Home
Unlabelled
kp leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mzee wetu njoo OLD TRAFFORD(Ukumbi wa MAELEZO) ili wadau wakupige maswali kama walivyopigwa kina Membe wa Foreign na Rweyemamu wa Jumba Jeupe(State House) hapo ndipo tutakapoamini unachosema. Huko Lupaso(Masasi) sidhani kama wanaelewa nini kinaendelea ktk dunia hii ya mafisadi.
ReplyDeleteBeny naye ni Binadamu,nawaombeni kidogo tumsamehe na tumheshimu bwana.Si vizuri kuanza kumdhalilisha rais mstaafu.Kazi ameifanya huyu mdingi ila basi tu amekuwa na mkosi(Ni maoni yangu tu).Tu-focus kudhibiti hii hali isitokee tena,unaona huu ufisadi wa cku zilizopita unavyotusumbua kwa sasa.Dawa ni serikali 'kuziba mianya'.ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI.ZIDUMU
ReplyDeleteMzee Che Nkapa bora ungenyamaza tu!!!
ReplyDeleteSIJI N'GOOO.
ReplyDeleteMimi NKAPA
Mie chichemi,chitemi wala chimung'unyi.Ukinchema Nkapa atakuchapa chio utani!Yeye ankula Pencheni tu.Hana nchimamo wa kuwa Fichadi.Ntu njuli kwelikweli.Hapendi kuchika nchanga.Mipesa anayo Kibao.Uchitetemeke wala uchichikite.Uchije ukapigwa nchumali wa moto au nchale wa chingo njomba Palanchichi.Mbona Kunoga?
ReplyDeletehana lolote fisadi huyu tena ndie baba wa ufisadi tanzania.yote yaliyokuwa yanafanyika wakati wa awamu yake yalikuwa na baraka zake.Tunapozungumzia ufisadi wake tusimuache nyuma mkewe maana aliyofanya na machafu sana,mfano "kujichukulia" nyumba za TTCL pale Ilala.Familia chafu sana hii hata watoto wao waliwafundisha ufisadi na ni mafisadi haswaa!
ReplyDeleteby mangi
Laana ya mwenyezi mungu iwe nawe na wale wote ulioshirikiana nao kutumaliza. kweli moto wa ahera wawangoja.bado waendelea kupata pesheni kwa jasho la walalahoi walioibiwa!Inshallah Mungu yupo.
ReplyDeleteby Mangi
Jamani mwacheni mzee wa watu. Unadhani atatolea wapi gubu lake? Wengine walienda Arusha na Mwanza. Sasa akiendelea kufuga hiyo pressure ndani yake, na hivyo alivyo mtu wa kilo, si utashangaa siku moja PUFF!!!
ReplyDeleteSoma hapo chini, imetoka kwenye IPP leo May 28, 2008. HIVI HII NI KWELI? NA KAMA NI KWELI, HIVI WATU WENGINE HAWANA HAYA YA KUSEMA STATEMENTS KAMA HIZI HADHARANI? HASWA IKIWA NI RASI MSTAAFU?
ReplyDeleteMkapa hujajibu hoja - Baregu
2008-05-28 09:50:15
Na Lucy Lyatuu
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, amemshangaa rais mstaafu Benjamin Mkapa kwa kutoa majibu ya jumla dhidi ya tuhuma nzito zinazomkabili.
Alikuwa anazungumza na Nipashe kwa njia ya simu kuhusu utetezi alioutoa Bw. Mkapa huko Masasi mkoani Mtwara kuwa wanaodai kuwa ni `fisadi` wana chuki binafsi kwa vile aliwanyima madaraka akiwa Ikulu.
Profesa Baregu ambaye ni mtaalamu wa sayansi za siasa alisema tuhuma dhidi ya Rais mstaafu zinajulikana na zinaeleweka, hivyo hakutakiwa kutoa majibu ya jumla na ya juu juu.
Alimtaka kiongozi huyo kuweka wazi idadi ya watu aliowanyima vyeo au madaraka wakati akiwa madarakani ili kuipa nguvu hoja yake.
``Kwa mfano mimi sijawahi kutafuta kazi kwake sasa atatoaje majibu ya jumla kuwa wanaotoa madai hayo wana chuki binafsi wakati masuala ya Benki M na mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira unafahamika?`` alihoji Profesa Baregu.
