mdau katuma hii sasa hivi kusema kwamba siku hizi dar tambarare. yaani ili kupunguza mashimozzzz barabarani jiji limeamua kupanda minazi kwenye hayo mashimozzzz ikiwa ni mojawapo ya teknolojia ilobuniwa na wataalamu wetu kwa karne hii ya 21

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2008

    Simchezo kweli hio teknolojia.sasa kweli hapo si tunaongeza ajali au?mambo ya kukwepa mnazi kati kati ya barabara.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2008

    Hebu nielimiisheni. Ndo kusema Emirates wamehama toka Haidary Plaza? Kama wamehama hapa walipo ndo wapi sasa? Mimi ni mteja wao. Nisije nikapata taabu siku nyingine nikitaka kusafiri.

    Mdau wa Osaka

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2008

    Kwako anon 6:04 pm hapo nahisi hapo ni Haidery plaza ndugu yangu ila ndio pamechakaa kinoma yaani.

    Hii picha imenikumbusha mbali sana. Asante mdau kwa kutuma hii picha. Panakera sana hapo kukiwa na foleni.

    Mdau- Amsterdam

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2008

    Yaani nimecheka mpaka basi .Duuuu!
    Mnazi katikati ya barabara,yote kukwepa kukarabati.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2008

    Mdau wa Osaka, Mnazi tu umekupoteza ramani? Au umeona kwamba Haidary Plaza hapawezi kupandwa Mnazi?

    Hata hivyo mnazi huo si kweli kwamba umepandwa. Baada ya kuona Mamlaka husika 'hawaoni' kwamba hapo kuna shimo msamaria mwema alijitolea kuweka hayo Makuti ili angalau waendesha Magari wsijeharibu magari yao kwa kuyatumbukiza kwenye Korongo hilo.

    Wahusika wote wako bize na mambo ya ufisadi. Hakuna muda wa kufukia mashimo....

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2008

    Michuzi acha kupotosha maana ya 'kupanda' huo mnazi! Lengo ni kuwatahadharisha madereva uwepo wa shimo katika barabara ili waweze kulikwepa hilo shimo!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2008

    PUNDA NA FARSI WOTE NI WANYAMA NA KAMA UNAMAKENGEZA HUWEZI KUWATOFAUTISHA, JAMANI KWA WANAOJUA MINAZI ILIVYO WATAKUBALIANA NAMI KUWA HUO SI MNAZI BALI NI MTENDE. HATA HIVYO WABONGO TUKO TAMBARARE TUMEZOEA KUSEMA SI MRADI UJUMBE UMEFIKA! HUWA HATUKUBALI KOSA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...