fAMILIA YA MBUNGE WA BARIADI MH. ANDREW CHENGE IMEKANUSHA UVUMI ULIOENEA KILA MAHALI KWAMBA WAZIRI HUYO WA ZAMANI WA MIUNDOMBINU KABWIA SUMU NA KUFA.

MAI WAIFU WA MH. CHENGE, MAMA TINA CHENGE (AKIWA NA MUMEWE PICHANI) , AMELONGA NA GLOBU HII DAKIKA CHACHE ZILIZOPITA NA KUSEMA KWAMBA HABARI HIZO AMBAZO HATA YEYE AMEANZA KUZISIKIA TOKA JANA KWA KUPIGIWA SIMU KILA DAKIKA KUPEWA POLE SI ZA KWELI NA KWAMBA MAI HAZBENDI WAKE YUPO HAI NA ANAENDELEA NA SHUGHULI ZAKE ZA KILA SIKU KAMA KAWAIDA.


NAOMBA KUWASILISHA, HABARI NDIO HIYO...






"MZEE YUPO DAR NA YU BUHERI WA AFYA NA LEO KENDA MJINI KWENYE SHUGHULI ZAKE" AMESEMA MAMA CHENGE.

O

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2008

    Kumbe hajafa bana! Noma sana!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2008

    Aaaaaaaaaaah kumbe habari ndio hiyo mimi sijazisikia kabisa!! sasa kwa nini watu wanatunga faida iko wapi haswa?? kwani kufa kuko na kila mtu atakufa kwa hiyo kum zushia mtu ambaye ni mzima kabisa hata hajaumwa ni soooo, acheni sheria ifanye kazi yake jamani!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2008

    Mhh! Wabongo kwa kuzusha ndio wenyewe! Mzee ana vijisenti kwanini afe bwanaaaa! Kule Bariadi mkewe anajulikana na Komandoo Tina/Suzzy maana alicharuka na kufanya vimbwanga wakati wa uchaguzi kuhakikisha baba anapata ubunge!! She is very tough!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2008

    ah waende zao huyo mai waifu mwenyewe kama mwanaume

    ReplyDelete
  5. ASAVALI MUNGU AMETUEPUSHIA NA HILO. MAANA USHAHIDI WAKE NI MUHIMU. KESI INGEFUTWA HIVIHIVI KAMA YA KAKA DITO

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 02, 2008

    KAMA MICHU, SALAMU SANA.
    HAO WANAOTAKA BABA YETU CHENGE AFE. NASEMA HATOKUFA KATIKA JINA LA YESU. WATAKUFA WAO WATAMUACHA HAPA HAPA DUNIANI. KAMA YEYE CHENGE NI FISADI JE MBONA LOWASA YUPO MPAKA LEO. CHENGE HAWEZI KUFA KWA HIVYO VIJICENT.
    NI MZIMA WA AFYA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 02, 2008

    KWANINI WASIMTANGAZIE ROSTAM AZIZ?TEHE TEHEEE INGEKUA PATASHIKA NGUO KUCHANIKA

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2008

    wabongo wachawii,mtu anakuua hivi hivi kwa midomo yao,bongo noma sana,fisadi si chenge mwenyewe.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 02, 2008

    WEWE ANON 2:17 PM,ACHA UFALA KAMA HUNA POINT YA KUSEMA FUNGA BAKULI LAKO.WEKA PICHA YA MAI WAIFU WAKO TUONE.MKE WA MTU ANAKUHUSU NINI??ETI ANAFANANA KAMA MWANAUME..SHENZI TYPE

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 02, 2008

    ivi mtu anavyomtangazia mwenzie kafa ni kwa faida ya nani????wabongo akili fupii sana

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2008

    Pole sana bwana chenge na familia yako.Tunajua watanzania wametokea kukuchukia lakini tusimwombee mwenzetu kifo.Please Tanzanians.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 02, 2008

    SASA WATU WANAELEKEA PABAYA KUTANGAZIANA KIFO WAKATI BADO MZIMA.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 02, 2008

    watu wenye wivu wanaweza kuua mtu hivi hivi kwa kumfwatafwata, kwa maneno kumkatisha tamaa, tabia hii ipo ughaibuni, hata kwenye ofisi za serikali ni tabia mbaya inatakiwa iachwe haraka sana,uswahilina hado maofisini.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 02, 2008

    I have a feeling kuwa uzushi wa aina hii huwa unaanzishwa na marketing departments za kampuni za simu hapa bongo..Can u imagine the amount of money generated kwa huu uzushi thru SMS and calls? Roughly kila watu waliowasiliana kwa hii ishu wametuma a minimum of 3 msgs na wale walipigiana simu ni calls za a minimun of 1 minute..Wadau mnaionaje hii?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 02, 2008

    MAYEGO umeongea point muhimu sana....