Aliongeza kuwa kama Bw. Mkapa anataka kujibu tuhuma dhidi yake azungumze kwani mambo mengi yameandikwa kwenye vyombo vya habari.
Alimtaka asiandame watu kwa ujumbe mbaya na kumkumbusha kuwa ni vyema akafahamu kuwa majibu ya jumla hayamsaidii.
?Asitake kumuua tarishi kwa kuleta ujumbe mbaya,`` alisema Profesa Baregu.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa awamu wa pili, Jaji Joseph Warioba alipohojiwa hakuwa tayari kutoa maoni na kuongeza kuwa yaliyosemwa dhidi ya kiongozi huyo yanatosha.
Rais Mkapa alipochukua madaraka mwishoni mwa 1995 alianza kazi kwa kuunda Tume ya Kuchunguza Kero za Rushwa iliyoongozwa na Jaji Warioba.
Mkapa aliyeingia madarakani kwa jina la aliyetakata (Mr Clean) aliahidi kutumia ripoti ya Jaji Warioba kupambana na rushwa na kuondoa ufisadi serikalini, kitu ambacho hakikuwahi kuonekana waziwazi.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, akizungumzia utetezi huo alisema , Bw. Mkapa hajajibu hoja badala yake ameleta propaganda na poroja za kisiasa.
Akitoa maoni yake kwa njia ya simu kufuatia majibu ya Rais mstaafu, alisema Bw. Mkapa alitakiwa kujibu taarifa zilizopo kuwa amesajili makampuni wakati akiwa Ikulu na sio kuleta hoja za kwamba kuna waliokuwa wakitaka madaraka.
``Kama itakumbukwa, mwaka jana Septemba 27. mimi na Bw. Tundu Lissu, tulikuwa watu wa kwanza kutaja orodha ya mafisadi 11 akiwemo Bw. Mkapa,`` alisema.
Alisema binafsi hajawahi kupiga magoti akimuomba Bw. Mkapa ampe cheo au madaraka na alichonacho ni uchungu na rasilimali za Watanzania.
Alisema Bw. Mkapa akiwa madarakani alisajili makampuni ya ANBEN na Tanpower Resources Ltd ambayo rais huyo mstaafu na Waziri wa zamani wa Madini na Nishati, Bw. Daniel Yona walitajwa kuwa na hisa ndani ya Tanpower Resources.
Aliongeza kuwa hajawahi kufanya kazi serikalini na hategemei kuwepo na pia hana chuki ya kutokuwa na madaraka kama anavyodai Bw. Mkapa, kwa misingi hiyo anadhani kauli aliyoitoa haina ukweli.
Alisema anachotakiwa kufanya mtuhumiwa huyo ni kujibu hoja ya kwamba ni kweli alisajili kampuni hizo kwa anuani ya biashara ya Luthuli Street namba 15 ambayo ni ya Ikulu.
``Tunataka tu kujua alilipa kiasi gani kama gharama ya pango la kutumia Ikulu?`` alihoji.
Dk. Slaa aliongeza kuwa jambo lingine ambalo alitakiwa kujibu ni umiliki wa ANBEN, kampuni iliyokopa Sh. milioni 500 NBC na kushinikiza benki hiyo ibinafsishwe.
Aidha alisema jambo lingine ambalo anatakiwa kujitokeza na kulijibu ni nyaraka zilizoko kwa Wakala wa Kusajili na Kutoa Leseni kwa Kampuni (BRELLA) kwamba anamiliki makampuni hayo akiwa kama mjasiriamali.
Alimtaka kujitokeza hadharani na kujibu hoja hizo ili zionyeshe wazi ukweli wa kauli alizozitoa.
Jitihada za kuwapata kwa simu Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe na Katibu Mwenezi wa CCM Bw. John Chiligati hazikufanikiwa.
KAFUNGUA MDOMO BAADA YA SHAHIDI KUFA.ANAJUA TU ATAUZIWA MAFAILI YOTE KWA VIJISENTI TU.
ReplyDeleteanon 3:05 ACHA PUMBA,HUNA UCHUNGU NA NCHI WEWE!
