Mama Salma Kikwete akikagua baadhi ya madini yaliyokuwa yanaoneshwa na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania(TAWOMA) katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Mama Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika kuadhimisha siku ya wachimbaji madini iliyoandaliwa na chama hicho. Katika hotuba yake wakati wa hafla hiyo Mama Kikwete amewahimiza wanawake hao kuimarisha vyama vyao vya ushirika ili kupata mitaji ya kutosha na kuratibu shughuli zao kwa ufanisi Zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2008

    Mie nilidhani hao akina mama wanadoa macho kuangalia aina za chatini... kumbe aisee ni madini,yaani 'best friend of a woman'!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2008

    mama salma huwa anapendeza wajameni haswa akivaa kiafrika na sio kimagharibi.umependeza sana mama.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2008

    MAMA KIKWETE UMEPENDEZA MUNGU AKULINDE AFYA YAKO MAMA YETU KILA LKHERI KATIKA SHUGHULI ZOTE ZA KIJAMII

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2008

    Binti nimekubali mapigo yako....ama kweli uu mrembo kweli kweli.......hongera mdada.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2008

    tunashukuu na kuona kwamba akina mama wanakuja juu katika biashara mbalimbali na kujitahidi kujiinua kiuchumi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 08, 2008

    NYIE KINA MAMA NA KINA DADA. KWANZA HONERENI. LAKINI MBONI MNA ROHO MBAYA? MNATAKIWA KUWASAIDIA WANAWAKE WENZENU AMBAO HAWANA KAZI YOYOTE ILA KUKAA TU KAMA VILE KINA LILIAN MZIRAY. WAHAMASISHENI KATIKA BIASHARA HIZI. HATA KAMA HAWANA ELIMU, SI HOJA, KWANI MAMBO YA MADINI NI RAHISI KUJIVUNJA NINAUHAKIKA WATAMUDU. TANGAZENI KUPITIA MICHUZI BLOG, KAMA MNAVYOONA WENGINE WANATANGAZA KUTAFUTA KAZI HUMU, NA WATAFANIKIWA. HII BLOG IMESAIDIA MENGI NA KULETA MAENDELEO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...