Home
Unlabelled
kama kawa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
MASENDEU HILO NDIO JINA LAKE KAKA MICHUZI
ReplyDeletemichu jina lingine la iyo kitu maarufu hapa a town ni ''maraiyoo''
ReplyDeletepj
Kimasai ni Irmashombereta au kwa kizungu MBT(Masai Bare Foot Technology)MBT hutengezwa Uswisi lakini good sales America
ReplyDeleteZamani enzi za Mchonga kule kwetu magharibi tulikuwa tunaita "KATAMBUGA", Ila alipoingia mzee ruksa yalipotea sijui siku hizi kama kule kwetu bado yapo. Ila ni imara sana kwa watu wanaochunga na kuwinda ambao hawawezi kupata protective boots.
ReplyDeleteSi mchezo ila haya masendeu mimi ninayo tena makali kinyama hapa na massai blanket yake na hakuna mtu ananieleza kitu!
ReplyDeleteYes umenikumbusha aisee.."maraiyooo" au "katambuga"nimecheka sana na nimekumbuka wakati nasoma Klimanjaro Primary miaka hiyo..ivo viatu Mwalimu mkuu alikuwa anvipiga sana vita,alikuwa anaitwa Mama Minja...du tumetokambali sana
ReplyDeleteNyaningedere
Aaah niseme nini? Umenikumbusha nilikotoka. Hivi ndo viatu nilivyokulia. Nakumbuka sana, kila mtoto nyumbani ana "peya" ya viatu (au raba)ya Bora na peya ya "Maaraiyoo". Na kwa undani zaidi wasichana walipendelea yale ya mtindo wa "Malapu", wavulana tulipendelea maaraiyo (aina inayobeba jina). baadae zilikuja aina nyingine maarufu kama "Yeke yeke" au "la Kuchumpa". Hizi zimetengenezwa mithili ya zile open shoes maarufu kama Chacha. Alipoingia mzee mwinyi mipaka ikafunguka ndo zikaja hizo chacha na viatu vya plastiki ( wavulana tukapendelea "Gogo"). Pia nikimuona Mh Mrema (wa TLP) nakumbuka kuhudhuria mkutano wake wa kampeni, kwenye viwanja vya iliyokuwa shule ya msingi Umbwe, sehemu ya Kibo (sasa ni Mlama sekondari). Siku hiyo ya Jumamosi, nilikuwa nimepewa pesa na Baba yangu, shs 35. Nikaenda sokoni kombo nikanunua toleo jipya la maaraiyo "yekeyeke" ndo nikapitia kwenye mkutano wa kampeni. Wakati huo ndo anagombea ubunge kwa mara ya kwanza dhidi ya Mh Joe Macha. Mrema alishinda ila ilifungulia kesi ya kupinga ambayo nayo alishinda. Aaaa, ama kweli nyakati zinaenda. we wa K'njaro Primary, Mwl wako hakuwatendea haki, sisi tuliruhusiwa kuvaa shuleni bila ya hivyo tungeenda peku peku. Wakati wa mapumziko tunavua na kuvilundika katika ya uwanja kwa ajili ya usalama, kisha tunapiga cha ndimu. Hiyo ni miaka ya mwanzoni na mwishoni mwa 1980. Natamani sana nyakati hizo, maisha yalikuwa muruwa.
ReplyDeleteHivi kule Dodoma tulikuwa tunaita makatambuga au masakanyoka. Mazuri sana hayo ya shughuli ya kusakia nyoka porini!! yaani umenikumbusha mbali kweli, shule tulikuwa tunaruhusiwa kuvaa, basi hapo wanafunzi mnashindana kwa unene wa soli tu ilimradi mwiba usipite ndani.
ReplyDeleteHee hee heee! Umenikumbusha mwaka ya 1986/87 kule Oljoro JKT viliitwa Antena! Akina Ephata Sozigwa, Vedasto Makota, Sekou Toure, Tax Agap, Suwezi Abdallah na Frank Kallaghe walitesa navyo saaaana! Haviogopi miiba wala mbigili!! Wiii...Waaa!!!
ReplyDelete