ReplyDeleteWewe anon 12:57 unanishangaza sana,Nkapa amejidharirisha mwenyewe kwa vitendo alivyofanya alipokuwa hapo jumba jeupe! Unasema tufocus kudhibiti hali hii...tutafocus vipi pasipo kutoa adhabu kali kwa MAFISADI wote ili hata hapo baadae MAFISADI wengine wajue mshahara wao!
ReplyDeleteAnayesema tumuache mzee wa watu namuambia hivi.
ReplyDeletePesa zetu zirudishwe ndio atakua salama, la sivyo itakua fundisho kwa marais wote watakaofanya ufisadi na biashara hapo ikulu
Ooh... Mkapa!
ReplyDelete2008-05-28 20:50:03
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Siku moja tu baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Benjamin William Mkapa kusema kuwa yote mabaya yanayoelezwa kuhusu yeye yametokana na chuki binafsi za baadhi ya watu, mjadala zaidi kuhusu mali zake umezidi kuzua soo ambapo sasa wanasiasa wanazidi kumkomalia yeye na hata mkewe.
Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi, mhadhiri wa sheria wa Chuo Kikuu Dar es Salaam ambaye aliwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2005 kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi, amesema Mkapa anapaswa kuwafafanulia Watanzania juu ya taarifa mbalimbali za utata kuhusu kujilimbikizia mali yeye na mkewe wakati akiwa madarakani.
Aidha, D. Mvungi amesema maelezo ya jumla ya Mkapa wakati akiwa Kijijini kwao Lupaso kule Masasi mkoani Mtwara hivi juzi kwamba yote yanayosemwa kuhusu kutumia vibaya madaraka kwa kujilimbikizia mali ni uongo, hayatoshi na badala yake anatakiwa ajibu zaidi hoja zinazotolewa na wanaomlalamikia.
``Na tena si kutolea maelezo ya kina kuhusu mali zake tu... Mkapa anatakiwa pia kuwa muwazi zaidi kwa kueleza na mali nyingine zinazodaiwa kumilikiwa na mkewe.
Watanzania tunataka maelezo ya kina ili Rais wetu huyu mstaafu tumuweke katika kundi la walio safi,`` akasema Dk. Mvungi.
Mhadhiri huyo akasema miongoni mwa yale anayotakiwa kueleza Mkapa ni kuhusiana na majumba anayodaiwa kumiliki na kampuni ya ANBEM, uhusika wake katika mgodi wa makaa ya mawe Kiwira na kwingineko kwingi.
``Aseme ukweli kwamba hata Kiwanda (cha sukari) hahusiki nacho... wala nyumba iliyoko karibu na Aghakan ama Masaki hahusiki nayo... na hekalu lake kule Lushoto halina utata. Aeleze,`` akasema kabla ya kuongeza.
``Akishamaliza azungumzie pia mali za mkewe, mashamba na nyumba za huko Bagamoyo na ghorofa lililopo Ilala (sasa ni hoteli).``
Akasema Watanzania wanataka kuelezwa na kufahamu kama kweli alikwenda Ikulu kwa ajili ya kuongoza na si kuchuma mali.
``Hakuna mtu aliomba kazi kwake akanyimwa na aje aseme sasa itasaidia nini wakati yeye ameshastaafu,``akasema.
Madai ya kumbana Mkapa ili afafanue kuhusu tuhuma za kujilimbikizia mali pia yamenukuliwa leo kutoka kwa Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), ambaye amesema kinachitakiwa ni yeye (Mkapa) kujibu hoja za wabunge na wananchi wengineo kuhusiana na tuhuma alizo nazo.
Pia Mbunge wa Karatu, Dk. Willbroad Slaa amemtaka Mkapa ni kutoa ufafanuzi wa tuhuma azilizoelekezwa kwake hadharani na si kutolea maelezo ya jumla akiwa kijijini kwao .
Akasema Dk. Slaa kuwa Mkapa pia atoe ufafanuzi kuhusu kampuni ya ANBEM Limited kuendesha kazi zake kwa kutumia majengo ya Luthuli 15 pale Ikulu na pia ajibu kuhusu kampuni ya Tanpower Resources anayodaiwa kumiliki na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini, Bw. Daniel Yona.