    Mimi nilisikia kuwa CHENGE kafa na kichwa chake chenye kipara kinapelekwa burundi kufyonzwa damu... tehe te te te he he he tehe

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 02, 2008

    HUO WANJA!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 02, 2008

    KUNAKITU KINANIUDHI SANA SISI WATANZANIA KWA UJUMLA PAMOJA NA MIMI MWENYEWE NI WANAFIKIII SANA HIVI KWANINI.MIMI BINAFSI NAPENDA MTU WA KAULI MOJA KAMA UNIPENDI BASI USINIPENDE KABISA MAANA HATA MIMI SIPENDI KILA MTU HAPA DUNIANI NA KAMA UNANIPENDA BASI USIFUATE MKUMBO WATU .

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 03, 2008

    Wow! hela mwana haramu na ni sabuni ya roho. Huyu mama hazeeki. Nilianzaga kumwona akiwa mdada sana tu na mimi nilikua na miaka kama 12 yrs old. Mara nikaja kumwona Dar tena nikiwa na miaka kama 18. Baada ya hapo ni miaka imepita mingi tu toka nimeondoka Dar kwa mara ya kwanza lakini hii picha na mumewe ni kama vile nilivyowaona the last time. Yaani tukisimama naye utazania mimi ni dada yake kumbe anaweza kunizaa huyu mama.

    Vijisenti vitamu sana narudi bongo kuvitafuta lakini mambo ya kuombeana kufa sio mazuri. Wabongo bwana

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 03, 2008

    Why is this fool not in custody yet? Why do we look up to thieves, he is no different from someone who breaks into another's home, the only difference is he did it inthe comfort of his office. These people are traitors and they should not be allowed to walk free. I want to see legal action being taken against them all, starting with Lowassa, Msabaha, Karamang, Chenge and even Mkapa if he implicated inthe whole mess. Where is our law enforcement officers, anyone?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 03, 2008

    MAALIM ISSA TUNASHUKURU KWA PICHA "..MURUA.." KAMA HII CHENGE NA "..MWADANI.." WAKE WAMEPENDEZA SANA HASWA."..RESEPSHEN YA MAMA.." ANA.."..WANJA..HEA STAIL YANGUVU PAMOJA NA BLING..BLING SHINGONI..".."..WAWILI..".. HUFANANA..".. HASWA WAKIISHI PAMOJA KWA MUDA MREFU.."

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 03, 2008

    MICHUZI NOMA SANA TENA MSHAMBA, SIJUI HAELEWI MAANA YA BLOG KAMA NCHI ZA WENZETU ZILIZOENDELEA, I THOUGHT UNEIGA MIFANO HALISI NDIO UKAFUNGUA BLOG.
    MAONI YA MAANA YANAANDIKWA BUT YOU DO NOT POST THEM. WADAU WENGI PIA WAMELALAMIKA KWA JAMBO HILI.
    FUNGA BASI HII BLOG, BULLSHIT, MAMBO YA KUPENDELEA BAADHI YA WATU, SIO FRESH. KAMA WATU WANATUKANA NA KUTUMIA LUGHA CHAFU SAWAAAAA USIYATOE, LAKINI WANAOMWAGA UKWELI, HUWATENDEI HAKI, MAULANA.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 03, 2008

    good job he has done.

    10 years as AG. One of the top jobs in the country.

    i think he deserves to be the current president.

    keep it up , the nation is behind you. we are all behind you , and we will support you now and forever,.
    kidumu chama cha mapinduzi

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 04, 2008

    FISADI AND FISADESS

    Yaani mdau wa May 3rd, 12:51am umeyatoa hayo maneno kinywani mwangu. Halafu hata English kwako naona ni richebo kabisa. Waswahili we see people who broke into our homes and stole our life savings and we treat them as heroes!! This kind of behaviour disgusts me. In my opinion hawa vigogo tuwalipe hela nzuri sana, I am talking Tens of Thousands of dollars a month, halafu tukiwashika wizi tuwafunge mpaka washangae. Maana hawa jamaa wanauza nchi hivi hivi bora tuwalipe tu wafanye kazi vizuri kama issue ni njaa.. Instead majangili bado yanaroam bungeni bila haya!! Crazy!!


    Mdau - Boston, US

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 04, 2008

    Huyo mama mbona amekaa kama dansa?

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 04, 2008

    Weew kama huna hoja nyamaza umempenda nini mkewe unataka akudansie? akili fupi hizi muhdini usiziingize hawa ndio wanaleta kichefuchefu

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 04, 2008

    Pole Mh kwa yote. sisi wana bariadi wapenda maendeleo tuko pamoja nawe. Hawa wazushi hawana hoja sasa wanatafuta kuuza magazeti kwa gharama ya watu wengine. Mwambie commando suzie afunge buti hata kwa hili tumawaaminia, IDUMU BARIADI YENYE KUTAKA MAENDELEO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...