KK akisalimiana na Waziri mkuu wa Japan Mhe. Yasuo Fukuda kwa mazungumzo kwenye Hoteli ya Yokohama Grand Intercontinental leo, ambako Mkutano wa nne wa TICAD unafanyika jijini Yokohama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2008

    Raisi wetu safari zimezidi washauri wake sjui wako wapi? Nchi ina matatizo mengi ambayo yanahitaji utatuzi kutoka kwake. Hivi kweli tutafika huko kwenye maisha bora kama raisi kila kukicha yeye na safari na safari na yeye!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2008

    Huyu ni mtalii

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2008

    we jamaa unavyommaind huyo JK mpaka unakosea kumuandika jina lake? umezidi tena michuzi!!! KK ndo nani?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2008

    mwe !! huyu bwana kaishasafiri tena?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2008

    wajameni mtasema sana...kutesa kwa zamu!
    kama unataka nawe gombea!
    wewe wa mabonde kuinama unajua rais anasafiri kwa madhumuni gani!?

    thinking aloud!!


    fanyeni kazi..sio domo kaya

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2008

    KK ni Kitwana Kondo...siyo Kikwete

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2008

    Tunajua fika kwamba safiri kwa rais ni sehemu ya kazi yake, lakini huyu jk tunaamini anakazi za muhimu nyumbani ambazo kuwepo kwake mambo yanaweza kwenda fast, mfano halisi kuna tatizo kubwa la umeme na maji, sehemu kama zenji haikuwa na umeme from last wed mpaka juma2. ni ushauri wa bure kwa muheshimiwa inabidi utufanyie kazi uliyo tuahidi walala hoi , we just need reliable basic needs like water and energy. wacha kujirusha kwa sana mheshimiwa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2008

    Watu nyinyi wa ajabu kabisa!
    Mbona mnamawazo ya kiuchwara!

    Mnataka JK abaki nyumbani kwani mmeambiwa yeye ni Receptionist(kwamba hawezi kutoka kwa sababu hakuna mpokea simu)? au mnafikiri uraisi ni nini? Aaahhhh, hebu tuongelee suala Jingine.

    ... aka Chinga

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2008

    Huyu raisi kwa safari anatia fora.2010 hiyo inakuja itamkuta bado yuko safarini.Kwa safari hizi tutafika kweli kwenye nchi ya asali na maziwa au tutabaki omba omba tu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2008

    Smiling Faces show no choices and they never reveal the truth,so you be carefull.All that glitters is not gold I was once told.You can fool people one time but you can never fool all the people all the time!Ostritch is my bird.When confronted with a problem my dear Ostrich always knows what to do.If you keep on running away from the problems,the problems will run after you.Dear Readers Be Blessed.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 28, 2008

    Raisi apunguze safari ashughulikie matatizo ya wananchi.Tulimchagua ili atutumikie na kutuletea maisha bora kama alivyotuahidi.Kuna matatizo ya mfumuko wa bei ambalo anatakiwa akae na wasaidizi ili kuyatafutia ufumbuzi.Hizo safari za kila mara atajuaje matatizo ya watanzania wajameni????.Wenzake wote waliukataa uwenyekiti wa OAU kwa sababu wanatakiwa kuwatumikia wanatu wao.JK yeye aliona yuko free ndiyo maana akakubali.Raisi ashauriwe apunguze safari watanzania tunataka ashughulikie matatizo yetu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 28, 2008

    OMBA OMBA ITAJENGA UCHUMI KWELI? NCHI HAIJENGWI KWA KUWA OMBA OMBA. JE TUNATOFAUTI GANI MATONYA? SIMAMIA UKUAJI UCHUMI, ONDOA RUSHWA NA UFISADI, SIMAMIA KILIMO, FUTA MIKATABA YOTE MIBOVU YA MADINI, TANESCO NK. KAMATA MAFISADI NA TAIFISHA MALI ZAO. PESA TUNAZOPOTEZA KIHOLELA ZINGEIJENGA TANZANIA ZAIDI YA HIYO OMBA OMBA. HAPO UTAJENGA NCHI LA SIVYO KALAGABAHO. UNAOGOPA NINI? AU NDIYO HIVYO TENA...