Mbona hatuielewi hii serikali yetu ya sasa??? Inawezaje waziri Yona na rais Mkapa kuwa na tuhuma zote hizi na serikali imenyamaza kimya? Mbona baba zetu waliokuwa mawaziri enzi ya mwalimu nyerere walikuwa wakiitwa within 24 hours kujieleza kuhusu mali yeyoye vijana wa system wakinong'ona kwa tume ya kuchunguza tabia za viongozi iliyokuwa ikiongozwa na mzee kitundu? Siku hizi haya matume yanayoindwa mengine yanatuletea habari za uongo. Kwa nini kusiwe na tume permanent ya kuchunguza tabia za viongozi na pakiwa na tetesi yoyote juu ya ufujaji mali basi mtuhumiw huitwa kujieleza mbele ya tume hiyo. Maana hawa kina mkapa, Yona, Chenge, Karamagi by now wangeishaitwa na kutakiwa kutoa statements na siyo kwenda kuitolea masasi kwa wanavijiji, Im sure wenye degree labda hata watu 100 hawafiki kwenye halaiki aliyohutubia na nani alikuwepo wakumchallenge. Yale yale yaliyotokea kwa marehemu balali yasije yakarudia tena. Maana tuhuma zilianza tangu akiwa mzimaaa! Na hamna tume iliyomuita kumhoji kuhusu tuhuma hizi hadi mauti yalipomfika, halafu wanatuambia alikuwa huru, huru????? wakati kuna mabilioni ya pesa yamepotea chini ya uongozi wake? NAOMBA MTU ANIFAFANULIE MAANA YA KUSEMA KUWA HAWA WATUHUMIWA WAPO HURU!!!! NA NINAWAHAKIKISHIA CCM WAKIENDELEA NA STYLE HII,MTAONA UCHAGUZI WA 2010 MTAKAVYOLAZWA!!!!!JUST AN ADVISE, HUKO BONGO WALA SIRUDI I WISH NINGEONGEZA KURA HATA YA KUMPA MREMA IS BETTER
ReplyDeletekweli, kuishi kuona mengi. kama kuna mtu ambaye amepata kazi kwa kupendelewa....basi namba moja ni mkapa. mkapa ameingia madarakani kwa kupendelewa na hayati nyerere kwa sababu zisizojulikana, ameingia amekuta nchi taabani kutokana uongozi ambao ulitangulia, baadaye kaitia kaputi nchi,.sasa aliyependelewa ni nani? haingii akilini kwa watanzania wa ukiwambia kwamba mimi na mke wangu tumejinyima.....watanzania wamejinyima tangu tupate uhuru,sasa kama familia ya mkapa imeanza kujinyima, basi wawe wazi na hiyo migodi, majumba,viwanja mashamba,NGO na kadha wa kadha. hii ni nchi yetu, tuna haki ya kudai portion yetu na kama kuna jamii nyingine wajinyakulia portion kubwa tutadai, tutapiga kelele, tutawazomea mpaka waone aibu. wanaoshindwa kuvumilia aibu......they gone.
ReplyDeleteONLY THE TRUTH WILL SET YOU FREE
Hii hali ya kujifanya kuwaonea huruma hawa MAFISADI,eti tumuache mzee wa watu apumzike!ni ujinga uliopindukia.hivi hawajiulizi wazazi/ndugu zao wanavyopata shida kuona,njaa na kila ukali wa maisha unao waandama,mwisho wanaishia kuja mijini kupanga foleni kuomba kwao misaada???Huyu mkapa anatakiwa atueleze mkewe alikua anafanya wapi kazi kiasi cha kupata mijisenti yote ya kumuwezesha kulinunu Jengo la Twiga House mt samora.Wote tunajua jinsi alivyo lipata.na kama yeye ni masikini aliwezaje kuanzisha hiyo ANBEN na alipata wapi 70mil kuununua mgodi wa makaa ya mawe ambao uligharimu serikali hela yetu ya kodi zaidi ya 7bil shillings na kuuziwa kwa 700mil ambazo wao walilipa 70mil tu.
ReplyDeleteHesabu hiyo nayo wanaomtetea hawiwezi??? ama ni ulimbukeni wa mambo tu.kwa hara haraka hawa wanaonekana ndio waliomba kazi wakanyimwa.
Lazima tuwatolee macho Mafisadi mpaka kieleweke.
**Kisoda**