Nchini kwetu),wanapenda kuona na wao siku moja wanasafiri na nembo yao ya twiga kwenda huko nje ya nchi.Kazi kwenu ATCL,ni kweli mafisadi wameichezea sana ATCL ingekuwa mbali.Michuzi ATC waba roho ya paka I tell you.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 02, 2008

    wabongo tuone uzushi kwa hii sasa hivi wamejitahidi ingawa bado tuko nyuma
    huwezi kulinganisha ethiopian au kenya airways na air tz, wanacheza ligi mbili tofauti kabisa
    aliyekodi hii hongera angalau kidogo tongotongo za macho zimewatoka sio kama vile vipanya vya propeller walivyonunua precision air

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2008

    Michu,nimejaribu kuikuza picha na kuisoma vizuri.Hizo 'Godowns'kwenye background zimeandikwa FORTALEZA ambao ni mji uko Brazil(not sure).Nadhani ilikuwa inatake off kutoka airport ya Fortaleza.Wallice trading company?inawezekana walikuwa wameitunza huko.Hiyo picha uliipataje?Michuzi una mtandao mkali wee mbaba wee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...