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 28, 2008

    Mh. raisi hapaswi kuwaogopa na kuwalea mafisadi. Punguza safari ili upambane nao vilivyo.Hakuna aliendelea kwa kuomba omba.Tuna rasilimali za kutosha ila usimamizi mbovu pamoja na mikataba mibovu inarudisha nyuma juhudi za watanzania kujiletea maendeleo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 28, 2008

    Nasikia president ameishakwenda hadi sayari nyingine na mwezin,jaman anaojua uhakika naomba aniambie

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 28, 2008

    Watanzania mbona mnakuwa na vichwa vigumu kutoelewa historia ya viongozi wetu...Rais wa awamu ya kwanza jina la utani tulimwita "Mchonga" au "Mwalimu" na kweli alikwa mwongeaji.. na mfundishaji kweli kweli , Rais wa awamu ya pili tumlimwita "Mzee ruksa" kweli kila tulichoomba tulipata , mzee asiye na makuu..mzee wa watu popote umwitapo utamwona , Rais wa awamu ya tatu "Mwandishi mbabe" si mnaona wenyewe mambo ya mgodi amekula "kobisi ya kibabe"...Rais wa awamu ya nne "Msafiri" tangu yupo wizara ya nanii.. kila siku alikuwa nje ya nchi kama wizara yake ilivyoukuwa ..sasa tatizo ni nini mmempa wenyewe kazi ya kusafiri mwacheni asafiri

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 28, 2008

    Nilikuwa nasikia kuwa mataifa makubwa yanatoa rushwa kw aviongozi wetu nao bila kujua wanipokea na kisha inakuwa nd kamba yao ya kunyongwa.

    Ona umsikia waziri mkuu wa japan ametoa msaada wakujenga barabara ya dar - bagamoyo. Nadhani iatkuwa double streets. Hiyo kama si rushw autaiitaje mtu mwenye akili timamu. wamejua Kikwete anatoka bwagamoyo hivyo wakimjengea watamfurahisha kisha wao watakuja serengeti na mwadui kunanhiii.

    wangesema wanjenga barabara ya dar kwenda arusha kupitia bagamoyo ili kupunguza foleni ya dar chalinze ningewaelewa. MMMh basi serikali kufuta aibu ya kupewa rushwa ya mchana kweupe waongeze hela waijenge hadi mkata ili magari ya arusha yaache kupita chalinze.

    Kama si rushwa kwanini wasiendeleze barabara nyingine zilizoanza kujenhgwa wakt wa magfuli na sasa zimekwama ktokana na kukosa hela?

    Huu umaskini wa mwazo ndo tatizoletu kubwa. Wanatuchekea na kutikisa vichwa tunadhani wantukubali kumbea wanatucheka na kutujaza ahadi kibao. JK akitoka madarakani atajatuambia wazungu si waaminifu na wanafiki. ajue ndivyo wazungu walivyo. hawana ubinadamu na hawafanyi kitu bila sabb. ukitaka kujua wape mradi wa maana uone watakavyoutolea nje. au ne matunda ya DR Kawambwa?

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 28, 2008

    Mweh! vasco anazidi kudagama tu we haya wee tutaishi tukitazama ningeshukuru sana ageenda pemba akasuluhishe ugomvi ndani yake halafu hayo masuala mengine baadaye no wonder mafisadi wanajichotea tu si unajua tena paka akiondoka vipanya vinatawala

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 29, 2008

    kamua baba kamua baba Vasco da Gama.
    endeleaaaaaaaaa,mwaanaaumeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 29, 2008

    Vasco da Gama kesha fika Japan mara hii?? eee!!Raisi wetu kwa safari hajambo.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 29, 2008

    mhh jamani muacheni asafiri mnategemea atafanyaje nchi yetu hamna cha kufanya ukianza kumfunga mwizi sijui uanze toka lini, au tuamue tu tuanze upya sio kuuliza yaliyopita utamfunga kila mtu! ehhehe
    rais ukitoka japani tafadhali ukatoe pole kwa wafiwa iringa lakini kuzikwa marekani , sijui uende wapi, utajua mwenyewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...